Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Tuesday, July 30, 2013

HAWA NDO WANAWAKE KUMI TANZANIA WENYE VYEO VIKUBWA

Dk. Asha-Rose Mtengeti Migiro.
WANAWAKE wengi nchini wameshika vyeo mbalimbali vya juu serikali au kwenye taasisi binafsi. Wafuatao ni wanawake 10 ambao wanakalia au wamekalia vyeo hivyo hapa nchini kama walivyomulikwa na Elvan Stambuli.
JULIET  KARIUKI
HUYU ni Mkuruggenzi Mtendaji wa kwanza mwanamke katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) . Uteuzi wake ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete Aprili 12 mwaka huu na akakabidhiwa ofisi siku hiyohiyo.
Bibi Kariuki ana shahada ya kwanza ya sheria na ya uzamili, kwenye sheria ni mtalamu wa ubia kati ya serikali na watu binafsi (Public Private Partnership). Aliwahi kufanya kazi katika Chama Cha Mabenki ya Afrika Kusini.

MIZINGA MELU
NI  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC tangu  Machi 20 mwaka huu. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa  Lawrance Mafuru. Ni mzaliwa wa  Zambia katika Kijiji cha Mazabuka na ana shahada ya juu ya biashara (MBA), Zambia National Commercial Bank na Standard CharteredBank.
SAUDA S. RAJABU
NAYE ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu wa Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air hapa nchini. Alianza kutumikia nafasi hiyo Machi Mosi, mwaka huu baada ya aliyekuwa akikalia kiti hicho, Alfonce Kioko kumaliza muda wake.
Ana shahada ya kwanza ya biashara na sasa yupo mbioni ‘kuchimbua’ shahada ya juu ya biashara. Amewahi kufanya kazi katika mashirika mengine ya ndege kama vile Kenya Airways na ya Rwanda na Burundi.
ANNE MAKINDA
NI mwanamke wa kwanza nchini kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Samwel Sitta ambaye aliliendesha Bunge kwa msimu mmoja tu mwaka 2005 hadi 2010.
Makinda amevunja rekodi kwa kukaa bungeni kwa miaka mingi kwani alianza kuwa Mbunge wa Jimbo la Njombe mwaka 1975 hadi leo. Tayari ametangaza kung’atuka (2015).
BALOZI LIBERATA MULAMULA
NI Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico. Amewahi kuwa balozi wetu nchini Canada kuanzia mwaka 1999 hadi 2002. Amewahi kuteuliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa mgogoro wa Rwanda. Ni msomi mwenye shahada ya kwanza na ya pili ya sanaa,alisomea Chuo Kikuu cha St. John’s, Marekani, 1989. (Pichani akiwa na Rais Obama.)
MCHUNGAJI G.RWAKATARE
HUYU ni Mchungaji na kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na mwanzilishi wa shule za  St. Mary’s International alizozifungua mwaka 1997.
Licha ya kazi ya kuhubiri Injili, Mama Rwakatare ana chombo cha habari ambacho ni
Praise Power Radio 99.2 FM inayoelimisha jamii na kutoa burudani za kiroho.
GETRUDE MONGELLA
ALIKUWA mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Bunge la Afrika, amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini India 1991 hadi 1992 na akawa Katibu Mkuu katika Mkutano wa Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China  mwaka 1995.
Aliwahi kuwa mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco na aliwatumikia wananchi wa Ukerewe akiwa ni mbunge kuanzia 2000 hadi 2010 na Februari mwaka 2008 alikuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya African Press Organization (APO).
ASHA ROSE MIGIRO
Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasheria na mwanasiasa. Licha ya kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mama huyu aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania. Lakini kikubwa zaidi ni pale alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Juni 2012. Baada ya kumaliza muda wake Umoja wa Mataifa, Migiro hivi sasa yupo nchini akiongoza kitengo cha Mambo ya Nchi za Nje cha Chama Cha Mapinduzi.
SUSAN MASHIBE
HUYU ni rubani na ni injinia wa ndege, hivyo kuwa mwanamke wa kwanza nchini kuwa na elimu hizo alizopatia Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani. Ni Mwanzilishi na kiongozi wa Tanzanite Jet Centre Ltd, kampuni aliyoianzisha mwaka 2003 ambayo sasa inajulikana kama  Via Aviation  na inajishughulisha na biashara ya mambo ya anga nchini na barani Afrika. Alikutana na Rais Barrack Obama alipokuja nchini hivi karibuni.
JOYCE MHAVILE
NI Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One kuanzia 1994. Amekiongoza kituo hicho cha runinga hadi kushika nafasi ya kwanza kwa ufanisi mwaka jana.
Amebobea kwenye taaluma ya uandishi wa habari.  Ni mmoja wa wanawake katika Bara la Afrika walioongoza chombo cha habari kwa mafanikio na kuwa mfano kwa wasichana wanaochipukia hivi sasa katika nchi yetu.
 
