Unaambiwa
kwenye mji wa Berlin huko Ujerumani kwenye supermarket tano
yamepatikana mabox yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikua na dawa za
kulevya zilizofichwa ambazo ni kilo mia moja arobaini.
Ni kosa
ambalo limefanywa na wauza dawa au wasafirishaji wa hizo dawa wenyewe
manake mzigo ulianzia kusambaa kwenye duka la jamaa anaeuza matunda kwa
jumla kwenye mji hamburg ikiaminika ni baada ya kuwasili kwa meli kutokea Colombia.
Wafanyakazi wa hizi supermarket ndio walitambua haya mabox ambayo
ndani yake ndio kulikua na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa
kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.
Unaambiwa
mzigo huu wa Cocaine ndio mzigo mkubwa kukamatwa kwenye mji huu mkuu wa
Berlin kwenye kipindi cha miaka 15, ni mzigo wenye thamani ya dola za
Kimarekani milioni 8 na laki mbili.
Polisi
wanasema kwa Ujerumani, wauza dawa za kulevya wana kawaida ya kutumia
sana njia ya posta kusafirisha dawa za kulevya kwenye sehemu tofauti
kuliko njia nyingine ambazo zimekua zikitumika.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.
Miaka minne iliyopita wafanyakazi kwenye supermarket nyingine waligundua dawa za kulevya zinazokaribia kilo themanini zilizokua zimefichwa kwenye maboxi ya ndizi, mzigo ulioingizwa Ujerumani kutokea Ecuador.
0 comments:
Post a Comment