Tuesday, May 28, 2013
SABABU 4 KWANINI RAFIKI ZAKO NI HATARI ZAIDI KULIKO ADUI ZAKO, SOMA MAKALA HII KUTOKKA MBUKE TIMES BLOG
3:58 AM
No comments
Pamoja na ukweli kwamba rafiki ni muhimu katika maisha, makala hii inachambua namna nne (4) ambapo rafiki wanaweza kuwa hatari zaidi ya adui zako. Kinachoelezwa katika makala hii ni kuwa uhatari wa rafiki upo katika namna urafiki unavyoendeshwa. Jisomee mwenyewe:-
1. Kioo: Mara nyingi tunajikuta kuwa tunaamini zaidi mtazamo wa rafiki zetu kuhusu sie, kuliko vile utashi wetu unavyotuambia. Tunafanya mambo mengi kwa imani na ufahamu tuliojijengea kichwani kuwa kufanya hivyo ndio kunakotarajiwa na rafiki zetu. Kwa kifupi, yale yanayoonekana kuwa yanafaa machoni mwa rafiki zetu –iwe mavazi, lugha, matumizi ya fedha, hata aina ya mwenza wa maisha, ndio hayo tunayojitahidi kuyafanya. Hivyo kama rafiki zetu wana mtazamo usio chanya, basi tunajikuta tunaelekea pabaya pia.
2. Tunajiweka watupu mbele zao: Kwakuwa tumewapa ‘kitambulisho’ cha kuwa wao ni rafiki zetu, tunajihisi tupo salama kuelezea mambo yetu ya msingi kimaisha kama vile habari za familia, biashara, masomo, na hata mapenzi. Tena kuna nyakati tunadiri hata kuwaambia siri zetu. Hali hii ya ‘kujiweka mtupu’ mbele yao ni hatari kwani taarifa tunazo ‘share’ nao zinaweza kutumika kutuangamiza, si umewahi kusikia “Information is Power” ? Kwa sababu hii ni rahisi kwa marafiki kutudhuru kama mwanamuziki Shaa alivyoimba katika wimbo Shoga.
3. Ushindani: Kwakuwa rafiki ndio watu wa karibu zaidi kwetu, na kama tulivyoeleza hapo juu mara nyingi wao ndio kioo chetu, tunajikuta tukijiingiza kwenye ushindani nao kwa kusudia au bila kutarajia, kwakutaka kuwa kama wao au zaidi yao. Na wao pia kwa kukusudia au bila kukusudia kwakuwa wanatufahamu vizuri nao wanajikuta wakianzisha ushindani ili kuwa kama sisi au zaidi yetu. Hali hii ya kutaka ushindani kati yetu, ukizingatia kuwa tumekwishajiweka ‘watupu’ mbele za rafiki zetu, inafanya rafiki hao kuwa ni hatari zaidi ya hata adui zetu wa sasa.
Wakati mwingine ushindani wa marafiki zetu hujidhirisha waziwazi kama mwanamuziki Nyota Ndogo alipokeza kwenye wimbo Watu na Viatu.
Wakati mwingine ushindani wa marafiki zetu hujidhirisha waziwazi kama mwanamuziki Nyota Ndogo alipokeza kwenye wimbo Watu na Viatu.
4. Dhambi ya kutenga watu: Tunaposisitiza kutazama binadamu wenzetu katika makundi mawili ya adui na rafiki, twaweza kujikuta tukiwapa umuhimu na thamani kubwa rafiki, na kuwatenga maadui. Kutenga huku kutaendelea kwani ndani ya hao unaoona rafiki, unaweza chambua zaidi na zaidi na kuona kumbe baadhi sio rafiki, ni maadui. Kutenga huku mara nyingi hufanyika wazi wazi, hivyo kumfanya rafiki kujihisi wa kipekee, nap engine kutumia nafasi hii kukuumiza, bila wewe kutambua kwa haraka, kwani ni unajua huyo ni mmoja wa watu wako.
HITIMISHO:
Ni jambo zuri sana kuwa na rafiki, na rafiki ni muhimu sana. Hata hivyo, ni jukumu lako kusimamia vema urafiki wako na watu wengine. Haitoshi tuu kuwa na rafiki wema, bali unapaswa kujua namna ya kuishi na hao rafiki wema. Endelea kuwa na maamuzi binafsi, tafuta uhuru wa fikra na usiogope kuwa na mtazamo tofauti na rafiki zako.
Nimalizie makala hii kwa nukuu hizi:
“ Tunaweza kuwamudu adui zetu, Mungu tulinde dhidi ya Rafiki Zetu” – Martin Luther
“ Nilimuomba Mungu aniondolee maadui, nikaanza kuona rafiki wakipungua”- Meek Mill.
Sunday, May 26, 2013
ANGALIA PICHA YA BABA ALIVYOMCHOMA MOTO MWANAE SEHEMU ZA SIRI KISHA KUTOKOMEA PASIPOJULIKANA:
7:22 AM
No comments
![]() |
| The father of two year old girl has absconded after his attempts to cure her with boiling water left her with severe burns on her buttocks and genital parts. The father, who is unidentified, is said to have held the little girl over boiling water to cure her of candidyasis. But she fell into the hot water and sustained severe injuries. The young girl is currently at the 37 Military Hospital where she is receiving treatment. Doctors attending to the girl say she is responding to treatment. Women’s rights group, WILDAF, which is assisting the mother of the girl to seek treatment, has condemned the father’s action. Programme Coordinator Bernice Sam says his act constitutes abuse and negligence, for which he must be arrested. She would however not ask for his imprisonment if found guilty. She suggested counseling for the man who is said to have fathered seven children with his wife |
Saturday, May 25, 2013
HAYA NI MAAJABU YA DUNIA !!!, AMA MAAJABU YA MWENYEZI MUNGU ?.
11:15 PM
No comments
![]() |
| KUKU MWENYE VICHWA VIWILI SIJUI KWELI !. |
HII NI NGOZI ILIYOTOBOLEWA CHINI YA KIDEVU CHA MWANAMKE IKIWA NGOZI HIYO IMEVUTWA NA WAYA, KWA WALE WA WAKAZI WA KUS
INI HASA MIKOA YA LINDI NA MTWA SEHEMU HIYO HUITA SEHEMU YA KUWEKEA NDONYA. (KIPANDE CHA MTI KILICHONGWA KAMA SALAFU)
HUYU MBABA AKIWA AMETABASAMU
![]() |
| HUYU NI MBWA NAFIKIRI ATAKUWA MBWA MREFU KULIKO WOTE DUNIANI KAMA MFUMO WA KOMPUTA HAUKUFANYA KAZI YAKE. |
KUNDI BORA LA MWAKA NI TYM YAO JAMBO SQUAD SASA.
12:52 AM
No comments

