Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Tuesday, November 26, 2013

Diamond Aumbuka baada ya kudai alihudhulia harusi ya Peter Okoye wa P square huu ndio ukweli wake


Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja afrika, Aliko Dangote.
Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi yake.
hapa diamond akicheza ngololo kwenye part hiyo
Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?

Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani.

Friday, November 22, 2013

BABU SEYA ALIA DUNIA HAINA HURUMA

Stori: Richard Bukos
Hukumu iliyokaziwa na Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam, juzi (Alhamisi), ikipigilia msumari adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya mwanamuzi mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, imesababisha maumivu makali kwa wahusika.
                                 Mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Uthibitisho wa hilo unatokana na kauli ya Babu Seya, aliyoitamka mahakamani akimnong’oneza Papii Kocha, akisema: “Kweli hii dunia haina huruma, hukumu hii imeniuma sana kuliko zote ambazo zimetangulia.”
Akizungumza kwa upole kwa sauti ya majonzi, huku sura yake ikionesha dhahiri kutokuwa  na furaha, Babu Seya aliendelea: “Kinachoniuma zaidi ni wewe, nakusikitikia sana, wewe ni kijana mdogo ambaye ulipaswa kuwepo uraiani ukitimiza ndoto zako na ukiisadia nchi yako.
...Akiwa katika huzuni na majonzi makubwa.
“Ndoto zako zimeishia hapa. Tumejitahidi sana kukwepa hiki kifungo lakini imeshindikana, wewe unajua.”
Hata hivyo, wakati akitoka nje ya ukumbi wa mahakama, Babu Seya alimweleza mwandishi wetu: “Hili jambo sijalifanya, nitaendelea kupambana mpaka mwisho.”

NI HUKUMU YA MWISHO
Msajili Mwandamizi wa Mahakama, Zahra Mruma, akisoma hukumu  hiyo alisema: “Ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao ni Jamhuri, umeendelea kuwa na nguvu, kwa hiyo vipengele vya utetezi vilivyowasilishwa na mawakili wa utetezi vimekosa nguvu ya kutengua hukumu ya awali.”
...Ndugu na jamaa wakiangua kilio baada ya hukumu.
Zahra, alisoma hukumu hiyo kwa niaba ya jopo la majaji watatu ambao waliipitia upya hukumu hiyo, baada ya mawakili wa utetezi, Mabere Marando na Gabriel Mjele, kuomba Mahakama ya Rufaa ifanye mapitio ya mwisho, baada ya kutokuzikubali zote zilizotangulia.
Mawakili wa upande wa utetezi, walitaka mapitio hayo yafanyike kwa hoja kwamba haiingii akilini kwa Babu Seya na mwanaye kushiriki tendo la mapenzi kwa pamoja, tena kwenye nyumba wanayoishi.
Hoja hiyo ilishibishwa na maelezo kuwa Babu Seya na Papii ni Waafrika, kwa hiyo kitamaduni haiwezekani kushiriki mapenzi kwa pamoja.
Utetezi mwingine ni kuwa nyumba ya tukio ni ya kifamilia, kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa tendo husika kutendeka, maana wengi wangekuwa wanashuhudia.

KESI YA MSINGI
Babu Seya na Papii, walishtakiwa na baadaye kukutwa na hatia ya kuwabaka, kuwalawiti na kuwaambukiza Virusi Vya Ukimwi, watoto nane, wenye umri wa kati ya miaka saba na sita.
Mahakama ilielezwa kuwa Babu Seya alikuwa akiwaita watoto hao na kuwanunulia pipi kisha kuwaingiza ndani ambako waliwaingilia kwa zamu na baada ya kitendo, waliwapa mgao wa kati ya shilingi 100 na 150.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na mwaka 2004, hukumu ilitolewa, ikiwatia hatiani Babu Seya na wanaye watatu na kuwahukumu kwenda jela maisha.
Watoto wengine wawili wa Babu Seya, waliokuwemo kwenye kesi hiyo ni Francis Nguza na Nguza Mbangu ‘Nguza Mashine’ aliyekuwa mpiga drum wa Bendi ya FM Academia, mpaka wakati anaingizwa kwenye mashtaka.
Mwaka 2005, rufaa ya kwanza ilisomwa ambayo ilikazia hukumu ya awali lakini Februari 2010, Mbangu na Francis waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia, huku Babu Seya na Papii, ikipitishwa na Mahakama ya Rufaa kwamba waendelee na kifungo cha maisha jela.

