Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, November 13, 2013

HURUMAA...HUYU NDO Mtu Asiye na Uso, Anahofu Mtoto Wake Mtarajiwa Atafanana na Yeye


Baba mtarajiwa amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kuishi bila kuwa na uso na kwa namna gani anahofia juu ya hali atakayozaliwa mtoto wake mtarajiwa. Anaitwa Mohammad Latif Khatana, 32, kutoka Kashmir, India, hawezi kuona wala kufanya kazi kutokana na ngozi zilizofunika uso wake. Watu humkimbia barabarani kutokana na hali yake huku wakionekana kuogopeshwa nayo.
  Kwa sasa ni mwenye faraja kutokana na ukweli kwamba mke wake ni mjamzito wa miezi saba, ila ana hofu labda huenda mtoto wake anaweza kuzailiwa akiwa anfanana naye.
Alisema: “Naingoja kwa hamu hii hali ya kuwa baba na kupata furaha ya maisha. Ila nahofu kila siku na kusali ili mwanangu asije kuzaliwa kama mimi.”
  Latif, ambaye anaishi milimani na mke wake mwenye miaka 25 aitwaye Salima, eneo la Tuli Bana, ndani ya Jammu and Kashmir, huwa anatembea mpaka Srinagar mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kuomba misaada na ili kupata hela.
  Alizaliwa na kinundu kidogo kwenye uso wake ili kimeendelea kukua na ktengeneza tabaka kubwa la ngozi kwenye paji la uso wake, linalomfanya ashindwe kuona.

Anasema: “Mama yangu bado analia kila aniangaliapo, anajiona kama mtu mwenye kosa na anashindwa kuelewa kwa nini mtoto wake wa mwisho amekuwa hivi.”
  Latif ni mdogo kati ya wakaka wawili na dada watatu huku yeye pekee akiwa na tatizo hilo.
  Bila ndugu zake angeweza kuishi maisha ya upweke sana udogoni kutokana na kutokuwa na marafiki.
  “Hakuna aliyetaka kucheza na mimi utotoni,” akaongeza. “Wavulana kijijini kwangu walikuwa wananipiga na kunitesa kila siku. Nilipoteza jicho langu la kushoto nilipokuwa na miaka minane na wakawa wananiita mjinga mwenye jicho moja.”
  Alipokuwa kijana Latif alikumbana na changamoto mbalimbali za kimaisha. Ni mtu mwenye nguvu zake ila kutokana na kushindwa kuwa anaona na kwa namna uso wake ulivyo hakuna aliyeweza kumpa kazi.
Alisema: “Ningependa kufanya kazi ya uhakika kama wanaume wengine wanavyofanya ili kuweza kuzitunza familia zao, ingenifanya nijisikie fahari sana, ila hakuna aliyenipa nafasi. Inabidi niombe  na naamini watu wanaweza nisaidia ili niweze kulisha familia yangu.”
Miaka minne iliyopita Latif alikutana na mwanamke wa maisha yake, awali wazazi wake walijitahidi sana kumtafutia mke ila hakuna msichana liyejitokeza, mpaka Latif aliposikia kuhusu Salima.

“Mke wangu ana mguu mmoja tu na kwa muda mrefu amekuwa akitafuta mume, punde tulipokutana tulijua tulikuwa sahihi kwa kila mmoja wetu,” anakumbuka. “Wote tulikuwa hatujakamilika, hakika tuliendana.”

Walioana kwenye harusi ya Kiislamu wakiwa na wageni 400 mnamo August 2008 na wamekuwa wenye furaha toka kipindi hicho.
 
Akaongeza: “Najiona nimebarikiwa sana kwa kukutana na Salima, ni mwanamke mzuri kwangu.
 

“Sasa naona kawaida nina mke, ni kitu kikamilifu zaidi ya awali. Na sasa ana ujauzito wa mtoto wetu wa kwanza nina furaha sana.  Haijalishi kwa namna yoyote ile nnavyoonekana ila sasa ni mwanaume mwenye furaha.”
  Ila Latif, ambaye hana maumivu na hapati matibabu yoyote, anahofu mtoto wake kama anaweza kuzaliwa na hali kama aliyonayo yeye.
Anasema: “Hatuna uwezo wa kumuona daktari, sisi ni masikini sana. Hakuna daktari kwa siku za nyuma aliyenieleza nisipate mtoto. Ninakuwa na tumaini na kuomba kwamba mtoto wetu atakuwa mwenye afya.”
Kaka yake na Latif aliamua kuuza sehemu ya ardhi miaka minane iliyopita ili aweze kulipia safari ya kwenda kumuona daktari ila hakukuwa na namna ambayo wangeweza kuifanya.
  Anakumbuka: “Daktari aliniambia kwamba hali yangu ilitokana na mionzi ya jua wakati mama alipokuwa na ujauzito wangu. Ila sijui kama nahitaji kumuamini.
“Na sasa kuna vitu vingi vinanijia kichwani mwangu kwamba kufanya upasuaji inaweza kuwa ni kitu cha hatari sana.
Nimepoteza tumaini lote la msaada. “Hivi ndivyo nitakavyokuwa daiama.”
HAKIKA KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA na pia tukumbuke BINADAMU HUJAFA HUJAUMBIKA
source-danchibo

Tuesday, November 12, 2013

PICHA 50 ZA MASTAA MAARUFU DUNIANI WANAOSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA..!!

Wentworth Miller, Maarufu zaidi kama Michael Scofield

Mwigizaji Victor Garber
Ricky Martin

Adam Lambert
Anne Burrell na patna wake
Neil Patrick Harris na patna wake
Boy George
Broadway actor Cheyenne Jackson
Broadway actor Nathan Lane
Chaz Bono
Chris Colfer maarufu zaidi kama Kurt Hummel
Clive Davis
Mtangazaji wa CNN, Don Lemon
Mwanamieleka Darren Young
Elton John na patna wake David Furnish
Rosie O'Donnel
David Hyde Pierce
Wanda Sykes
George Michael
Matt Bomer na patna wake
Jane Lynch
Jason Collins
Jodie Foster
Nate Berkus
Mitchell Pritchett
Mtangazaji Anderson Cooper
Aliyekuwa mwanamuziki wa kundi la NSYNC, Lance Bass na patna wake
Mtangazaji mahiri Ellen DeGeneres na mke wake Portia De Rossi
Tabatha Coffe
Sean Hayes
Melissa Etheridge
Sir Ian McKellen
Mcheza soka Stud Robbie
Mwanamuziki Charice
Cynthia Nixon na patna wake
Jim Parsons na patna wake
Martina Navratilova.. alikuwa star wa tennis
Johnny Weir
Anne Burrell
Staa wa YouTube na Nickelodeon Lucas Cruikshank
Mwigizaji Zachary Quinto

P-FUNK APATA AJALI YA KUSHANGAZA CHOONI

LEGEND wa kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.
Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.
KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.
‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.
“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?
Chooni alipodondoka P-Funky na kupata majeruhi kichwani.
P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.
Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”