kupitia
kundi bora la mwaka, Jambo Squad ndio tym yao sasa, wewe kama funs
wakaribu wa machalii ya R, watoto wa bibi wapigie kura kuwa KUNDI BORA
LA MWAKA, Jinsi ya kuwapigia kura unaandika CF1 kisha unatuma kwenda 15345
kuchagua Jambo Squad kuwa kundi bora la mwaka. Tuwape support watu na
tuendeleze na kuipresent game ya music A.Town.
Friday, May 24, 2013
LADY JAY DEE NAYE AMSHANGAA MWANA FA. KUTOKANA NAYE KUANDAA SHOW TAREHE MOJA NA KUAMUA KUMCHUKUA LINNAH..Soma Alichosema
7:40 PM
No comments
Kutokana na JIDE kuwa na show yake kubwa
mnamo tarehe 31 mwezi huu pale nyumbani lounge ,Sasa rafiki yake wa karibu
sana MwanaFA inaonyesha naye ameanda show yake siku hiyohiyo ya Tarehe
31,Zaidi ya yote mwanaFA akawachukua wasanii walio jitoa katika show
ya JIDE kama Linnah kutokana na sitofahamu chanzo kimoja cha habari kiliweza kumtafuta JIDE kupitia twitter na kumuuliza juu ya
hili swala naye aliweza kutoa yake anayo yafikiria,pia chanzo hicho kiliwezakumtafuta MwanaFA lakini mwanaFA hakuweza kutujibu swali alilo ulizwa hadi muda huu

Hivi ndivyo jide ALIVYO TUJIBU
ANGALIA HAPA PICHA YALIOJIRI WAKATI WA SHOTING YA MAJANGA YA SNURA
12:22 PM
No comments
Hapa ndio ile sehemu kupigwa nipigwe mie,police kawahi yeye, kibao nimegeuziwa mie

Malaika ameshashuka kutaka kusikiliza majanga ya wananchi yalivyokuwa mengi.

Mainda nae alikuwepo
Watoto wanaomba majanga yapungue kwa mana majanga yamezidi sana duniani
Kupata msosi maeneo hayo kidogo ni tabu mara kapita muuza samaki du watu wacha wamgombanie
Mamaa majanga
Profesa Jay akana kuumendea ubunge mwaka 2015
11:16 AM
No comments
Mchawi wa rhymes, Profesa Jay amesema hakujiunga na CHADEMA ili mwaka 2015 awanie ubunge kama wengi wanavyodhani.
Rapper huyo wa ‘Machozi, Jacho na Damu’ ambaye jina lake halisi ni
Joseph Haule, ameliambia gazeti la Mwananchi la leo kuwa amejiunga na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kukisaidia chama katika
changamoto za kuikomboa nchi.
“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango wa
kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea
hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama
ili kuyafikia malengo,” ameliambia gazeti hilo.
Ameliambia kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na amekuwa
karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua kuingia
rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa vijana.
“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa muda
mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria kumkomboa
msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani nipo
sahihi katika uamuzi wangu.”
“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini haina
maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi kinanifaa,
lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati wowote chama
kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J.
CHANZO: bongo5.com
AIBU: HUYU HAPA YULE MUME WA MTU ALIYENASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI
10:30 AM
No comments
INAUMA sana! Wakati
wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze
kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi
wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki
Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika
dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili
wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala
soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma
vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na
mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.
Chanzo
chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya
tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye
sare za shule.
Kikao cha
dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya
habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri
uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla
timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya
kumuondoa denti huyo.
Wikiendi
iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu
kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine
amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu A
iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini
ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi
na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi
wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba
hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama
walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa
darasani.
Binti
huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo,
alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya
kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni
kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni
Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki
aliniambia nije kwake.
“Naombeni
mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na
ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba
(Taliki),” alisema denti huyo.
Denti
huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika
eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye
akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha.
Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI WA TALIKI
“Ni
kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila
naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu
shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu
zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma
(utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa
anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi
wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi
Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 –
KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
GPL
Subscribe to:
Posts (Atom)























