Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, July 1, 2013

HUU ndo UJUMBE MZITO TOKA KWA ZITTO KABWE KWENDA KWA OBAMA


    Obama: Tunataka Uwazi wa Mikataba. Omba radhi Kwa mauaji ya Lumumba

    Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.


    Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa.

    Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
    Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

    Tanzania inapokea kiongozi wa Taifa kubwa duniani wa pili sasa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu. Kwanza alikuja Rais wa China na sasa wiki hii anakuja Rais wa Marekani. Maneno ya mtaani na kwenye mabaraza ya majadiliano ni kwamba viongozi hawa wanakuja kugombea maliasili tulizo nazo kama gesi asilia na madini. Nadhani haya ni maneno ya kusema katika kupiga soga maana kunyonywa kwa rasilimali hakuhitaji Rais wa Marekani aje Tanzania. Makampuni yote makubwa yanayochimba dhahabu hapa nchini ni makampuni ya nje na marais wao hawakuja ili waweze kupata mikataba minono ya kuvuna utajiri wetu. Katika kitalu namba 2 cha utafutaji wa mafuta na gesi huko Bahari Kuu kampuni ya kimarekani ya ExxonMobil ina ubia na kampuni ya Norway ya StatOil. Kampuni hiyo haikusubiri Rais wa Marekani aje ili wapate mikataba.

    Kuna makampuni mengi sana ya kichina yanajenga barabara zetu hapa nchini yakiwa na mikataba minono sana. Kule Mchuchuma na Liganga kuna kampuni ya kichina inajiandaa na uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe. Makampuni yote haya hayakusubiri Rais wao aje.

    Hoja inayojengwa hapa ni kwamba ujio wa Marais mbalimbali nchini ni ujio wa kujijenga kidiplomasia na wakati mwingine kama sehemu ya kutuma ujumbe Fulani kwa dunia. Nchi inayotembelewa pia inaweza kuona kuwa diplomasia yake inaheshimiwa na mataifa yanayoitembelea.

    Hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba Obama anakuja kwa ajili ya maslahi ya nchi yake kama ilivyo kwa wachina walivyokuja. Tumesikia Rais Obama ataambatana na mamia ya wafanyabishara kutoka Marekani kwa ajili ya kupata fursa za kuwekeza nchini. Pia tutasikia matangazo kuhusu msaada wa pili wa Millenium Challenge ambapo Wamarekani wanaendelea kumwaga pesa nchini kusaidia miundombinu lakini pia kushawishi kuungwa mkono na nchi zetu kwenye maamuzi Fulani Fulani jumuiya za kimataifa.

    Tumesikia Obama atakwenda kutembelea mitambo ya kampuni ya Symbion. Hii ni mitambo ambayo miaka 4 iliyopita ilipigiwa kelele kuwa ni mitumba na hivyo TANESCO wasiinunue. Hawakununua na badala yake kampuni hiyo ya kimarekani ikainunua, wakaingia mkataba na TANESCO kuwauzia umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo chakavu. Wakati tunasuburi kulipa takribani tshs 105 bilioni kwa Dowans baada ya kutubwaga kwenye kesi, tunasubiri kuona wanasiasa watakaokwenda kumsindikiza Obama kwenye matembezi hayo ya kutembelea mitambo chakavu.

    Kampuni kubwa ya kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme ya GE imetangaza kuingia ubia na kampuni ya Symbion kuzalisha umeme nchini. Takribani 400MW zitazalishwa kutoka Mtwara na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Pia sehemu kubwa ya umeme utakaozalishwa Mtwara tayari umepata soko kwenye kiwanda cha kuzalisha udongo ulaya (simenti) cha bwana Dangote kule Mtwara. Mtendaji Mkuu wa GE bwana Jeff Immelt ametangaza kuwa kampuni yake itauza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi mingi zaidi Afrika Mashariki kuliko Marekani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ni biashara tu!

    Nishati naona ni kipaumbele kikubwa sana kwa ziara ya Rais Obama. Kwa nchi kama yetu yenye watu asilimia 21 tu wenye umeme, ni dhahiri kipaumbele hiki watu wengi watakiiunga mkono. Hata hivyo Obama ni lazima asimame kidete kuhakikisha kuwa kampuni za nchini mwake zinazopata miakataba hapa nchini ziweke wazi mikataba hiyo na kulipa kodi inavyostahili. Makampuni ya mafuta kutoka Marekani hayana historia nzuri duniani na hivyo ni lazima tulisisitize mapema kabisa. Uwazi wa mikataba na uwezo wa kupambana na ukwepaji kodi ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ufisadi na ubadhirifu.

