Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Thursday, October 31, 2013

Ney wa Mitego asimulia kilichotokea

 
Rapa wa muziki wa kizazi kipya, Ney Wa Mitego akiwa katika pozi, amesimulia yaliyomkuta kuhusu sare ya jeshi la Polisi. Picha na Maktaba 
Na Herieth Makwetta, Mwananchi
 
Akizungumza na Mwananchi, rapa huyo alisema sare hizo za polisi zilishonwa kwa ajili ya kazi hiyo na wala hazikuwa sare halisi za kipolisi.


Dar es Salaam. Siku chache baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kutumia sare za polisi bila kibali katika video ya wimbo ‘Salamu Zao’, na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Urafiki Manzese Jijini Dar es Salaam, rapa wa muziki wa kizazi kipya, Ney Wa Mitego amesimulia mkasa mzima na kusisitiza kuwa wabaya wake ndiyo waliycheza mchezo huo.
Akizungumza na Mwananchi, rapa huyo alisema sare hizo za polisi zilishonwa kwa ajili ya kazi hiyo na wala hazikuwa sare halisi za kipolisi.
“Mavazi haya ya kipolisi yalikuwa rasmi kwa ajili ya kutengeneza video ya Salamu Zao na hayakuwa halisi, ila nilishangaa pale nilipokamatwa na watu wasiojulikana jumamosi ya wiki iliyopita wakati tukitengeneza video, wakidai kwamba wao ni askari.Walinichukua hadi kituo cha urafiki, pale niliwekwa sero kwa kipindi cha dakika 20 hivi, baada ya kutoa maelezo ya kutosha niliachiwa”.
Baada ya kuachiwa, alirudi na kukamilisha kazi yake ambayo ameweka wazi kuwa itakuwa hewani wiki hii.
“Video ya Salamu Zao itaachiwa hewani Ijumaa ya wiki hii, hivyo watarajie kitu kipya na adimu kuonekana,” alisema Nay na kuongeza “Sijajua bado ni nani aliyenichomea lakini naahidi kuwa itaendelea kula kwao wale wote wanaonichukia na kamwe siwezi kuacha kuusema ukweli.”
Uongozi wa kituo cha Polisi Urafiki jijini Dar es Salaam ulithibitisha kumtia mbaroni msanii huyo kwa kukutwa akitumia sare zinazofanana na mavazi ya polisi kinyume cha sheria. Ofisi mmoja wa polisi ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini anasema waliamua kumuachia kwa vile waliridhika na maelezo yake.

BALOZI SEPETU ALIVYOAGWA JIJINI DAR MAPEMA LEO, NA USOME WASIFU WAKE HAPA

Hivi ndivyo Balozi Isaac Abraham Sepetu alivyoagwa jijini Dar es Salaam Oktoba 29, mwaka huu nyumbani kwake Sinza-Mori. Balozi Sepetu amezikwa jana Visiwani Zanzibar.
WASIFU WA BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU
Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa Oktoba 16, 1943  mkoani Tabora na kabila lake ni Myamwezi.
Alihamia Visiwani Zanzibar alipokulia na kupata elimu yake chini ya uangalizi wa Said Sepetu Langa pamoja na Mzee Abeid Amaan Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
1952 - 1963 Balozi Sepetu alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mt. Joseph iliyopo Zanzibar.
1964-1970 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Berlin, Ujerumani na kupata Shahada ya Uzamili katika Uchumi (Masters Degree in Economics).
1971-1972 Balozi Sepetu aliajiriwa katika Serekali ya Mapinduzi Zanzibar akiwa Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Shirika la Biashara ya Nje Zanzibar.
Pia aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ikulu ya Zanzibar.
1972-1977  Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1977-1979  Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habri na Utangazaji katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1979-1982 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1982- 1989 Aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la Usoviet (Soviet Union).
1989-1990 Aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zaire.
1990-2000 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Mipango katika Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.
Pia aliwahi kuwa Mshauri wa Rais katika Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Tume ya pamoja ya (IPC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Balozi Sepetu aliwahi pia kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

ALICHOKIANDIKA DIAMOND MARA BAADA YA KUHUDHURIA MAZISHI YA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU




Babu Tale, Zamardi na Diamond ndani ya Zanzibar kwaajili ya mazishi ya Balozi Sepetu 

Monday, October 28, 2013

‘FIESTA PART TWO’ YAFANA KINOMA LEADERS CLUB

Diamond akifanya mambo yake na madensa wake.
 
