Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, October 9, 2013

DIAMOND, ACHAFUKWA NA ROHO KWA PRODUCER ALIYEVUJISHA "NIKIFA KESHO"

 

Kuvujisha Nyimbo yangu hakuwezi kunipunguzia 
wala Kunidhuru chochote... Sanasana utanizidishia 
Umaarufu na kunipa Show zaidi... Kama nimeacha kurecord nyimbo
 Studio kwako Uspanick, Relax.. tafta Msanii mwingine 
 Mkali zaidi yangu umrecordie Ngoma Ahit kushinda mimi...
.ila Kuvujisha Unajisumbua bure!

Hisia zangu za pelekea kuandika haya nikiwa na uzuni 
ndani yake kwa kuwa muda nilioutmia na akili nliotumia
 dhairi ni Mungu Pekee anajua ndio Maana aina budi 
namwachia Mungu pia....Imani iliyo ndani yangu nikiamini 
kuwa kutoa ya Moyoni uufanya Moyo kujengeka
 Upya,Mwenyezi Mungu Atanijenga Upya na kuwaandalia kitu kipya hiv
 karibun.Hii ni changamoto kwangu na Kuweza 
kujua sheria na katiba za Muziki wangu na
 kusimamia Haki zangu...... Nawapenda Sana Mashabiki Zangu..... 
 #WCB #CocaBoy for Life

DIAMOND PLATINUMZ ASIKITISHWA NA PRODUCER ALIYEVUJISHA WIMBO WAKE MPYA WA "NIKIFA KESHO"

Written By Emmanuel Shilatu on Wednesday, October 9, 2013 | 2:21 PM


"Kuvujisha wimbo wangu hakuwezi kunipunguzia 
wala kunidhuru chochote... Sana sana utanizidishia 
umaarufu na kunipa Show zaidi... kama nimeacha ku-record wimbo
  studio kwako usi-panick, relax.. tafuta msanii mwingine 
  mkali zaidi yangu umrekodie ngoma a- hit kushinda mimi...
.ila kuvujisha unajisumbua bure!

Hisia zangu za pelekea kuandika haya nikiwa na huzuni 
ndani yake kwa kuwa muda nilioutmia na akili nliotumia
 dhahiri ni Mungu pekee anajua ndio maana sina budi 
kumwachia Mungu pia....imani iliyo ndani yangu nikiamini 
kuwa kutoa ya moyoni hufanya moyo kujengeka
  upya, mwenyezi Mungu Atanijenga upya na kuwaandalia kitu kipya hivi
 karibuni. Hii ni changamoto kwangu na Kuweza 
kujua sheria na katiba za muziki wangu na
 kusimamia haki zangu...... Nawapenda mana Mashabiki wangu..... #WCB #CocaBoy for Life"
- See more at: http://shiladeux.blogspot.com/2013/10/diamond-platinumz-asikitishwa-na.html#sthash.q7RwEwNC.dpuf

DIAMOND PLATINUMZ ASIKITISHWA NA PRODUCER ALIYEVUJISHA WIMBO WAKE MPYA WA "NIKIFA KESHO"

Written By Emmanuel Shilatu on Wednesday, October 9, 2013 | 2:21 PM


"Kuvujisha wimbo wangu hakuwezi kunipunguzia 
wala kunidhuru chochote... Sana sana utanizidishia 
umaarufu na kunipa Show zaidi... kama nimeacha ku-record wimbo
  studio kwako usi-panick, relax.. tafuta msanii mwingine 
  mkali zaidi yangu umrekodie ngoma a- hit kushinda mimi...
.ila kuvujisha unajisumbua bure!

