NA MAKONGORO OGING'
MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray
C’ ambaye aliwahi kuathirika na utumiaji wa ‘unga’, hivi karibuni
alitinga ofisi ya kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya
na kuomba kupatiwa majina, idadi na sehemu walipo watumiaji wa
mihadarati hiyo ili aweze kuwasaidia kwa kuwapa somo, kitu
kinachotafsiriwa kama bado unamtesa.
Ray
C katika harakati zake akifanya mahojiano na msanii wa Hip hop, ambaye
yupo mbioni kuachana na madawa ya kulevya, Ibra the Hustler.
Ray C anadaiwa kufika katika ofisi hizo, Aprili Mosi, mwaka huu, saa
nne asubuhi hali iliyozua gumzo kwa askari waliomuona ambao walijiuliza
kitu alichokifuata.
Akizungumza na Uwazi, kamanda wa kitengo hicho cha madawa ya kulevya,
Godfrey Nzowa alikiri kufika kwa msanii huyo ofisini kwake na kutoa
madai hayo lakini alimwelekeza kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani
huko kuna kitengo kinachoshughulika na watu wenye matatizo ya akili
wakiwemo watumiaji wa madawa ya kulevya.
Kamanda huyo alionesha kufurahishwa na kitendo cha msanii huyo ambaye
pia anamiliki taasisi yake yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa
matumizi ya madawa hayo kwa kuwapa elimu, akisema atatoa msaada mkubwa
kwa wenzake.
Aliwataka watumiaji wa madawa hayo ambao wameshindwa kuacha, wamfuate
msanii huyo ili awape elimu na amewaonya wote wanaotumia na kusafirisha
madawa hayo.
“Wote wanaotumia na kuuza madawa hayo waache mara moja kwani kikosi
kazi kinachopambana na biashara hiyo kimejipanga kila kona ili kukomesha
biashara hiyo haramu,” alisema Kamanda Nzowa.
chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment