Saturday, August 25, 2012
AMSHA AMSHA YA SERENGETI FIESTA 2012 NDANI YA TANGA YAWAFUMBUA MACHO WAKAZI WA HUKU
10:23 AM
No comments
YALIOJIRI KWENYE SHANGWE ZA FIESTA MOSHI
9:04 AM
No comments
CMB Prezzo doin his thing kwa stage ya Fista Moshi
Nidanganye danganye danganye tuuuuu
Bongo movies ndani ya nyumba
Baadhi yao tu
Mungu niongezeeeee amen, amen amen
Ray na Steve Nyerere
Queens wa Movies, Wema na Aunt Ezekiel
Recho
Dj zero
Thursday, August 23, 2012
Hukumu Igunga Yaivuruga CCM
11:18 AM
No comments
WAKATI
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitangaza kusudio lake la kukata rufaa
dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyotengua ubunge wa
aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalali Kafumu, wadau mbalimbali
wameipongeza hukumu hiyo wakiita ni darasa tosha kwa demokrasia ya mfumo
wa vyama vingi.
Miongoni
mwa waliosifu hukumu hiyo ni pamoja na Spika mstaafu, ambaye pia ni
Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema kuwa
maamuzi hayo inafaa yaheshimiwe.
Akizungumza
jana mjini Tabora, Sitta alisema kuwa mahakama ina mamlaka yake
kisheria, hivyo wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani
imefanya kazi yake inavyotakiwa.
“Kama
kuna mtu anaona hukumu hiyo haikutenda haki, anaweza kwenda mahakamani
kukata rufaa, lakini mimi nashauri ni vema tujipange upya tuingie
ulingoni.
“Hapa
mimi sina maoni juu ya jambo hilo, bali cha msingi ni vema tukakaa na
kutafakari yaliyotokea huko Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa
sawa, na kama tuingie ulingoni, yote ni sawa,” alisisitiza Sitta.
Katika
hukumu yake juzi, Jaji Mary Nsimbo Shangali, aliyekuwa akisikiliza kesi
hiyo, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA, Joseph
Kashindye, alisema kuwa alipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na
pande zote mbili, lakini yakaongezwa madai mengine mawili na kufikia 17.
Mbali
na Dk. Kafumu, washitakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali
pamoja na Msimamizi wa uchaguzi jimboni humo, Protace Magayane na kwamba
mahakama hiyo ilithibitisha madai saba ya kutengua matokeo hayo.
Hata
hivyo, wakati Sitta akiwa na mtazamo huo, CCM kupitia kwa Katibu wake
wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilieleza
kutoridhishwa na hukumu hiyo, hivyo kuamua kukata rufaa.
Pamoja
na CCM kuchukua hatua hiyo, wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa na
wanaharakati waliliambia Tanzania Daima kuwa, hukumu hiyo ni darasa
tosha la demokrasia linaloonesha jinsi sheria za uchaguzi zinavyovunjwa.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashir Ali, alisema hukumu hizo
za uchaguzi ikiwamo hiyo ya Igunga, zina maana sana kwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa, wanasiasa na wananchi.
“Tatizo
letu huwa hatusomi hukumu hizi kwa undani, kwani tungekwishajua kuwa ni
darasa tosha la demokrasia. Suala la takrima lilikuwa halieleweki kama
ni rushwa, ushindani wetu wa kisiasa si wa kuvumiliana, una matumizi
makubwa ya fedha, mali za serikali na madaraka kwenye kampeni,” alisema.
Ali
alifafanua kuwa hukumu hiyo imetoa mwanga kuwa, kama hakuna chombo huru
cha kusimamia sheria zinazokiukwa ni sawa na bure, akitolea mfano Tume
ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa licha
ya kuwapo wakati wa mchakato huo, vilishindwa kuchukua hatua.
“Kuna
mjadala kuhusu uwepo wa sheria ya Tume ya Uchaguzi, maana tangu kuanza
kwa mfumo wa vyama vingi hakuna sheria ya Tume ya Uchaguzi, badala yake
chombo hiki kinatambuliwa na sheria za uchaguzi, jambo linalotoa mwanya
kwa mapungufu yanayojitokeza sasa,” alisema.
Kuhusu
uwajibikaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi
huo mdogo, Ali alisema kuwa mpaka sasa umuhimu wa ofisi hiyo hauonekani
maana kama hoja ni kusajili vyama, kazi hiyo inaweza kufanywa hata
mahakamani.
