Sunday, December 23, 2012
Saturday, December 22, 2012
Friday, December 21, 2012
SERIKALI YABEBA JUKUMU LA KUMSAIDIA SAJUKI HADI KUPONA
11:41 PM
No comments
Serikali
imechukua jukumu la kumhudumia msanii na muongozaji wa filamu Sadick
Juma Kilowolo ambaye anatarajia kuondoka wiki ijayo kuelekea India kwa
matibabu.
Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi, alisema Sajuki ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, amegundulika kuwa ana tatizo la kufeli kwa figo na kwamba yuko chini ya uangalizi na uchunguzi zaidi.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imejitolea kumsafirisha msanii huyo kwa gharama zake na kusaidia katika gharama za matibabu akiwa nchini India.
“Sajuki anatarajiwa kusafiri wiki ijayo baada ya taratibu zote kukamilika, hivyo sisi kama TAFF tunathibitisha kuwa hali yake bado haijatengemaa kama ilivyojulikana hapo awali,” alisema Makubi.
Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ambapo mwaka jana alianza na uvimbe ulioanzia mikononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sehemu tofauti za tumbo.
Msanii huyo alipelekwa India kwa ajili ya kutibiwa, kisha akarejea nchini baada ya kupata nafuu, ambapo kwa sasa ameugua tena na anahitaji matibabu ya haraka ikiwamo upasuaji.
Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi, alisema Sajuki ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, amegundulika kuwa ana tatizo la kufeli kwa figo na kwamba yuko chini ya uangalizi na uchunguzi zaidi.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imejitolea kumsafirisha msanii huyo kwa gharama zake na kusaidia katika gharama za matibabu akiwa nchini India.
“Sajuki anatarajiwa kusafiri wiki ijayo baada ya taratibu zote kukamilika, hivyo sisi kama TAFF tunathibitisha kuwa hali yake bado haijatengemaa kama ilivyojulikana hapo awali,” alisema Makubi.
Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ambapo mwaka jana alianza na uvimbe ulioanzia mikononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sehemu tofauti za tumbo.
Msanii huyo alipelekwa India kwa ajili ya kutibiwa, kisha akarejea nchini baada ya kupata nafuu, ambapo kwa sasa ameugua tena na anahitaji matibabu ya haraka ikiwamo upasuaji.
MACHINGA WAFUNGA BARABARA MJINI MOSHI HII LEO
9:46 AM
No comments
MACHINGA
wa Mji wa Moshi leo walileta kizaa zaa katika mji wa Moshi baada ya
Wafanya biashara hao wadogo kufunga barabara ya Ghala, wakipinga
kitendo cha Uongozi wa Manispaa ya Moshi, kuvunja Gereji ya Bantu,
wanayoitumia kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa zao.
Akizungumza
na Machinga hao katika juhudi ya kuhakikisha usalama unarejea kama
kawaida, RCO Nga’azi aliwataka viongozi wa Wamachinga kuwatuliza wafuasi
wao, nakuangalia njia nyingine ya kutafuta haki kwa amani.
Alisema
kuna umuhimu wa kila mwananchi kutambua wajibu wa kudumisha amani na
kuwakumbusha umuhimu wa kuhakikisha haki wanayoitafuta haikiuki haki za
binadamu na Raia wengine wa nchi hii.
Akizungumza
na wamachinga hao, muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la tukio,
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi, aliwaahidi wachinga hao
kufanyia kazi tatizo lao na kuwaomba wateue wawaklishi wao wanne ambao
aliandamana nao hadi katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,
Bernadeta Kinabo, kuzungumza Tatizo na kulipatia ufumbuzi.
“Nimesikia
tatizo lenu na kilio chenu ndio maana niko hapa, nataka niwahakikishie
kwamba le oleo mtapata majibu kutoka kwangu, kwa sasa ninachowaomba nim
kila mtu arejee katika shughuli zake za kawaida ili amani ya mji wetu
uendele kuwepo,” alisema Msengi.
Kwa
upande wao, baadhi ya Machinga wanaodaiwa kuvunjiwa na kuharibiwa mali
zao katika tukio hilo lililotokea jana , majira ya saa saba usiku,
Abdallah Abushehe na Mwamedi Ally, walisema kuwa, asubuhi ya leo
waliamka na kufika katika gereji hiyo wanayo itumia kuhifadhia bidhaa
zao na kukuta eneo hilo limevunjwa na baadhi ya mali zao kupotea.
“Mimi ni
fundi viatu, kawaida yetu ni kuhifadhi bidhaa zetu hapa gereji,
wamevunja usiku usiku hata taarifa hawajatupa, hawa wagambo wamezidi
kutuonea sana, kila siku wanatukimbiza wanatunyima raha kweli ya kufanya
kazi, sasa hivi mkokoteniwangu na magunia yangu ya viatu siyaoni, kwa
kweli sisi tumechoshwa na uongozi wa Manispaa,” alisema Ally.