    Rais Obama atambue kuwa iwapo Tanzania ingekuwa inakusanya nusu ya kodi zinazokwepwa na makampuni makubwa yanayotumia mbinu kali, basi tungehitaji misaada ya Marekani na hapa nchini angekuja kama mbia wa kweli na sawa katika dunia. Hivyo ni vema aungane na Waziri Mkuu wa Uingereza kuhakikisha kuwa makampuni makubwa hayatumii ‘tax havens’ kukwepa kodi katika nchi kama Tanzania. Uwazi wa mapato yao na kilicholipwa kwa Serikali ni vema usisitizwe sana na Obama mwenyewe ili makampuni yao yasikie na yaache kupora utajiri wa Afrika kiujanja ujanja.

    Mwisho ni vema kama Rais Obama ataomba radhi kwa ushiriki wa Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba. Hivi Tanzania inahangaika zaidi ya uwezo wake kupeleka majeshi huko mashariki ya Kongo kulinda amani. Waafrika wengi tunaamini kuwa mauaji ya Lumumba ilikuwa ni kama laana kwa Taifa lile na hivyo limekuwa ni taifa la vurugu na vita licha ya utajiri mkubwa ulioko nchini humo. Nyaraka za CIA zinaonyesha dhahiri kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo Lyndon Johnson aliagiza kuuwawa kwa mwanamapinduzi Patrice Lumumba. Kuwaomba radhi Waafrika na hasa Wakongo kuhusu mauaji ya Lumumba ni jambo litakaloweza kusaidia sana kurejesha amani Kongo.
    Karibu Afrika, Karibu Tanzania ndugu Barack Hussein Obama.

    Zitto Z Kabwe

    Makala haya yanatarajiwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI, mfululizo wa makala kuhusu ziara ya Obama.

Brand new Hiphop Track toka kwa Magenge ya mwenge ndani yuko JCB, G NACO


Brand new Hiphop Track toka kwa Magenge ya mwenge akiwemo D wa maujanja, K wa maujanja, Moplus, Gnako pamoja na JcB katika "Kipande na wana" ikiwa ni mkono toka Noizmekah, pata kusikiliza
HAPA nakwa mawasiliano/mahojiano na MaujanjaSaplayaz check na +255
714 992 306 au +255 713 233 203 

KILI MUSIC TOUR MKWAKWANI TANGA YAACHA GUMZO .... JIONEE MWENYEWE HALI ILIVYOKUWA




...kutoka nyuma...


Rachel na Roma Mkatoliki


Unaona?


...nimekuuliza umeona?


...sasa je?


Wapiga picha wetu


Rachel akiwajibika katika jukwaa hilo


..aga...


Le Grand show...


Wadau wa Kili wakifurahia Tamasha


Wary wanamtaja huyu kuwa mwanamuziki bora kabisa wa baadae


Majangaaaaaa


Ilipigwa bonge ya show jana Mkwakwani


Shughuli ya Snura ilikuwa kiboko


Ikaja zamu ya Ally Kibba


Dushelele


..tena...


...hapo sasa...


Akaja Kala Jeremiah






Mzuka wa Hip Hop kama


mwanaFA akifanya show ya kitemi mkoani kwake


Nini tena?


yalaiti, ...live


Roma akiwaimbisha watanga tanga




Jizzle


Huh...


Nyomi lake sasa mwanangu mwenyewe...


BackStage

PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://shiladeux.blogspot.com

UJIO WA OBAMA TANZANIA... WAKENYA WACHAFUKWA?

 
Na Mwandishi Wetu

RAIS Barack Hussein Obama wa Marekani anaanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania leo akitokea Afrika Kusini kwenye mfululizo wa ziara zake barani Afrika akianzia Senegal, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha kilichopo nyuma ya ziara hiyo.

Wakati Obama akitua Bongo, mwandishi wetu aliyepo jijini Nairobi, Kenya amesema kuwa baadhi ya Wakenya wamekinunia kitendo cha kiongozi huyo mkubwa duniani kutofika nchini humo ambako ndiko kwenye chimbuko lake.

Baba wa Barack, marehemu Sir Hussein Obama alizaliwa Kenya katika Kijiji cha Nyang’oma, Kogelo, Wilaya ya Siaya. Kabila lake ni Mluo kwa hiyo Obama…

Na Mwandishi Wetu
RAIS Barack Hussein Obama wa Marekani anaanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania leo akitokea Afrika Kusini kwenye mfululizo wa ziara zake barani Afrika akianzia Senegal, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha kilichopo nyuma ya ziara hiyo.