Davido akiwasalimia mashabiki.
 
Mmoja wa wapambe wa Davido.
Davido na mwenzake wakiwaimbisha mashabiki.
 
 Mrisho Mpoto na jamaa kutoka Push Mobile wakimtangaza mshindi wa gari mkoa wa Dar es Salaam.
 
Mtangazaji wa kipindi cha XXL, Adam Mchomvu, akiwapagawisha mashabiki.
 
TID Mnyama akifanya ‘mavitu’ yake.
 
…Akiendelea kukamua.
Diamond na Davido wakiimba My Number One Remix.
 
Fid Q naye alikuwapo.
TAMASHA la Fiesta awamu ya pili lililofanyika jana mchana katika viwanja wa Leaders Club, Kinondoni, Jijini Dar es Salaam,  lilifana na kuvuta maelfu ya mashabiki na kuwasahaulisha wengi yote yaliyojitokeza juzi usiku.
Onyesho hilo ambalo lilikuwa la bure, lilitoa burudani ya kukata na shoka ambapo lilihusisha majina makubwa ya wanamuziki wa kutoka nje ya nchi na ndani.

FIESTA 2013... LAIVU!

Na Waandishi Wetu
SHOO kubwa ya Serengeti Fiesta 2013 jijini Dar usiku wa Jumamosi ilifunga mitaa na kusababisha kila aliyehudhuria kutoka na msemo mmoja tu, yaani noma sana, Ijumaa Wikienda lilikuwa laivu kukupa ripoti kamili.
Snura akionyesha mbwembwe zake jukwaani.
Katika burudani hiyo, timu ya gazeti hili ilijipanga kukuletea kila kilichojiri ambapo mapaparazi wake, Musa Mateja, Richard Bukos, Shakoor Jongo na Erick Evarist walikuwa wakiwasiliana na mkuu wao aliyekuwa makao makuu, Bamaga-Mwenge na kuanika matukio yote katika mtiririko wa moja kwa moja (laivu) kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni.
Linah akicheza sambamba na Amin ndani ya Serengeti Fiesta 2013.
SAA 2:45 USIKU
Shakoor: Mkuu nipo nyuma ya jukwaa, huku mastaa wamefunikana vibaya kwa mavazi, daah! Aisee.
Makao Makuu: Shakoor ondoka eneo ulilopo, nenda katafute vituko na matukio zaidi siyo kushangaa mavazi ya hao wasanii.
Shakoor: Sawa mkuu, nimekuelewa.
SAA 3: 30 USIKU
MKE ABEBWA JUUJUU NA MUMEWE
Erick: Mkuu nipo getini hapa nje kuna bonge la msukumano kutokana na umati mkubwa wa watu wanaogombea kuingia.
Makao Makuu: Kuna kituko au tukio lolote umelishuhudia hapo?
Erick: Mkuu ngoja kuna mama mmoja amebebwa juujuu na mwanaume mmoja anadai ni mkewe alikuwa anamsaka tangu mchana akatonywa yupo Fiesta ndiyo amekuja kumchukua hivyo wanakabana makoo.
Makao Makuu: Waambie kama vipi tutume kikosi cha OFM, achana nao, ingia ndani unipatie kinachojiri.
Erick: Mkuu nimeshafika mbele kabisa hapa, baada ya H. Baba kumaliza shoo, Juma Nature ndiyo yupo stejini anapiga bonge sla shoo.
RAY C AGEUKA MPAMBE WA RECHO THT
Makao Makuu: Sijapata vituko vinavyojiri ‘back stage’, hebu chepuka upande huo mara moja.
Erick: Ndiyo naingia hapa, namuona Ray C kageuka mpambe wa Recho wa THT anampepea kabla ya kupanda stejini.
Makao Makuu: Sawa, huyu hapa Bukos, hebu sema kuna tukio gani hapo?
Bukos: Kwa sasa Walter Chilambo ndiyo amepanda anapagawisha.
Makao Makuu: Hebu tafuta matukio makubwa kwa mashabiki.
Bukos: Sawa lakini mkuu sasa ni zamu ya Godzillah anawaimbisha watu na wamemkubali kinoma na Lakuchumpa Lakuparama.
SAA 4: 40 USIKU
LINAH, AMINI MAHABA MH!
Makao Makuu (anampigia Shakoor): Shakoor mbona kimya ina maana huoni matukio?
