Thursday, June 20, 2013
HATARIIII.....ANGALIA PICHA ZA MAJERUHI MAPOKEZI YA BECKHAM CHINA
11:06 AM
No comments
Nyota
wa zamani wa Manchester United, Los Angel Galaxy, Real Madrid, PSG na
timu ya taifa ya England, David Beckham amewasili leo nchini China na
kusababisha wanafunzi watano kujeruhiwa vibaya katika harakati za
kumpokea katika chuo cha Tongji University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
Beckham
ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira wa miguu ya chuo hicho
kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye lengo la
kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha
ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono na nyota huyo,
imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha watu
kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo
la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa kutimia kufuaia fujo
hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika mtandao wake wa
kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile
kilichotokea.
Samahani
sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo kikuu pale uwanjani,
kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia watu wachache
wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri wapone
salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani
watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo na kuhitaji kumshika
nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa maofisa wake
watu wamejeruhiwa katika fujo zoezi hilo.
Beckham
mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka msimu uliopita ambapo
aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, Ligue 1.
NU-Joint: Umbwa aka Chindo Man from Watengwa
11:01 AM
No comments
![]() |
| Ni mkono wa Umbwa aka Chindo Man from Watengwa Family na Vocals zikiwa chini ya Defxtro wa Noizmekah Productions na Humu wanapita Sister P-Culture na JCB. Ngoma inakwenda kwa Jina Life Can Be,ni inspirational hiphop joint yenye mistari ya kuelimisha jamii, Pata kuusikiliza HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania, kwa mawasiliano zaidi na Mwanadada P-Culture chek naye kupitia nambari +255 782 123 700 powered by www.vmgafrica.com |
WOLPER NA HALIMA MDEE WANATARAJIWA KUTOANA MANUNDU USIKU WA MATUMAINI
10:57 AM
No comments
MSANII wa
filamu nchini Jacqueline Wolper ameenda kujichimbia Afrika Kusini
akifanya mazoezi ili ajiweke katika nafasi ya kuzichapa na mbunge wa
CHADEMA Halima Mdee, katika tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7
mwaka huu.
Wolper
ambaye atapigana na Halima Mdee, alisema kuwa amejikita nchini humo kwa
ajili ya kujiweka sawa ili aweze kumkabiri mbunge huyo.
Alisema
mbali ya kujiweka fiti kwa ajili ya kumkabili mbunge huyo pia anajiweka
fiti kwa ajili ya kujenga mwili wake ili kupunguza magonjwa pamoja na
kujinginga na magonjwa ya kisukali yanayotokana na mafuta.
"Naamini
nitamgaragaza mbunge huyo na sitochukua hata dakika tano kwenye mchezo
huo kwani naamini mazoezi yangu ninayoyafanya ni njia moja wapo ya
kujiweka vizuri kimwili" alisema Wolper.
Siku ya
Usiku wa Matumaini utapambwa na mashindano kibao yakiwemo mbunge wa viti
maalumu Ester Bulaya ambaye naye anatarajia kuzichapa na Aunt Ezekiel,
huku Zitto Kabwe atazichapa na Vincent Kigosi
pro 24
Chief Mufasa, msanii anetisha na stlye yake ya Afropop, cheki ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la JaiveJaive
10:48 AM
No comments
Pata kumsikiliza ChiefMufasa msanii anayewakilisha vema Tanzania kule
nchini Kenya,na hapa ni katika kipande kidogo cha Bonus track yake
aloipa jina "JaiyeJaiye"
ambayo ni Afropop itakayokuwa katika mixtape ya Fresh 2
Twenty,itakayodrop mtaani mwezi huu mwishoni,Mixtape itakuwa na ngoma 12
za muundo wa HipHop, Crunk, Afropop na fusion zingine nyingi tofauti
zikiwa zimerekodiwa Noizmekah Production Stiudios kwa Defxtro, sikiliza
Jaiye Jaiye Snippet HAPA na endelea kussuport muziki wa Tanzania,Kwa mawasiliano zaidi check na ChiefMufasa kupitia +
Furaha ya burudani ya miaka ilee sasa imerejea: Isumba lounge ndio jibu lako.
10:42 AM
No comments