Hisia zangu za pelekea kuandika haya nikiwa na huzuni 
ndani yake kwa kuwa muda nilioutmia na akili nliotumia
 dhahiri ni Mungu pekee anajua ndio maana sina budi 
kumwachia Mungu pia....imani iliyo ndani yangu nikiamini 
kuwa kutoa ya moyoni hufanya moyo kujengeka
  upya, mwenyezi Mungu Atanijenga upya na kuwaandalia kitu kipya hivi
 karibuni. Hii ni changamoto kwangu na Kuweza 
kujua sheria na katiba za muziki wangu na
 kusimamia haki zangu...... Nawapenda mana Mashabiki wangu..... #WCB #CocaBoy for Life"
- See more at: http://shiladeux.blogspot.com/2013/10/diamond-platinumz-asikitishwa-na.html#sthash.q7RwEwNC.dpuf

ANGALIA HAPA JINSI MTANGAZAJI WA CLOUDS FM EPHRAHIM KIBONDE ALIVYOPATA AJALI MAPEMA HII

Ephraim Kibonde akishuka kwenye gari baada ya ajali.
..Akilikagua gari lake.
Trafiki akiwa eneo la ajali.
Gari la Kibonde likiwa eneo la ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City baada ya ajali.
Fundi akirekebisha gari hilo baada ya ajali.
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde amepata ajali ya gari leo asubuhi  katika barabara ya Sam Nujoma kwenye ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City. Gari alilokuwa anaendesha Kibonde aina ya Toyota Carina lenye nama za usajili T 733 BVE limeharibika kwa mbele katika ajali hiyo.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)

HAYA SASA..!! UKIFANYA HIVI HUMKOSI MSICHANA YEYOTE YULE WA FACEBOOK..!!


Hello cool peoples. Thanks for stopping by let's go straight to the point(s).
1) Your username must be appealing! For example; 2buff, ImHotterThanFire, LadiesMan, IhaveSixPacks, ExtraSwag, etc.
2) Don't be too desperate. Chill out. Don't go around asking for babes' phone numbers and email addies.
3) Concentrate/Focus on the on their profiles, single ladies full ground for facebook.
4) If you're fine enough, put your picture on your profile. If you're not, PLS DON'T BOTHER. If you want extra attention and you're not so fine, go steal a believable picture of a Fine man from the internet and claim it as yours. You don hammer be that! 
5) Post sensibly. Don't be too LefuLefu-ish, or C0rk-ish, or 190-ish. Post like a normal human being.
6) ALWAYS SUPPORT THE LADIES! BE A MALE FEMINIST! Don't hesitate to argue with your fellow men while you take the ladies' side (even when you know your argument is not making any sense). Relax buddy- Take the insults hurled at you. You're earning cool points from the ladies! 
7) When you see that ladies have started noticing you; LEAVE YOUR EMAIL ADDY ON YOUR PROFILE. Leave it there! No remove am o! 
Now sit back and watch females fall for you, even when they know you have no intention of catching them . You'll thank me later.

Tuesday, October 8, 2013

UNYWAJI POMBE KUPINDUKIA CHANZO CHA KUTOPATA / KUTOSABABISHA MIMBA.




Hii inaweza kuwa habari mbaya kwa watengenezaji au wauzaji wa vinywaji hivi au hata kwa uchumi wa Nchi, lakini huu ndio ukweli halisi.
Kwamba, tatizo la unywaji pombe kupita kiasi linaongezeka katika jamii kila siku za hivi karibuni na linawahusisha wote, vijana, watu wazima na hata wazee.

Pombe za aina mbalimbali na ujazi tofauti zimekuwa zikizalishwa viwandani au kwa njia za kienyeji kila siku na kasha kuuzwa kwa bei ndogo ya hadi sh 200 ya kitanzania ili mradi mtu aweze kuimudu.

Kwa vijana wanaotumia vileo hivyo, wengi wao hujitetea wakisema kuwa wanajiburudisha huku wengine wakisema kuwa wanatumia kinywaji husika ili kupunguza msongo wa mawazo, kupunguza au kujiepusha na ugumu wa maisha.

Hizi zote zinaweza kuwa sababu nzuri kulingana na mazingira ya mhusika mwenyewe, lakini nyuma yake kuna madhara.
Unaweza kuijuliza je, wengi wanao kunywa aina mbalimbali za pombe katika maisha yao wanafahamu kuwa unywaji huo hasa ule wa kupitiliza kiasi unaweza kuwasababishia matatizo kiafya likiwamo la kupunguza uwezo wa kupata watoto?

