Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, September 23, 2013

Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate

Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate
Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate.
BOFYA HAPA KUPATA HABARI ZOTE LIVE


15:33 Waziri wa usalama wa Kenya Joseph Ole Lenku asema kuwa wanajeshi wameweza kudhibiti jengo lote la Westgate
15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati zao hizo dhidi ya Al Shabaab

Juhudi za uokozi Westgate
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa

14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi wote ni wanaume, kutokana na taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa wanaongozwa na mwanamke

14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili

14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao


Moshi mkubwa ukitoka ndani ya jumba la Westgate
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao


Waathiriwa wa shambulizi la Westgate
13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa

HUYU NI TAPELI ANAYETUMIA JINA LA WEMA SEPETU KUTAPELI NA KUHACK AKAUNTI ZA WATU FACEBOOK.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOER3ektVeAQodLoywyHxsFNg6MGIN_n3UEVnp8B60X98l0vaIUcKsyZTbS-tur1WLbyUoMHO2QrG175kOLoDdz-lTW-RvmMotEiKTzb4_4g_Iei_k7hWHfZrknxnivw9qwaUAdtebnog/s1600/WEMA1.JPG


  UJUMBE MAALUM KWA WANAOTUMIA FACEBOOK NA FANS WETU PIA.


TUMEPOKEA MSG KUTOKA KWA MTU ANAYEJIFANYA NI MSANII NGULI ( Wema Abraham Sepetu ) Akidai Global-Publisher kuna shindano walilo anzisha, na akituomba tu mpe kura zetu ili ashinde shindano la facebook team Page,baada ya kufanya uchunguzi wakina tumegundua ni (Hackers) na kUNA LINK ambayo ukifungua ina kudirect kwenye facebook login na ukisha Log hapo Automatical inakuwa detected Kwa system zaO na kuweza kupata taarifa zako zote pia wanatapeli watu njia ya mitandao wakidai kuanzia vyama vya kukopesha watu pesa na kuwalipa kwa njia ya Tigopesa,

JAMANI SIO WEMA SEPETU NA USIJARIBU KUWASADIA LOLOTE

NA Hii ni Account nayotumia Facebook akijifanya Wema Sepetu Bofya uone Wall yake anavyotapeli watu Akijifanya kutoa Mpoko kama Saccos -https://www.facebook.com/wema.sepetu.946

:: SOMA HAPA CHINI NI MOJA YA UJUMBE ALIOTUTUMIA NA LINK::


Wema Abraham Sepetu
Hi, please nakuomba kwa hisani yako na upendo wako support kazi yangu kuna shindano limeandaliwa na Global Publisher katika facebook team page naomba ukaweke Like yako katika picha yangu ili niweze kushinda. Naomba kura yako, unavyoweka Like ndio kura yako kwangu! Bofya hapa www.facebook-team.wapka.mobi

UPDATES:HALI YAZIDI KUWA MBAYA JIJINI NAIROBI... NI BAABA YA KUSIKIKA MILIO YA RISASI MCHANA HUU

-Milio ya risasi yasikika kutoka ndani ya jengo
-Moshi mkubwa unatoka kwa sasa
-Waliouawa wafikia 69, majeruhi 175
-Magaidi wawili wameripotiwa kuuawa leo asubuhi
-Yadaiwa magaidi wote ni wanaume
HALI ya sintofahamu imeendelea eneo la jengo la Westgate lililopo jijini Nairobi lililovamiwa na magaidi wa Al Shabaab tangu Jumamosi mchana.
Milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo ikifuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo lenye maduka na migahawa zaidi ya 80. Mpaka sasa hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo mkubwa na idadi ya mateka.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, ni kwamba magaidi wawili wameuawa leo asubuhi na waliovamia jengo hilo wote ni wanaume.