Alibainisha
kuwa, kwa sasa ofisi ya msajili na Tume ya Uchaguzi ni kama idara tu
ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo wananchi wanapaswa kutumia hukumu
ya Igunga kama tathmini wakati huu wa mchakato wa katiba mpya
kusahihisha makosa ya kuvifanya vyombo hivyo huru.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Mtatiro Julius,
alisema hukumu hiyo itawafungua wananchi kuona umuhimu wa kubadilisha
mfumo wa uchaguzi ili kuepusha taifa kuingia gharama zisizokuwa za
lazima pale kiongozi anapokufa ama kuenguliwa.
“Hii
naiona kama hatufikirii sawa sawa, maana matumizi ya mabilioni ya fedha
kwenye uchaguzi yalikuwa kwa vyama vyote kule Igunga hasa CCM, CHADEMA
na CUF. Lakini hili linaweza kuepukwa mana kama upuuzi unafanywa na watu
wawili, hatuna sababu ya kulisababishia taifa hasara,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mtatiro, inapotokea hali kama hiyo ya mbunge kuenguliwa au
kupoteza maisha, mshindi wa pili kutoka chama kingine ndiye achukue
nafasi badala ya kurudia uchaguzi.
“Igunga
tuliona Dk. Kafumu walipishana kidogo na Kashindye wa CHADEMA, hivyo
kwa vile huyu alikiuka taratibu, basi mshindi wa pili apewe nafasi
kuliko kurudia uchaguzi, kwani kufanya hivyo kunaweza kukipa chama
kilichoenguliwa ushindi tena wa mtu asiyefaa,” alisema Mtatiro.
Mwanasiasa
huyo pia hakusita kuinyoshea kidole Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, akisema kuwa, John Tendwa (msajili) ameonesha wazi ni wakala wa
CCM anayefanya mbinu za kukisaidia chama hicho kishinde badala ya
kusimamia kanuni na sheria.
Mtatiro
aliweka bayana kuwa makosa yaliyoainishwa kwenye hukumu iliyomtia
hatiani Dk. Kafumu na kumnyang’anya ubunge wake, yalilalamikiwa mapema
na wapinzani kwa Msajili wa Vyama wakati wa kampeni, lakini hakuchukua
hatua yoyote.
“Msajili
wa vyama hana meno, na huyu amekuwa na kashfa ya kusajili hata vyama
visivyo na sifa ilimradi tu aweze kuvidhoofisha vyama makini vya
upinzani. Hata kwenye uchaguzi ameonesha wazi anataka CCM ishinde,”
alisema.
Mtatiro
aliongeza kuwa, umefika wakati nafasi hizo nyeti za vyombo kama Tume ya
Uchaguzi, Msajili na nyinginezo zitangazwe ili watu wenye taaluma zao
washindanishwe na kuchujwa na chombo maalumu badala ya kuteuliwa na
rais.
Naye
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea
Nkya, alizungumzia hukumu hiyo ya Igunga akisema imetoa tafsiri mpya kwa
wananchi kuelewa demokrasia ya vyama vingi na namna ya kumpata
mwakilishi makini bila rushwa na vitisho.
“Hili
litakuwa fundisho kwa wanasiasa wanaochezea fedha nyingi kwenye
uchaguzi kununua watu, maana watatambua sasa kuwa kufanya hivyo
kutawapotezea viti vyao. Lakini na wagombea wanapaswa kuwa makini na
wapiga debe na vyama vyao, kwani wanaweza kuingizwa mtegoni kama
alivyoponzwa Dk. Kafumu,” alisema.
Akisoma
hoja zilizothibitishwa na mahakama hiyo juzi, Jaji Shangali alisema ni
pamoja na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutumia nafasi yake ya
uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja
ya kero kubwa kwa wananchi wa Igunga.Waziri Magufuli akiwa katika
uchaguzi mdogo huo katika moja ya kampeni, alitumia nafasi ya uwaziri
kuwatisha wapiga kura wa jimbo hilo kuwa kama hawatamchagua mgombea wa
CCM watawekwa ndani.
Jaji
Shangali pia alisema kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, alipita
mitaani akitangazia wananchi kuwa mgombea wa CHADEMA amejitoa.
Katika
hoja nyingine ni kwamba Imamu Swalekh Mohamed wa Mskiti wa Ijumaa
Igunga, aliwatangazia waumini wa Kiislamu kuwa wasiichague CHADEMA kwa
kuwa baadhi ya viongozi wake walimdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga,
Fatuma Kimario.
Nayo
matamshi ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kudai kuwa CHADEMA
imeleta makomandoo kuuvuruga uchaguzi huo ni mojawapo ya hoja ambazo
mahakama hiyo ilizikubali.