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha SURREY cha uingereza unathibitisha suala hilo na kueleza kuwa kutokana na kuongezeka kwa matatizo ya uzazi kwa wanandoa katika miaka ya hivi karibuni, pombe imekuwa chanzo cha kuparanganyika kwa ndoa, kukosa watoto pia.
Kwa sababu hiyo, chuo kikuu hicho kiliamua kufanya utafiti kwa kuwahusisha wanandoa kadhaa waliokuwa wanakabiliwa na tatizo la mmoja wao kushika mimba.

Utafiti huo ulibainisha kuwa ongezeko la tatizo hilo katika miaka ya karibuni limechangiwa na kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfum wa maisha ya binadamu, hususani katika masuala ya ulaji vyakula.
Utafiti huo ulonyesha kuwa wanandoa ambaowalikuwa na historia ya matatizo ya uzazi walibadilisha mfumo wao wa maisha, kwa kufuata kanuni za ulaji wa chakula na kuacha au kupunguza matumizi ya pombe walifanikiwa kwa asilimia 80 kuondokana na tatizo hilo.

Pia, utafiti huo ulibainisha kuwapo kwa uhusiano mkubwa uliopo kati  ya chakula anavyokula mtu na uwezo wake wa kuweza kuzaa.
Wataalamu wanasema kuwa unywaji wa pombe kwa kiasi Fulani huchangia katika kupunguza uwezo wa kuzaa kwa mwanamke na mwanamume
Imebainika kuwa unywaji pombe kwa kiwango chochote huunguza nusu ya uwezo wa uzazi kwa mhusika

Kwa upande wa mwanamke anayekunywa chini ya uniti 5 ambazo ni sawa na ujazo wa glasi ya milimita 175 anao uwezo mkubwa wa kupata ujauzito ndani ya kipindi cha miezi sita ukilinganisha na Yule anaye kunywa zaidi.
 
Utafiti huo unaonyesha kuwa unywaji pombe husababisha kupungua kwa idadi za mbegu za kiume kwa mwanamume na pia hupunguza kasi yake katika mwili kiasi kwamba pindi uzazi zinapotoka na kuingia sehemu za uzazi za mwanamke zinakuwa hazina nguvu na hivyo kuathiri ubora wake.

Pia, unabaini utafiti huo kuwa pombe hufanya mwili wa binadamu kushindwa kufyonza vimeng’enyo vinavyopatikana katika vyakula  kama vile madini ya zinki, ambayo ni muhimu kwa kurutubisha mbegu za mwanamume na kiandaa mwili wa mwanamke kwa ajiri ya kutunga ujauzito.
Utafiti huo unabainisha kuwa kama unajitayarisha kupata motto inabidi kuachana na matumizi ya ombe na kahawakwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa katika hilo.


NINI UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA POMBE.

Daktari wa magonjwa ya kinamama kutoka Hospitali ya taifa ya muhimbili, anasema kuwa japo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya pombe na viungo vya uzazi vya binadamu lakini kuna ukweli kwamba pombe huchangia katika kupunguza uwezo wa mtu kutunga mimba au kusababisha mimba.
Kama mtu hana tatizo lolote la kiafya linalomfanya ashindwe kupata motto, pombe inaweza ikasababisha kutokea kwa tatizo hilo kwa mtu huyo.


Suala zima la mfumo wa uzazi linaendeshwa na ubongo ilihali unywaji pombe kupita kiasi nako huathiri mfumo wa fahamu , hivyo ni lazima kwa mtu anayetumia pombe katika kiwango hicho kukumbana na tatizo hilo.
Hata katika hali ya kawaida ili mtu aweze kusababisha au kusika mimba ni lazima ashiriki kikamilifu katika tendo la kujamiiana na ikiwa amelewa atashindwa kushiriki kikamilifu kwani tendo hilin huhusisha akili zaidi.

Mfumo wa uzazi unaendeshwa na ubongo hivyo mtu akiwa mlevi wa kupindukia kuna uwezekano mkubwa uwezo wake wa kupata au kusababisha mimba ukawa mdogo.
Pia unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu kunaweza kusababisha uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni na kusababisha kupoteza tamaa na kutosisimka wa mwanaume.
Pombe ina athari nyingi kwa mwili wa binadamu kwani pamoja na kuathiri  kondo la uzazi na mayai ya uzazi kwa mwanamke na mwanaume, Pia huleta madhara kwa viungi vingine kama figo na ini.

