Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Tuesday, December 17, 2013

WEMA JEURI YA FEDHA KWISHA!

Wema Isaac Sepetu.
Stori: Oscar Ndauka na Richard Manyota
NI kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani, Risasi Mchanganyiko limepashwa ‘ei tu zedi’.

Baadhi ya magari anayomiliki Wema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda kujirusha kama zamani.

SABABU NI NINI HASA?
Chanzo kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.
Wema akiwa ofisini kwake.
Inadaiwa kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa kutoka kazini.

MKONO WA MKEWE WATAJWA
Katika madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.
Wema akiwa ndani ya nyumba aliyodai yake.
KILICHOTOKEA SASA
Chanzo kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha, mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu (juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”

INADAIWA AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana, Wema aliamua kuuza magari mawili kati ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya kila siku.
Magari hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.

YALIYOMPATA CLEMENT
Habari zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.
Benki hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa ‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye marejesho.
Madai mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa rafiki zake.

WEMA ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa 4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, gazeti hili liliamua kumwendea hewani meneja wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.
Risasi Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala hilo. Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi  (hakusema hospitali gani) yuko nyumbani.”
Mapaparazi wetu wakafunga safari kutoka Bamaga – Mwenge, Dar yalipo Makao Makuu ya Nyumba ya Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni Kijitonyama).
Getini alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au kumwambia kuna waandishi wa Global wapo nje, alisema:
“Mh! Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda si mrefu.”
Alipochombezwa kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe, alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.

WEMA ATUMIWA MESEJI
Baada ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi (SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema, lakini pia haikujibiwa.

TUNARUDI KWA CLEMENT  
Simu yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema lolote kuhusu sakata hilo.

MKE WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu hilo la nyumba ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.
“Unajua ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.

KUHUSU KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu hapa mke wa Clement: “Hilo si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe mimi kwa lolote lile.”
KUHUSU KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda huo alikuwa akidraivu.

PRODYUZA WA WEMA ALIJUA HILI?
Wiki mbili zilizopita, gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI.
Katika habari hiyo, Wema alidaiwa kumtimua kazi prodyuza wake katika Kampuni ya Endless Fame, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ kwa sababu ya kumtuhumu kufanya ufuska kwenye magari yake maeneo ya Ufukwe wa Coco, Dar.
Siku chache mbele, prodyuza huyo alifunguka katika gazeti lingine pendwa ndani ya mjengo, Amani kuwa, Wema ‘amechoka’ siku hizi, halipi mishahara wafanyakazi wake na alitaka yeye awe kuwadi ndiyo wangeendana jambo ambalo yeye hakuwa tayari.
Baadhi ya habari zilizowahi kuandikwa na magazeti ya GPL kuhusu jeuri ya fedha ya Wema.
HABARI NYINGINE YA MJINI
Yapo madai kuwa, kutokana na maswahibu hayo ya kuwa kwenye wakati mgumu kifedha, kampuni yake imeanza kudoda na mbaya zaidi, marafiki zake anaokuwa nao kwenye raha, wamemkacha na kumwacha akihangaika mwenyewe.
“Msiniandike gazetini lakini ukweli ni kuwa, huu ndiyo wakati wake wa kujifunza kuchagua marafiki. Ona sasa, wale wote aliokuwa akila nao raha, wamekaa pembeni. Ni tatizo sawa, lakini pia ni funzo kwa upande mwingine,” alisema mpambe mmoja anayefanya naye kazi kwa karibu sana.

chanzo: www.globalpublishers. com

Friday, December 13, 2013

LOWASSA ANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE

 
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
ABIRIA kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua. Matairi yote manne ya nyuma yamepasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao…
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
ABIRIA kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua. Matairi yote manne ya nyuma yamepasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Lowassa ni miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuwania urais 2015 na amekuwa na nguvu kubwa katika harakati hizo.

Sunday, December 8, 2013

WOSIA WA MANDELA WAZUA UTATA

 
Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ au ‘Tata’ (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini.

Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana.…

Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake.
Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ au ‘Tata’ (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini.
Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana.

Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela.
FAMILIA INAVYOTAKA
Habari za ndani zilisema kuwa familia inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile viongozi wa nchi mbalimbali duniani watahudhuria.
“Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani, mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa kawaida,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na Mandela.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia msimamo huo, wapo wanandugu wanaotaka azikwe kama alivyoandika katika wosia wake huo.
SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA WOSIA
Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa kuendelea na maandalizi ya mazishi kama haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya watu nchini humo inaheshimu wosia wa marehemu.
WOSIA UNAVYOSEMA
Mzee Madiba alishauandika wosia huo kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe. Alisema kuwa akifa azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko ‘Sauzi’.

Waombolezaji wakiweka maua katika sanamu la Mandela.
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA
Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari, 1996 wakati bado akiwa rais ambao ulijaa maelekezo yote juu ya mazishi yake. Aliagiza kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni kukiuka wosia wa mzee.
KABURI ALILOLITAKA MANDELA
Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki yake wa karibu, Mzee Madiba aliandika kuwa akifa azikwe katika eneo la familia lenye makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo.
Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia nchi.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
KABURI LISISAKAFIWE
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana, akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano wake barani Afrika kama, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda (aliyekuwa Rais wa Malawi).
WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE MMOJA WA KARATASI
Magazeti ya nchini humo, South African Mail na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa familia ya Mandela akisema: “Madiba hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha fahari wakati wa kumzika.”
Cha ajabu, wosia huo wa Mandela ulitosha kwenye upande mmoja wa karatasi ya kawaida ya kuandikia licha ya kwamba mauzo ya kitabu chake cha Long Walk to Freedom na michoro yenye jina lake vilimpatia mamilioni ya fedha.

Nelson Mandela (kulia) akiwa na Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wao.
FAMILIA YACHUKIZWA NA WOSIA
Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika kulingana na uwezo wake.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, suala hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake akiwemo yule mjukuu wake ambaye ni chifu, Mandla Mandela aliyewahi kufikishwa kortini kwa kuhamisha makaburi hayo ya ukoo na kuyapeleka sehemu nyingine. Pia ndiye msemaji wa familia ya Mandela.
DUNIA YAMKATALIA
Baadhi ya wanaharakati ulimwenguni kote walisema wosia huo unapingana na matakwa ya dunia nzima, ambapo walitaka maziko ya mzee huyo yawe  makubwa na ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea.Ilifahamika kwamba dunia inataka mazishi hayo yavunje ile rekodi iliyoshikiliwa na mazishi ya Papa John Paul II aliyefariki dunia Aprili 2, 2005.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.
SAFARI HII HAKUKIMBIZWA HOSPITALI
Mzee Madiba ambaye alitimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, alikuwa hospitalini kwa karibu miezi  mitatu nyuma akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine. Baadaye alipata nafuu na kurudishwa nyumbani ambako usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita aliugua ghafla na kufariki dunia.

chanzo. GPL

Tuesday, November 26, 2013

Diamond Aumbuka baada ya kudai alihudhulia harusi ya Peter Okoye wa P square huu ndio ukweli wake


Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja afrika, Aliko Dangote.
Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi yake.
hapa diamond akicheza ngololo kwenye part hiyo
Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?

Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani.

Friday, November 22, 2013

BABU SEYA ALIA DUNIA HAINA HURUMA

Stori: Richard Bukos
Hukumu iliyokaziwa na Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam, juzi (Alhamisi), ikipigilia msumari adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya mwanamuzi mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesababisha maumivu makali kwa wahusika.
                                 Mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Uthibitisho wa hilo unatokana na kauli ya Babu Seya, aliyoitamka mahakamani akimnong’oneza Papii Kocha, akisema: “Kweli hii dunia haina huruma, hukumu hii imeniuma sana kuliko zote ambazo zimetangulia.”
Akizungumza kwa upole kwa sauti ya majonzi, huku sura yake ikionesha dhahiri kutokuwa  na furaha, Babu Seya aliendelea: “Kinachoniuma zaidi ni wewe, nakusikitikia sana, wewe ni kijana mdogo ambaye ulipaswa kuwepo uraiani ukitimiza ndoto zako na ukiisadia nchi yako.
...Akiwa katika huzuni na majonzi makubwa.
“Ndoto zako zimeishia hapa. Tumejitahidi sana kukwepa hiki kifungo lakini imeshindikana, wewe unajua.”
Hata hivyo, wakati akitoka nje ya ukumbi wa mahakama, Babu Seya alimweleza mwandishi wetu: “Hili jambo sijalifanya, nitaendelea kupambana mpaka mwisho.”

