Marehemu
Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino
kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.
Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni
Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze
safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia
GAIRO mjini.
Katika
gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na
wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa
mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika hospital ya mkoa
Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
Kweli
ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha
yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili
yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu
maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote
mliotutangulia.
Picha zote kutoka DJ Choka Music.
0 comments:
Post a Comment