Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, February 26, 2014

Maneno ya Diamond Platnumz kuhusu wasanii wanaomtengenezea ugomvi.

Screen Shot 2014-02-27 at 9.37.36 AM
Staa huyu wa ‘Number 1 rmx’ ft Davido ameiandika hii na kuisambaza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na facebook.

Screen Shot 2014-02-27 at 9.36.11 AM 

baada ya bifu zito la muda mrefu baina ya Mecca Cheka na Jambo Squad lafikia ukingoni kwa style hii. soma hapa

baada ya bifu zito la muda mrefu baina ya Mecca Cheka na Jambo Squad limefikia ukingoni na kurekebisha tofauti zao walizokuwa nazo na hiki ndicho alichopost facebook Almando Mwiroro
"MECCA CHEKA vs JAMBO SQUAD nw we ar together again.. so MAALMANDO WATOTO WA BIBI is back again no bifu wala nin.. tunawapenda sana na tunaomba radhi kwa yote yalitokea mashabik wetu"

theHOODinfotainment inawapa BIG-UP KUBWA n MUCH RESPECT 

Wednesday, February 12, 2014

HUYU NDIO DIAMOND KABLA HAJAWA SUKARI YA WAREMBO,TAZAMA PICHA NA UJUE MAMBO AMBAYO ULIKUWA HUYAJUI.

Diamond-Wema-Baba-yake

Mambo matano Yatakayokugusa katika maisha ya Diamond Platnumz
01. Diamond Platnumz aliachwa na baba yake
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake diamond.
02. Chumba  kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko tandale na ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake apangishe chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba kimoja na bibi na mama yake.
Diamond-na-bibi-yake
03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na
alipomaliza elimu yake ya O’level ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa elimu yake.
diamond-utotoni-slider
04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.
Diamond-zamani
05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.
Diamond-na-mama-yake

MAMA KANUMBA AJA NA MPYA INAYOMUHUSU WEMA SEPETU

Hamida Hassan na Gladness Mallya
SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kukiri kwamba Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikuwa mkwe sahihi kwake, safari hii ameibuka na kumbariki Wema Sepetu ambaye naye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye, akisema ana huruma, roho nzuri na utu.
Mama Kanumba, Flora Mtegoa.

Akizungumza kwa kujiamini, mama Kanumba alisema: “Hili nalizungumza kutoka moyoni mwangu, huyu mtoto ana moyo wa upendo sana. Angalia namna anavyowasaidia wenzake wanapopata matatizo. Anajitoa kwa moyo, siyo mchoyo. Kwa kweli Mungu amwongezee.”
Wema Sepetu.
“Kiukweli Wema anajitoa sana... nakumbuka hata kipindi akiwa na mwanangu, maana uhusiano wao niliutambua, Kanumba mwenyewe alinitambulisha; walikuwa wakija kunisalimia nyumbani ananiita pembeni na kunipa pesa ili Kanumba asione, akitaka na yeye anipe. Huo ni moyo wa kipekee sana,” alisema mama huyo. Hiki ni kama kipindi cha mama huyo kuonesha hisia zake kwa wakwe zake (wasichana waliowahi kuwa na uhusiano na marehemu mwanaye) kwani takribani wiki tatu zilizopita, alimzungumzia Lulu kwa maelezo kuwa alikuwa mkwe sahihi kwake.

gpl

ANGALIA MBINU MPYAILIYOTUMIKA KUSHAFIRISHIA MADAWA YA KULEVYA

 b4
Unaambiwa kwenye mji wa Berlin huko Ujerumani kwenye supermarket tano yamepatikana mabox yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikua na dawa za kulevya zilizofichwa ambazo ni kilo mia moja arobaini.
Ni kosa ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa wenyewe manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza matunda kwa jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa meli kutokea Colombia.

B1 
Wafanyakazi wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo ndani yake ndio kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.

Unaambiwa mzigo huu wa Cocaine ndio mzigo mkubwa kukamatwa kwenye mji huu mkuu wa Berlin kwenye kipindi cha miaka 15, ni mzigo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 8 na laki mbili.

b2 
Polisi wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.
b3