Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Friday, January 4, 2013


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013.PICHA NA IKULU.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Picha Na Ikulu

 Wakazi wa Jiji La Dar Wakifukia Kaburi la aliyekuwa Msanii wa Bongo Movie Juma Kilowoko maarufu kama SAJUKI
 
 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu 
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.
Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi. 












Thursday, January 3, 2013

DIAMOND AFUNGUKA JUU YA FUJO ZLIZOTOKEA KWENYE SHOO YAKE NA HATUA ATAKAZOCHUKUA

Usiku wa january 1 2013 Maisha Club ulikua usiku maalum kwa show ya WASAFI ambao wanaongozwa na Diamond Platnums, usiku huu umeingia kwenye Headlines baada ya fujo kubwa kutokea za kurushwa chupa, viti na mayai viza.  Noma ilianza dakika 15 baada ya Diamond kuanza kuingia kwenye stage ambapo anakiri kwamba alijua kulikua kuna watu wamepanga kuja kumfanyia fujo na aliuambia uongozi wa Maisha Club mapema kwa tahadhari na wakamwambia aendelee manake wameshaongea na wahusika lakini kumbe maongezi hayakubadilisha chochote. 
 
 Anavyosema Diamond ni kwamba waliofanya fujo ni washkaji zake wa siku nyingi ambao alikua nao Kariakoo, hao washkaji walikua wamegombana hivyo kugawanyika katika makundi mawili ambapo kundi moja lilikua linataka Diamond awe nalo alafu jingine alitenge, anasema yeye alikataa hilo wazo kwa sababu wote ni washkaji zake.  
 
Huo msimamo ulifanya hilo kundi lililomshawishi kukasirika na kuamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo Maisha Club, taarifa alizipata mapema kwamba wangekuja kumzomea ambapo kweli hao jamaa walipofika Maisha wakati wa show walianza kuzomea lakini Diamond akatangaza kwa mashabiki ambao walimsupport Diamond na kupiga kelele zilizowashinda hao wazomeaji ambao baada ya kuona hivyo walianza kufanya fujo. 
 
 Mmoja wa hao wazomeaji ambae aliongea na millardayo.com usiku huo huo kwenye eneo la tukio alisema wao hawahusiki na fujo zilizotokea, waliofanya fujo ni mashabiki tu ambao pengine walichoshwa na show ya Diamond, wao walichokuja kufanya ilikua ni kuzomea tu kwa sababu Diamond alikiuka makubaliano yao.  Makubaliano yenyewe ni kwamba kwa sababu Diamond ni mshkaji wao toka kitambo kabla hajajulikana kisanii, walishakubaliana toka wakati huo kwamba akifanikiwa kimuziki inabidi asaidie na washkaji wengine wa kundi hilo ambao ni wasanii wachanga kitu ambacho jamaa wanadai Diamond hajakifanya kabisa, siku ya tukio alitakiwa kuperform na msanii mmoja wapo aitwae Papaa Masai lakini Diamond alikataa na hicho ndicho kilichowapa hasira.  
 
Baada ya mambo kuharibika hili kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia. 
 
Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.  Kitu kingine alichokisema ni kwamba kati ya hao waliokwenda kumfanyia fujo ni pamoja na mdogo wa msanii ambae aliwahi kuwa na ugomvi nae wakapatana (huyo msanii) lakini bado huyo msanii amekua na chuki dhidi yake.  
 
Yani Diamond aliwahi kuwa na beef na huyo msanii wakayamaliza lakini bado jamaa ana chuki, hawezi kumtaja kwa sasa na anachofanya ni kuacha uchunguzi wa polisi ufanyike kwanza, ikigundulika ni kweli atamtaja hadharani. 
 
 Kuhusu huyo msanii namkariri zaidi Diamond akisema “Uhusiano wangu na huyu msanii hauko vizuri, tulishahitilafiana kama mwaka umepita tukapatana lakini bado ana chuki dhidi yangu, tatizo niliona liliisha lakini nikaona mwenzangu kama bado ananionyesha chuki hata nikikutana nae najifanya kama hakuna tatizo lakini moyoni najua mwenzangu kuna vitu ana viendeleza vya chinichini ambavyo sivielewi”  Diamond amesema hasara ya vitu vyake kwenye hizo fujo ina thamani ya milioni zaidi ya 13 kutokana na kuibiwa simu yake ya iPhone5, cheni pamoja na camera ya video ya thamani kubwa ambayo aliinunua kwa ajili ya website yake.

PICHA 15 ZA MOJA YA MAJUMBA YA TAJIRI WA NIGERIA, NYUMBA INA MSIKITI NA KANISA NDANI.

.
Hili ni moja ya majumba ya kifahari yanayomilikiwa na Mnigeria anaeshika nafasi ya pili kwa utajiri Nigeria kwa mujibu wa jarida la Forbes Mike Adenuga, hili ni jumba la mabilioni ya Naira ambalo liko kwenye ardhi ya bei ghali inayomilikiwa na wachache wenye pesa Nigeria, panaitwa Banana Island.
Mike Adenuga mfanyabiashara mkubwa Nigeria ambae pia ni mwenyekiti wa Globacom, pamoja na utajiri alionao nimeona ripoti mbalimbali kwamba amekua akitoa misaada ya mamilioni kwenye majanga tofautitofauti Nigeria.
Kwa mujibu wa blog ya Linda ni kwamba His billion Naira estate consists of 8 duplexes and an additional one for his personal residence with home office (the gold one), two watch towers and a multipurpose hall that sits 200 people, kuna swimming pool ya ndani, car park, helipad, yacht deck and it sits on roughly 3 hectares.
Ni jumba la kifahari ambalo pia lina msikiti na kanisa ndani yake ambapo kama haufahamu huyu ndio tajiri ambae aliwahi kuingia kwenye headlines Africa baada ya stori yake ya kumlipa Beyonce kuja kuimba kwenye harusi ya mtoto wake wa kike mwaka 2010.
.
.
.
Ujenzi bado unaendelea.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PICHA 4 ZA USHAHIDI WA BALOTELLI KUTAKA KUPIGANA NA KOCHA MANCINI MAZOEZINI LEO JAN 3.


