Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Saturday, May 11, 2013

HIZI HAPA PICHA RASMI ZA MAZISHI YA DEVID RIMISHO



Mwili wa Devid Rimisho ukihifadhiwa  katika makazi ya milele

Mwili wa Devi Rimisho ukiwa Unawekwa Tayari kwa kusafirishwa kuelekea Rombo.

Baadhi Ya waombolezaji ambao pia ni waandishi wa habari na watangazji na pia waliwahi kusoma na marehemu wakijadiliana jambo kabla ya safari kuanza ya kusafirisha mwili kuelekea wilayani Rombo.

Mwili wa Devid Rimisho
PICHA HIZO KWA HISANI YA  DOTTO MZAVA na DAVID ERNEO

****************************************************************************


NI MAMAMIA YA WATU HII LEO WAMEFURIKA HUKO MKOANI KILIMANJARO WILAYANI ROMBO  KATIKA MAZISHI YA ALIEKUWA MWANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI  DEVID RIMISHO .AMBAE HII LEO AMEHIFADHIWA KATIKA NYUMBA YA MILELE.
DEVID ALIJIUNGA NA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI AJTC MWAKA 2010 AMBAPO ALIENDELEA NA MASOMO,KATIKA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA AMBAPO WAKATI ANAMALIZIA MASOMO YAKE  KATIKA NGAZI YA DIPLOMA MAY 6 2013 TAARIFA ZILISAMBAA KATIKA MITANDAO NA TOVUTI MBALIMBALI KUWA DEVID HAYUPO TENA DUNIANI "Devid alikutwa mauti ndani ya chumba walichokuwa wamelala na mwenzake amefariki na katika kumchunguza hakuwa na kovu lolote katika mwili wake la kuonyeshwa kupigwa hivyo naweza kusema ni kifo cha gafla." kauli hii imetolewa na mmoja wa watu wa karibu wa familia.

Thursday, May 9, 2013

CHEKI PICHA 40 ZA SHOW KALI ALIYO PIGA DIAMOND HUKO UINGEREZA. ZICHEKI HAPA



Written By Emmanuel Shilatu on Wednesday, May 8, 2013 | 4:32 PM

 KUDADADEKI MDADA HUYU NI HATARIIIIIII" MBUTA NANGA" HABARI ZAKE NITAWALETEENI SOON BAADA YA KUWARUSHIENI MAMBO YOTE YA USIKU WA SHOW YA DIAMOND IN UK'READING PAMOJA NA NEXT DAY AT CROWN PLAZA !









 MBUTA NANGA" MBUZI NI YA NINI KAMA SIYO YA KUKALIWA NA KUKUNA NAZI''



 WEWE CHEKA TU DANCER WETU KWANI KUFANANA NA DIAMOND KUZURI JE"ONA DIAMOND HAPA NA KIFUA CHAKE WAZI YANI FULL TOCHI KUMULIKAAAA''MBUTA NANGA!!









 JAMANI MPENI VIUNGO TARATIBU KWANI ANAWEZA KUZIMIA STAGE BUREE"







KUDADADEKIIIIIIIIIIIIIIII'''NIMT*MBE NANI ''X2 a.k.a. NIMPENDE NANI " HAHAHAAA' WATU WALIANZA KUSEMA WEMAAAAA,WEMA'WEMAAA!!





































 MWAUONA HUO ULIMI,ALAMBA ,ALAMBA TENA''X2'MBUTA NANGA!!

 NILIKUWA NA JIPEPEAJEAJE HAPA BAADA YA JOTO KUZIDI MLE NDANI"







CREDIT TO FLORA LYMO FASHION BLOG

FAHAMU KUHUSU KOCHA ANAYERITHI MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON PALE OLD TRAFFORD .... KOCHA MWENYEWE NI HUYU HAPA


 

Kuna taarifa kuwa mabingwa wa England, Manchester United wameanza mazungumzo na Kocha wa Everton, David Moyes.

 Man United wanataka Moyes achukue nafasi ya Alex Ferguson ambaye ametangaza kustaafu mara baada ya msimu huu kwisha.
Ferguson ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi England, ameamua kutundika daruga zake za ukocha na sasa Man United inaamini Moyes ndiye chaguo sahihi.
Inawezekana kama hawatawezakana, basi mazungumzo yatahamia kwa Jose Mourinho inagawa Man United inaonekana kuhofia tabia ya Mreno huyo ya kutopena katika timu moja.

Imeelezwa Ferguson aliwaeleza wachezaji wake kuhusiana na uamuzi wake wa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu baada ya kuwaalika kuhudhuria mbio za farasi.
Ferguson aliwaalika wachezaji hao na walikuwa wametokelezea katika vazi la suti na mwisho akawaeleza uamuzi wake huo akionyesha hakuwa ametaka kuwashitua sana

ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO


Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.
 ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka. Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.
Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza. “Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo, walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia! Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa. “Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake

 

Wednesday, May 8, 2013

PICHA INAYOHUZUNISHA SANA BAADA YA KUANGUKA KWA KIWANDA CHA NGUO NCHINI BANGLADESH



waathirika wawili wakiwa kwenye kifusi baada ya kuanguka kwa jengo la kiwanda cha nguo Savar, Bangladesh, Aprili 25, 2013. Picha na Taslima Akhter.Picha nyingi poweful zilipigwa baada ya kuanguka vibaya kiwanda hicho  nchini Bangladesh, lakini picha hii imeibuka kama picha inayoumiza sana na kusikitisha na kusababisha huzuni nchi nzima, ukiiangalia tu picha hii moja.