chanzo.http://audifacejackson.blogspot.com

Nicki Minaj amcheka Dj Khaled ‘He is crazy’ aijibu video aliyoombwa uchumba


634.minaj.mh.092812

 Nicki Minaj na DJ Khaled kamwe hawawezi kuwa mtu na mke wake. Kwa mara ya kwanza Diva huyo wa Young Money amelijibu ombi la kuolewa na Dj Khaled.
Alimpigia simu Funkmaster Flex wa Hot 97 jana kuielezea video hiyo ya MTV News iliyomuonesha Khaled akielezea jinsi anavyompenda rapper huyo na pia kutoa pete ya thamani aliyopanga kumvisha.
“Nilishtuka kama dunia yote, nilikuwa nikicheka kama wengine Khaled ni master katika kile anachokifanya,”alisema Nicki.
KUMBE, Khaled alirekodi video hiyo kupigia promo single yake mpya kutoka kwenye albam yake mpya Suffering From Success, “I Wanna Be With You” aliyomshirikisha Nicki, Future, na Rick Ross.
“Ilikuwa ni njia nyingine ya yeye kuionjesha dunia feeling ya wimbo huo. Nobody in my real life took it seriously. Everybody just hit me like, ‘LOL. Yo, Khaled is crazy.”
Nicki aliamua kuzima matumaini yote ya kuwa mke wa Dj huyo kwa kudai kuwa ni kaka yake.
“Khaled is my brother and Khaled was not serious with that damn proposal, ya’ll. Please let it go. He was kidding. He’s not attracted to me, he doesn’t like me. We’re brother and sister.”
Licha ya Nicki kukataa, Khaled aliendelea kuwa serious na mpango hasa baada ya weekend hii kuongea kwa simu na DJ Felli Fel wa Power 106.
“She might say yeah tonight or tomorrow, she might say yeah next year. What am I gonna do, give up? Never. I ain’t never give up on nothing I do,” alisema.
Hata hivyo baada ya interview ya Nicki, Dj huyo alitweet: “Salute @NICKIMINAJ!!! … Bringing the excitement back to the game!”

kwa hisani ya:  BONGO 5

Samsung yaingiza sokoni simu ya ‘Galaxy S4 Active’ isiyoingia maji wala vumbi ‘waterproof and dustproof version’