Shakoor: Mkuu ameshuka Joh Makini na Weusi G-Nako na Nikki wa Pili wamefanya bonge la shoo, wamekula bonge la shangwe kisha wamewapisha Linah na Amini ambao wanaimba kimahaba.
Makao Makuu: Ngoja nimpokelee Erick anapiga.
Erick: Mkuu sasa hivi Barnaba amepanda kuungana na Amini, wamefanya bonge la shoo kwa kutumia ‘laivu bendi’.
Makao Makuu: Oke.
Bukos: Mkuu sasa ni zamu ya Msechu, shangwe ni za kawaida.
Makao Makuu: Bukos sasa hivi nataka matukio kwa mashabiki.
Bukos: Nyuma yangu kuna sharobaro kavamia ‘maji’ anafanya fujo kabebwa na mgambo wanamtoa nje, lazima akifika huku pombe zitamuishia.
Makao Makuu: Piga picha nazitaka ofisini.
SAA 05: 05 USIKU
SHADEE ‘AJIBEBISHA’ KWA YOUNG DEE
Erick: Mkuu hapa kwenye steji ni zamu ya Mabeste ambaye amewarusha mashabiki na Baadaye Sana kisha akampisha Christian Bella.
Makao Makuu: Oke. Shakoor anapiga ngoja nimsikilize.
Shakoor: Hapa nilipo namuona mtangazaji Shadee ‘amejibebisha’ kwa Young D, wamegandana kama ruba.
Makao Makuu: Nirushie picha fasta ngoja nimcheki Mateja.
SAA 05: 50 USIKU
RAY C STEJINI KWA MARA YA KWANZA
Erick: Mkuu stejini ni zamu ya Recho wa THT, anapagawisha na nyimbo za Ray C. Mashabiki wanapiga kelele baada ya Ray C kupanda stejini kwa mara ya kwanza na kuimba naye Wimbo wa Umenikataa. Ray C amekula shangwe kubwa kinoma.
Makao Makuu: Dah! Kweli ni mshtuko ngoja nimcheki Bukos.
6:05 USIKU
SNURA AMFUNIKA SHILOLE
Bukos: Mkuu baada ya Shilole amepanda Snura, wewe mwenyewe unaweza kusikia anavyopigiwa kelele jinsi alivyomfunika Shilole kwa mauno na ngoma zake za Nimevurugwa na Majanga.
Makao Makuu: Safi sana ngoja nipokee simu ya Erick.
Erick: Sasa hivi ndiyo Linex anashuka Mkuu, naye kapagawisha kwani ameimba kwa kushirikiana vizuri na mashabiki wake na sasa anampisha Kassim Mganga ambaye anawarusha kinoma.
SAA 6:25 USIKU
KILA MTU NA WAKE ‘TOILETI’
Makao Makuu: Sawa, sasa hebu nipe vituko nje ya steji.
Erick: Hapa nilipo kiongozi ni kwamba kila mwanaume anakatiza kuelekea ‘toileti’ na ‘kiburudisho’ chake kwa sababu akiacha aende mwenyewe lazima midume wapite naye.
Makao Makuu: Duh! Kuna kingine?
7:02 USIKU
SHILOLE AZICHAPA
Erick: Upande wa pili karibu na nyuma ya steji kuna vurugu…ngoja niwahi. Mkuu hapa namuona Shilole anazichapa kavukavu na mrembo aitwaye Finance.
Makao Makuu: Kisa ni nini?
Erick: Shilole kamuomba tishu alipomnyima ndipo akammwagia maji kisha zikapigwa. Yule anaelekea Oysterbay kumshitaki Shilole.
7:00- 8:00 USIKU
WASANII WA KIMATAIFA
Makao Makuu: Bukos vipi wasanii wa kimataifa?
Bukos: Kwa sasa Allaine wa Jamaika ndiyo yupo stejini, anawaimbisha watu kibwagizo cha ‘nakupenda pia’, naona shangwe zimekolea.
Makao Makuu: Baada ya huyo nani anafuata?
Bukos: Mkuu listi ya wasanii wa kimataifa bado ni ndefu, kuna Davido, Mohombi, J-Martins na Inyanya. Pia bado wasanii kibao wa Kibongo hawajakamua kwa hiyo ngoma inaonesha itakesha mpaka majogoo.
Makao Makuu: Sawa Bukos, wewe na timu yako endeleeni kufuatilia kila kitu hatua kwa hatua, tunasubiri mzigo mzima asubuhi ya kesho. Shoo ikiisha waambie wenzako mkapumzike, asubuhi muwahi ofisini.
Bukos: Sawa mkuu.

