Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Saturday, October 6, 2012

HII NDO TICKET YA FIESTA 2012 ZINAPATIKANA KATIKA MADUKA YA ROBBY ONE FASHION

MI KAMA BLOGGER NSHACHKUA YANGU WEWE UMEKAA UNASUBIRI NINI CHANGAMKA BADO HUJACHELEWA....!!!!

KAMA ULIKUA UJAONA PIC ZA RICK ROSS ALIVYOTUA BONGO JANA, ZIANGALIE HAPA.

                     

Rick ross akitoa saluti kwa mashabiki wake baada ya kuwasili katika kiwanja cha Airport jijini Dar es Salaam kwa kupiga show yake kali ya Serengeti Fiesta pale maeneo ya Leaders Club.
Rozay akiwa na Meneja wa prime Time promotion huyu si mwingine anajulikana kwa jina la Balozi kindamba hapo walikuwa wakielekea katika gari ambalo atapanda mtu mzima Rick ross mpaka katika Hotel ya kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko.
Hapo wakazi wa Dar es Salaam wakimuangalia mtu mzima Rick ross baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Airport.

Hapo mtu mzima Rozay akiwa na Dj wake katika gari wakipelekwa katika ya Hotel inayofahamika kwa jina la kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko.
Hapo Rick ross akiwa katika  msafara wa magari akipelekwa katika Hotel ya kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko.
Rozay akiwa amewasili katika hotel ya kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko na watu wake aliokuja nao kutoka pande za state wakiwa wanatoa mizigo katika gari.
Muonekano wa The boss baada ya kuwasili  katika hotel ya kilimanjaro kwa ajili ya mapumziko
Hapa Rick ross akiwa ndani ya lift akielekea juu kwa ajili ya mapumziko baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana usiku huu.
             Hii ndiyo hotel ambayo mtu mzima The boss ndiyo dzain amepumzika hapo kwa jili ya show yake ya Serengeti Fiesta ddaaaaaaaaaaaahh!!!!!!! bhhaaaaasss!!!! kwelli muonekano mpya,burudani ile ile

Thursday, October 4, 2012

YANGA NA SIMBA HIKI NDICHO KIASI KILICHOPATIKANA JANA UWANJA WA TAIFA.

                                                                 Release No. 161

                                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
                                                               Oktoba 4, 2012 

                                 PAMBANO LA YANGA, SIMBA LAINGIZA MIL 390/- 

Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,

Wednesday, October 3, 2012

chumba cha habari cha tff kilivyo hoi bin taaban

Pichani ni sehemu ya paa la chumba cha habari cha chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF),ambacho kinatumika kukutana na Wanahabari wa vyombo mbalimbali  kuhusiana tasnia ya michezo kwa madhumuni ya kuihabarisha jamii.Kwa wanahabari za Michezo naamini kabisa mtakubaliana na mimi kuhusiana na hali iliyopo ndani ya ofisi hiyo,ambayo kimsingi nayo una umuhimu wake mkubwa,lakini imetelekezwa kama hivyo.

CHINA YAMSHTAKI OBAMA...



Kampuni moja ya Marekani inayomilikiwa na Uchina imemshtaki Rais Barrack Obama kwa kuizuia kununua mashamba manne. 

 Mashamba hayo yaliyopo karibu na kambi ya Wanamaji katika eneo la Oregon, yalipangiwa kutumika kuzalisha kawi ya upepo .

 Kampuni hiyo, Ralls Corporation, inasema ni kinyume cha sheria na maonevu kwa Obama kutoa uamuzi wa kuizuia kununua mashamba hayo wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama. Kambi hiyo ya Wanamaji inatumika kufanyia majaribio ndege zisizo na marubani. 

Shirika la habari la Uchina limesema uamuzi huo wa Obama unahusiana zaidi na Uchaguzi wa Marekani kuliko masuala ya kiusalama. Hii ni mara ya kwanza kwa Mwekezaji wa kigeni kuekewa kikwazo nchini Marekani katika muda wa miaka 20.

                  Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

MTOTO ANAYEKADIRIWA KUWA NA MWEZI MMOJA AKUTWA AMETUPWA

 Msamaria mwema aliyrfahamika kwa jina moja Lina akiwa amembeba mtoto ambaye alikutwa ametupwa katika bomba la Nyumba moja wilayani Sengerema.
                                     Mtoto ambaye alitupwa akionekana katika picha..
 Umati wa watu waliofika kwenye tukio la utupwaji wa mtoto mchanga wakishangaa sana kutokana unyama huo ambao haukubaliki kwa jamii ya Kitanzania.
                              Sura ya Mtoto aliyetupwa kama inavyoonekana pichani.

MTOTO mchanga anayekadiliwa kuwa na umri wa mwezi mmoja amekutwa ametupwa kwenye boma la nyumba moja iliyopo katika kata ya Ibisabageni wilayani sengerema mkoani mwanza.

Tukio hilo limetokea jumatatu majira ya asubuhi katika kata hiyo ambapo mtoto huyo amekutwa ametupwa na msamalia mwema ambaye ni mtoto aliyefahamika kwa jina la KUBUNGA na kuamua kutoa taarifa kwa ndugu jamaa na ndipo walipofika eneo la tukio.

Akielezea kuhusu tukio hilo amesema kuwa wakati anapita eneo hilo alisikia sauti ya mtoto ikilia  na ndipo aliposogea karibu na kukuta mtoto huyo mchanga akiwa amelazwa chini.

Naye Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw. JAPHET MASHALA  ambaye alikuwepo eneo la tukio amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuwaomba wananchi kuwa na moyo wa ubinadamu wa kuthamini maisha ya wengine kwani mtoto huyo hana hatia yoyote.