Wakati Obama akitua Bongo, mwandishi wetu aliyepo jijini Nairobi, Kenya amesema kuwa baadhi ya Wakenya wamekinunia kitendo cha kiongozi huyo mkubwa duniani kutofika nchini humo ambako ndiko kwenye chimbuko lake.
Baba wa Barack, marehemu Sir Hussein Obama alizaliwa Kenya katika Kijiji cha Nyang’oma, Kogelo, Wilaya ya Siaya. Kabila lake ni Mluo kwa hiyo Obama ni Mluo (Mjaluo).

KWA NINI WANUNE?
Kwa mujibu wa paparazi wetu nchini humo, baadhi ya Wakenya wanahoji iweje Rais Obama atue Tanzania kwa ziara na kuiacha pembeni nchi yake ya Kenya?
“Nimeongea na baadhi ya Wakenya, wanahoji ni kwa nini Obama asifike kwao? Wanasema afadhali angepanga ziara ya nchi zote mbili kuliko kuipitia pembeni Kenya na kutua huko Bongo.
“Lakini wapo Wakenya wenye uelewa ambao wametambua kwamba ziara ya Obama nchini Tanzania ni ya kiserikali, hakuwa na ratiba ya Kenya. Kama atataka kuja Kenya kumsalimia bibi yake atafanya hivyo binafsi siku nyingine,” alisema paparazi wetu akiwakariri watu aliozungumza nao nchini humo.

 
KWA NINI KAIKWEPA KENYA?
Akizungumza na Amka na BBC kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC Jumamosi iliyopita, profesa mmoja alisema Obama hatafika Kenya kwa sababu viongozi waliopo madarakani kwa sasa, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wana kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita iliyopo jijini The Hague, Uholanzi.
“Si rahisi Obama kwenda Kenya kwa sababu viongozi wake, Uhuru na Ruto wana kesi kwenye Mahakama ya The Hague…,” alisema profesa huyo.


KIKWETE KAANDIKA HISTORIA AFRIKA
Ujio wa Obama Tanzania umeandika historia ya pekee kwa Rais Jakaya Kikwete barani Afrika kwani katika kipindi cha utawala wake, marais wawili wa Marekani walio madarakani wameitembelea nchi anayoiongoza.
Mwaka 2008, Rais wa 34 wa Marekani, George Walker Bush (67) aliitembelea Tanzania na kukutana na Kikwete kama mwenyeji wake.


TANZANIA NDIYO NCHI BORA AFRIKA
Mbali na Kikwete kupokea marais wawili wa Marekani, lakini Tanzania inaonekana ndiyo nchi bora zaidi barani Afrika kwa vile ndiyo pekee iliyotembelewa na marais wengi kutoka Marekani.
Mwaka 1999, William Jefferson ‘Bill’ Clinton (67) akiwa Rais wa 42 wa Marekani alitua nchini kwa ziara ya kiserikali na hivyo kuanzisha mfululizo wa waliomfuatia, Bush na Obama.
Clinton aliwahi kuja tena Bongo baada ya kuachia madaraka, Bush naye anaingia nchini leo akiwa ameongozana na mkewe, Laura ambapo Julai 2 na 3, 2013 anatarajiwa kuhutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani. Mke wa Obama, Michelle atahudhuria.


NI OBAMA DAY
Jijini Dar es Salaam, hali si ile iliyozoeleka. Tangu harakati za maandalizi ya ujio wa Obama uanze, jiji limekuwa safi kwa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo na wale ombaomba wazoefu.
Maeneo ya katikati ya jiji, baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na Wikienda, Jumamosi iliyopita walisema wana uhakika kwa siku ambazo Obama atakuwepo Bongo, kazi zitasimama kutokana na kukosekana kwa usafiri na kuwepo kwa foleni za kusubiri misafara.
“Jumatatu na Jumanne naamini hakutakuwa na kazi, Obama amesababisha mabasi yasije mjini tangu juzi (Alhamisi). Mji ni mweupe. Mi nadhani hii tuiite Obama Day,” alisema Samson Isaya anayefanya kazi katikati ya Jiji la Dar.


