Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Tuesday, February 26, 2013

hivi ndivyo TCRA ilivyotaka kuifungia Clouds FM kutokurusha matangazo yake tena, Radio nyingine mbili nchini zafungiwa. SOMA HABARI HII HAPA UJUE NI KWANINI.

TCRA (800x534)
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia kitengo cha maudhui imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita vituo vya radio viwili nchini kwa kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo ni pamoja na Kwa Neema FM ya Mwanza iliyofungiwa kwa kuendesha mjadala uliokuwa ukihusiana na watu wa dini gani wenye haki ya kuchinja wanyama kati ya waislam na wakristu hali iliyosababisha mgongano wa waumini wa dini hizo.

Kingine ni Imani Radio FM ya mjini Morogoro ambayo imefungiwa kwa kosa la kupinga zoezi la sensa mwaka jana na kuwashawishi waumini wa dini ya kiislam wasijiandikishe.

Nayo Clouds FM imepigwa faini kwa kuendesha mjadala kuhusiana na ushoga pamoja na kuwa na kipengele kwenye kipindi cha Power Breakfast kiitwacho ‘Jicho la Ng’ombe’ ambacho wametakiwa wakifute kutokana na kuendeshwa kinyume na maadili. 

 CHANZO: http// :www.bongo5.com

RAGE: TUTAFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MATOKEO HAYA

kiemba_thumb[18]
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kutoa uamuzi mgumu kuhusiana na mwenendo mbaya ulionayo timu hiyo katika ligi kuu ya Vodacom.
Aidha, Rage amekanusha taarifa za kujiuzulu kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema kwamba kamati ya utendaji ya Simba ilitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao.
Alisema kikao hicho kitajadili kwa kina hali iliyopo sasa ambayo imesabababisha timu yao kupoteza hata matumaini ya kutetea ubingwa wao.
“Tutakuna baadaye leo na kujadili hali hii maana tukiiacha hivi hivi inaweza kutuletea madhara makubwa sana…pia tutatoa maamuzi mazito baada ya kikao chetu,”alisema.
Kuhusu na taarifa za kujiuzulu kwake, Rage alisema anashangazwa na taarifa hizo zinapotoka kwani kama atafikia uamuzi huo ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia hatua hiyo
…..Continue reading here: http://lindiyetu.blogspot.com/2013/02/rage-tutafanya-maamuzi-magumu-kwa.html


WASANII BONGO FLAVA KUSINGIZIANA UCHAWI NI KUKOSA UBUNIFU KATIKA KAZI ZAO

YAMOYONI:Shindano la mkali wa rhimes kama lingefanyika mwaka 2012 au 2013 nadhani tungesema Afande sele amechinja kondoo 100 wa kafara ili ashinde ama ameua albino,kipindi kile Juma nature anatamba na album yake ya ugali ,Ferooz na nyimbo yake ya ukimwi,Professor,Dully & Mr Nice kipindi kile wanaonekana miungu watu nadhani ingekua kile kizazi ni kizazi kama tulichonacho sisi kwasasa ungesikia hawa ni mafremason,mwingine angesema hawa ni wachawi wanatembelea nyota za akina Ngurumo,jumbe,shaban dede ama mzee issa matona.Lakini kuonesha tofauti ilokuepo kati ya kizazi kile na hiki wale walikua wamekaa kimya kila mtu akijaribu kutafuta njia ya kupata mashabiki kupitia staili mbalimbali za kimziki.Amini ninachokwambia kuna tofauti kubwa sana kati ya kizazi kile cha mziki ule na kizazi hiki cha sasa cha kina Bob jr na Ney wamitego,na ndomana kikaitwa kizazi kipya na upya umedhihirika.Sasa nirudi kwenye mada yangu.Kwamimi ninachofahamu ni kwamba mganga ndo siku zote atakaekwambia nani anakuroga,na unapomsikia mtu anasema karogwa ujue alienda kwa mganga sasa jiulize alifuata nini?Hapa tunapause kwanza……Inaendelea: http://lindiyetu.blogspot.com/2013/02/wasanii-bongo-flava-kusingiziana-uchawi.htmlq-chief6


MAONI MBALIMBALI BAADA YA LADY J DEE KUOMBA MUONEKANO MPYA WA CD YAKE. TAKE TIME YAKO PIA KUTOA MAONI YAKO. Cheki hapa

Jana kupitia katika mtandao wa facebook mwanadada Lady J Dee,baada ya kuomba maoni kwa mashabiki wake kuhusu muonekano mpya wa CD ambayo itakuwa ina ngoma yake mpya aliyofanya collabo na Professa Jay "JOTO HASIRA"

