Lamborghini ‘Veneno’ kuuzwa kwa watu 3 tu duniani @ zaidi ya Tshs bilioni 6.
Katika
kuadhimisha miaka 50 ya uzalishaji, watengenezaji wa magari ya
kifahari duniani ya Lamborghini wa nchini Italia wametengeneza toleo
jipya la magari hayo liitwalo Veneno, ambayo itauzwa dola milioni 4
(zaidi ya shilingi bilioni 6 za Tanzania) kwa watu watatu tu duniani
ambao tayari walishalipia hata kabla haijatengenezwa.
Gari hizo tatu zitakuwa na rangi nyekundu, nyeupe na kijani kufanana na rangi ya bendera ya Italia.
No comments:
Post a Comment