Tuesday, June 18, 2013
Picha: Nyuma ya pazia 'Diamond Platnumz' akiandaa picha kwaajili ya mashabiki wake
10:23 PM
No comments
Leo katika website ya This is Diamond, mwimbaji wa Bomgo Fleva 'Diamond Platnumz'
ameachilia picha ambazo zinaonyesha nyuma ya pazia juu ya picha
zitakazo toka kwaajili ya mashabiki wake ku share na kuzitumia kwenye
mitandao ya kijamii.
Hiki ndicho alicho kiandika.
"Siku ya jana nilikuwa na ratiba nyingi lakini hii ilikuwa moja ya ratiba muhimu sana kwa siku ya jana.....
Ratiba hii ilikuwa kwaajili ya kupiga picha zangu binafsi kwa matumizi yangu kwenye Social Networks zangu na Website kwa ujumla na pia bila kusahau baadhi ya picha ni zawadi kabisa kwenu mashabiki zangu wa nguvu kwa matumizi yenu kwenye social networks zenu binafsi......
Zifuatazo ni picha kadhaa nikijianda na Photoshoot hiyo kutoka home hadi studio.....nimeamua kushare na nyinyi muweze kujua kinachojiri ndani ya ulimwengu wangu."
Zitazame hapa picha zaidi juu ya tukio hilo.
Hiki ndicho alicho kiandika.
"Siku ya jana nilikuwa na ratiba nyingi lakini hii ilikuwa moja ya ratiba muhimu sana kwa siku ya jana.....
Ratiba hii ilikuwa kwaajili ya kupiga picha zangu binafsi kwa matumizi yangu kwenye Social Networks zangu na Website kwa ujumla na pia bila kusahau baadhi ya picha ni zawadi kabisa kwenu mashabiki zangu wa nguvu kwa matumizi yenu kwenye social networks zenu binafsi......
Zifuatazo ni picha kadhaa nikijianda na Photoshoot hiyo kutoka home hadi studio.....nimeamua kushare na nyinyi muweze kujua kinachojiri ndani ya ulimwengu wangu."
Zitazame hapa picha zaidi juu ya tukio hilo.
SOURCE: 24Hours Mix | Infotainment site
MAJINA YA KIDATO CHA SITA 2013 WANAOKWENDA JKT NI HAWA HAPA.
9:05 PM
No comments
MAJINA YA VIJANA KIDATO CHA SITA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA TAREHE 24 JUN 13.
Vijana wa Mujibu wa Sheria Awamu ya Pili.
Wabunge wahudhuria mafunzo ya JKT.
Amiri Jeshi Mkuu atembelea JKT.
Vijana wa Mujibu wa Sheria waliohamishwa toka Makambi ya Mafinga Iringa na Oljoro Arusha.
Tangazo la Jeshi la Kujenga Taifa
Mada kwa Vijana wa Mujibu wa Sheria.Tangazo la Jeshi la Kujenga Taifa
Update: Habari za kufariki Saida Karoli zakanushwa
8:25 PM
No comments
UPDATE:
Taarifa mpya zinasema ajali ya boti imetokea lakini Saida Karoli
hakuwemo kwenye boti hiyo na yuko hai. Kwa taarifa hizo za kukanusha
kufariki msanii huyo, nenda kwenye link ifuatayo: Taarifa: Saida Karoli yuko hai. Kweli ajali ya boti imetokea lakini Saida hakuwemo
Kwa mujibu wa Mjengwa blog
mwanamuziki mashuhuri Afrika Mashariki, Saida Karoli amefariki dunia
baada ya kuzama maji kufuatia ajali ya boti iliyotokea kwenye ziwa
Victoria. Ajali hiyo ilitokea baada ya boti aliyokuwa akisafiria kutoka
Kisiwa cha Goziba kukumbwa na dhoruba na kuzama katika Ziwa Victoria.
Taarifa
hizo zinasema pamoja na Saida Karoli, kuna watu wengine pia wamefariki
dunia katika ajali hiyo. Idadi ya waliofariki kwenye ajali hiyo bado
haijapatikana
Picha: Jinsi marehemu Langa Kileo alivyozikwa jana (June 17)
6:10 AM
No comments
Ndugu, marafiki, wasanii, watu mashuhuri na watu wa aina mbalimbali jana wamejumuika kwenye mazishi ya rapper Langa Kileo aliyefariki wiki
iliyopita kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Langa amezikwa kwenye makaburi ya Kinondoni ambapo mazishi yake
yameongozwa na wazazi wake wote wawili. Hizi ni baadhi ya picha za
mazishi hayo.
Kaka yake Langa na Baba yake Mzee Kileo
Lady Jaydee akitoa heshima zake za mwisho
M 2 THE P
Mama mzazi wa Langa
Aliyekuwa meneja wa Langa
B12 na Petit
Dada yake Langa
Dr Cheni
Mdogo wake Langa
Mwili wa Langa ukiombewa
Mwili wa Langa kwenye jeneza wakati ukiagwa
Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu
Nikki Mbishi akitoa heshima zake za mwisho
Rafiki wa Langa akilia kwa uchungu
Rafiki wa Langa akilia kwa uchungu

Sauda Mwilima na Keisha

Wazazi wa Langa























































Mungu ailaze roho ya marehemu Langa pepeni, Amen.
Sauda Mwilima na Keisha
Mungu ailaze roho ya marehemu Langa pepeni, Amen.
Subscribe to:
Posts (Atom)



