Haya ndiyo maoni mbalimbali ya watu wakimshauri Lady J Dee achukua cover kati hizo hapo juu itakayohusika katika kubeba ngoma yake mpya 'JOTO HASIRA'



Monday, February 25, 2013

SIKU CHACHE BAADA YA KUZINDUA OFISI YAKE WATU WAPANGA NJAMA KUMTEKA WEMA SEPETU


 


Ikiwa ni siku chache tu baada ya kufungua ofisi yake "endless fame", iliyoko maeneo ya mwananyamala, jana usiku wema alipokea simu akitahadharishwa na msamaria mwema kuhusu kundi la watu waliokuwa wanamzungumzia kwa kumpangia njama ya kumteka, watu ambao walikua katika moja ya baa zilizoko Sinza inayopitwa Shkamoo pesa bar
"ni jana tu around jioni jioni hivi, nilipokea simu kutoka kwa msamaria mwema, akiniambia wema jihadhari, yaani baada tu ya kupokea hiyo sim, kwanza i was shoked halafu mwisho wa siku nikiona kama ma haters wanataka kunijaribisha, halafu mwisho wa siku kama vile hawawezi, maana hawajui how well am prepared......."
wherever they are trying to do, they should just understand that, wasije wakajikuta wao ndio wako in trouble, in deep shit, because naskia kuna jopo la watu wanataka kunivamia and its not right, kama mwenzako anafanikiwa muombee mema sio kumdidimiza...."amesema wema 

HIZI HAPA PICHA ZA MSIBA WA GOLDIE, MUME WAKE NA WENGINE WALIOHUDHURIA.



http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/02/1100.jpg
.
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/02/249.jpg
Andrew Harvey mume wa Goldie.
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/02/346.jpg
.
Dada wa Goldie akiwa na marafiki
.
.
Wa pili kutoka kushoto ni mtangazaji wa Channel O Denrele Edun ambae alikua rafiki mkubwa wa Goldie na ndioGoldie alifia mikononi mwake akiwa amembeba, huu msiba ulihudhuriwa na watu wachache walioalikwa tu huko Ikoyi Lagos Nigeria.
.
.
.
.
.
.
.
Mwimbaji Tiwa Savage na mchumba wake.
.
Gazeti la Daily Post liliripoti leo asubuhi kwamba msanii Goldie ambae aliiwakilisha Nigeria kwenye jumba la Big Brother 2012 anazikwa leo, baada ya muda kupita ndio nimezipata hizi picha za msiba wa Goldie ambae alifariki siku ya Valentine feb 14 2013.
Imeripotiwa kwamba manenoya mwisho ya Goldie yalikua ni kumuomba baba yake amuombee apone maumivu makali ya kichwa aliyokua nayo ambapo Daily Post wameripoti tena kwamba staa huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali, foleni ya magari siku hiyo ya wapendanao ilichangia kuchelewa kufika hospitali.
Chanzo mojawapo cha kifo chake ni shinikizo la damu na maradhi ya moyo.

Hii hapa ile simu ambayo Nokia wameizindua inayotunza chaji kwa mwezi mzima (itauzwa shilingi 30,000 tu) SOMA HAPA UJUW UNAWEZA KUIPATA VIPI

nokia 2
Baada ya Nokia 1100 huenda Nokia 105 ikaja kuwa simu maarufu zaidi hasa kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Hii ni baada ya kampuni hiyo ya simu kuzindua simu hiyo yenye uwezo wa kutunza chaji kwa siku 35 kila unapochaji.
Simu hiyo imetengenezwa maalum katika maeneo ambayo umeme hakuna ama unasumbua lakini pia kama ‘backup phone’ pale zingine zinapozima.
nokia
Ikiwa inatarajia kuingia sokoni wiki kadhaa zijazo, Nokia 105 ambayo bei yake ni paundi 13, sawa na shilingi 30,000 za Tanzania pia ina tochi na FM radio.

