Wednesday, May 15, 2013
PICHA YA LEO: HIVI NDIVYO LADY JAYDEE NA MME WAKE WALIVYOKWENDA MAHAKAMANI, LIKE BEYONCE NA JAY Z
12:29 AM
No comments
MWANAMUZIKI
Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' alifika Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia
kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. Katika hati ya madai
hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group
ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo
zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27
mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G.
Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha
makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.
MAAJABU: ANGELINA JOLIE AAMUA KUONDOA MATITI YAKE YOTE MAWILI NA KUNG'OA KIZAZI KWA UPASUAJI!!
12:22 AM
No comments
Mcheza sinema maarufu wa Kimarekani,
Angelina Jolie, ametangaza kwamba amefanyiwa operesheni ya kuondosha
matiti yake yote mawili ili kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya
maziwa na ya kizazi.
Kwa mujibu wa makala yake
iliyochapishwa leo kwenye gazeti la The New York Times na kupewa jina
"Chaguo langu la kitabibu", Angelina Jolie amesema ameamua kutangaza
jambo hilo hadharani ili kuwapa moyo wanawake wengine wenye historia ya
familia zinazouguwa saratani.
Mama yake mwenyewe Angelina alifariki
akiwa na miaka 56 kutokana na maradhi hayo. Sasa muigizaji huyo maarufu
wa sinema duniani, anasema anawataka wanawake wenye hali kama yake
kutafuta ushauri wa kitabibu na kufanya uamuzi baada ya kuwa na taarifa
za kutosha ili waweze kuendelea kufanya kazi, kama alivyofanya yeye.
"Licha ya kuweza kulifanikisha hili
na kubakia kimya kwa muda mrefu, sasa naandika kulitangaza kwa sababu
natarajia kuwa wanawake wengine wanaweza kufaidika na uzoefu wangu."
Ameandika mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya
wakimbizi.
Uamuzi mgumu lakini muhimu
Jolie aliamua kufikia uamuzi huo wa
kuyaondosha matiti yake yote mawili, kwa sababu alifahamishwa na
madaktari wake kwamba alikuwa na chembechembe inayoongeza hatari ya
kupata saratani kwenye maziwa yote mawili na kwenye fuko lake la uzazi.
Kutokana na chembechembe hiyo iitwayo
BRCA1, madaktari walikisia kwamba alikuwa kwenye kiwango cha asilimia
87 ya hatari ya kupata saratani ya maziwa na asilmia 50 ya kupata
saratani ya kizazi.
"Baada tu kujua kwamba huo ndio
ukweli kuhusu hali yangu, niliamua kuchukua hatua za kabla na angalau
kupunguza kiwango hicho cha hatari kadiri nilivyoweza. Nikafanya uamuzi
wa kuondosha matiti yangu yote mawili. Nilianza na maziwa kwa kuwa
saratani ya maziwa ni kubwa zaidi kuliko hatari ya ile ya fuko la uzazi,
na operesheni ya fuko la uzazi ni kubwa zaidi," ameandika Jolie.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37
amesema kwamba tarehe 27 Aprili alikamilisha miezi mitatu ya taratibu
za kitabibu kuhusiana na operesheni hiyo ya kuondosha matiti na kwamba
sasa kiwango cha uwezekano wa kupata saratani kimepungua hadi asilimia
tano.
Jolie na mumewe, ambaye pia ni
muigizaji maarufu, Brad Pitt, wana watoto watatu wa kuwazaa na watatu wa
kuwalea, na ameandika kwamba sasa anaweza kuwaambia watoto wake kwamba
hawapaswi kuwa na hofu ya kumpoteza mama yao kwa sababu ya saratani.
Diamond avaa gandwa za kijeshi za Congo (military police) kwenye show ya nchini humo
12:03 AM
No comments
Diamond anafahamika kwa kujaribu idea tofauti za kukonga nyoyo za mashabiki wake kwenye stage.
Akiwa kwenye ziara yake ya Burundi na Congo, Diamond alijaribu
kufanya kitu tofauti zaidi kwa kutinga nguo za military polisi (MP) za
jeshi la Congo. “Chef de l’armée… #CoNgo ,” ameandika Diamond kwenye
picha hiyo aliyoweka Instagram.
