Wednesday, February 26, 2014
baada ya bifu zito la muda mrefu baina ya Mecca Cheka na Jambo Squad lafikia ukingoni kwa style hii. soma hapa
11:34 PM
No comments
baada ya bifu zito la muda mrefu baina ya Mecca Cheka na Jambo Squad limefikia ukingoni na kurekebisha tofauti zao walizokuwa nazo na hiki ndicho alichopost facebook Almando Mwiroro
"MECCA CHEKA vs JAMBO SQUAD nw we ar together again.. so MAALMANDO WATOTO WA BIBI is back again no bifu wala nin.. tunawapenda sana na tunaomba radhi kwa yote yalitokea mashabik wetu"
theHOODinfotainment inawapa BIG-UP KUBWA n MUCH RESPECT
theHOODinfotainment inawapa BIG-UP KUBWA n MUCH RESPECT
Wednesday, February 12, 2014
HUYU NDIO DIAMOND KABLA HAJAWA SUKARI YA WAREMBO,TAZAMA PICHA NA UJUE MAMBO AMBAYO ULIKUWA HUYAJUI.
4:03 AM
No comments
Mambo matano Yatakayokugusa katika maisha ya Diamond Platnumz
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya
Amana Dar es salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba
yake kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake
diamond.
02. Chumba kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko
tandale na ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake
apangishe chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba
kimoja na bibi na mama yake.
03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na
alipomaliza elimu yake ya O’level
ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa
elimu yake.
04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi
kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.
05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi
usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona
anamdekeza mwanae.
MAMA KANUMBA AJA NA MPYA INAYOMUHUSU WEMA SEPETU
3:41 AM
No comments
Hamida Hassan na Gladness Mallya
SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kukiri kwamba Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikuwa mkwe sahihi kwake, safari hii ameibuka na kumbariki Wema Sepetu ambaye naye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye, akisema ana huruma, roho nzuri na utu.
Akizungumza kwa kujiamini, mama Kanumba alisema: “Hili nalizungumza kutoka moyoni mwangu, huyu mtoto ana moyo wa upendo sana. Angalia namna anavyowasaidia wenzake wanapopata matatizo. Anajitoa kwa moyo, siyo mchoyo. Kwa kweli Mungu amwongezee.”
gpl

Mama Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa kujiamini, mama Kanumba alisema: “Hili nalizungumza kutoka moyoni mwangu, huyu mtoto ana moyo wa upendo sana. Angalia namna anavyowasaidia wenzake wanapopata matatizo. Anajitoa kwa moyo, siyo mchoyo. Kwa kweli Mungu amwongezee.”
Wema Sepetu.
“Kiukweli Wema anajitoa sana... nakumbuka hata kipindi akiwa na
mwanangu, maana uhusiano wao niliutambua, Kanumba mwenyewe
alinitambulisha; walikuwa wakija kunisalimia nyumbani ananiita pembeni
na kunipa pesa ili Kanumba asione, akitaka na yeye anipe. Huo ni moyo wa
kipekee sana,” alisema mama huyo.
Hiki ni kama kipindi cha mama huyo kuonesha hisia zake kwa wakwe zake
(wasichana waliowahi kuwa na uhusiano na marehemu mwanaye) kwani
takribani wiki tatu zilizopita, alimzungumzia Lulu kwa maelezo kuwa
alikuwa mkwe sahihi kwake.gpl
ANGALIA MBINU MPYAILIYOTUMIKA KUSHAFIRISHIA MADAWA YA KULEVYA
3:35 AM
No comments
Unaambiwa
kwenye mji wa Berlin huko Ujerumani kwenye supermarket tano
yamepatikana mabox yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikua na dawa za
kulevya zilizofichwa ambazo ni kilo mia moja arobaini.
Ni kosa
ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa wenyewe
manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza matunda kwa
jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa meli kutokea Colombia.
Wafanyakazi wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo
ndani yake ndio kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa
kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.
Unaambiwa
mzigo huu wa Cocaine ndio mzigo mkubwa kukamatwa kwenye mji huu mkuu wa
Berlin kwenye kipindi cha miaka 15, ni mzigo wenye thamani ya dola za
Kimarekani milioni 8 na laki mbili.
Polisi
wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia
sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti
kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.

Subscribe to:
Posts (Atom)