Monday, January 28, 2013
WATU 233 WAFARIKI KATIKA UKUMBI WA STAREHE BAADA YA KUZUKA MOTO HUKO BRAZIL
12:54 AM
No comments
Zimamoto wakiwakwenye uokoaji katika ukumbi huokatika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Watu wakiwa kwenye simanzi katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Uhokoaji ukiendelea katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .
Wengi wa waliofariki wanaaminika kuwa kati ya miaka 16 na 20
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki. Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo. Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa. Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
Sunday, January 27, 2013
RAYUU ASEMA HATA SIELEWI SINTA ANATAKA NINI KWANGU
3:20 AM
No comments
Muigizaji Rayuu ambaye yupo kwenye beef zito na actress mwenzake Christina Manongi maarufu kama Sinta amesema kuwa kama akipewa filamu acheze pamoja na Sinta yupo tayari akipewa pesa ya maana lakini filamu ikiisha hana time nae. theHOODinfotainment ilimuuliza Rayuu kama yupo tayari kucheza filamu na Sinta kama akitokea director na kuwa-cast pamoja, Rayuu akasema "mm naangalia mkwanja nikilipwa pesa nzuri nacheza km kawa bt nikitoka hapo cna tym naye mm!". Pia theHOODinfotainment ilimuuliza je anafikiri nini chanzo cha Sinta kumfuatafuata ni picha zake zilizodaiwa kuwa chafu au ni uzuri wake ndio unaomnyima Sinta usingizi kama baadhi ya mashabiki wa Rayuu wanavyodai na hata ku-comment katika page yake facebook, Rayuu akajibu "mimi cmuelewi yule dada anataka nn??,mm cjaona pic chafu pale labda anapenda kuweka habari zangu kwake cz hana habari za maana zaidi ya umbea!ss akiniandika blog inashine mayb!cz xmuelewi!!. theHOODinfotainment ilimtafuta Sinta na kumtumia ujumbe wiki iliyopita lakini bado hajaujibu mpaka sasa ila bado tunamtafuta ili ujue nini kipo kwa upande wake.
TIMBERLAKE NA JAY Z WAINGIA MTAANI KUSHOOT "SUIT AND TIE
2:42 AM
No comments
Ijumaa ya wiki iliyopita, katika mitaa ya LA, mida ya mchana, walionekana wakishoot video ya wimbo wao mpya Suit and Tie, huku wakionekana tayari kuimudu hali ya hewa ambapo kulikua na mvua za hapa na pale.(under umbrella). collable lao saa hii limepanda mpaka nafasi ya 4 katika billboard chart top 100, kutoka nafasi ya 84 wiki yake ya kwanza. album inayofata ya Timberlake 20/20 experience itakua ni album yake ya kwanza ndani ya miaka saba, ambapo mara ya mwisho aliachia mwaka 2006
Friday, January 25, 2013
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZIKIONESHA MUONEKANO WA UKUMBI AMBAO SHOW YA KIHISTORIA NDANI YA CHUO CHA ajtc KATIKA MAANDALIZI
9:50 AM
No comments
![]() |
| huyu hapa ndio DJ Stone ambaye atatuonesha mikono yake ilivyo michafu, kuanzia mwanzo wa show mpaka mwisho, hapo alikua katika tym yakurekebisha sound ikae poa. |
![]() |
| kwa wale raia ambao watakua wanahitaji vinywa tofauti wametengewa Counter yao special ambayo haitakuwa inahudumia wateja wengine zaidi ya wanachuo wa AJTC |
![]() |
| yes katika suala la msosi sasa ambao watakua wanahitaji nyama choma wametengewa pia sehemu yao special ambayo haitakuwa inahudumia wateja wengine zaidi ya wanachuo wa AJTC |
show yakihistoria ambayo itajengeka katika chuo cha Uandishi wa habari na utangazajia Arusha muda mchache kutoka hivi sasa, maandalizi yakiwa yanaendelea, kwa wanafunzia/wadau wote wa AJTC ambao uwezekano wakufika umeshindikana bado pia tutakuwa tunatambua mchango wenu kiujamla. Kupitia the HOOD infotainment tutawaletea picha zenye matukio mazima kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa show.