WEMA AZIMIA MARA TATU

Stori: Makongoro Oging’ na Jelard Lucas
MISS Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu, wikiendi iliyopita aliingia katika kipindi kigumu zaidi katika maisha yake, kwa vile lilikuwa tukio zito kulibeba baada ya kuzimia mara tatu ndani ya saa 7.
Wema Isaac Sepetu akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi.
Wema ambaye ni nyota wa filamu Tanzania, alizingirwa na maumivu makali, yaliyotokana na kumpoteza mtu anayempenda sana, baba yake mzazi, marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.
Balozi Sepetu, alifikwa na mauti Jumapili iliyopita saa 12 asubuhi, ikiwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na shinikizo la damu ambavyo vilimsababishia kupata ugonjwa wa kupooza viungo (kiharusi).
Mzee huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, alifikwa na mauti akiwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Awali, Balozi Sepetu alitolewa Zanzibar alikokuwa anaishi baada ya kuzidiwa kisha akapelekwa TMJ, alipopata nafuu aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Hata hivyo, aliporuhusiwa hakurejeshwa Zanzibar, badala yake alipelekwa kwenye nyumba yake iliyopo Sinza Mori, jijini Dar es Salaam ambako alihudumiwa kwa muda kabla ya afya yake kubadilika na kukimbizwa TMJ ambako mauti yalimfika.
Wema akiwa na majonzi wakati wa msiba wa baba yake nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar.
WEMA KUZIMIA
Chanzo chetu kilisema: “Wema bado mdogo, katika maisha yake hakuwahi kupatwa na msiba mkubwa kama huu, kumpoteza baba yake kipenzi, ni jambo zito ndiyo maana mpaka sasa tunaongea ameshazimia mara tatu, yaani anazimia na kurejewa na fahamu.”
Jumapili saa 7 mchana baada ya kurejewa na fahamu, alisema: “Nimeumia sana kwani huu ni msiba mkubwa kwangu, Baba yangu alikuwa nguzo imara katika maisha yangu, sikuwahi kufikiria kama ningepata msiba mkubwa kama huu.
“Taarifa hizi wakati nazipokea nilijua kama utani lakini yote ni mipango ya Mungu, inaniuma sana,” alisema Wema.
WASIFU MFUPI WA MAREHEMU MZEE SEPETU