Naye
mmiliki wa Gereji ya Bantu lililovunjwa na kuzaa mzozo huo, Abdillahi
Ally, alikiri kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Moshi,
Bernadetta Kinabo kuhusu eneo hilo kuwepo katika ramani za ujenzi wa
Nyumba za shirika a Nyumba Taifa (NHC).
Alisema
kuwa aliwahi kupata Barua kutoka kwa Meneja wa NHC, iliyosainiwa na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, ikimtaka kuachia sehemu hiyo ndani ya
siku mbili, lakini kutokana na kutoridhika na maamuzi ya hayo alifungua
kesi Mahakamani.
chanzo na>> http://audifacejackson.blogspot.com
chanzo na>> http://audifacejackson.blogspot.com
MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAMPA DHAMANA LULU
9:40 AM
No comments

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana
msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa vya sheria na kuona kesi
yake ya kuua bila kukusudia anauwezo wakupata dhamana
Kwa maana hiyo, Lulu
sasa yuko na familia yake vilevile atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013
akiwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Msanii huyo
ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba -
The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia,
ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa
atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka
kadhaa au kuachiwa huru. Endelea kutembelea theHOODinfotainment itakuleta muendelezo wa stori hii mwanzo hadi mwisho.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam asubuhi ya leo imempa dhamana
msanii Elizabeth Michael baada ya kupitia vifungu kadhaa vya sheria na kuona kesi
yake ya kuua bila kukusudia anauwezo wakupata dhamana
Kwa maana hiyo, Lulu sasa yuko na familia yake vilevile atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru. Endelea kutembelea theHOODinfotainment itakuleta muendelezo wa stori hii mwanzo hadi mwisho.
Kwa maana hiyo, Lulu sasa yuko na familia yake vilevile atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya wa 2013 akiwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru. Endelea kutembelea theHOODinfotainment itakuleta muendelezo wa stori hii mwanzo hadi mwisho.
Thursday, December 20, 2012
11:49 PM
No comments
Lema Arudishiwa Ubunge Na Mahakama Ya Rufaa
Lema,Mbowe na nassari mahakamaniMawakili wakiwa kwenye viti vyao
Hawa ndiyo waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya lema
Mahakamani,lissu,nassari,mwenyekiti mbowe na kilewo wakiteta na mke wa lema
Lema akianza kutoa hotuba fupi baada ya kutoka mahakamani.kulia ni joshua nassari
Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza
Tundu lisu,mtetezi wa lema.aliingia baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa.ameshangiliwa sana
Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA
hapa lema akiwa na kilewo wakati wa maandamano ya kutoka mahakamani kuelekea makao makuu ya chadema
Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa kadiri ya pingamizi ya mawakili wa lema kimomogoro na Tundu Lissu,waliofungua shitaka dhidi ya lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.kwa hiyo mengine yote yanakuwa null and void.hukumu haikuchukua hata nusu saa.so lema ni mbunge halali wa arusha mjini kuanzia hii leo
GODBLESS LEMA ASHINDA KESI
11:18 PM
No comments
Bw. Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha mji ameshinda kesi, endelea kutembelea theHOODinfotainment baadae itakuletea stori hii nzima.
Wednesday, December 19, 2012
Mitambo ya Digitali sasa kuzimwa kwa hatua
12:55 AM
No comments

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Desemba
31 mwaka huu, haitazima mitambo yote ya analojia kwenda dijitali na
badala yake, itazima mitambo hiyo katika mikoa kadhaa nchini.
Imesema imechukua uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa maeneo mengi nchini, hayajafikiwa na huduma ya digitali na kwamba inatoa nafasi katika maeneo hayo, ili kufikia hatua hiyo kwanza.
Akihojiwa kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1 hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma (pichani), alisema si sahihi kuzima mitambo hiyo kwa nchi nzima.
“Mikoa tutakayozima ni ile iliyoenea mfumo wa analojia tu, hatuwezi kuzima mahali ambako hata hiyo analojia haijaenea sana, tutakuwa hatujatenda haki,”alisema Profesa Nkoma.
Mkurugenzi huyo alisema hatua ya kuzima mitambo inahusu maeneo yote nchini, lakini kwa mpangilio kulingana ongezeko la huduma ya digitali katika eneo husika.
Pia akizungumza katika warsha ya kujadili changamoto na fursa zake jijini Dar es Salaam, iliyowakutanisha wadau wa utangazaji, Profesa Nkoma alisema kuanza kwa mfumo huo, kutasaidia kurahisisha matangazo .
