Msanii Dizzo toka Kwa Iddi Arusha anakuja na " Nyoosha Mkono" sikiliza HAPA endelea kusupport muziki wa Tanzania, powered by www.vmgafrica.com
Pages - Menu
▼
Wednesday, July 31, 2013
SERIKALI YAFANYA UPYA UTAFITI KUHUSU MAFUTA YA UBUYU
![]() Moja ya aina za bidhaa za mafuta ya ubuyu. |
Utata wa
kauli kuhusu usalama wa mafuta ya ubuyu, umesababisha Serikali
kuyafanyia utafiti na hivi karibuni itatoa tamko la kumaliza gumzo hilo.
Akizungumza na mwandishi jana kuhusu utata huo, Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, alisema Serikali
iko katika hatua za mwisho za utafiti huo, na muda si mrefu itatoa
msimamo ili kuondolea wananchi utata.
“Tumeona kila mtu anazungumzia usalama wa mafuta ya ubuyu, lakini
siku chache zijazo tutawaita na kutoa msimamo wa Serikali ili
kuwaondolea wananchi utata uliopo wa kila mtu kusema lake,” alisema Dk
Mmbando.
Utata kuhusu usalama wa mafuta ya ubuyu, ulianza mwezi uliopita baada
ya Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA), kueleza kuwa mafuta hayo si
salama kunywewa, kwani yana tindikali inayosababisha saratani.
Kauli ya TFDA, iliungwa mkono na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
iliyoweka wazi kuwa haitambui mbegu za ubuyu kuwa zinatoa mafuta ya
tiba, isipokuwa inatambua tiba inayotokana na mti huo ni majani, magome
na unga.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Mbadala wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk Paulo Mhame, alisema Serikali haitambui mafuta ya
ubuyu kama tiba.
Hata hivyo, mwanzoni mwa wiki hii, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, ilitangaza kuwa mafuta hayo ni salama yakitumiwa vizuri.
Daktari Bingwa wa Udhibiti wa Saratani wa taasisi hiyo, Dk Crispin
Kahesa, alinukuliwa akisema hadi sasa hakuna utafiti wowote wa
kitaalamu, uliopata kufanywa na kuonesha kuwa mafuta hayo ni chanzo cha
saratani ya ini.
“Mafuta ya ubuyu si dawa bali yanazuia maradhi sugu yasiyoambukiza,
ikiwamo saratani kwa sababu kitaalamu yana ‘anti oxidant’ (uchachu)
ambayo pia hupatikana kwenye baadhi ya matunda kama maembe, machungwa na
mananasi.
“Tofauti iliyopo, ni kwamba mafuta hayo yana anti oxidant nyingi
tofauti na iliyomo kwenye matunda. Anti oxidant husaidia kukinga maradhi
ambayo mengi si ya kuambukiza - maradhi sugu kama vile saratani,
kisukari na shinikizo la damu,” alikaririwa Dk Kahesa.
Kazi nyingine ya anti oxidant mwilini ilitajwa kuwa ni kuondoa sumu na kusaidia kutengeneza chembechembe hai mwilini.
“Narudia, mafuta ya ubuyu hayana madhara yakitumika vizuri, bali
madhara ambayo watu wanayasema, yanatokana na jinsi wanavyoyatumia,
kwani wajasiriamali wanaoyatoa hawajui ni mgonjwa gani anapaswa
kuyatumia na kwa wakati gani,” alikaririwa Dk Kahesa.
Kutokana na tamko hilo, wiki hii pia Naibu Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii, Dk Seif Rashid, jana alitangaza kuwa mafuta hayo si salama na
kusisitiza kuwa huo ndio msimamo wa Serikali, hivyo wananchi waamue
kuyatumia au kutoyatumia.
Dk Rashid alitoa kauli hiyo kujibu maswali ya waandishi wa habari
baada ya kufungua semina ya siku mbili, iliyoandaliwa na TFDA na
Shirika la Afya Duniani (WHO).
“Tayari chombo cha Serikali ambacho kina mamlaka juu ya hili
kimeshatoa tamko, hivyo ni hiari ya wananchi kuamua kuyatumia au kuacha.
“Kwa sababu ni sawa na sigara, tumesema kabisa sigara inasababisha
saratani na matatizo mengine, tukaweka na onyo kwenye kasha la sigara,
hivyo ni hiari kutumia au kutotumia,” alisema.
Kesi ya Wema Sepetu yaahirishwa mpaka tarehe 20

Kesi ya jinai inayomkabili muigizaji Wema Sepetu, ya tuhuma za kumpiga
vibao vitano meneja wa hoteli ya Mediterano , pamoja na kuharibu mali za
hoteli hiyo, imeahirishwa leo hii pia mpaka tarehe 20 mwezi wa nane.
sakata hilo lilitokea siku ya tarehe 4 mwezi wa 4, kesi yake ya kwanza
ilisomwa siku ya tarehe 17, na kuahirishwa mpaka leo hii, na baada ya
kufika mahakamani leo hii na Wema kukataa mashtaka hayo, kesi
imeahirishwa tena mpaka tarehe 20 mwezi wa 8.
"Siku ya kwanza ya keshi hiyo wanaume walikuwa wengi, lakini leo hii
imekuwa tofauti, wasichana walikuwa wengi yaani marafiki zake
wakiongozwa na Kajala, walifika majira ya saa mbili na robo na waliitwa
sehem maalum (chemba) kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo, na keshi hiyo
ilisomwa ila ilihairishwa mpaka tarehe 20/08/2013" amesema Mwahija
(mwandishi wa habari wa kujitegemea).
Irene Uwoya kuja na TV show ya tofauti kabisa, unajua inahusu nini?.
Msanii bongomovie Irene Uwoya anakuja kwenye TV yako kwa njia
nyingine tofauti na ya kiubunifu zaidi. Duniani kuna mastaa kadhaa ambao
wanafanya reality show zao, lakini Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa
Instagram ametoa news kwamba anaanzisha show yake binafsi kupitia kituo
cha Clouds TV ambayo ni tofauti kabisa na show za mastaa wengine. Undani
kuhusu show hiyo ni kwamba kila kitu humo ndani kitahusu mambo ya
nyumba. Irene na crew yake watakuwa na kazi ya kutembelea nyumba zenye
hali mbaya na kuzifanyia ukarabati ili kuboresha hali ya mazingira ya
kuishi ya muhusika mwenye nyumba au chumba. So, show yake itakuwa
inaonyesha mwanzo nyumba ikiwa kwenye hali mbaya hadi atakapo ikamilisha
na huo ukarabati. Hii picha inamuonyesha akiwa setting ku-shoot sehemu
ya show hiyo.
Wasanii wajitolea kwenda kujenga kabuli la Bibi Kidude
Bibi Kidude mkongwe wa muziki Tanzania ambaye alifariki huko Zanzibar
na kuzikwa visiwani hapo, kifo chake kilipata maombolezo ya watu
tofauti tofauti pamoja na wasanii. Hivi sasa wasanii wa kizazi kipya
wamejiunga pamoja kwenda kusimamia swala zima la kujenga kabuli la
mkongwe huyu katika historia ya muziki Tanzania. Msafara wa wasanii hadi
sasa unategemewa kwenda Zanzibar siku ya Jumamosi hii kukamilisha mpango huu.
Bibi Kidude alipewa heshima ya pekee kwa kupata kumbukumbu ya heshima kwenye tamasha la Ziff ambalo lilifanyika Zanzibar kwa wasanii kuimba nyimbo zake kwenye stage kubwa ya ZIFF. Msanii Linah ambaye alirudia wimbo wa Yalaiti akiwa na Mwana F.A aliperform wimbo huu kwenye kumbukumbu hiyo.
Bibi Kidude alipewa heshima ya pekee kwa kupata kumbukumbu ya heshima kwenye tamasha la Ziff ambalo lilifanyika Zanzibar kwa wasanii kuimba nyimbo zake kwenye stage kubwa ya ZIFF. Msanii Linah ambaye alirudia wimbo wa Yalaiti akiwa na Mwana F.A aliperform wimbo huu kwenye kumbukumbu hiyo.
Jiandae kwa kitu hiki kipya kutoka kwa Ney wa Mitego
Ney wa Mitego ambaye bado collabo yake na Diamond “Muziki gani” inafanya vizuri, ameamua kukujuza kuhusu kitu kingine kutoka kwakwe. Ney ametoa hiyo poster hapo chini ambayo inaweza kuwa ndiyo official art cover ya ngoma hii inayokuja. Bado hajaweka wazi ni lini atatoa hii ngoma, endelea ku-click to millardayo.com kwa ajili ya updates za ngoma hii.
List ya mastaa wa bongo ambao wamefanya/walifanya kazi kama mabalozi wa kampuni kubwa.
Tukirudi hapa nyumbani Tanzania kuna makampuni ambayo yamesha amini nguvu na nafasi ya wasanii kwenye kuzitangaza bidhaa zao japokuwa bado wasanii wanaendelea kupeleka kilio chao mbele kama alivyofanya Ommy Dimpoz kwenye Kili Music award wakati anapokea tuzo yake.
Hii hapa ni list ya watu maarufu wa hapa nchini Tanzania ambao waliweza kupewa na wengine wanaendelea hadi sasa hivi kufanya kazi na brand ili kufikia malengo ya kibiashara na kijamii ya brand hizo.
MWANA F.A NA SAMSUNG
Sio muda mrefu sana umepita tangu Samsung Tanzania kumtangaza Mwana F.A kama balozi wa bidhaa za Samsung hasa simu. Hii ilikuja mara baada ya kampuni hii ya vifaa vya electronic kuzindua simu ya Samsung Galaxy S4. Mwana F.A ni msanii ambaye amejijengea personality nzuri na uwezo wake mkubwa kwenye sanaa kwa miaka mingi, vinaweza kuwa ni baadhi ya vitu vilivyowavutia Samsung kumpa hili dili bwana Hamisi Mwinjuma.