kupitia TheClassicMcInTown
KUMRADHI, PICHA MNAZOZIONA HAPO JUU NI PICHA AMBAZO TULIZIPIGA MAJIRA YA SAA SITA MCHANA HII LEO, ILA KUTOKANA NA MATATIZO YALIYOKO NJE (umeme kukatika) YA UWEZO WETU TUKASHINDWA KUZIPULISH.
Thursday, January 24, 2013
MAWAZIRI WA JK WATOLEANA UVIVU
10:53 PM
No comments
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Hawa Ghasia amempasha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Hussein Mwinyi kuhusu ajira za madaktari akisema, wizara hiyo ina
utaratibu mbovu wa kuajiri unaowavunja moyo watumishi hao wa afya.
Ghasia na Mwinyi walitofautiana kuhusu suala hilo juzi kwenye kikao
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kilichofanyika Dar es
Salaam baada ya Dk Mwinyi kutoa taarifa ya wizara yake ambayo pamoja na
mambo mengine, ilieleza kuwapo mmoja wa madaktari wastaafu aliyeajiriwa
na kupewa cheo cha Mganga Mkuu wa Mkoa.
Katika taarifa yake zaidi, Dk Mwinyi alieleza kuwa kuna watumishi
ambao hupata mishahara bila kufanya kazi mkoani Manyara na kwenye Chuo
cha Mtapika, wakati pia kuna watoa huduma asilimia 50 waliopata mafunzo
lakini hawazingatii viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizi katika
utoaji huduma za afya.
“Utunzaji wa dawa na vitendea kazi hauzingatii taratibu husika za
uhifadhi na uhakiki wa ubora wa vipimo vya maabara, kuna uagizaji wa
dawa nyingi kuliko mahitaji mkoani Mtwara, huduma zinazotolewa hazikidhi
matarajio ya wateja katika vituo vingi vya afya,”alisema Dk.
Mwinyi.
Ghasia
Baada ya kumaliza kusoma taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa kamati
hiyo chini ya mwenyekiti wao Dk Faustine Ndungulile, Ghasia alisema
baadhi ya matatizo kwenye wizara hiyo siyo ya msingi.
“Nina historia
yake huyo daktari alishawahi kufanya mambo ya ajabu tu hadi yakaripotiwa
kwenye vyombo vya habari sasa karudishwa na ndiye mganga mkuu, wakati
nikiwa utumishi nililipata hilo na nikashauri aondolewe kwenye nafasi
hiyo kwa kuwa hana sifa hiyo,” alisema.
Hatua hiyo ya Waziri, Ghasia ilitokana na taarifa aliyoiwasilisha Dk
Mwinyi kwa kamati hiyo aliyoeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2012/2013
wizara yake kupitia Idara ya Uhakiki na Ubora wa Huduma za Afya na
Ustawi wa Jamii imefanikiwa kufanya ukaguzi katika idara, taasisi na
vituo vya kutolea huduma vilivyopo chini ya wizara na kubaini kuna
upungufu mkubwa wa kiutendaji. MWANANCHI
MAJAMBAZI YATEKA MAGARI ZAIDI YA MANNE NA KUWAPORA ABIRIA HUKU WAKIWAACHIA MAUMIVU MAKALI WALIOCHARAZWA VIBOKO NA MAJAMBAZI HAO
9:54 PM
No comments
Kwa ufupi:
Mashuhuda wameeleza kuwa majambazi hao wakiwa na silaha za kivita, waliweka
kizuizi na kuyasimamisha magari hayo moja baada ya jingine kasha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi.
KUNDI la majambazi limeteka mabasi matano,
mojawapo likiwa la wanajeshi wa Rwanda na kupora abiria na kisha kuwacharaza
viboko.
Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi alfajiri katika Kijiji cha Kikoma kilichoko Kata ya Rusahunga, Wilaya ya Biharamulo.
Mashuhuda wameeleza kuwa majambazi hao wakiwa na silaha za kivita, waliweka kizuizi na kuyasimamisha magari hayo moja baada ya jingine kisha, kuwashusha abiria na kuwapora kila kitu.
“Baada ya kuwapora abiria, waliamua kuwacharaza viboko mmoja baada ya mwingine, kisha kutokomea kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe na kuongeza:
“Magari yaliyotekwa ni Toyota Hiace, gari moja ni la wanajeshi waliokuwa wakitokea Rwanda kwenda Dar es Salaam.”
Diwani wa Kata ya Rusahunga, Amon Mizengo alisema tukio hilo lilihusisha majambazi wanane waliokuwa na bunduki sita za kivita.
Diwani huyo alisema magari yaliyotekwa yalikuwa yakitokea Ngara na Benaco na kuwa baada ya abiria kuporwa kila kitu, waliamuriwa kuendelea na safari zao.
Kamanda Kalangi alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi... “Ni kweli taarifa za awali zilieleza kuwa moja ya magari hayo lilikuwa na wanajeshi wa Rwanda, lakini mimi ndiyo naelekea katika eneo la tukio.”
Msemaji wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema hana taarifa za tukio hilo wala ujio wa askari hao wa Rwanda nchini. “Sina taarifa zozote, lakini inawezekana wakawa wageni wa Kanda ya Magharibi.”
Hata hivyo, alisema katika hali ya kawaida, wageni wengi wa jeshi wanaokuja nchini, hutumia usafiri wa ndege.
Tukio hilo limetokea siku chache, baada ya wananchi wa vijiji vya mpakani wilayani Ngara, kuanza kuendesha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu kwa kile walichodai ni Serikali kushindwa kuwasaidia.
Wananchi hao wamelalamikia wahamiaji hao haramu wenye makundi makubwa ya mifugo, kukingiwa kifua na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Wananchi hao wa vijiji vinavyopakana na nchi za Burundi na Rwanda, kwa nguvu zao, walikamata makundi makubwa ya ng’ombe na kuwaweka chini ya ulinzi.
Katika kutuliza jazba za wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu aliwataka wananchi kusitisha operesheni hiyo akiwaeleza kuwa Serikali inajipanga kuondoa tatizo hilo bila kukiuka sheria.
Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi alfajiri katika Kijiji cha Kikoma kilichoko Kata ya Rusahunga, Wilaya ya Biharamulo.
Mashuhuda wameeleza kuwa majambazi hao wakiwa na silaha za kivita, waliweka kizuizi na kuyasimamisha magari hayo moja baada ya jingine kisha, kuwashusha abiria na kuwapora kila kitu.
“Baada ya kuwapora abiria, waliamua kuwacharaza viboko mmoja baada ya mwingine, kisha kutokomea kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe na kuongeza:
“Magari yaliyotekwa ni Toyota Hiace, gari moja ni la wanajeshi waliokuwa wakitokea Rwanda kwenda Dar es Salaam.”
Diwani wa Kata ya Rusahunga, Amon Mizengo alisema tukio hilo lilihusisha majambazi wanane waliokuwa na bunduki sita za kivita.
Diwani huyo alisema magari yaliyotekwa yalikuwa yakitokea Ngara na Benaco na kuwa baada ya abiria kuporwa kila kitu, waliamuriwa kuendelea na safari zao.
Kamanda Kalangi alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi... “Ni kweli taarifa za awali zilieleza kuwa moja ya magari hayo lilikuwa na wanajeshi wa Rwanda, lakini mimi ndiyo naelekea katika eneo la tukio.”
Msemaji wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema hana taarifa za tukio hilo wala ujio wa askari hao wa Rwanda nchini. “Sina taarifa zozote, lakini inawezekana wakawa wageni wa Kanda ya Magharibi.”