Birdman aongelea uhalisia wa Drake, amtaja kama 'Mwenye kipaji zaidi katika industry ya Music'



 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgJUoinYQfRRayrDYXwMITaLxuD7Ul_771PKrzY590fexX5l8eE1h3bd32_-DVzYjdIud0mHAx1SjuRY75yLBqW8rCD9cxK83pZSDMTdEb6xWr_5P_z5kCWBnaZ1h4Mk89LHVqDy22XOk/s640/drake+and+birdman.jpg

Birdman baada ya kukisikia kibao kipya cha Drake kwa mara ya kwanza kinachokwenda kwa jina la 'Started From the buttom' ameshindwa kuzificha hisia zake na kuthibitisha imani juu yake kwamba Drake mtu halisia na ni miongoni mwa watu wenye vipaji zaidi katika muziki kuwahi kuwepo.
Katika mixtape aliyoiachia hivi majuzi, Birdman ameamua kuwaonjesha fans wa Music ni kitu gani ambacho wakitegemee kutoka 'Young Money' na moja kati ya vitu hivyo ni Album yake Drake na ambapo aliongelea ujio huo wa Drake 'Started from  the buttom'  umemfanya aendelee kumpa credit nyingi zaidi kwani unaendelea kuthibitisha ni kwa jisni gani drake anaweza kazi hiyo isivyo kawaida.
Kuhusiana na hili Birdman alikaririwa akisema
"Drake sio mtu wa kawaida ikija kwenye masuala ya music.... ni kipaji halisia. Harudii rudii kazi zake, hujjiandalia tone yake mwenyewe, na kila kitu katika mziki wake hufanya mwenyewe."
Pia Birdman aliuongelea uvumi juu ya Drake kuihama YMCMB na kusema Drake haendi popote na kuwa hii ni biashara, watu wanaongea, blogs zinaongea lakini yote ya yote jambo hilo halina ukweli wowote ndani yake....
 "Our relationship with Drake ... that's my lil brother. That's the homie. That's family. So there's never been no friction. We're just working hard, trying to give people great music."  

NGOMA MPYA YA ‘KAMA ZAMANI’ YA MWANA FA YAZUILIWA, Kwanini soma hapa

Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za mkononi.

Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
 
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.

Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.
Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama  Zamani kama ilivyopangwa hapo awali.

Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.

Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
 
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.

BREAKING NEWS: WAZIRI WA MICHEZO AIFUTA KATIBA YA TFF

 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara
 
 Rais wa TFF, Leodger Tenga.

SERIKALI imeingilia kati sakata la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya shirikisho hilo na badala yake kuamuru itumike katiba ya zamani (mwaka 2006) baada ya kubaini kuwa iliyopo ina kasoro nyingi.  Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeeleza kuwa katiba ya sasa ya TFF si halali.   Imeelezwa vilevile kuwa msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa.   Mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF umesimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais.  Kamati ya rufani ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo iliyozua balaa lote la sasa baada ya kuwaengua kina Malinzi na mwishowe kumuacha makamu wa sasa wa rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.  Hata hivyo, tayari mchakato wa uchaguzi huo uliozua mabishano makali umeshasimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na maafisa wa chombo hicho cha juu cha mchezo wa soka duniani wameshaanza kuwasili kufuatilia kinachotokea nchini.  Uamuzi wa serikali wa kufuta katiba ya sasa na kutaka itumike ya 2006 unampa ahueni kubwa Wambura ambaye alishasema hadharani kuwa  ataiburuza TFF mahakamani kama isipoachana na katiba mpya na kufuata ya zamani.  Huku akitoa sababu kadhaa za kupinga matumizi ya katiba mpya, mojawapo ikiwa ni kupitishwa kwake kwa njia ya waraka wa barua pepe (e-mail) kwenda kwa wajumbe badala ya kufuata maelekezo ya katiba yanayotaka mabadiliko kufanywa na wajumbe kupitia mkutano mkuu.  Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za FIFA, ni marufuku kwa shughuli za soka kuingiliwa na serikali au mahakama na nchi yoyote inayokwenda kinyume na taratibu hizo hujikuta ikifungiwa kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya. 

CHANZO: straikamkali.blogspot.com.

WANAWAKE WAKIRI KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE. soma hapa ujue ni kwanini

Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR. 
***
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za  Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.

Hayo yalielezwa na Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) wakati akiwasilisha utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na maumbile katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

“ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.

Aidha alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5%  huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufanhamu njia hiyo ya kufanya mapenzi.

Wilayani Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.

Wanaume waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai kupunguza raha wanayo ipata.

Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.

Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.

Aidha imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.

Watafiti hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.
 
Watafiti walioshiriki katika utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth  H Shayo,  Irene Mremi , Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson Kagaruki, Anjela  Shija, Judith Msovela, Dk. Leornad Mboera, Dk.Julius Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana Emid wote kutoka NIMR.