Ushindani wa biashara ya smart phone unazidi kukuwa na kufanya kila kukicha makampuni pinzani kama Samsung na Apple kuja na matoleo mapya ya bidhaa zao zinazoleta ushindani mkubwa wa soko. Kampuni ya Samsung imepeleka sokoni toleo jipya la Galaxy S4 Active isiyongia maji wala vumbi ‘waterproof and dustproof version’.
samsung waterproof
Kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu Korea kusini imesema imetengeneza toleo hili la Galaxy S4 Active isiyopitisha maji wala vumbi, ikiwalenga wazazi kwa kuwasaidia kuepusha ajali na uharibifu unaoweza kusababishwa na watoto.
“We know a lot of parents use their phones to show children content. We ended up going to a lot of family homes where we were shown a graveyard of smashed phones”. Alisema Luke Mansfield mkuu wa ‘ Samsung’s Europe innovation team’ alipozungumza na The Times.
Simu hiyo inauwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 30 na kupiga picha majini kwa kutumia ‘waterproof camera’.
Simu ya Galaxy S4 Active ambayo ilitambulishwa (May) imeingia sokoni mwezi huu (July) na inagharimu £480 sawa na karibia million 1 na laki 2.

Roma Mkatoliki kuvunja ukimya kwa kuachia video 2 kwa mpigo ikiwemo ya 2030

Mwana Hip Hop, Roma Mkatoliki anatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia video mbili. Moja ni ya wimbo wake alioutoa mwaka jana nyingine ni ya wimbo mpya.
ROM
Roma amesema ameamua kufanya hivyo kama njia ya kuwapoza mashabiki wake aliowaangusha kwa kushindwa kutoa video ya hit yake Mathematics. Amesema alikuwa ameshalipia kufanya video hiyo lakini muongozaji kutingwa na kazi nyingi na hivyo kuichelewesha sababu iliyomfanya rapper huyo aweke kabatini tu kwakuwa ilikuwa imekaa muda muda mrefu sana.

“Tulichojipanga Roma na Tongwe team mzima tufanye video mbili au tatu inawezekana tukatoa video ya 2030 na nyingine mbili mpya na pia video ya Mathematics tulifanya lakini producer alitucheweshea kuturudishia kwahiyo ushauri wa watu wakasema tuiache tufanye kama kumbukumbu,” Roma aliambia Bongo5.

Kutokana na ucheleweshaji wa kazi yake, Roma ameamua kumtafuta director ambaye hajulikani ili mradi afanye kazi nzuri.
“Sijajua kuna matatizo gani kwa kampuni ambayo tuliichagua walikuwa na kazi nyingi, sio kwenye video hata kwenye audio napenda kushauriana mawazo yangu yapewe kipaumbele lakini sijajua tunapishana mawazo na makampuni makubwa kwasababu hawataki kushauriwa. Yeye umuachie kazi yako siku ya siku anakupa cd yako kama amekosea ukimwambia kuna vipande sivitaki au viongezwe anaweza akakujibu vibaya. Kwa sasa tutatafuta kampuni hata iwe ndogo ilimradi itafanya vitu ambavyo nahitaji vifanyike. Unaweza ukamshauri twende Tanga kuna location Nzuri mkaenda lakini sasa wengine ukiwashauri wanaweza kukujibu vibaya.”

chanzo: bongo 5

Jay Z atembelea makao makuu ya Facebook California, Marekani

Ijumaa (July 26) rapper na CEO wa Roc Nation Shawn Carter a.k.a Jay Z alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya mtandao maarufu wa kijamii Facebook yaliyoko California, Marekani.
Jay Z and Mark
Jay Z alipita katika makao makuu ya Facebook na kupata nafasi ya kuonana na kuzungumza kidogo na CEO wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg pamoja na wafanyakazi wa Facebook kabla ya kuelekea San Fransico katika tour yake na Justin Timberlake, kwa mujibu wa Global Grind.
Hii ilikuwa ni surprise kwa wafanyakazi wa Facebook ambao walipata nafasi ya kumuona live baba Blue Ivy na hip hop mogul Jigga.

chanzo: bongo 5

Interview ya TV ya staa huyu, Yawa gumzo baada ya kuingia akiwa amevaa vazi la bafuni

Mkali wa filamu maarufu za Die Hard, Bruce Willis amekuwa gumzo katika media kutokana na safari hii kuamua kutokea katika mahojiano ya TV akiwa amevalia taulo - bathrobe kama moja ya 'mitupio' /vazi lake, na hivyo kuvunja mtazamo uliozoeleka na watu hususan mastaa, wa kujipanga saana kimavazi pale wanapokuwa wana mchongo wa interview ya TV.