Balozi Sepetu aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar, vilevile akawa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miaka ya 1970 wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwaka 1982, alteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, wadhifa ambao aliendelea kuushikilia mpaka kipindi cha Awamu ya Pili chini ya Rais Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Kati ya mwaka 2001 na 2006, Balozi Sepetu alichaguliwa kuwa mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, Zanzibar.
Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi visiwani humo (Zipa).
Machi 27, mwaka huu, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alimteua Balozi Sepetu kuendelea na wadhifa huo wa Zipa kabla ya mauti kumchukua.

Saturday, October 26, 2013

DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA YEYE KURUDIANA NA WEMA NA KUACHANA NA PENNY

 
MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.
Akizungumza  kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.
Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.

SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.
Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.
“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.
Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.
“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.” SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.
 
SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

 
SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye. 

 
SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

 
HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.
“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.
 
PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.

Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

Friday, October 25, 2013

MWANAMUZIKI MOHOMBI NZASI AWASILI JIJINI DAR

Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo (kulia) akifanya mahojiano na wanahabari baada ya kutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kufanya shoo kali ya Serengeti Fiesta inayotegemea kufanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club.
Mohombi (kulia) akisindikizwa kutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kushuka na ndege ya Turkish Air Lines na Afisa wa ndege hiyo Ebubekir Ekici ambaye pia alifurahia ujio wake Tanzania.
Msanii wa kimataifa anayetamba na kibao chake kikali cha “Kiss Me” akiwa amepozi na mtangazaji wa Clouds TV baada ya kupokelewa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya shoo kali ya Serengeti Fiesta itakayofanyika kesho katika Viwanja vya Leaders Club. Mbele yake ni Fauzia mratibu wa shughuli za Serengeti Fiesta kutoka Prime Time Promotions.

DINI MPYA YA AJABU ILIYOANZISHWA HUKO MBEYA INAWAFAA WENGI.SOMA HAPA UJIONEE MAAJABU

Diniinayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine 
zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya 
mkoani Mbeya,
Dinihiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka 

wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU 
mali zake Mwnyewe.!
Dinihiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na 

MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO,
sasa imeanza kuenezwa Mbeya
=========================
Ufafanuzi
=========================
By GAMBISHI DWESE
Yawezekana
kweli Bwana Domy umekutana nami. Mimi Ndiyo PAPA-DIMAYO 1: GAMBISHI 
DWESE,( nabii wa kwanza wa DIMAYO) hata hivyo pengine umeninukuu 
kimakosa.Kwanza kabisa Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muumbaji 
aliye hai wala aliyekufa anayedaiwa kuhusika na kila kinachoendelea 
ulimwenguni.
Na
nimeshatoa kitabu kinachoitwa HAKIKA HAKUNA MUNGU MUUMBAJI ALIYE HAI 
WALA ALIYEKUFA anayehusika na kila kinachoendelea. kijitabu hiki 
kinaeleza kinagaubaga kwanini Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu 
muuumbaji. nikipata nafasi nitakiingiza kwenye mtandao ili watu wengi 
wakisome.
Ni
kweli hakuna kitu Dhambi bali kuna makosa. na kosa linaweza kuwa kosa 
kulingana na mazingira na wakati katika jamii tofauti. Na ni kweli 
kwamba dini yetu ni ya starehe wala si ya mateso, maana tunaamini hakuna
maisha zaidi ya haya tuliyonayo. Dimayo haijampa mtu ruksa ya kuvunja 
kanuni halisi asili wala sheria halali ya serikali yake halali na wala 
haina upotoshaji hata kidogo. 
Kinachoitwa
sadaka kwetu huwapa watu wenye matatizo. Ni kweli kuna michango mingine
lakini ni ya hiari na ni kwa ajili ya ushirika. Ni kweli kwenye JUMADI 
(jumba la makutano la Dimayo kutakuwa na kaunta ya vinywaji). unajua 
kunywa na ulevi ni vitu viwili tofauti; ulevi ni tabia ya mtu ya kutumia
vileo kupindukia, lakini kwetu tunasema kunywa uwezavyo ilimradi huumii
wala kuumiza vyote kisaikolojia na kimwili, kwa mantiki hiyo ulevi 
kwetu noma ila unywaji ni safi.
Uchawi
ni sayansi, ila utumike kwa faida siyo kwa kuleta madhara. kuwaambia 
watu eti acheni ngono eti mungu hapendi wataacha?. wambie wafanyeje 
ngono kulingana na wakati na mazingira. Dimayo inamfundisha mtu kutenda 
inavyofaa yanayofaa kutendwa kwa kufuata kha na kahaka.