Hata hivyo, alisema katika hali ya kawaida, wageni wengi wa jeshi wanaokuja nchini, hutumia usafiri wa ndege.
Tukio hilo limetokea siku chache, baada ya wananchi wa vijiji vya mpakani wilayani Ngara, kuanza kuendesha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu kwa kile walichodai ni Serikali kushindwa kuwasaidia.
Wananchi hao wamelalamikia wahamiaji hao haramu wenye makundi makubwa ya mifugo, kukingiwa kifua na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Wananchi hao wa vijiji vinavyopakana na nchi za Burundi na Rwanda, kwa nguvu zao, walikamata makundi makubwa ya ng’ombe na kuwaweka chini ya ulinzi.
Katika kutuliza jazba za wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Constantine Kanyasu aliwataka wananchi kusitisha operesheni hiyo akiwaeleza kuwa Serikali inajipanga kuondoa tatizo hilo bila kukiuka sheria.
Eneo hilo limekuwa likiripotiwa matukio kadhaa ya ujambazi na mwaka 2007 wabunge wanaotokea maeneo hayo waliomba kuwekwa kwa minara ya mitandao ya simu ili kuwa na mawasiliano.
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI 2012 YA ZANZIBAR HAYA HAPA
9:48 PM
No comments
Jumla
ya Wanafunzi 11,195 wamechaguliwa kujiungia Kidatu cha Tatu kwa mwaka
wa masomo 2013 katika Skuli mbalimbali za Unguja na Pemba ambapo kati
yao wasichana ni 6,768 na wavulana ni 4,427.
Aidha Wanafunzi 17,511 wamefaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu ambapo kati yao Wasichana ni 9,652 na Wavulana 7,859 .
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna amebainisha hayo leo wakati alipokuwa akitoa tathimini ya matokeo ya mitihani hiyo huko ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Amesema kuwa Wanafunzi waliofanya mtihani wa kuingilia Kidato cha Tatu walikuwa 19,679 ambapo kati yao Wasichana walikuwa 11,045 na wavulana 8644 sawa na asilimia 93.6 %.
Aidha ameongeza kuwa ufaulu wa kidato cha Tatu umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa upande wa Mtihani wa Darasa la Saba Waziri Shamhuna amesema jumla ya Wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 23,039 kati yao wasichana walikuwa 12,236 na wavulana 10,803.
Akielezea Skuli zilizoshika nafasi ya juu kwa matokeo ya Darasa la Saba Waziri Shamhuna amesema ni pamoja na Kizimbani iliyopo Wilaya ya Wete Pemba na Skuli za Wazazi na Mkunazini zote za Wilaya ya Mjini Unguja.
Aidha amezitaja Skuli zilizofanya vibaya matokeo ya Darasa la Saba kuwa ni Kojani, Ukunjwi na Makoongwe zote za Kisiwani Pemba.
Kwa upande wa Matokeo ya Kidato cha Pili skuli zilizofanya vyema kuliko nyingine ni Mtoni iliyopo Wilaya ya Magharibi Unguja na Skuli za Msuka na Kiuyu zote za Wilaya ya Micheweni Pemba.
Akielezea Skuli zilizofanya vibaya mtihani wa Kidato cha Pili Waziri Shamhuna amesema ni Skuli za Mwenge iliyopo Wilaya ya Magharibi na Skuli za Mfuru matonga na Kinyasini zote za Kaskazini A Unguja.
Waziri Shamhuna amezitaja pia Skuli ambazo zitalazimika kufungwa kutokana na kupasisha idadi ndogo ya Wanafunzi ambazo ni Bwefum, Umbuji, Uzi, Ubago,Pongwe Pwani, Michanvi,Mtende,Kisiwa Panza,Makongwe na Ndagoni.
Ameongeza kuwa jumla ya Kesi za udanganyifu 12 ziliripotiwa kwa wanafunzi wa Kidato cha pili ambapo Wizara imeamua kwafutia matokeo wanafunzi waliohusika na Udanganyifu huo.