HII HAPA MISTARI YA WIMBO WA DIAMOND My # one SOMA HAPA

 

VERSE1:
Kwanza mapenzi safari, ujana ni maji ya moto
Walinenaga zamani...
Pili tumetoka mbali, matatizo changamoto
tu visa visa fulani...
tatu kidonda chako kwangu maradhi
Mama tu usononekapo kwangu simanzi..
Kwa mahaba uliyonipa nimenogewa 
ni vurugu patashika punguza kidogo..
Na mengine kadharika toto si unanielewa?
Hapo hapo uliposhika...ukiongeza kidogo mi mwenzako ntaumia
CHORUS:
Your my number one - my sweety sweety
Number one - my baby ooh oh 
Your my umber one...oooh my darling
Number one - roho yangu mama x2
Roho yangu mama...
VERSE 2:
Na nna wivu sikatai, maana uchungu wa mapenzi naujua 
So Usije kunilaghai nikaja kuzama ukanizingua x2
Now show me how they do..
Ngololo x6

FIESTA SHINYANGA YAFUNIKA MBAYA, TAZAMA PICHA ZA MAKAMUZI YALIYOFANYIKA VIWANJA VYA KAMBARAGE SHINYANGA


 Anajiita Mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake kwa shangwe huku mayowe yakitawala kila kona ya uwanja wa Kambarage usiku huu ndani wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea kurindima usiku huu.
 Mtoto wa Mama Saidi a.k.a Cheke akiimba kwa hisi jukwaani.
Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake.
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoko akiimba jukwaani usiku huu sambamba na madensa wake (hawapo pichani). 
Tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu.

Mashabiki wake wanamuita Kinga Zilla kutoka Sala Sala,lakini pia jina la Godzilla limemuongeza umaarufu kwa mashabiki wake kutokana na umahiri wake wa kushusha mistari ya hip hop mikavu mikavu,kama aonekavyo jukwaani akiwaimbisha mashabiki wake ndani ya uwanja wa Kambarage usiku huu.
  Baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga,ambapo tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kufanyika.
Mwanadada Linah akiimba sambamba na shabiki wake jukwaani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Kambarage,mkoani Shinyanga usiku.
 Baadhi ya Wadau wakubwa na wadhamini wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kutoka kampuni ya Serengeti Breweries,Octavian,Bahati pamoja na mdau wao,wakiwa katika picha ya pozi usiku huu ndani ya uwanja wa Kambarage,mkoani Shinyanga
 Mwanadada ambaye kwa sasa ameonekana akifanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2013,Neylee akiwaimbisha mashaniki wake (hawapo pichani). 
 Anajiita Jita Man kutoka jijini Mwanza akitumbuiza jukwaani usiku huu.

Dj Zero kutoka Clouds FM akiburuza mangoma usiku huu.
Mwanadada Shilole na madensa wake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Kambarage.mkoani Shinyanga. 
 Masbabiki kibao waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,usiku wakifuatilia na kushangweka vilivyo mbele ya jukwaa la fiesta.
 mashabiki wakifuatilia
 Kutoka Wanaume TMK,wakiongozwa Mh Temba na Chege kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa kambarage mjini Shinyanga.
 Weusi wakitumbuiza jukwaani usiku huu.
 Shabiki akifurahi jamboo.
Kundi la Wanaume TMK-Halisi likiongozwa na Sir Juma Nature wakilishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Kambaraje,mjini Shinyanga.


 

HUYU NDIYE MWANAMKE ANAYEDAIWA NDIO KIONGOZI WA MAGAIDI WA AL SHABAAB WALIOSHAMBULIA NA KUUWA WESTGATE MALL KENYA





Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.


Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.
Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.

Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.

Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.
Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza kuhusika na shambulio la jana.

Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?
Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.

Akitokea Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.

Mwezi May hati ya kumkamata ilitolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani nchini Kenya kwa kesi ya kutengeneza bomu.

*anahisiwa* – Habari haijathibitishwa

HISTORIA FUPI YA HAPPINESS WATIMANYWA MISS TANZANIA MWAKA HUU(2013)

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa kipindi cha Skonga, utamkumbuka Happiness Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.
Kipindi ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu, alipata wakati mgumu wa kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la Miss Dodoma, na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya Miss Tanzania.
Akiwa Miss Tanzania, Happy alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013.