Mtoko huu wa Bruce ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 58 ulikuwa ni katika  kipindi maarufu cha televisheni huko UK ambacho kinafahamika kwa jina 'Daybreak' cha mtangazaji maarufu KateGarraway.


Tazama picha za tukio hili hapa;

Bruce ambaye ni Baba wa mabinti wanne, Mabel 15, LaRue 22, Tallulah Belle 19, Rumer 24, kutokana na aina ya maisha anayoishi na familia yake hii ya mabinti, ametajwa kama moja ya mzazi na mwanafamilia bora, Tofauti kabisa na tabia za ugomvi na ukorofi anazohusishwa nazo na wengi hasa kutokana na aina ya filamu anazoshiriki.

(News) Kumbe OSTAZ JUMA NA MUSOMA aliamua kuimba ili kumkata ngebe MR. BLUE......!!!!

Ostaz Juma  
Manager wa Kampuni na label ya Mtanashati Entertainment inayosimamia Wasanii kama vile Dogo Janja, PNC, Happy Balice na wengineo, Maarufu kama Ostaadhi Juma Namusoma ameamua kufunguka live kuwa Sababu ya yeye kuingia kwenye Muziki kwa upande wa Kuchana na kuachia ngoma yake aliyofanya na Young Killer haikuwa na maana ya kutaka tu kuonyesha kuwa anaweza pia upande wa pili bali pia nikumkata Ngebe Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye anadai kuwa alimdiss kwenye kipindi cha Mkasi wakati akihojiwa na Salama Jabir.

Ostaadhi Juma amefunguka hayo wakati akipiga short Interview kwa njia ya simu na Mtangazaji wa Mambo Jambo Radio Arusha DJ Haazu ndani ya Kipindi cha Mtaa wa Pili Round II ambapo bila kuficha Jamaa alifunguka maneno hayo ambapo anasema baada ya Mr. Blue kumdiss kwenye kipindi cha Mkasi kuwa haujui Muziki yeye hakujibu chochote.

Mr. Blue alimdiss jamaa huyo pale alipoulizwa na Salama Jabir kuwa angependa apate Manager wa aina gani ambapo Mr. Alimjibu Salama kuwa anataka Manager anayejua mziki na sio vimanager kama Ostaadhi sijui Juma....jamaa yeye alikaa kimya na kwa sasa Kaamua kufunguka

 
MSIKILIZE HAPA CHINI AKIFUNGUKA

HABARI NA DJ HAAZU MJ RADIO 93.0 FM ARUSHA

TID ALITOLEA UVIVU GAZETI LA BABKUBWA KWA UWONGO. SOMA HAPA ALICHOKIANDIKA

Katika hali isiyo ya kushangaza msanii TID amefunguka kupitia ukurasa wake wa facebook na kuonekana kukerewa na gazeti la Baabkubwa na kuandika kifuatacho
Hahahaha jamani acheni kumuudhi TID na Ramadan yote hii. Kama mnataka ukweli mfateni atawaeleza na si kumzushia kama mwenyewe anavyo dai.

Mfahamu Director wa Video aliyehukumiwa kifungo cha miaka 90 gerezani kwa kuwabaka watoto wake

aswad 
Director wa Video Aswad Ayinde amehukumiwa kifungo cha miaka 90 gerezani kwa kosa la kuwabaka watoto wake mwenyewe na kuwazalisha watoto katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 iliyopita .
Aswad mwenye umri wa miaka 55 alipewa hukumu hiyo hapo jana huko Marekani baada ya mahakama kumkuta na hatia ya makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wake mwenyewe.
Aswad alikuwa na tabia ya kuwabaka watoto wake ambapo aliwazalisha watoto kadhaa huku mwenyewe akisema kuwa alifanya hivyo ili kuweka damu yake karibu .

