Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, April 28, 2014

ANGALIA PICHA ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA SUDAN YA KUSINI,TUITUNZE AMANI YETU.

http://www.ufukunyuku.blogspot.com/ 
Umoja wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini.Umoja huo umesema kuwa watangazji katika baadhi ya vituo vya redio walitumia lugha ya chuki na uchochezi na kuwataka watu wa kabila fulani kuondoka mjini humo huku wakiwashauri wanaume kuwabaka wanawake.



UNGA WAZIDI KUMTESA RAY C

Rehema Chalamila ‘Ray C’ katika pozi.
NA MAKONGORO OGING'
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye aliwahi kuathirika na utumiaji wa ‘unga’, hivi karibuni alitinga ofisi ya kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya na kuomba kupatiwa majina, idadi na sehemu walipo watumiaji wa mihadarati hiyo ili aweze kuwasaidia kwa kuwapa somo, kitu kinachotafsiriwa kama bado unamtesa.
Ray C katika harakati zake akifanya mahojiano na msanii wa Hip hop, ambaye yupo mbioni kuachana na madawa ya kulevya, Ibra the Hustler.
Ray C anadaiwa kufika katika ofisi hizo, Aprili Mosi, mwaka huu, saa nne asubuhi hali iliyozua gumzo kwa askari waliomuona ambao walijiuliza kitu alichokifuata.
Akizungumza na Uwazi, kamanda wa kitengo hicho cha madawa ya kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kufika kwa msanii huyo ofisini kwake na kutoa madai hayo lakini alimwelekeza kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani huko kuna kitengo kinachoshughulika na watu wenye matatizo ya akili wakiwemo watumiaji wa madawa ya kulevya.
Ray C.
Kamanda huyo alionesha kufurahishwa na kitendo cha msanii huyo ambaye pia anamiliki taasisi yake yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa matumizi ya madawa hayo kwa kuwapa elimu, akisema atatoa msaada mkubwa kwa wenzake.
Aliwataka watumiaji wa madawa hayo ambao wameshindwa kuacha, wamfuate msanii huyo ili awape elimu na amewaonya wote wanaotumia na kusafirisha madawa hayo.
“Wote wanaotumia na kuuza madawa hayo waache mara moja kwani kikosi kazi kinachopambana na biashara hiyo kimejipanga kila kona ili kukomesha biashara hiyo haramu,” alisema Kamanda Nzowa.

chanzo: GPL

NAY WA MITEGO ATAFUTWA KWA KESI YA KUTISHIA KUUA

Msanii wa Hip Hop Tanzania Emanuel "Nay wa Mitego True Boy" anatafutwa kwa kosa la kutishia kuua.
Kwa mujibu wa Suddy Baya ambae ndie alietishiwa kuuliwa na Nay, anasema kuwa amekuwa akipokea ujumbe wa vitisho mara kwa mara kutoka kwa Msanii huyo pia amekuwa akiwatumia watu tofauti tofauti ili wamteke, na kuthibitisha kwa hilo ameshapokea simu za vitisho kutoka kwa watu tofauti huku akisema walikuwa na lengo la kumteka.

Hapo mwanzo walikuwa wakiishi pamoja huku akiwa kama msaidizi wa msanii huyo katika mambo yake ya Muziki na hata huduma za nyumbani kwa maana walikuwa wanaishi nyumba moja. Mpaka anafukuzwa na Nay tayari alishafikisha miaka mitano wakiwa pamoja huku akiwa amepoteza muda wake mwingi bila mafanikio yoyote. Lakini licha ya kufukuzwa na kuondoka anasema aliendelea kufatiliwa na kupigiwa simu mara kwa mara na Nay akimuuliza maswali ambayo kwa msingi wake hayana hata maana, Moja ya swali ambalo Nay alimuuliza Suddy kama ana namba ya Mpenzi wake Siwema lakini alimjibu kuwa hana bali ana ya Dada yake Siwema ambae anaitwa Mage ndipo utata ukaanzia hapo na kumwambia afute hiyo namba na asiwasiliane na watu hao wawili, kwa mujibu wa Suddy alikubali kufanya hivyo ili kuepusha mzozo.


