Maisha yetu wengi ni ya mikiki mikiki ya hapa na pale ya kutafuta..nimekuwa bize mwaka mzima ..lakini siku yangu ya leo baada ya Swalt Ijumaa niliitumia
kujumuika na watoto waishio kwenye mazingira magumu kilichopo
Buguruni ambapo nilipata wasaa wa ..kula nao pamoja ,kucheza..kubadilishana mawazo. lakini pia kutumia nafasi hiyo kuwaonyesha kwamara ya ,kwanza kabisa,video yangu ya number 1 remix
niliyoifanya na Davido .nimefanya hii kwasababu ,hawa ndio mashabiki wetu wakubwa.mara nyingi show zetu tunafanya usiku..mda ambao watoto
hawaruhusiwi na ukizingatia watotot hawa ,wanaishi katika mazingira ambayo hawawezi kuhudhuria maonyesho yetu hivyo leo nimeamua kwa mara ya kwanza niwaonyeshe wao kwanza,kabla sijaisambaza kwa wananchi wote...lingine la mhimu ni kwamba..mwezi huu tarehe
25..nimeandaa onyesho maarum pale Readers
club kwa ajili ya watoto wote ambao
kawaida hawapati nafasi ya
kuhudhuria,show zetu za usiku na nimetoa
complimentary 50 kwa hawa watoto niliokuwa nao leo ...
Cha kukumbushia tu ni kuwa..zoezi hili ni
endelevu..nitaendelea kutembelea
maeneo mbali mbali kutoa sadaka kwa
watoto wenye mazingira magumu
lakini pia nitoe wito..kwa yeyote
atakaye wiwa kufanya nami zoezi hili..anakalibishwa kuungana nami..
Wasiliana nasi kupitia0715333346.
Mama na Anko wakiwa mtaani kununua zawadi
Baada ya kuwasili tukishusha zawadi mbali mbali tulizoandaa
Wadogo zangu wakiniskiliza kwa makini wakati nikizungumza nao machache
Mama mlezi wa kituo
Babu Tale alikuwepo pia
Mkubwa fella pia
Mama yangu pia alipata nafasi ya kuzungumza
Tukila pamoja,tukitaniana,kubadilishana mawazo..pia kushauriana
Nikitoa mausia kwa wadogo zangu jinsi ya
kupambana katika maisha pasipo kukata tamaa