Katika
hoja kuu ya mahindi, Jaji Shangali alihoji kama wananchi wa Igunga
walikuwa na njaa sana. Na kwamba, kama jibu ni ndiyo, ni kwanini
uchaguzi usifanyike wakati hawana njaa.
Chanzo: http://wotepamo
Wednesday, August 22, 2012
AMSHA AMSHA YA TAMASHA LA FIESTA 2012 YAANZA KWA KISHINDO NDANI YA TANGA
5:21 AM
No comments
Mkuu
wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga (wa kwanza kulia) akitoa
maelekezo kwa watangazaji wa redio hiyo Lovenes Love na Adam Mchomvu
wakati walikuwa wakiongea na wasikilizaji wa redio ndani ya Tanga katika
amsha amsha ya Tamsaha la Fiesta 2012 linalotegemea kufanyika tarehe
26.8.2012 Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hilo litakalopambwa na msanii
maarufu wa kimataifa kutoka nchini Kenya Prezzoo.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu akionyesha t-shirt ambazo zimetoka kwa ajili ya kusherekea tamasha hilo la Fiesta 2012.
Mwanadada Loveness Love akisababisha ndani ya amsha amsha ya tamasha la Fiesta linalofanyika wikend hii ndani ya Tanga.
Mkuu
wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akiendeleza harakati za
kukamata matukio ndani ya kitaa cha Chumbageni, pale Clouds Fm
ilipotembelea vijana hao wa maskani na kupata mawili mawili matatu
kuhusiana na tamasha hilo.
Mazungumzo ya haopa na pale yakiendelea.
...vijana wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga, pembeni yake ni Adamu Mchomvu.
Vijana walipata mzuka wa kufunguka na kuonyesha vipaji vyao.
...Mzuka ulipata na kuanza kuchana.
Mmoja
ya maproducer wakali wa msanii Moraka akiongea machache mara baada ya
kukutwa akiwa amekaa na vijana wenzake ndani ya maskani ya Chumbagenino.
Moja ya staili niliyokutana nayo.
Picha ya Kumbu kumbu kwa vijana wa Chumbagenino.
Mara
baada ya Clouds Fm kutoka Kitaa cha Chumbageni maskani ya Chumbagenino
Clouds Fm ilihamia kitaa kingine ambapo alijitokeza kijana mmoja na
kuomba awe mtangazaji hapa alikuwa alimfanyia mahojiano Mwanadada
Loveness Love.
Aha... Sudi Brown (kushoto) akiwa na Mchomvu.
Ukumbusho Muhiumu sana.
Aha...mambo
yalinogeshwa na kuwekwa sawa. Unaweza kufuatilia kinachoendelea katika
amsha amsha za tamsaha la Fiesta 2012 kupitia yushathehood.blogspot.com
BI KIDUDE TAABAN KITANDANI
3:21 AM
No comments
Taarifa toka Zanzibar zinadai kuwa Legendy wetu 'Bi.Kidude' anaumwa sana na hana msaada wowote.
Inadaiwa kuwa mjukuu wake alizungumza na Television ya Zanzibar na kulalamika kuwa Bibi yake hana msaada na hivyo anamuuguza kwa shida. Taarifa zaidi zinasema Bibi anaumwa tangu wiki iliyopita, hamna mdau hata mmoja wa muziki aliyejitokeza kumsaidia hivyo anatoa wito kwa wadau wenye uwezo wajitokeze kumsaidia Bibi ili apate matibabu na kurejea kwenye hali ya kawaida.
MUNGU AWE NAWE OUR LEGENDARY
Wasanii wa Arusha wamwandikia barua marehemu Vivian
2:46 AM
No comments
Mpendwa Vivi,
Ni miaka saba sasa tangu uondoke na tunakukumbuka sana
michano yako na mambo mengine mengi....(jalini ubinadamu msifanye mavitu kama
sanamu.....). Natumai umeonana na Faza Nelly,DOG Nacko.Papaa,Mlost na Pacha
Izzy na wengine wengi waliokuja huko.
Dhumuni la barua hii ni kukusalimu na kukujulisha
yanayoendelea Arusha. Mengi yametokea ila ya Muhimu kukufahamisha kuhusu
harakati za Muziki hapa Arusha.
Imagine eti siku hizi Metropole,Ricks,Mawingu na Crystal
club hazipo tena.Machizi wengi wamehamia Dar es salaam(just like you...) ila
wao wamebadilisha hadi majina wanakuja Arusha kufanya show na kusepaz. Machalii
wapya kibao kwenye Game na wanakalisha usipime wengine wako mbele na wanafanya
harakati zilezile Kzz wa X plastaz hajarudi bado tangu aende na anatoa Mixtape
moja kali sana hivi karibuni,Chindo pia anawakilisha akiwa huko si unajua tena
Jamaa alivyo mbishi.