Anyway nashukuru kwa kuianzisha mada hii, nafikiri nitachukua nafasi kuielezea zaidi kila inavyowezekana.


Nina uhakika kwa mtu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zake hawezi kupingana hata kidogo na DIMAYO.


-JF

DANGURO LA MADENTI LAFUMULIWA

Na Waandishi Wetu
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wamefanikiwa kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo mbalimbali jijini Dar.
Madenti hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro hilo lililopo ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.
KERO
Awali kikosi kazi cha OFM kilipokea malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Mzazi:Halooo…nazungumza na OFM?
OFM: Ndiyo…tukusaidie nini?
Mzazi: Mna habari?
OFM: Tunazo nyingi lakini ukitupatia ya kwako tutaifanyia kazi ipasavyo.
Mzazi: Tunawaamini OFM mnatisha kama njaa. Sisi ni wazazi wa hapa Buguruni-Sokoni. Kuna danguro hapa kwa kweli yanayofanyika ni aibu tupu. Tunaomba mje mjionee wenyewe mfanye kazi yenu.
OFM: Nini hasa kinafanyika?
Mzazi: Yaani vitendo vya ngono vinafanyika na sasa hivi hata kwa nje wapo watu wanafanya biashara haramu ya ngono hivyo watoto wetu wanashuhudia vitu vya ajabu na kondomu zimezagaa kila kona.
OFM: Sawa, tuachie tufanye kazi yetu.
Mzazi: Oke, lakini naomba chondechonde msinitaje wala kuonesha namba yangu kwa sababu hii ni biashara ya watu nitamwagiwa tindikali bure!
OFM: Tunaheshimu vyanzo vyetu hatuwezi kukutaja popote kwani siyo maadili ya kazi yetu.
OFM KAZINI
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, vijana wa OFM waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya makachero wa OFM walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za kutosha huku wakiwarekodi wahusika (madenti wanaojiuza na wanaume wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya kazi bila wao kushtuka.
BEI
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia buku mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na kuendelea.
Mmoja wa vijana hao wa OFM alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji ambapo alipofika na kujionea mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo kuwa alikuwa amepokea simu ya dharura.
USHUHUDA MBAYA
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani, anasimulia: “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.”
TAARIFA POLISI
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua danguro hilo, OFM iliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo.
Bila kusita, kamanda huyo aliteua vijana wake kutoka Kituo Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.
DENTI IFM
Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa na polisi, mmoja wa madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.
Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja hicho cha maasi ni denti aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.
Denti mwingine aliyekamatwa katika msala huo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.
MUUZA KONDOM NAYE MBARONI
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa njemba mmoja aliyekuwa ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.
Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza mwili.
NYUMA YA NONDO
Baada ya kuhojiwa kuhusika na biashara haramu ya ngono na kukiri, watuhumiwa hao wote waliwekwa nyuma ya nondo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la kesi namba BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
WAZAZI SOMENI HAPA
Uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa madenti hao na wengine wengi jijini Dar, wamekuwa wakiaga kwao kuwa wanakwenda masomoni lakini kumbe wanaishia kwenye madanguro yaliyojazana jijini kwa ajili ya kujiuza.
Huku wazazi wakitoa fedha nyingi na huduma nyingine wakiamini watoto wao wanasoma, hali ni tofauti kwani madenti wengi wamekuwa wakiishia kwenye vitendo vya kihuni na kufeli masomo na maisha kwa jumla kisha kugeuka mzigo kwa familia.
Gazeti hili linawataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao wanaowasomesha ili kuwakanya juu ya kujiingiza kwenye uhuni ambao huhatarisha maisha yao -Mhariri.