Mke wa Aswad ambaye alikuwa mmoja wa watu waliotoa ushahidi dhidi ya director huyo Beverly Ayinde amesema kuwa baba yao aliwalazimisha mabinti zake kufanya nao mapenzi na kuwazalisha watoto ambao alihakikisha wanazaliwa chini ya uangalizi wake na hawakuruhusiwa kusoma shule za kawaida ambapo walifundishiwa nyumbani.
Beverly anasema kuwa aliogopa kuripoti vitendo vya mumewe kwa kuwa alikuwa akimtishia yeye na wanawe uhai wao na alikuwa akiwanyanyasa kwa kuwapiga .
Waendesha mashtaka wamedai kuwa Aswad alianza kufanya ngono na mtoto wake mkubwa wakati akiwa na umri wa miaka nane na alimpa mimba mara nne huku akijifungua watoto mara zote nne.
Aswad anakumbukwa kwa video ya kundi la Hip-Hop la The Fugees ambao aliwatengenezea video ya wimbo wa Killing Me Softly na kupata tuzo ya Video Bora ya MTV  mwaka 1996.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/07/mfahamu-director-wa-video-aliyehukumiwa.html#ixzz2aahTADLZ

MWANAFUNZI WA KITANZANIA AUNDA NDEGE YA ABIRIA SHUHUDIA HAPA

Picha ya ndege inayoundwa na kijana, Denis
Kijana wa Kitanzania ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Arusha aitwaye Denis, amefanikiwa kuunda ndege ya abiria. Kijana huyo alianza kuiunda ndege hiyo zaidi ya miezi mitatu iliyo pita na sasa ipo katika hatua za mwisho kabla hajaifanyia majaribio.
Hii ni mara ya pili kwa kijana huyu kuunda ndege baada ya kufanya majaribio mengine huko mkoani Mara ambayo yalikuwa na matunda mazuri. Ndege inayo endelea kutengenezwa na kijana huyu ipo katika eneo la Chuo kikuu cha Arusha kilichopo katika mji mdogo wa Usariver karibu na hifadhi ya wanyama ya Arusha (Arusha National Park).
Endapo majaribio ya Denis yakifanikiwa basi atakuwa ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania na Africa kwa ujumla. Ni wito wangu kwa Serikali na taasisi binafsi kujitokeza na kumuunga mkono kijana huyu katika majaribio haya makubwa na yakimapinduzi.
 
 

ANGALIA PICHA JIDE NA MUMEWE GADNER WAKIWA MAHAKAMANI KUSIKILIZA KESI YAO LEO


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.
Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.

Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/07/angalia-picha-jide-na-mumewe-gadner.html#ixzz2aYMg3cyr

MAAJABU YA MWAKA..HIVI NDIVYO KABULI LILIVYO FUKULIWA NA MAITI KUIBIWA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, familia ya Said Abdallah inayoishi Buguruni jijini Dar es Salaam imelazimika kutokwa machozi upya baada ya maiti ya mtoto Sophia Said
(1) aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria, kuibwa na watu wasiojulikana na kaburi lake kuachwa wazi, Uwazi limechimbua.
Kaburi alipozikwa mtoto Sophia Said likiwa wazi.
Tukio hilo la aina yake na lililoacha maswali mengi, lilitokea usiku wa Julai 20, 2013 kwenye Makaburi ya Buguruni Kwamkanda, Mtaa wa Mnyamani jijini Dar es Salaam. Marehemu alizikwa Juni 20, 2013.
Uwazi lilifika eneo la tukio na kukuta umati, ikiwemo familia ya Said ukitokwa machozi huku wakiliangalia kaburi hilo likiwa wazi.
Mbao na miti iliyotumika kwenye mazishi ya mtoto huyo vilikutwa pembeni ya kaburi.