Tuesday, May 14, 2013
HUYU NDO MSICHANA ANAYELALAMIKA KUA MBUNGE KAMBAKA, SOMA FUL STORY HAPA
1:59 AM
No comments
BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya karne.
Katika uchunguzi wake, hivi karibuni gazeti hili lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
VYANZO
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
MAZITO
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).
MAZOEA YAANZAVYANZO
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
MAZITO
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).
Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.
KISA KUJISAIDIA HAJA NDOGO
“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.
HADI KITANDANI
Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”
AITA POLISI
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”
UBAKAJI/KUTISHIA KUUA
Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.
“Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz.
“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi kunisaidia, nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana kunifahamu.ASHINDA MAHAKAMANI
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule …. (anataka jina) ni mbakaji.
“Nimesharipoti mashirika mengi ya haki za binadamu ya Uingereza. Kuna siku nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame kizimbani ndipo dunia itajua ninachokisema.”
ASUBIRIWA KIZIMBANI
Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela.”
Uwazi, kabla ya kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Kilimanjaro, RPC Robert Boaz, Jumamosi iliyopita lilimtafuta RCO Ng’anza ambaye alisikiliza mkasa mzima na kudai kuwa hamfahamu Flora lakini alipobanwa alidai yeye siyo msemaji wa jeshi hilo kisha akakata simu.
KAMANDA WA POLISI
Kwa upande wake RPC Boaz alisema kuwa kipindi kinachotajwa cha mwezi Januari yeye alikuwa likizo ndefu na hajawahi kusikia habari kama hiyo lakini akaahidi kuifuatilia kwa RCO Ng’anza na baadaye arudishe majibu kwa Uwazi.
Alipotafutwa tena Jumapili iliyopita kwa njia ya simu yake ya mkononi hakupatikana hewani.
SASA NI ZAMU YA MBUNGE
Kama ilivyo desturi ya Uwazi, Jumamosi hiyohiyo lilimtafuta mbunge anayetajwa katika aibu hiyo kubwa huku akiwakilisha wananchi wa jimbo lake ambapo alisomewa kisa kizima kisha akapewa nafasi kuzungumzia au kufafanua kashfa hiyo ya karne.
Huku akirekodiwa neno kwa neno, mheshimiwa huyo alisema: “Huyo mwanamke (akatajiwa jina la Flora Lyimo) simfahamu lakini usikubali kushiriki kwenye dhambi ya kunichafua kwa sababu ni uongo.
Uwazi: Kwa hiyo mheshimiwa hujawahi kusikia habari hiyo?
Mbunge: Niliisikia, ninaifahamu. Ina karibia miezi nane sasa kwani ameibuka sasa hivi?
Uwazi: Sasa kama hiyo habari ni ya uongo kwa nini usimshitaki?
Mbunge: Habari hiyo ipo mtandaoni, kama nikisema nishitaki mitandao nitashitaki mingapi? Mbona …(anautaja mtandao wa kijamii wa Tanzania) wameshanichafua sana. Nikianza kuhangaika na kesi najua miaka yote mitano nitakuwa mahakamani badala ya kuendesha harakati jimboni mwangu.
Uwazi: Kama anakusingizia kwa nini wewe?
Mbunge: Huyo ametumwa na …(jina la mwanasiasa mkubwa nchini) na …(jina la chama), huko ni kuchafuana kwa sababu kama ni kunikamata, nani asiyejua jimbo langu, ofisi yangu, nyumbani kwangu na umaarufu wangu? Mwambie aje sasa hivi anikamate.
TURUDI KWA MLALAMIKAJI
Baada ya kusikia majibu ya mbunge huyo, Uwazi lilirudi kwa mlalamikaji Flora na kumweleza alichokijibu mbunge huyo ambapo na yeye alisema:
“Nawatumia picha wakati akiingia na kutoka kwangu kwani huku kuna kamera za mtaani zinachukua kila tukio. Unajua lazima abishe kwa sababu ni aibu kubwa kwake na chama chake.”