KUMBE JIJI LINAWEZA KUFANYA USAFI!
Cha ajabu, ni Manispaa za Jiji la Dar es Salaam, hasa Ilala na Kinondoni zilivyoweza kulisafisha jiji na kuwa safi kiasi cha kuvutia.
Wasomaji wengi wa gazeti hili walisema kumbe Dar kuwa chafu ni uamuzi wa wahusika wenyewe na si wakazi wake kwani wahusika hao wameweza kuingia mitaani na kufanya usafi kwa zana zilezile za siku zote.
“Sasa jiji wanachoshindwa ni nini? Mbona jiji ni jeupe? Nenda Posta, nenda Mwenge, angalia pale Stesheni, kweupe. Siku nyingine wanasema vifaa hakuna, sasa hivi vimetoka wapi? Kama mimi ndiyo JK (Kikwete) nawaambia jiji liwe hivi kila

siku,” alisema mama Swebe wa Magomeni, Dar.


GPL

MASANJA, SHILOLE WAFIKA ULIPO MJENGO WA UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI


 Juu na chini ni Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakiwa nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC mara walipopita na kupiga picha nje ya mjengo Jumapili June 30, 2013 walipokua wakitokea uwanja wandege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Kesho mchana Jumanne April 2, 2013 watatembelea rasmi mjengo huo na kusaini kitabu cha wageni.
 Masanja na Shilole wakiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wakiangalia menyu tayari kwa kuagiza dinner ya mchana walipokwenda mgahawa wa kijiji cha Swahili uliopo Beltsville, Maryland
 Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na mmiliki wa mgahawa wa Swahili Village Bwn.Kelvin.
Masanja na Shilole wakiingia kwenye usafiri wao kuelekea Hotelini walikofikia.

BAADA YA LIL WAYNE KUM-DISS JAY Z,JAY Z SASA AANZISHA VITA



  Jay Z ameamua kum-diss Lil Wayne kupitia wimbo wake mpya wa La Familia ambao utakuwa kwenye album yake mpya inayoitwa Magna Carta Holy Grail.
Kama unaweza kukumbuka Jay Z alimchana Birdman kwenye wimbo wa H.A.M na kusema
“I’m like, ‘Really, half-a-billi?’ / Nigga, really, you got baby money / Keep it real with niggas, niggas ain’t got my lady money,”. Maneno hayo yalimuuzi sana Lil Wayne na kupelekea Lil Wayne kumjibu Jay Z kupitia wimbo wa I’m Good ambao ulikuwa kwenye Carter IV.
Lil Wayne alisema “I got your baby money / Kidnap your bitch, get that how much you love your lady money.”
Jay Z bado hajasahau maneno hayo ya Lil Wayne na kuamua kumjibu hivi “Wanna kidnap wifey / Good luck with that bruh / You must gonna hide your whole family / What you think we wearing black for / Ready for that war / Ready for that war ready / You ain’t ready, yo, you radio,” spits Jay on La familia song.

HIVI NDIVYO M 2 THE P ALIVYOSHINDWA KUONGEA KATIKA USIKU WA NGWEAR, SOMA HAPA ALICHOKISEMA

Habari Mpya :

Msanii wa hip hop M 2 the P ambae ni rafiki wa Marehemu Albert Mangwair alias CowBoma jana alishindwa kuongea kitu katika USIKU WA NGWAIR uliofanyika CITY CENTER(Samaki Samaki).
Sababu ni kwamba M2-THE-P anaumia sana kila inapofikia hali ya kumkumbuka swahiba wake Mangwair,
“Habari, am so happy kuwaona mkit-show real luv kwa mshikaji(Ngwair) siwezi kuongea kitu ila na ushukuru Uongozi wa Samaki Samaki kwa kusimamia event hii pia nawashukuru wadau wote mliohudhuria katika USIKU WA NGWAIR peace and luv to him”. by Bongoclan

TUJIKUMBUSHE MAMBO MACHACHE YANAYOTENDEKA KUHUSU OBAMA AMBAYE TAYARI YUPO TANZANIA


Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa zara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.
Obama ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais. NA MPEKUZI

Festive: The President was seen dancing along to the music on the red carpet at the airport
Rais wa Marekani akicheza muziki wa band wakati alipotua uwanjani   

Rais Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na kisha Obama atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali hapo baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.

Aidha hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme Barani Afrika.

Mpango huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.

Welcome: Well-wishers line up in Dar es Salaam in anticipation of Mr Obama's visit
Karibu Barack Obama kanga pamoja na vitenge waliova wananchi wa waTanzania 

Katika ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini na hatimaye nchini Tanzania Obama amekuwa akisisitiza suala la demokrasia ambapo ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.

Katika ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani
 
kwa hisani ya: http://audifacejackson.blogspot.com