NI HUKUMU YA MWISHO
Msajili Mwandamizi wa Mahakama, Zahra Mruma, akisoma hukumu  hiyo alisema: “Ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao ni Jamhuri, umeendelea kuwa na nguvu, kwa hiyo vipengele vya utetezi vilivyowasilishwa na mawakili wa utetezi vimekosa nguvu ya kutengua hukumu ya awali.”
...Ndugu na jamaa wakiangua kilio baada ya hukumu.
Zahra, alisoma hukumu hiyo kwa niaba ya jopo la majaji watatu ambao waliipitia upya hukumu hiyo, baada ya mawakili wa utetezi, Mabere Marando na Gabriel Mjele, kuomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya mwisho, baada ya kutokuzikubali zote zilizotangulia.
Mawakili wa upande wa utetezi, walitaka mapitio hayo yafanyike kwa hoja kwamba haiingii akilini kwa Babu Seya na mwanaye kushiriki tendo la mapenzi kwa pamoja, tena kwenye nyumba wanayoishi.
Hoja hiyo ilishibishwa na maelezo kuwa Babu Seya na Papii ni Waafrika, kwa hiyo kitamaduni haiwezekani kushiriki mapenzi kwa pamoja.
Utetezi mwingine ni kuwa nyumba ya tukio ni ya kifamilia, kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa tendo husika kutendeka, maana wengi wangekuwa wanashuhudia.

KESI YA MSINGI
Babu Seya na Papii, walishtakiwa na baadaye kukutwa na hatia ya kuwabaka, kuwalawiti na kuwaambukiza Virusi Vya Ukimwi, watoto nane, wenye umri wa kati ya miaka saba na sita.
Mahakama ilielezwa kuwa Babu Seya alikuwa akiwaita watoto hao na kuwanunulia pipi kisha kuwaingiza ndani ambako waliwaingilia kwa zamu na baada ya kitendo, waliwapa mgao wa kati ya shilingi 100 na 150.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na mwaka 2004, hukumu ilitolewa, ikiwatia hatiani Babu Seya na wanaye watatu na kuwahukumu kwenda jela maisha.
Watoto wengine wawili wa Babu Seya, waliokuwemo kwenye kesi hiyo ni Francis Nguza na Nguza Mbangu ‘Nguza Mashine’ aliyekuwa mpiga drum wa Bendi ya FM Academia, mpaka wakati anaingizwa kwenye mashtaka.
Mwaka 2005, rufaa ya kwanza ilisomwa ambayo ilikazia hukumu ya awali lakini Februari 2010, Mbangu na Francis waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia, huku Babu Seya na Papii, ikipitishwa na Mahakama ya Rufaa kwamba waendelee na kifungo cha maisha jela.

MAJAJI WALIVYOTOA HUKUMU
Zahra, alisema jopo la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Masati na Mbarouk Salim Mbarouk, lilichambua hoja za utetezi na kuona hazina nguvu, kwa hiyo wakajiridhisha kuwa Babu Seya na Papii, wanastahili kuendelea na adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Hukumu hiyo, ilikuwa ni ya rufaa ya nne, lakini imeshindikana kwa kuwaondoa Babu Seya kwenye kifungo.

MAWAKILI WASALIMU AMRI
Mmoja wa  mawakili wa utetezi, Mjele, alisema kuwa hukumu hiyo ndiyo ya mwisho na kwamba wao hawana njia nyingine ya kukata rufaa kisheria.
“Hatuna njia nyingine, hapa ndiyo mwisho,” alisema Mjele na kuongeza: “Labda tusubiri msamaha wa rais kwa sababu ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutengua hii adhabu.”

RAIS AZIDI KUTUPIWA MZIGO
Watu kadhaa waliohudhuria mahakamani juzi, waliungana na Wakili Mjele kwamba kesi hiyo iachwe mikononi mwa rais kwa sababu ndiye mwenye nafasi ya kufanya lolote katika kesi hiyo kama anavyoruhusiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mahakama imefanya kazi yake, mawakili wa utetezi wamejitahidi lakini imeshindikana, sasa hatutakiwi kuijadili sana hukumu, badala yake tumuachie rais kwa sababu ndiye mwenye mamlaka,” alisema Fredrick Mwaluwanda wa Kinyerezi.
Mosha Kabogo alisema: “Katika hukumu hii, kila mmoja anaweza kuwa na hisia zake, jambo la msingi ni kumuacha rais afanye anachoona kinafaa. Uzuri ni kwamba siyo rais wa sasa peke yake, kwani hata ye yote anayekuja, anaweza kutumia mamlaka yake kikatiba kuwaachia huru au kuwapunguzia adhabu.”