Wananchi wakishangaa tukio hilo.
Wakati watu wakiendelea kumwaga machozi huku wakiulizana nini maana ya tukio hilo, Said ambaye ndiye baba mzazi wa marehemu alifika na kushuhudia maajabu hayo ambapo naye alishindwa kujizua na kuanza kulia.
Baada ya hali kutulia kidogo, mwandishi wetu alihojiana na mfiwa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nashindwa hata kuelezea vizuri kwani tangu nizaliwe sijawahi kuona kaburi limefukuliwa, maiti haipo na isijulikane ilikopelekwa.
“Nikiwa kazini muda si mrefu uliopita nilipigiwa simu na shemeji yangu Said Masoud ambaye anaishi maeneo haya, akaniambia kaburi lipo tupu na haoni maiti ndani yake.
“Akasema mbaya zaidi, mbao na miti iliyotumika siku ya mazishi viko pembeni kuashiria kwamba waliofanya kitendo hiki ni watu waliokusudia.
“Niliishiwa nguvu, baadaye nilijikaza na kuja hapa. Ndiyo nimefika kama hivi na kukuta watu wengi nao wanashangaa. 
“Nilipochungulia kaburi niliona ni kweli lilibaki tupu. Marehemu alikuwa ni mtoto wangu wa kwanza, niliwazaa mapacha na kwa sasa amebaki mwenzake aitwaye Salah.
‘Kinachonishangaza ni kwamba, marehemu tulimzika Juni 20 na kaburi limefukuliwa Julai 20, ina maana ni mwezi mmoja umepita.
“Sijajua kwa nini imetokea hivi! Mpaka sasa hakuna mtu ninayemshuku kuhusika na tukio hili, inawezekana ni mambo ya kishirikina, nakwenda kutoa taarifa polisi na kisha tutarudishia mchanga kaburini.
“Kusema ule ukweli inauma sana jamani! Mwanangu yuko wapi? Hata kama ni marehemu lakini nijue alipo.”
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnyamani, Jabir Sanze ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alipoulizwa na mwandishi kuhusu kitendo  hicho, alisema:
“Hili ni tukio la ajabu, polisi wanahaha kutafuta maiti na wanafanya uchunguzi wa kina kwani tukio hili linaonekana halikufanywa na mtu mmoja.”

KUMFANYIA MWENZI WAKO KITU HIKI NI HATARII SANA..MWANAUME AKATWA ULIMI NA MKEWE KISA WIVU HUKO -NGARA

Bw.Anord Nyabenda akionesha Ulimi wake namna ulivyokatwa kwa meno na mkewe. Imeelezwa kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi kati yake na mkewe. Hadi sasa mwanamke hajafika Hospitalini alikolazwa kwa matibabu ili kujulia hali mwenzake.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA IDD AZAN AFUNGUKA: “WANACHAMA WA CCM WANANICHAFUA”


Siku chache zilizopita mbunge wa Kinondoni Mh Idd Azan aliandikwa kwenye vyombo vya habari tofauti tofauti kwamba 
anajiusisha na madawa ya kulevya.
Chanzo za tuhuma hizo ni barua iliyoandikwa na mtanzania aliekamatwa huko china kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya. Ndani ya barua hiyo Mh Idd Azan alitajwa kama kigogo ambaye anashughulika na biashara ya madawa ya kulevya. 
Siku ya jana Mh Idd Azan alifanya mahojiano na radio ya Clouds Fm na kusema kwamba tuhuma hizo ni za uwongo na hiyo barua pia ni ya uwongo.
Mh Idd Azan aliendelea kwa kusema kwamba wanachama wa CCM wanajaribu kumchafua kwa sababu wanajua uchaguzi unakaribia. Idd Azzan aliwataka wananchi wote wa kinondoni kutozitilia maanani habari hizo potufu zisizo na misingi yoyote.