Suddy alisema hivi "Iko siku tukiwa na wasanii flan ivi tunakula chakula cha usiku kijitonyama nikiwa na (Climax Bibo), (Shebby Love) na (Smocka) alisema mimi na roho mbaya sana naweza muwekea sumu kwenye chakula kiukweli iliniuma nikamuona mtu wajabu sana.. Kwa kuwa mimi mdogo wake niko naye mwaka wa 5 napika miaka yote nafanya kazi zote za ndani leo hii eti nikamuweke sumu kwa kuwa ashakuwa Staa au!! Ndipo nikawa niko na hasira nikimfikria kauli yake ya mimi kumuuwa basi kuna siku akaniita mimi na dogo anaitwa dogo b.. Akatufuza tukaondoka ila dogo kupitia (Cwema aliniomba nimshawishi Dogo arudi kwa Nay ila mimi nika baki nakoma kwa sasa nina maisha yangu nashangaa cmu za vitisho kwa watu tofauti tofauti nakubali kufa ila kama Mungu atapanga, na navijuwa vingi kuhusu yeye nikisema kuongea nitampoteza afanye mziki ale ujana mimi nakula shida aniache..."
Pia akaongezea kwa ujumbe huu " Na Arusha kwa mama alienizaa tambuweni nasakwa Mererani Manyara  nitapigwa bastola  niayo tu!!!"
Mwisho kabisa akatoa baraka zake " Mungu ambariki sana awe na uwezo naenda kuchukuwa arabii yake muda cyo mwing kutoka sasa.!!"

Mkasa huu ndio umempelekea Suddy kutokuonekana maeneo ambayo Nay anajua huwa anapatikana kiurahisi na kuamua kuishi mbali na Jiji la Dar es salaam.

Na hii ndio RB ya Nay - K/RB11782014
Tarehe 25/04/2014

Mpaka dakika ya mwisho habari hii ikipanda kwenye Website.Blog yetu hatujafanikiwa kumpata Nay na kusikia kutoka kwake.

Tuesday, April 22, 2014

duh! kweli Wema ni kiboko. SOMA HAPA

 Stori: Mwandishi Wetu

WEMA Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ ameonesha ni kiboko katika sekta ya urembo baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano bab’ kubwa la kumsaka staa wa kike Bongo mwenye mvuto ‘Ijumaa Sexiest Girl 2013-14’.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’akikabidhiwa tuzo ya ‘Ijumaa Sexiest Girl 2013-14’ na msanii Nikki wa Pili.
Fainali za shindano hilo zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo Wema alikuwa akichuana na warembo wengine, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Nelly Kamwel ‘Dokyumetari’ kwanza

Kabla ya kumtangaza mshindi, maelfu ya watu waliokuwa wamefurika ndani ya ukumbi huo, walipata fursa ya kupata maelezo ya kila mshiriki aliyeingia ‘top 5’ sambamba na picha zao kali za mnato kupitia screen kubwa, hali iliyoamsha shauku ya kutaka kumjua mshindi. hariri aelezea mchakato.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akisalimiana na mashabiki wake.
Baada ya mashabiki kuangalia ‘dokyumentari’ hiyo, Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambalo ndilo lililokuwa likiendesha shindano hilo, Amran Kaima alitoa maelezo kuanzia mwanzo wa shindano na njia zilizotumika kupiga kura hadi kumpata mshindi.
“Shindano lilianza tangu mwezi wa tano, mwaka jana, wasomaji wa Gazeti la Ijumaa walipiga kura kupitia namba ya simu ya gazeti, Mtandao wa www. globalpublishers.info, mitandao ya kijamii na barua pepe.
...Akiwapungia mashabiki mkono baada ya kutangazwa mshindi.
“Mchuano ulikuwa mkali na hata warembo walioingia tano bora ilikuwa vigumu kutabiri mshindi kwani wote ni wakali,” alisema Kaima.Nikki wa Pili atangaza mshindi

Baada ya maelezo ya mhariri, msanii kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ aliyepewa dhamana ya kumtangaza mshindi aliitwa stejini ili kumaliza mchezo.
Wema akiwa na tuzo yake.
Bila kupoteza muda, Nikki alifungua bahasha iliyokuwa na jina la mshindi na Wema alionekana kung’ara hivyo kuibua shamrashamra kuashiria kuwa, mrembo huyo mwenye figa bomba na sura ya kuvutia alistahili kuvaa viatu vya mshindi wa mwaka 2012/13, Jacqueline Wolper.
Mbali na tuzo aliyopewa Wema, pia aliahidiwa shilingi milioni moja ambazo angepewa baada ya shindano hilo.
Baada ya Wema kutangazwa mshindi, burudani ya kufa mtu ilianza kuporomoshwa kutoka kwa Kundi la Wanaume Family na Weusi ambao walinogesha fainali hizo. Habari zaidi kuhusu shoo hiyo, nenda ukurasa wa 8.

Friday, April 4, 2014

ANGALIA PICHA ZA WEMA ALIVYOFANYA VURUGU OFISI ZA GLOBAL PUBLISHER


HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.


Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU

Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.

 Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
 Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.

Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!

 Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
 Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
 MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”

"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA

Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”

 Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
 “Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”

"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:

“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA

Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.

Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA

Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU

Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!

Wema akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).

 Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
 Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.

Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO

Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.

'Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mta
a.

Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!

APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.

Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando (kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA

Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.

WEMA: CHIZI in action......

 Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.