CHANZO UWAZI
Kwa mara nyingine anakuja Mwanadada Rappa Lady Yoo na young omega na ngoma yake mpya inakwenda kwa jina la KIVIPI
12:50 AM
No comments
Kwa mara nyingine anakuja Mwanadada Rappa Lady Yoo Akiwakilisha Sanawari akishirikiana na Yungo Omega toka River Camp Soldiers katika hili Hiphop Ragga Joint lilosukwa pande za Noizmekah Production Studios Arusha linakwenda kwa jina "Kivipi", Mpango mzima ni kuendeleza muziki wa Tanzania especially kwa Wanadada wanao struggle kuwakilisha katika fani. Download HAPA na kwa mawasiliano zaidi check na LadyYoo kupitia namba +255 758 394 470 Yung Omega kupitia +255 759 166 037
nu-joint<> ya cash clan yaja tena na 'wakali wa kitaa' icheki hapa
12:42 AM
No comments
Cash clan Yaja Tena na "Wakali wa Kitaa", Ngoma ambayo wamerekodi pande za noizmekah studios Arusha Tanzania kwa usimamizi wa producer Defxtro, Pata kuusikiliza HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania
huyu ndio rapper anayefanya zaidi muziki wa crunk na pia Trap kutoka A. Town. sikiliza na ku-download ngoma yake mpya hapa
12:31 AM
No comments
![]() |
| Anaitwa G-Hood toka Arusha, Newcomer aliyeanza harakati za kurekodi mwaka huu, na zaidi ni rapper anayefanya zaidi muziki wa crunk na pia Trap..Ngoma yake amefanya pande za Noizmekah studios akimshirikisha defxtro katika chorus ya wimbo huu wa "Naendelea Kutafuta" Download ngoma hii na endelea kusupport muziki wa Tanzania kwa mahojiano zaidi na mwasiliano check na G-hood kupitia +255 759 903 824 |
Monday, May 13, 2013
idea, aja na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "Kitambi show tu" sikiliza na ku-download hapa
8:33 AM
No comments
![]() |
| Msanii Chipukizi "Idea" toka kaskazini mwa Tanzania anakuja na wimbo wake wa "Kitambi show tu" Download HAPA na wasiliana naye kwa +255 755 673 156 |
HIVI NDIVYO LINEX ALIVYOMLIZA MAMA YAKE MZAZI MBELE YA UMATI WA MASHABIKI ZAKE
1:52 AM
No comments
Msanii Linex ambae amejizolea mashabiki kibao kutokana na umahiri wake katika kutumia sauti yake, jana amemliza mama yake mzazai pale alipokuwa akifanya show yake ya bure mkoani alipozaliwa, Kasulu, Kigoma.
Tangu Linex alipoanza safari yake ya muziki takribani miaka 3, mama yake mzazi hajawahi kumuona na kumshuhudia mtoto wake live akifanya show.Ni katika uwanja wa ambapo mama alimshudia mtoto wake akiwa amejaza umati wa watu kuja kumshuhudia akifanya show, ndipo alipokutana na umati huo na jinsi kila mmoja alivyokua akimshangilia na kujikuta akimwaga machozi na kumsababisha Linex kuangua kilio pia akiwa mbele za mashabiki wake.
Linex aliamua kufanya show hiyo bure mjini kwao kwa ajili ya kutoa sapotio kwa wanao msapoti..
"yaani nimeshangaa sana kukuta umati wa watu uwanjani, unajua Kasulu ni mji mdogo sana so kukuta watu wote wale sijui hata wametoka wapi, ki ukweli mama yangu hajawahi kuniona nikifanya show, jana ndio ilikua mara yake ya kwanza, na alishangaa sana kuona watu ni wengi na wanashow love ya hatari..wakati mi naimba pale, nilimuona mama yangu na furaha mpaka anatoka machozi, ki ukweli nilijikuta na mimi naangua kilio tu, ila ilikua nzuri sana na watu wamefurahi sana" amesema Linex
Saturday, May 11, 2013
Picha ya mtu anayefanana na Jay-Z ‘copyright’ ya mwaka 1939 yawashangaza wengi
2:23 PM
No comments
Jana wafanyakazi wa maktaba ya Schomburg Center ya New York Marekani
wamepata picha ya mtu ya mwaka 1939 anayefanana na Jay-Z kila kitu.
Picha hiyo imewafanya baadhi ya watu waamini kuwa hiyo ni Jay-Z na
aliishi mitaa ya Harlem, miaka ya 1930s. Tazama video hii ya TMZ uone
wanavyoijadili picha hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
























































