Vurugu
,matusi na lugha za kejeli ni miongoni kati ya mambo yaliyotawala semina
ya wabunge kuhusiana muswada wa sheria ya kutambulika hukumu
zitakazokuwa zikitolewa na mahakama za kadhi hapa nchini wa mwaka
2014/2015.
Ni sehemu
ya hali ilivyokuwa wakati wabunge waliposhindwa kuvumuliana na
kuheshimiana walipokuwa wakichangia mara baada ya Jaji Robert Makaramba
alipowasilisha mada kuhusiana na muswada huo hali iliyolazimu ulinzi
kuimarishwa ndani ya ukumbi huo kwa hofu kwamba huenda waheshimiwa
wabunge hao wakatwangana makonde na ndipo semina ilipoendelea.
Mbunge wa kuteuliwa, Kassim Issa mbunge baraza la wawakilishi,
Dakika
chache baadaye ikafika kipindi cha kila mtu kumtafuta mbaya wake ama
suluhu ya anachokiamini huku lugha za kutishana zikitawala.
Wakihitimisha
semina hiyo muwasilisha mada Jaji Robert Makaramba pamoja na Waziri
mkuu Mh.Mizengo Pinda wamesema ujumbe umefika na mapungufu yaliyoonekana
yatafanyiwa kazi.
Chanzo:ITV.