B12 NA REDBULL
Hamisi mwingine huyu baada ya Hamisi Mwinjuma, kati ya watu maarufu wa kwanza sana kipindi hicho kupewa kazi ya kuwa balozi wa kinywaji cha Redbull. B12 kutokana na kuwa ndiyo mtangazaji mkuu wa kipindi cha XXL ambacho ni moja ya vipindi vinavyosilizwa sana na vijana. Hivyo kumfanya moja kati ya vijana wanaosikilizwa sana na vijana wenzao hasa kwenye upande wa burudani. B12 au Hamisi Mandi alikuwa balozi wa RedBull kwa muda kadhaa ambapo ilifika wakati hadi alipata a.k.a nyingine ya B-Balozi. Kama ulikuwa hujui, B12 weekend hii ametajwa kwenye list ya moja ya watu maarufu kwenye kazi ya radio ndani ya Africa ambapo alishika namba tisa. Hii ni sababu nyingine ya kupata ubalozi wa brand tena.
MAREHEMU KANUMBA NA STARTIMES
R.I.P The great pioneer kama alivyokuwa anajiita, lakini jina lake lingine alilokuwaga nalo ni balozi wa Star Times. Kampuni hii ya ving’amuzi wakati inaingia kwenye soko la Tanzania ilitumia pia mbinu ya kimasoko kwa kumtumia mmoja kati ya watu maarufu kwenye TV. Baada ya kufanya tamthilia kwa muda mrefu na baadae kuhamia kwenye movie na kufanya vizuri zaidi, Kanumba alijipatia hili dili na kulifanyia kazi vizuri.Steven Kanumba alizunguka mikoa mbalimbali kwenye ziara za kuhamasisha bidhaa ya Startimes. Kazi hii haikuishia hapo, Kanumba alipiga picha za kutosha kutengeneza mabango ya matangazo kwa ajili ya promotion ya Startimes.
MZEE MAJUTO NA SHARO – AZAM
Marehemu Hussein Mkietti maarufu kama Sharo millionea akiwa pamoja na Mzee Majuto walipata dili tofauti tofauti kutoka kwenye makampuni makubwa. Moja wapo ni kufanya tu matangazo ya Airtel lakini pia walipata nafasi ya kuwa mabalozi wa Azam. Kwa wale waliowahi kwenda sabasaba mwaka 2012 kwenye banda la Azam, basi waliwaona Mzee Majuto na Sharo millionea wakiwa nje ya banda hilo katika kazi ya Azam. Kutoka kwenye moja ya vyanzo vya uhakika Mzee Majuto alisema ,”Mkataba wetu na Azam ni mzuri na tunamshukuru mungu kwa hili. Mkataba wetu unasema kwamba tutahusika kwenye kutengeneza matangazo ya bidhaa za Azam,promotion za wazi pamoja na kupewa udhamini kama tukifanya shughuli yetu ya pamoja na mwanangu Sharo”. Hii ilikuwa kabla ya Sharomillionea kufariki, lakini hivi sasa Mzee Majuto anaendelea na dili hili kama kawaida.
AMBWENE YESAYA (A.Y) NA AIRTEL
Boss wa Unity Entertainment, mkali toka kipindi cha ngoma yake kali “Raha tu” hadi “Bed and breakfast” hadi siku hizi na “Party Zone” ali-sign mkataba kufanya kazi na Airtel Tanzania. Kama Mzee Majuto na Sharo walivyofanya matangazo ya Airtel na baadaye kupata dili lingine na Azam. A.Y aliwahi kufanya tangazo la T.V, Radio na printing aki-promote moja bidhaa za Vodacom Tanzania. Lakini baadaye baadaye sana akapata dili la kufanya kazi na Airtel.
ADAM MCHOMVU NA COCACOLA
Mtangazaji wa XXL na Bongoflava vyote vya Clouds FM, aliwahi kuwa balozi wa Cocacola kwa muda kadhaa. Adam Mchomvu alihusika katika vitu kadhaa vya Cocacola kama kuwapa watu mbalimbali zawadi kutoka Coca Cola.
DIAMOND PLATINUMZ NA COCACOLA
Huyu jamaa anajiita Coca Boy, kama unataka kujionea hilo nenda kwenye account ya Instagram ya huyu jamaa ndiyo utaona jinsi gani anautendea haki ubalozi wake. Diamond akiwa kwenye interview na XXL alisema kwamba, “Mimi nilipata nafasi ya kufanya tangazo la mashindano ya Cocacola, lakini nilikuwa na malengo na nikaamua kuwapa zaidi. Nilijifanya kama balozi wakati kabla sijawa balozi kamili. Kwa hiyo jamaa wakaona duh huyu jamaa hatujampa hii kazi anafanya hivi. Je tukimpa kazi itakuwaje?. Hapo ndiyo nikapata hii kazi”.
Diamond ni msanii ambaye anatajwa kupata mafanikio sana hapa Tanzania, kwa upande huu wa kuwa balozi wa Cocacola anafanya vizuri sana kitu ambacho kinaweza kuyavutia hata makampuni mengine.
Mwana F.A akikabidhiwa Samsung4