WANAMUZIKI WAANDAA UJUMBE KWA RAIS
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, alisema mahakamani hapo kuwa anakusudia kuitisha kongamano la wanamuziki halafu watafanya mkutano na waandishi wa habari kumuomba rais awaachie huru Babu Seya na Papii.
“Hili suala linauma sana, hatuwezi kukaa kimya tukiwaacha wanamuziki wetu nyota wakienda na maji. Lazima tufanye kitu na tutakachofanya  ni kujikusanya na kuandaa mkutano wa waandishi wa habari ambao tutautumia kutuma ujumbe kwa mheshimiwa rais,” alisema Dully.

PAPII NI WA KUMJADILI KIDOGO
Papii Kocha, wakati alipoingia kwenye mashtaka hayo, alikuwa ni kijana mdogo ambaye nyota yake kwenye muziki ilikuwa inang’ara kwa kiwango cha juu sana nchini Tanzania.
Alifanya vizuri sana akiwa na Bendi ya FM Academia na Tot Plus kabla ya kutoka na albamu yake binafsi iliyokuwa na nyimbo nyingi kama vile Salima, Fanta na Seya ambayo uliimbwa mithili ya wimbo wa taifa.
Alitabiriwa kwamba angeweza kuendelea kufanya vizuri kutokana na uwezo aliokuwa nao lakini nyota yake ilizimwa na kesi hiyo.
Kwa upande wa Babu Seya, ni nguli aliyejenga jina na heshima kubwa nchini kupitia muziki wake, huku akipigiwa mfano kama mpiga solo bora kabisa, lakini historia yake imehitimishwa kwa kifungo cha maisha jela.

TAZAMA VIDEO YA SNURA "NIMEVURUGWA" UONE JINSI SNURA ALIVYOVURUGWA HUMO NDANI, MAUNO MWANZO MWISHO..!!

snura 234 
August 2013 ndio Snura aliishusha single yake ya ‘nimevurugwa’ kwenye radio za bongo ikiwa ni miongoni mwa single zinazopata airtime bila kuwa na video lakini leo November 22 2013 kaishusha video on AyoTV… itazame hapa chini na uache maoni yako mtu wangu, atapita hapa baada ya saa 6. Snura alisema kwenye video ya ‘majanga’ hakuweza kucheza kama inavyotakiwa lakini huku kwenye ‘nimevurugwa’ ndio kajiachia.

Monday, November 18, 2013

Pichaz kutoka Club Bilicanas kwenye usiku wa ‘Ay road to #CHOAMVA’ @AyTanzania

20 
Wakati Watanzania wakiendelea kupiga kura kwa Mtanzania pekee alietajwa kuwania tuzo za Channel O 2013 (Ay) , usiku wa November 17 2013 kulifanyika party club Bilicanas Dar es salaam (AY Road to CHOAMVA 2013) ambapo mastaa kadhaa walionekana kwenye stage kumpa support Ay.

Kumpigia kura Ay unaweza kutembelea www.channelo.com au piga kura kwa Best Gifted male video: sms 1D kwenda +2783142100415 na kwa Best gifted East video: sms 12D kwenda +2783142100415.
1 
Watu wa nguvu kama kawaida walijitokeza.
2 
Rapper Stereo, Wakazi na mtu wa nguvu
3
4 
Dee Andy kutoka XXL ya Clouds FM, Reuben Ndege (Ncha Kalih) na Shadee kutoka @Clouds_TV
5 
B12 kutoka XXL ya Clouds FM, FidQ na Sajjo.
6 
Brothers wameshow love kwa Ay
7 
Young Dee na watu wa nguvu
8 
Jokate na Young D
9 
Hawa Warembo ni miongoni mwa waliofungua show
10
11
12 
Stere.
13
14 
Godzillah
Ommy Dimpoz kazini
16 
Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee
17
18
19
21
22 
T.I.D na Ommy Dimpoz
23
24 
Fid Q na shabiki
25
26
27 
Ikafika zamu ya AY.
28
29
30
31