HUYU NDIO YULE MBUNGE SHAROBARO WA KENYA
11:19 AM
No comments
Huyu ndio yule mbunge sharobaro
wa Kenya, umaarufu wake umeongezeka kutokana na usharobaro wake ambao
unamfanya mpaka avae hereni na kudunda mtaani kama kawa.
Nakumbuka 2012 moja kati ya
stori nilizoziona kwenye TV za Kenya ni wakati alipoamriwa kutoka nje ya
jengo la bunge baada ya kuingia akiwa amepiga suti fresh lakini
masikioni anazo hereni.
Ukimkuta kwenye mitaa huwa
anatupia pamba sio kitoto, na ni rafiki wa wasanii pia nakumbuka hata Z
ANTO wakati yuko juu kipindi kile na single ya binti kiziwi, huyu Sonko
alimpatia gari la kifahari kutembelea Kenya akiwa na mlinzi pembeni.
Wednesday, January 23, 2013
Flaviana Matata ashinda tuzo ya mwanamitindo bora wa Afrika 2012
5:16 AM
No comments
\
MWANAMITINDO wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa baaada ya kushinda
tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani
Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
MWANAMITINDO wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya
kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora
barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo hiyo utolewa kwa
wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana
amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba, Flaviana alishinda
tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.
Tuesday, January 22, 2013
BIG BROTHER AFRICA NDIO HII APA SASA MSIMU MPYA 2013
6:28 AM
No comments
Msimu
mpya wa Big Brother Africa tayari umeanza kubisha hodi kwa wanaotaka
kushiriki kuanza mchakato. shindano hilo maarufu ndani na nje ya bara la
africa linatarajiwa kuanza rasmi may mwaka huu na nchi 14 zikitarajiwa
kushiriki ambazo ni Tanzania iliyowahi kutoa mshindi, Uganda, Kenya,
Malawi, Ethiopia,Zimbambwe, Zambia,Nigeria, Namibia, Botswana, Angola,
South Africa, Sierra Leone, Ghana.baadhi ya vigezo vya kushiriki ni kama
vile uwe na umri kuanzia miaka 21,uwe raia wa nchi unayotaka
kuiwakilisha, ujue kuzungumza kiingereza vizuri, uwe na passport ya
kusafiria au uwezekano wa kuipata kabla ya mwezi march kuisha, uwe
mcheshi, mvumilivu na shabiki wa shindano hilo. form za kujiunga
zinapatikana www.africamagic.tv/bigbrother .pia fomu za kujiunga
zitapatikana katika office za MultiChoice katika nchi zinazoshiriki
kuanzia february mosi mwaka huu. Huu ni msimu wa 8 wa shindano hilo
tangu kuanzishwa kwake.
JACK CLIFF NA JUX VUITTON WAZUA MANENO BAADA YA KUTUMA PICHA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM
5:58 AM
No comments
Kama utakuwa unamfahamu mwanadada Jack Cliff ambaye ameshawahi kushirikishi katika video mbili kama Queen Video ambazo ni Nataka Kulewa na she got a gwan ya Ngwair na nyinginezo,
sasa mrembo huyu baada ku post picha hii katika mtandao wa instagram watu wengi sana wanauliza na maswali mengi juu ya Jux na Jack Cliff huko China.
Huku Jux kupitia katika akaunti yake ya instagram alipost picha hiyo hapo juu ambayo jack Cliff akijaribisha kuvaa viatu vyake na kuandika Baby Tryn them #me Jordan...#dope though.
sasa mrembo huyu baada ku post picha hii katika mtandao wa instagram watu wengi sana wanauliza na maswali mengi juu ya Jux na Jack Cliff huko China.
Huku Jux kupitia katika akaunti yake ya instagram alipost picha hiyo hapo juu ambayo jack Cliff akijaribisha kuvaa viatu vyake na kuandika Baby Tryn them #me Jordan...#dope though.
Subscribe to:
Posts (Atom)


