Alisema Desemba 31 mwaka huu, itakuwa mwisho wa kutumia mfumo wa analojia katika meneo yote yaliyoanza kutumia mfumo wa digitali.
Aliitaja mikoa ambayo mfumo wa dijitali umefika kuwa ni Mwanza, Mbeya, Tanga, Dodoma, Arusha, Moshi na Dar es Salaam.
“Tutaanza na mikoa hii wakati mikoa mingine ikiwa inaendelea kufikiwa na mfumo huu kwani tusipokuwa makini tunaweza kuuharibu mfumo huu,” alisema Profesa Nkoma.
Mbali na hilo TCRA imewataka wananchi kuhakikisha wananunua ving’amuzi ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza mara baada ya kuzimwa kwa mitambo hiyo.
Tuesday, December 18, 2012
Lulu Sasa Abadilishiwa Mashtaka
1:26 AM
No comments
MSANII Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu,
ameepuka adhabu ya
kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba
baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kumbadilishia mashtaka, ambapo
sasa anatuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka
adhabu
hiyo kwani hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha
maisha au kuachiwa huru.
Hii inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za
adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anayepatikana na hatia
anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria walizungumza na theHOODinfotainment kwamba uzoefu wa adhabu nyingi za kuua pasipo kukusudia
zilizowahi kutolewa nchini, ni kati ya miaka 15 na wengine waliachiwa
huru.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za kumuua Kanumba
Aprili 7, 2012.
Alikuwa akidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na
kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), shtaka
ambalo mshtakiwa anayepatikana na hatia adhabu yake ni kunyongwa hadi
kufa.
Hata hivyo, jana upande wa mashtaka ulieleza
mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia
na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha CP.
Mshtakiwa huyo alitarajiwa kusomewa mashtaka
hayo
mapya jana pamoja na maelezo yote ya kesi, ambapo angesomewa ushahidi wa
mashahidi wote pamoja na vielelezo muhimu katika kesi hiyo.
Hata hivyo, hatua hiyo ilikwama kutokana na
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka anayeiendesha kesi hiyo
kutokuwapo mahakamani na badala yake aliwakilishwa na Wakili wa
Serikali, Ofmedy Mtenga.
“Upelelezi wa shauri lako umeshakamilika na
tungeweza kukusomea comital (maelezo ya kesi) leo, lakini kwa kuwa
waendesha mashtaka hawapo basi tunaliahirisha mpaka tarehe nyingine.”,
alisema Hakimu Mkazi Agustina Mmbando, anayesikiliza kesi hiyo katika
hatua hiyo ya awali.
Taarifa hizo za kukamilika kwa ushahidi wa
kesi
hiyo zilipokewa kwa furaha na shangwe na msanii huyo, kiasi kwamba
alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake.
Wakili wake Peter Kibatala aliiomba mahakama itoe
ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka haya
mapya pamoja na maelezo ya awali.
Hakimu Mmbando alikubaliana na ombi hilo la Wakili Kibatala na akaahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa.
Monday, December 17, 2012
SAJUKI KUFANYIWA MATIBABU NCHINI INDIA
4:54 AM
No comments
Msanii wa Bongo movie maarufu kama Sajuki ,baada ya kufanya matamasha mbalimbali huko mikoani ameonekana hali yake si nzuri ki afya.Kwa mujibu wa Dinno ambaye ni rafiki yake wa karibu alisema kwamba hali ya Sajuki ilibadilika ghafla kipindi wakiendelea na ziara yao huko mikoani lakini kwa sasa wako katika mipango ya kumpeleka nchini Indian kwa ajili ya matibabu. theHOODinfotainment inamtakia matibabu mema huko nchini Indian.
Thursday, December 13, 2012
KESHO HISTORIA MPYA ITAJENGEKA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI KWA KILE KITAKACHO KWENDA KUTOKEA
10:05 AM
No comments
kesho tar 14/12/2012 itajengeka historia nyingine tofauti ambayo ni kwamara ya kunza, haijawahi kutokea.... ni baada ya SALAMA SPOTRS CLUB, Club inayojihusisha na kuinua vipaji tofauti tofauti kama volleybal, football, riadha, netball na basketball. Club hiyo ambayo kesho ndio itaingia kwa kufungua rasmi club hiyo watacheza michezo miwili tofauti kwa mpigo. Ambapo timu ya mpira wa miguu ya SALAMA FOOTBALL CLUB itachuana vikali dhidi ya AJTC STAR'z ambao AJTC STAR'z ndio waenyeji wa mchezo huo, vilevile kutakuwa na mchezo wa pili ambao utahusisha riadha.