Hata hivyo mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio juhudi za kumtafuta aliyetenda unyama huo zilikuwa zinaendelea ili kumfikisha katika vyombo vya dola. Chanzo: B Plus Blog

Tuesday, October 2, 2012

YUNG OMEGA YUKO MBIO KUKAMILISHA VIDEO YA NGOMA YAKE YA "parry people"


Yung Omega ambaye anafanya vizuri kwa style ya miondoko ya ragge ilivyo tofauti na wasanii wenzake wa wanaotokea A.Town, Omega amefunguka na the HOOD infotainment na kusema kuwa, ngoma yake iko mbioni ya parii people, yuko mbioni kuanza kushot nchini ya Producer Isaack Chiwanga katika Studio ya Multmedia Production na kuwaambia  mashabiki wake wakae tayari kupokeo video yake hiyo mpya,
kwa mara ya kwanza ngoma hiyo utaiona hapahapa kupitia blog hii.
huyu ndie producer atakae simamia mchakato mzima kuanzia location, shooting, editing mpaka ngoma hiyo ikamilike chini ya multmedia production. Mr Isack Chiwanga

AJALI MBAYA IMETOKEA MUDA SI MREFU ENEO LA MBALIZI MBEYA, MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO . WATU KUMI WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO.

 
 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI
 HIVI NDIVYO GARI HILI LILIVYO PINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI


 HII NI GARI NYENGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA 
 FIRE WAKIWA WAMEWAHI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO

 ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKA ENEO LA TUKIO AMBAPO MAGARI HAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.

 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI
 HUU NDIO MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE
 HAYA NI MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE

WANANCHI MBALI MBALI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA WALIO PATA AJALI

KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU. PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWAALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYO UNGUWA MOTO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO HUO. HABARI KAMILI BAADA

Saturday, September 29, 2012

ALICHO KIANDIKA DIAMOND KATIKA WEBSITE YAKE KUHUSIANA NA BRITHDAY YA WEMA SEPETU



Mwaka 1990, mwezi na siku kama ya leo Mrs. Abraham Sepetu ama (Mama Sepetu) alipata bahati ya kujifungua mtoto wa kike ambae alimtunuku jina la Wema Abraham Sepetu, Mtoto ambae Nyota yake ilianza kama masihara tu pale aliposhinda taji la Miss Tanzania 2006, kisha baadae kuingia katika Muvie Industry kama utaniutani vile na ghafla kuwa DIVA wa Tasnia hiyo, na licha tu ya udiva pia kuwa ICON wa Tanzania.Siku hii ya leo ya tarehe 28/09/ anazaliwa upya na kutimiza miaka 22.
the HOOD infotainment inakutakia maisha marefu na yenye baraka

Friday, September 28, 2012

STR8MUZIK Free Style 2012 zang’ara Mwanza

Mmoja wa wanakundi cha waburudishaji cha BFB cha mkoani Mwanza akifanya vitu vyake katika mpambano wa kusaka ma-MCs na DJs wa STR8MUZIK Freestyle 2012 mkoani Mwanza uliofanyika katika ukumbi wa Stone mjini humo jana usiku.

RICK ROSS KUPANDA JUKWAA LA SERENGETI FIESTA, OKT 6

  Msanii nyota kutoka nchini Marekani, mzaliwa wa nchini  Marekani, anayetambulika kwa jina la kisanii kama Rick Ross, ambaye kwa jina halisi anajulikana kama William Leonard Roberts II, anatarajia kutua nchini Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kushiriki kikamilifu kushambulia jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, litakalofanyika Oktoba 6 ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa bin sawia kwa kila idara kuhusiana na tamasha hilo, waandaaji ambao ni Prime Time Promotions Ltd wakishirikiana na Clouds Media Group huku mdhamini wao mkubwa ikiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti,wameandaa shamara shamra mbalimbali za kuhakikisha tamasha hilo mpaka linafika kileleni,linaamsha na kuacha gumzo la kipekee kabisa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake, ikibidi mpaka Kigoma mwisho wa reli kwa namna moja ama nyingine.

Msanii huyo mwenye umahiri mkubwa wa kufloo awapo jukwaani mpaka sasa anatamba na nyimbo/albamu kadhaa kama vile  Hold Me Back 2012 God Forgives, I Don't, Hustlin' 2006 Port of Miami Diced Pineapples 2012 God Forgives, I Don't So Sophisticated 2012 God Forgives, I Don't 911 2012 God Forgives, I Don't Stay Schemin 2012 Rich Forever Aston Martin Music. 

Nyinginezo ni  2010 Teflon Don DJ Khaled 2008 Trilla Lemme See 2012 So Sophisticated Amsterdam 2012 God Forgives, I Don't Black Magic 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire The Boss 2008 Trilla You the Boss 2011 You the Boss Touch'n You 2012 Touch'N You Bag of Money 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire.

Wednesday, September 26, 2012

VITUKO VYA BEYONCE WA TANZANIA......

 Huyu ndio beyonce wa tanzania kwajina halisi anajulikana kama mwanaisha idd,ana watoto wawili mapacha wa kizungu .

Anaishi msasani,hana simu na wala hajawahi kumiliki simu hapendi kwasababu kila mara anajikuta akipoteza akiwa na simu, pia hajawahi kwenda club yoyote zaidi ya NEW MAISHA CLUB,

"Maisha ndio home hata nikiumwa nakuja kulala hapahapa au kunywa dawa hapahapa sijawahi kukosa new maisha club napaona kama nyumbani,hata baba watoto wangu nilikutana nae new maisha club."

 Miss triity live na beyonce wa tanzania kwenye stage

 Mashabiki wakicheza na miss trinity na beyonce kwenye stage

 Miss trinity akimshangaa beyonce wa tanzania

Hapa akitoa style zake zakujikunja kama kinyonga