Hii inaweza kuwa habari
mbaya kwa watengenezaji au wauzaji wa vinywaji hivi au hata kwa uchumi wa Nchi,
lakini huu ndio ukweli halisi.
Kwamba, tatizo la
unywaji pombe kupita kiasi linaongezeka katika jamii kila siku za hivi karibuni
na linawahusisha wote, vijana, watu wazima na hata wazee.
Pombe za aina
mbalimbali na ujazi tofauti zimekuwa zikizalishwa viwandani au kwa njia za
kienyeji kila siku na kasha kuuzwa kwa bei ndogo ya hadi sh 200 ya kitanzania
ili mradi mtu aweze kuimudu.
Kwa vijana wanaotumia
vileo hivyo, wengi wao hujitetea wakisema kuwa wanajiburudisha huku wengine
wakisema kuwa wanatumia kinywaji husika ili kupunguza msongo wa mawazo,
kupunguza au kujiepusha na ugumu wa maisha.
Hizi zote zinaweza kuwa
sababu nzuri kulingana na mazingira ya mhusika mwenyewe, lakini nyuma yake kuna
madhara.
Unaweza kuijuliza je,
wengi wanao kunywa aina mbalimbali za pombe katika maisha yao wanafahamu kuwa
unywaji huo hasa ule wa kupitiliza kiasi unaweza kuwasababishia matatizo kiafya
likiwamo la kupunguza uwezo wa kupata watoto?
Utafiti uliofanywa na
chuo kikuu cha SURREY cha uingereza unathibitisha suala hilo na kueleza kuwa
kutokana na kuongezeka kwa matatizo ya uzazi kwa wanandoa katika miaka ya hivi
karibuni, pombe imekuwa chanzo cha kuparanganyika kwa ndoa, kukosa watoto pia.
Kwa sababu hiyo, chuo
kikuu hicho kiliamua kufanya utafiti kwa kuwahusisha wanandoa kadhaa waliokuwa
wanakabiliwa na tatizo la mmoja wao kushika mimba.
Utafiti huo ulibainisha
kuwa ongezeko la tatizo hilo katika miaka ya karibuni limechangiwa na kiasi
kikubwa na mabadiliko ya mfum wa maisha ya binadamu, hususani katika masuala ya
ulaji vyakula.
Utafiti huo ulonyesha
kuwa wanandoa ambaowalikuwa na historia ya matatizo ya uzazi walibadilisha
mfumo wao wa maisha, kwa kufuata kanuni za ulaji wa chakula na kuacha au
kupunguza matumizi ya pombe walifanikiwa kwa asilimia 80 kuondokana na tatizo
hilo.
Pia, utafiti huo
ulibainisha kuwapo kwa uhusiano mkubwa uliopo kati ya chakula anavyokula mtu na uwezo wake wa
kuweza kuzaa.
Wataalamu wanasema kuwa
unywaji wa pombe kwa kiasi Fulani huchangia katika kupunguza uwezo wa kuzaa kwa
mwanamke na mwanamume
Imebainika kuwa unywaji
pombe kwa kiwango chochote huunguza nusu ya uwezo wa uzazi kwa mhusika
Kwa upande wa mwanamke
anayekunywa chini ya uniti 5 ambazo ni sawa na ujazo wa glasi ya milimita 175
anao uwezo mkubwa wa kupata ujauzito ndani ya kipindi cha miezi sita
ukilinganisha na Yule anaye kunywa zaidi.
Utafiti huo unaonyesha
kuwa unywaji pombe husababisha kupungua kwa idadi za mbegu za kiume kwa
mwanamume na pia hupunguza kasi yake katika mwili kiasi kwamba pindi uzazi
zinapotoka na kuingia sehemu za uzazi za mwanamke zinakuwa hazina nguvu na
hivyo kuathiri ubora wake.
Pia, unabaini utafiti
huo kuwa pombe hufanya mwili wa binadamu kushindwa kufyonza vimeng’enyo
vinavyopatikana katika vyakula kama vile
madini ya zinki, ambayo ni muhimu kwa kurutubisha mbegu za mwanamume na kiandaa
mwili wa mwanamke kwa ajiri ya kutunga ujauzito.
Utafiti huo unabainisha
kuwa kama unajitayarisha kupata motto inabidi kuachana na matumizi ya ombe na
kahawakwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo ili kujiweka katika nafasi nzuri
ya kufanikiwa katika hilo.
NINI
UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA POMBE.
Daktari wa magonjwa ya
kinamama kutoka Hospitali ya taifa ya muhimbili, anasema kuwa japo hakuna
uhusiano wa moja kwa moja kati ya pombe na viungo vya uzazi vya binadamu lakini
kuna ukweli kwamba pombe huchangia katika kupunguza uwezo wa mtu kutunga mimba
au kusababisha mimba.
Kama mtu hana tatizo
lolote la kiafya linalomfanya ashindwe kupata motto, pombe inaweza ikasababisha
kutokea kwa tatizo hilo kwa mtu huyo.
Suala zima la mfumo wa
uzazi linaendeshwa na ubongo ilihali unywaji pombe kupita kiasi nako huathiri
mfumo wa fahamu , hivyo ni lazima kwa mtu anayetumia pombe katika kiwango hicho
kukumbana na tatizo hilo.
Hata katika hali ya
kawaida ili mtu aweze kusababisha au kusika mimba ni lazima ashiriki kikamilifu
katika tendo la kujamiiana na ikiwa amelewa atashindwa kushiriki kikamilifu
kwani tendo hilin huhusisha akili zaidi.
Mfumo wa uzazi
unaendeshwa na ubongo hivyo mtu akiwa mlevi wa kupindukia kuna uwezekano mkubwa
uwezo wake wa kupata au kusababisha mimba ukawa mdogo.
Pia unywaji wa pombe
kupindukia kwa muda mrefu kunaweza kusababisha uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva
na mfumo wa neva za pembeni na kusababisha kupoteza tamaa na kutosisimka wa
mwanaume.
Pombe ina athari nyingi
kwa mwili wa binadamu kwani pamoja na kuathiri
kondo la uzazi na mayai ya uzazi kwa mwanamke na mwanaume, Pia huleta
madhara kwa viungi vingine kama figo na ini.
Kama pombe itatumiwa
katika kipindi cha ujauzito inaweza kuathiri hata ukuaji wa mtoto aliyeko
tumboni, kwani huyuka kizuizi cha kondo la nyuma (placenta) na inaweza
kudidimiza ukuaji wa kijusi.
Kwa ujumla pombe ina
madhara ya kiafya kwa mwili wa binadamu, hivyo kabla mtu hujaamua kuitumia
inabidi kutafakari athari na faida zake
ili akinywa awe na taarifa sahihi kuhusiana na kitu gani kinaingia mwilini mwake.
‘’UNYWAJI
POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO
KUNYWA
KISTAARABU’’
0 comments:
Post a Comment