theHOODinfotainment imepata fursa ya kuzungumza machache jioni ya leo na mmoja wa Viongozi wa SALAMA SPORT CLUB Bw. Nelson Dausen na kusema kuwa chanzo cha kuanzisha Club hiyo ni kwaajili ya kuwajenga vijana kiafya na kuwafanya wawewanajiepusha na masuala yasikuwa na lazima kwao kama vile kunywa pombe, au kujihusisha na masuala ya mapenzi. Bw. Dausen aliongekua, suala hili ni suala endelevu kwa kila siku kwani ndio mchakato umeanza rasmi.
vilevile Bw. Dausen ametangaza rasmi kikosi cha mpira wa miguu ambacho kitaanza kucheza kesho rasmi, ambao majina yao ni; 1. NDALIKE
2. ABDUL
3. SAID
4. ANTHONI (montana)
5. IMMA (manywele)
6. NELSON (mapesa)
7. GEORGE
8. LIVINGSTONE
9. ROBART (chonlee)
10. AMANI (moshono)
11. JOHN
hiki ndiko kikosi ambacho kitachuana na AJTC STAR'z kilichowekwa hadharani na Bw. Dausen, Hata hivyo theHOODinfotainment imefanya juhudi za kuwasaka wahusika wa timu ya AJTC STAR'z ili waweze kutupatia ata kikosi chao walicho kiandaa kwa kesho lakini juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya kuweka baya kwamba kikosi chao watakitangaza rasmi hiyo kesho uwanjani.
SALAMA SPORTS CLUB, Ni club iliyoanzishwa ndani ya chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha AJTC kwa dhumuni la kuwaweka sawa wanachuo wanaosomea taaluma hiyo, Hata hivyo timu hiyo imeanzishwa siku chache zilizopita ikiwa kwa kuwapata wanachama wengi na kuleta changamoto ya kimichezo chuoni hapo.
mchezo huo utafunguliwa rasmi majira ya saa 04:00 pm katika viwanja vya FILD FORCE na Mkurugenzi wa mafunzo AJTC Bw. Joseph Mayagila na kuitambulisha Rasmi Club hiyo itambulike chuoni hapo.
kesho theHOODinfotainment itakuletea mtanange wa tukio zima... usikose kesho kuangalia picha kali hapa pia kumbuka kushare na watu wako wa nguvu
karibu Arusha Journalism kwa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji tembelea
Wednesday, December 12, 2012
KAULI YA FAMILIA YA MAREHEMU SHARO MILIONEA KUHUSU SAUTI YA SHARO KUENDELEA KUTUMIKA KWENYE TANGAZO LA AIRTEL
9:05 PM
No comments
.
Ni watu wengi wamehitaji
kufahamu kuhusu kauli ya familia ya Marehemu mwigizaji/msanii Sharo
Milionea baada ya tangazo la Airtel lenye sauti yake kuendelea kutumiwa
na kampuni hiyo wiki kadhaa baada ya Sharo kufariki kwa ajali ya gari
iliyotokea novemba 26 2012 Tanga.
Mjomba wa Marehemu ambae ndio
msemaji wa familia Shaban Mkiete amethibitisha kwamba wamezungumza na
kukubaliana na kampuni ya Airtel na hapa namkariri akisema “ni kweli
tumekubaliana, kwa mujibu wa mkataba wao lilikua linaisha terehe 31
mwezi huu tumekubaliana kwamba liendelee kwa makubaliano ambayo
tumekubaliana nayo sisi kati ya mzee Majuto ambae bado yupo na familia
ya Marehemu, mama mzazi wa Sharo Milionea ameridhia hilo hakuna tatizo”
Siku ya msiba theHOODinfotainment
ilipopata nafasi ya kuongea na mwakilishi wa Airtel alisema Marehemu
Sharo Milionea alifariki ndani ya kipindi cha miezi 6 tu toka asaini
dili la kuwa balozi wa Airtel na kufanya matangazo mbalimbali yeye na
mzee Majuto.
Sio tu dili la Airtel,
imefahamika tayari Sharo Milionea alikua amesaini mikataba mizuri na
makampuni mbalimbali wakiwemo Wamarekani waliotengeneza filamu maarufu
Afrika kama Yellow Card, Neria na nyingine ambapo kwa sasa Wamarekani
hao wako hapa Tanzania na wametengeneza series kadhaa ikiwemo Wahapahapa
na Siri ya Mtungi ambayo ndio Sharo Milionea kashiriki ndani na mpaka
anafariki tayari alikua ameshaanza kucheza igizo hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)











.jpg)