Leo asubuhi Kocha wa Manchester City Roberto Mancini na mchezaji wake Mario Balotelli walitaka kupigana baada ya kocha Mancini kukasirishwa na kitendo cha Balotelli kumchezea rafu mchezaji mwenzake Scott Sinclair wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi ya Watford.
Baadhi ya makocha waliokua karibu ndio waliamua huo ugomvi ambao pamoja na kwamba Balotelli ndio alikua na makosa alikua mbishi wa kutokukubali au kukiri kosa na badala yake ndio akaendelea kupandishiana na Mancini tena mbele ya wachezaji wenzake.
Baada ya hapo Mario aliondoka zake na kuingia kwenye gari lake aina ya Bentley na kukutana na mashabiki nje ya uwanja waliokua wanahitaji awachoree autographs kisha akaondoka.
Wengi wamekua wakimshauri Mancini amuuze Balotelli lakini amekua akikataa na hata kwenye interview na Gazzetta mwezi uliopita Mancini alikaririwa akisema “nafikiri Balotelli ataendelea kukaa Man City ila inabidi akue  aache utoto, uhusiano wangu mimi na yeye ni mzuri siku zote hata akinikosea ila kwa sasa rungu la kazi halitakua na huruma tena kwake”
.
.
.

Wednesday, January 2, 2013

Angalia picha za show ya DIAMOND,OMMY,BEN POL NA DULLY SYKES kwenye usiku wa Wasafi @New Maisha Club




Iyobo sasa akifanya yake sasa....



President sasa nkaingia kwa stage....

















Msami Babyyyyyy

Zimepanda sasa...Nikumwaga ladhi tu LOL!
Chezea HK
Brother Dully mmmh! alikiamsha kinomanoma

Huenda hiki ndicho kilichomuua Sajuki....

Imegundulika kwamba Sadick Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki, aliyefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kumbe alipitiliza siku za kurudi kwa daktari ambapo alitakiwa kurudi hospitali India tangu tarehe 6 Desemba mwaka jana.
Hii ni kwa mujibu wa mke wa marehemu, Wastara ambaye aliwahi kumwambia mwandishi wa gazeti la Mwananchi kwamba Sajuki alipaswa kurejea India Desemba 6 mwaka jana, lakini alikwama kufanya hivyo kutokana na upungufu wa pesa. Hata hivyo alisema waliamua kuandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kutunisha mfuko wa matibabu yake.

Tamasha la kwanza la wasanii hao lilifanyika mkoani Iringa Novemba 25 mwaka jana na kupambwa na wasanii wengi wa muziki na filamu. Tamasha lingine lilifanyika Desemba 18 jijini Arusha.
Sajuki ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharimia matibabu yake, alifariki huku akiwa akipatiwa matibabu ya awali.
Alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, akisubiri kusafiri kwenda India kwa mara nyingine, kuendelea na matibabu

Kabla ya kulazwa Desemba 18 mwaka jana, Sajuki alifikishwa hospitalini hapo akitokea jijini Arusha, baada ya kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika, ili kumtazama katika Tamasha la Asante Tanzania.

Tukio hilo lilitokea katika tamasha hilo lililohusisha wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

Baada ya kupandishwa jukwaani, alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu,”ahhh” na kisha kudondoka akiwa juu ya jukwaa na kabla ya kutua chini, alidakwa na wasanii wenzake waliokuwa pembeni,”

Wasanii hao walimshusha jukwaani baada ya kumpumzisha kwa muda na kumtaka aende kupumzika zaidi. Akihojiwa baada ya tukio hilo, Sajuki alisema kwa sauti ya upole kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu. ”Hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana, sijisikii vizuri,”alisema Sajuki.

Hayo ndio maneno ya mwisho ya Sajuki kwa vyombo vya habari, wakati akiwa tayari amepitiliza siku zake za kurudi India, kuendelea na matibabu yake baada ya kukosa Sh28 milioni.

Tamasha la kwanza la wasanii hao lilifanyika mkoani Iringa Novemba 25 mwaka jana na kupambwa na wasanii wengi wa muziki na filamu. Tamasha lingine lilifanyika Desemba 18 jijini Arusha.

Ugonjwa wa Sajuki
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu, yalipamba moto.

Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini, mapema mwaka 2011 alipoanza kuugua. Mei mwaka 2012 alifanikiwa kwenda India kwa matibabu na baadaye alirejea nchini na kuonekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Waongoza Filamu wa Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri, hivi karibuni, Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu, uti wa mgongo na kansa ya ngozi.

Tuesday, January 1, 2013

TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI SAJUKI LEO. #RIP



Taarifa za uhakika ni kwamba kweli mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo asubuhi (jan 2 2013) katika hospitali ya Muhimbili.
Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012.
Dinno ambae ni rafiki wa karibu wa Sajuki ameiambia theHOODinfotainment kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.
Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.
Msiba upo Tabata, Mwenyenzi Mungu amlaze pema Sajuki.