WEMA SEPETU ATANGAZA NAFASI ZA KAZI KATIKA KAMPUNI YAKE MPYA"ENDLESS FAME FILM"

Msanii wa bongo movie 'Wema Sepetu' siku chache baada kufungua kampuni yake mpya Endless Fame Film.
Leo kupitia katika ukurasa wake wa twitter ametangaza nafasi za kazi mbalimbali ikiwemo,graphic designer,editor,camera man,usekretari.

Maelezo zaidi soma hili tangazo kutoka katika kampuni yake 'Endless Fame Film' wakitangaza nafasi za kazi!!!!!

Kumbe na ‘The Game’ kwa kiasi flani amehusika kumuua Osama bin Laden..!?

Habari zaidi zinazidi kusambaa kuhusu the Seal Team Six member ambaye alimpiga risasi na kumuua Osama bin Laden. Jamaa aliuambia mtandao wa Esquire.com kwamba kuna wimbo alikua akiusikiliza wakati anajifua kwa ajili ya misheni hiyo: 

"Red Nation by Game. Ni wimbo unaohusu umwagaji wa damu. Tulikua the Red Team na tulikua tunaenda kumwaga damu." — Alisema jamaa huyo aliyemuua Osama bin Laden.

Sasa basi Esquire.com walimpigia simu Rapper The Game ili kujua anafikiria nini kuhusu jambo hilo. Mahojiano yao yalikua hivi:

ESQ: So how does it feel to hear that your song was what the guy who killed bin Laden listened to as he got pumped up?

GAME: I think that's the shit, man. What's crazy about that is that bin Laden might have heard "Red Nation" right before he died. That's pretty cool. 'Cause if you're thinking about the speakers, sometimes it bleeds out, you know?

ESQ: [Laughs.] I don't think he was actually listening while he was on the mission, because they've got to listen to each other. But when he was in training, he did.

GAME: Oh. Maybe while he was on the way to kill bin Laden maybe he was doing an a cappella.

ESQ: So you were, in a small way, a part of the mission that killed Osama bin Laden.

GAME: I feel real patriotic. I feel real American. I feel like I had — 'cause what if he was listening to, like, John Mayer? Than he probably would've missed the shot or something. But I feel like "Red Nation" had him on-point.

ESQ: Even in your wildest dreams, did you feel like one of your songs could be involved in such a big part of American history?

GAME: I would've never imagined that they would be getting pumped up and ready to go on a mission, a field mission to kill bin Laden. I know dudes that do it in the locker room — football players, basketball players. You never just think that that secret, silent bin Laden team is pumping your music. But they've got to be pumping somebody. So I just appreciate that it's me, man. That's fking crazy.

ESQ: So have you been following the story of these guys at all?

GAME: I've seen Zero Dark Thirty, man. I thought it was a great fucking movie. It had me on-edge. I'm sure it was more intense in real life. I was real sad when the lady got killed.

ESQ: The song actually makes sense because you've got that line in there about killing Satan and putting a red flag in the ground.

GAME: It's perfect. Bin Laden was someone like Satan. And the American flag going into the ground. So yeah — maybe I pre-visualized that whole scenario. [Laughs.]

ESQ: And you've got that classic arena pump-up sample in it.

GAME: [Sings] "Oh oh oh oh-oh oh" — yeah it's crazy.

ESQ: So what is the red nation that you're actually talking about in the song?

GAME: For my whole life, I grew up into gang-bang culture, where you either pick blue or red. And I picked red. I started there. 

And as I got older and got a little bit away from gang life, my favorite basketball team growing up — well, of course, were the Lakers and the Clippers because I'm from L.A., but the Bulls were really my favorite team. And then football, it was the 49ers. 

It's always the red team, man. And so it's just the Red Nation, man. We bleed red. We all bleed red. That's it.

ESQ: And this guy's particular squadron within Seal Team Six was called the Red Squadron.

GAME: Now it's making too much sense, man. It's just getting scary. Once I get off the phone, I'm going to envision myself in one of the super-secret helicopters. I'm just going to put myself in that scenario, and I'm going to see if I can make that shot.

ESQ: You think you could make it?

GAME: You know, I've been going to the shooting range since I was, like, probably 16 or 17 years old. I think that under pressure, I'm pretty good, man. 

I think I probably couldn't make that shot, but I think I could definitely come up after somebody killed him and shoot him in the chest a couple times. I could definitely hit him if he's already down.

ESQ: A couple other guys might have.

GAME: Everybody wanted a shot, right? I could definitely hit bin Laden. I would've did a dome shot. Fuck it. If you're going to do it, go all the way out.

ESQ: So what's more badass: Navy Seal Team Six Red Squadron or Red Nation?

GAME: You know what, they're more badass, man.