Kama pombe itatumiwa katika kipindi cha ujauzito inaweza kuathiri hata ukuaji wa mtoto aliyeko tumboni, kwani huyuka kizuizi cha kondo la nyuma (placenta) na inaweza kudidimiza ukuaji wa kijusi.
Kwa ujumla pombe ina madhara ya kiafya kwa mwili wa binadamu, hivyo kabla mtu hujaamua kuitumia inabidi  kutafakari athari na faida zake ili akinywa awe na taarifa sahihi kuhusiana na kitu gani kinaingia mwilini mwake.

‘’UNYWAJI POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO
KUNYWA KISTAARABU’’

TAARIFA KAMILI KUTOKA KWA DIAMOND:I REAL LOVE MY PENNY,SINA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA WEMA



Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada
 Wema Sepetu tuna mahusiano ya Kimapenzi, kitu
 ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu 
yeye kucomment kwenye Account yangu ya Instagram?..

 Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko
 kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? 
Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana 
Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda
 wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania
 na si kuekeana chuki zisizo nanfaida..
I REAL LOVE MY PENNY,SIJARUDIANA NA WEMA.

Monday, October 7, 2013

WEMA, DIAMOND WAMTESA PENNY

Stori: Mwandishi Wetu
ISHU ya wapenzi zilipendwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kurudiana inadaiwa kumtesa mpenzi wa sasa wa Diamond ambaye ni mtangazaji wa DTV, VJ Penniel Mungilwa ‘Penny’ hivyo kulazimika kukiri kuwa hajawahi kupitia wakati mgumu kama anaopitia sasa.

 
Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ enzi za penzi lao.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Penny, mwanadada huyo amekuwa akikosa amani kila anaposikia habari za Wema kurudiana na Diamond hivyo kuwa katika wakati mgumu.
“Watu wanapomwambia au kumuuliza Penny habari za Diamond kurudiana na Wema amekuwa akiumia sema tu watu hawajui,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuwa habari ya mjini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Penny alifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anachokifanya ni kuhakikisha anamshikilia staa huyo wa Bongo Fleva hadi hapo Mungu atakapoamua vingine.
“Katika uhusiano niliowahi kuwa nao huu ni mgumu mno,” ilisomeka sehemu ya utetezi wa Penny aliouandika juu ya penzi lake na Diamond.

Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Hakuishia hapo kwani aliendelea kujitetea kwa wadau wake ambao walimjibu kuwa kinachoonekana anamhofia Wema ambaye akikita penzi lake kwa Diamond, kwa ustaa wake, atamfanya mwanamuziki huyo kuendelea kuliweka juu jina lake.
Katika maelezo yake, Penny alikiri kuwa mapenzi yanatesa lakini anaamini mateso hayo ni ya muda tu hivyo liwalo na liwe yeye anampenda Diamond.
Wiki iliyopita, Wema na Diamond waliripotiwa wakidaiwa kurejesha upya penzi lao lililozimika mwaka jana, jambo ambalo lilimpa Penny wakati mgumu huku akieleza kuwa anachoamini ni kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa penzi hilo.

Wednesday, October 2, 2013

DALILI NANE (8) ZA MWANAMKE ANAYETOKA NJE YA NDOA

Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume. 
Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa.  Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.

 Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:

 1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

 2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.
 Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unaofanywa.


 3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi. 
 Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4. KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda. 
Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.

 5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki. 

 Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

 6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana. 
 Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.
7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake. 

 Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.


 8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana. 

 Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe

Audio: Jinsi Chidi Benz na Cassim walivyowashiana Club Billicanas

Kuna sababu kubwa kwanini Bongo5 haikuandika habari iliyodai kuwa Nay wa Mitego na Chidi Benz wamepatanishwa na Cassim Mganga na sasa ni amani tu. Kilichotokea sasa ni kwamba, Chidi Benz anamuita Cassim Mganga Mchawi, kauli ambayo ambayo iliwafanya hivi karibuni watukanane matusi ya nguoni Club Billicanas, na kama wasingekuwepo watu waliowazuia, wangetoana meno siku hiyo.
IMG_9071
“Mwacheni asinizingue mimi, nakosea mimi kila siku,” anasikikia Cassim akiongea kwenye audio iliyorekodiwa na kuifikia mikono ya Soudy Brown wa U Heard. “Mimi nimekosea nini Benz apige was**ge wengine mimi hawezi kunifanya lolote, msimshike, aniguse halafu aone. Mimi si maisha yangu, nahangaika nafanya muziki wangu wanasema mimi mchawi, mimi nina familia yangu, mimi sio mchawi, namroga nini mimi, yeye stress zake, anavuta unga, mimi namsingizia? Kila mtu anajua, yeye si life yake amechagua? Asinizingue, mimi mwanaume power kama yeye.”
Sikiliza mwenyewe hapa.

TAZAMA BAADHI YA PICHA ZA MAZISHI YA MSANII MAC2B WA WATEULE/MACMALICK/SIMBA HAPA


 Moja ya wasanii ambae walikuwa pamoja kwenye kundi la Wateule...Mchizi Mox
Kaburi ambalo msanii MacMalick alizikwa jana hukoYombo kwa Abiola.
 Msanii huyo MacMalick alifariki juzi kutokana na miguu kujaa maji.Kwa mujibu wa familia yake msanii huyo hajaacha mke wala mtoto.Baadhi ya wasanii na maproduza waliofanya nae kazi kama Lamar wa Fishcrab,Mchizi Mox,Daz Baba na Enrico wa Sound Crafters walikuwepo kwenye mazishi hayo.

TISHIO LA AL-SHABAAB BONGO...HATARI NO.1

Na Richard Bukos

SIKU chache baada ya kundi la kigaidi la Al-Shabaab kutekeleza mauaji kwenye jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu 69, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar walipiga simu Global Publishers na kudai kuwa, baadhi ya maeneo Dar yamekuwa na ulinzi dhaifu kuhusu kupambana na ugaidi.
Walisema maeneo kadhaa Dar hususan yenye mikusanyiko ya watu, wapo wanaopita na silaha kama bunduki bila kugundulika, jambo ambalo walilitafsiri kama hatari kubwa katika nyakati hizi za vitisho vya kigaidi.
WATAHADHARISHA TISHIO LA AL-SHABAAB

Wakazi hao waliendelea…
Na Richard Bukos
SIKU chache baada ya kundi la kigaidi la Al-Shabaab kutekeleza mauaji kwenye jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu 69, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar walipiga simu Global Publishers na kudai kuwa, baadhi ya maeneo Dar yamekuwa na ulinzi dhaifu kuhusu kupambana na ugaidi.

HAYA NDIYO MANENO ALIYOANDIKA WEMA SEPETU BAADA YA KUCHAFULIWA NA GAZETI LA FILAMU


clip_image003                       C.E.O wa kampuni ya Endless Fame Film maarufu kma Wema Sepetu ameonekana kuchukizwa na kitendo cha kuchafuliwa kwa jina lake katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini.
Mapema asubuhi ya leo kupitia account yake ya Instagram mwanadada Wema alitupia picha ya gazeti hilo lililo mchafulia jina kwa kumuandika kuwa "Wema Kunyongwa China Awaomba Watanzania Wamuombee".
Pia dakika chache zilizopita kupitia account yake hiyohiyo ya Instagram wema amefunguka zaidi kwa kitendo hicho cha kuchafuliwa jina na kuandika hivi ...
Soma hapa chini ...

Taarifa kamili juu ya Irene Uwoya kaacha kuigiza na sababu iliomfanya achukue maamzi hayo

Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.
Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”

Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.

Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.

Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.

Show yake ya TV imeshaanza kuonekana Tanzania pamoja na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii kubwa ya kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba zao zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.
Show kama hii ambae inaitwa Extreme Makeover: Home Edition inapatikana kwenye BBC Lifestyle ikiletwa kwako kila siku saa 18:10 CAT.
                
               credit by  www.dstv.com