Jcb na Spark bado ni hardcore(...wana makid
asee).maprodyuza wengi wapya na Studio nyingi.WATENGWA kuna Daz Naledge,DX
amekuja na Noizmeka,hata Ngalimi siku izi kuna Studio asee KZ kaja na
KAZAWAZA.Grandmaster siku izi wanapiga mpaka VIDEO bana.zipo mingi siwez hata
kuzitaja zote.
Harakati zote zile za rap sasa hivi zimeamia Kijenge ya
Juu(S.U.A Free-Stage).
Watu kibao wanakutana na kupiga freestyle,michano na
magrafiit kibao.Si unakumbuka vile ulikua ukikasirika kuona hakuna mademu
kwenye HIPHOP concert na ukawa unaamua kuonyesha uwezo wako dah! ulikua
unakalisha asee(.....sa nani wakuongoza safari wote tunaujua
usukani.......siwaelewi! )
Juzi si kuna madem wakaibuka SUA bana asee tulikukumbuka
sana laiti ungekuwepo ungefarijika kinyama.
Kuna redio stesheni mingi niaje! karibu kila mtaa na
maclub za kutosha huko town usiku kama tu mchana. ... kuna masista Dread wengi
peace kama wewe.... inapendeza.
Arif mambo kibao yamebadilika... kutoka TAPE na disc man
siku izi kuna mavitu yanaitwa I-pod,I phone na ma-I pad kitu touch screen
maamaaa si unajua Swagga tena...(sorry i know you now know about Apples kama sio
matunda tena nikikuambia mambo ya Blackberry si ndo utadata
kabisa...hahahahaha!!)
I will tell you about it next time sahivi naenda misele
so kama vipi mpe hi Complex(Mwambie alivyosepa tu BTOWN CLAN wakaNYAMAZA ooh
SH**T MIKOSI WAMENYAMAZA.....),James Dandu,Drob,Steve2k,produza Roy na wengine
mlioko nao huko.
Jumapili tarehe 26 SUA itakua ni spesho kwako na Complex
wa2 watapiga mistari yenu..oooyyyy! .Nitakujulisha zaidi next time.
Wako Wapendwa
Katika HIP HOP
###teamSUA###
Monday, August 20, 2012
HALI KAMA HII TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA ITAISHA LINI?
10:39 AM
No comments

AFRIKA
ni bara linaloongoza kwa kuwa na sura za umaskini hasa ule unaowafanya
binadamu kukosa kile alichokiita Abraham Maslow haki za msingi yaani
chakula, malazi na mavazi. Nimepita hapa na kukuta taarifa na picha hii ambayo kwangu haijanifurahisha.
Haki chakula ni jambo ambalo nimekuwa nikilizungumza sana na ninatamai siku moja kila mwananchi kwa kuanza na Tanzania apate haki hii ya msingi. Kama tukikubali kurejesha sera za vitendo katika kilimo bila shaka tutamudu kuwezesha watu wetu kupata chakula wakati wote.
tunafahamu kuwa wakishapata chakula kiasi cha kushiba ni jukumu la pili kusisitiza juu ya chakula bora. Wimbo wa chakula bora hauwezi sasa kuimbwa ana serikali yetu kwa kuwa hata haki ya chakula tu kwa wananchi bado ni kitendawili. Kuna waziri wa Kilimo nchini anaitwa Wassira, ni maarufu sana kwa maneno matamu lakini utendaji wa wizara hiyo katika kutibu tatizo la upatikanaji wa chakula bado ni ndoto takayohukua siku nyingi kupata jibu. Tunasubiri sijui aje nani ili kuhamaisha kilimo cha chakula katika Afrika? Inakera na kuumiza sana!
Haki chakula ni jambo ambalo nimekuwa nikilizungumza sana na ninatamai siku moja kila mwananchi kwa kuanza na Tanzania apate haki hii ya msingi. Kama tukikubali kurejesha sera za vitendo katika kilimo bila shaka tutamudu kuwezesha watu wetu kupata chakula wakati wote.
tunafahamu kuwa wakishapata chakula kiasi cha kushiba ni jukumu la pili kusisitiza juu ya chakula bora. Wimbo wa chakula bora hauwezi sasa kuimbwa ana serikali yetu kwa kuwa hata haki ya chakula tu kwa wananchi bado ni kitendawili. Kuna waziri wa Kilimo nchini anaitwa Wassira, ni maarufu sana kwa maneno matamu lakini utendaji wa wizara hiyo katika kutibu tatizo la upatikanaji wa chakula bado ni ndoto takayohukua siku nyingi kupata jibu. Tunasubiri sijui aje nani ili kuhamaisha kilimo cha chakula katika Afrika? Inakera na kuumiza sana!
MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA BALOZI WA KENYA NCHINI OFISINI KWAKE,ATEMBELEA MAJERUHI ZAIDI YA 30 WALIONUSURIKA KWENYE AJALI YA FUSO
9:53 AM
No comments

Mmoja
wa majeruhi wa ajali ya Fuso iliyotokea Wilayani Nkansi jana Mkoani
Rukwa akiwa amelazwa katika Hospitali kuu ya Mkoa wa huo huku akiendelea
kupatiwa matibabu. Watu saba walifariki papo hapo katika ajali hiyo
iliyohusisha Fuso iliyokuwa imebeba mizigo na abiria ambapo majeruhi
walikuwa 37, Mpaka sasa jumla ya abiria waliofariki ni 10 na wengine
bado wapo hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu na wengine
walisharuhusiwa.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimpa pole mmoja wa majeruhi
walionusurika kwenye ajali hiyo mbaya kati ya ajali zilizowahi kutokea
Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa alisikitishwa na ajali hiyo iliyomfanya
apige marufuku usafiri unaohusisha mizigo na abiria kwa wakati mmoja.

Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Emanuel Mtika akitoa
maelezo ya majeruhi kwa Mkuu wa Mkoa huo alipotembelea kuwaona kufuatia
ajali mbaya iliyotokea jana na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine
zaidi ya 30 kujeruhiwa.

Agnes
ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali hiyo akiwa na watoto
wake wawili wadogo wanaonekana pichani na mumewe ambaye alisharuhusiwa
baada ya kupata nafuu.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Balozi wa Kenya
nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso ofsini kwake leo alipotembelewa
na balozi huyo ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi yenye lengo
la kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kuangalia
fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mikoa ya nyanda za juu kusini.
Balozi huyo anategemea kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo pamoja na
shughuli nyingine ataembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Mkuu huyo wa
Mkoa wa Rukwa amemuhakikishia balozi huyo uwepo wa fursa nyingi za
uwekezaji Mkoani Rukwa ikiwemo Kilimo, Utalii, Uvuvi, Elimu na Biashara.
Alimueleza kuwa kazi kubwa inayoendelea hivi sasa ni utengaji maeneo
maalum ya uwekezaji.

Mazungumzo yakiendelea ofsini kwa Mkuu wa Mkoa.

Balozi
wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso akielezea lengo la ujio wake
Mkoani Rukwa mbele ya Mkuu wa Mkoa huo na viongozi wengine wa Serikali
ya Mkoa mapema leo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo. Aliiomba pia Serikali
ya Tanzania kujenga urafiki na wageni ili kuimarisha mahusiano mazuri
amabayo yamekwishajengeka kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya.
Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimsihi balozi huyo na nchi yake
ya Kenya kusaidiana na Tanzania kudumisha amani iliyopo ili Afrika ya
Mashariki pawe pahala salama pa kuishi na kufanya maendeleo ikiwemo
uwekezaji ambao hauwezi kustawi pasipokuwa na amani.

Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima hapo kabla
akimtambulisha balozi wa Kenya kwa viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa
Ofsini kwake alipoenda kumsalimia kabla ya kuonana na Mkuu wa Mkoa huo.

Kutoka
kulia ni Afisa Mkuu wa Jeshi la Usalama Barabarani Mkoani Rukwa, Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Jakob Maruanda na Katibu Tawala Msaidizi
Miundombinu Francis Kilawe wakiwa kwenye meza ya mazungumzo na Balozi
huyo wa Kenya.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa agizo kwa Kamanda wa
Polisi Mkoa huo Jakob Maruanda mbele ya waandishi wa habari na viongozi
wengine wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed
Chima, agizo ambalo limepiga marufuku usafirishaji wa abiria katika
magari ya mizigo. Alimueleza kuwa yeyote atakayekutwa akisafirisha
abiria kwenye malori ya mizigo achukuliwe hatua kali za kisheria
kudhibiti ajali za namna hiyo kutokea.Picha na Habari zote na Hamza Temba-Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Subscribe to:
Posts (Atom)