Monday, October 21, 2013

Hii ndio list nzima ya wasanii watakao wakilisha stage ya Fiesta 2013

Alaine
Wiki iliyopita lista ya wasanii wawili kutoka nje ya Tanzania ilitangazwa, ambao ni Alaine (Jamaica) na Davido (Nigeria) ambae alithibitisha kushuka na J Martines, sasa leo hii wasanii wawili zaidi wamethibitishwa kushuka ikiwa ni
Mohombi ambae ametangazwa leo asubuhi pamoja na Iyanya kutoka Nigeria ambae ametangazwa kupitia xxl ya Clouds Fm.

Davido
na hawa ndio wasanii wetu watakao-share stage moa na wasanii hao, Ommy Dimpoz, mwana FA na AY, Rich Mavoco, Makomando, Weusi, Lina, Shilole, Snura, Recho, Young Killer, Stamina, Country Boy, Godzilla, Cassim, Quick Rocka, Juma Nature, Ney wa mitego, Madee, Nikki Mbishi, Kala Jeremiah, Linex, 

Iyanya
Chidi Benz, Shettah, H Baba, Samir, Darasa, Afande Sele, Baba Levo, Peter Msechu, Mabeste, Mirror, Menina, Walter, Nuhu, Cliff Mitindo, Blue, Young D, Dully, Amini, Christian Bella, TID, Kala Pina, Ney Lee, Fid Q, Ben Pol, Vanessa, Chege na Temba, Diamond na Gosby.

Mohombi

The Session - Mr T Touch HD ya KenedyThe Remedy, sindio hii hapa sasa,

Sunday, October 20, 2013

JOKATE AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIAMOND, HASHEEM - (GLOBAL TV) MAPYA YAIBUKA

Na Waandishi Wetu
KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.…

Na Waandishi Wetu
KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.
 
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.

DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;
Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.
 
Hasheem Thabeet Manka katika pozi na Jokate.
PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?
Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.

‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.

KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?
Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.
Diamond akimpatia Jokate T-shirt. katika shoo ya Diamond are Forever ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar mwaka jana.
DIAMOND ALIMTIBULIA
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.

ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?
Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.
Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.
Jokate akiongea na GPL.
HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?
Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…
Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...
Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?
Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.
Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.

SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.
Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?
Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.
Diamond akicheza na Jokate.

ZAWADI
Ijumaa Wikienda: Kati ya Diamond na Hasheem nani zaidi kwa zawadi?
Jokate: Naona sasa unataka kumkasirisha Diamond!
Ijumaa Wikienda: Tangu ulipoachana na Diamond una zaidi ya mwaka. Je, huna mpenzi mwingine?
Jokate: Nipo singo au unanishauri nani ananifaa?
Ijumaa Wikienda: Siwezi kuingia kwenye moyo wako wakati umesisitiza kuwa unampenda Hasheem!
Jokate: Yap…nilimpenda na ninampenda sana.

MWANA-FA VIPI?
Ijumaa Wikienda: Mbali na Hasheem, Diamond na huyo jamaa wa zamani, vipi kuhusu habari za wewe kutoka na mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana-FA’?
Jokate: Afadhali mnisaidie kwa sababu sijui hicho kitu kilianzia wapi. Ni uzushi tu uliosambazwa na mtu mmoja.