MAJAJI WALIVYOTOA HUKUMU
Zahra, alisema jopo la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Masati na Mbarouk Salim Mbarouk, lilichambua hoja za utetezi na kuona hazina nguvu, kwa hiyo wakajiridhisha kuwa Babu Seya na Papii, wanastahili kuendelea na adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Hukumu hiyo, ilikuwa ni ya rufaa ya nne, lakini imeshindikana kwa kuwaondoa Babu Seya kwenye kifungo.

MAWAKILI WASALIMU AMRI
Mmoja wa  mawakili wa utetezi, Mjele, alisema kuwa hukumu hiyo ndiyo ya mwisho na kwamba wao hawana njia nyingine ya kukata rufaa kisheria.
“Hatuna njia nyingine, hapa ndiyo mwisho,” alisema Mjele na kuongeza: “Labda tusubiri msamaha wa rais kwa sababu ni yeye pekee mwenye mamlaka ya kutengua hii adhabu.”

RAIS AZIDI KUTUPIWA MZIGO
Watu kadhaa waliohudhuria mahakamani juzi, waliungana na Wakili Mjele kwamba kesi hiyo iachwe mikononi mwa rais kwa sababu ndiye mwenye nafasi ya kufanya lolote katika kesi hiyo kama anavyoruhusiwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mahakama imefanya kazi yake, mawakili wa utetezi wamejitahidi lakini imeshindikana, sasa hatutakiwi kuijadili sana hukumu, badala yake tumuachie rais kwa sababu ndiye mwenye mamlaka,” alisema Fredrick Mwaluwanda wa Kinyerezi.
Mosha Kabogo alisema: “Katika hukumu hii, kila mmoja anaweza kuwa na hisia zake, jambo la msingi ni kumuacha rais afanye anachoona kinafaa. Uzuri ni kwamba siyo rais wa sasa peke yake, kwani hata ye yote anayekuja, anaweza kutumia mamlaka yake kikatiba kuwaachia huru au kuwapunguzia adhabu.”

WANAMUZIKI WAANDAA UJUMBE KWA RAIS
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, alisema mahakamani hapo kuwa anakusudia kuitisha kongamano la wanamuziki halafu watafanya mkutano na waandishi wa habari kumuomba rais awaachie huru Babu Seya na Papii.
“Hili suala linauma sana, hatuwezi kukaa kimya tukiwaacha wanamuziki wetu nyota wakienda na maji. Lazima tufanye kitu na tutakachofanya  ni kujikusanya na kuandaa mkutano wa waandishi wa habari ambao tutautumia kutuma ujumbe kwa mheshimiwa rais,” alisema Dully.

PAPII NI WA KUMJADILI KIDOGO
Papii Kocha, wakati alipoingia kwenye mashtaka hayo, alikuwa ni kijana mdogo ambaye nyota yake kwenye muziki ilikuwa inang’ara kwa kiwango cha juu sana nchini Tanzania.
Alifanya vizuri sana akiwa na Bendi ya FM Academia na Tot Plus kabla ya kutoka na albamu yake binafsi iliyokuwa na nyimbo nyingi kama vile Salima, Fanta na Seya ambayo uliimbwa mithili ya wimbo wa taifa.
Alitabiriwa kwamba angeweza kuendelea kufanya vizuri kutokana na uwezo aliokuwa nao lakini nyota yake ilizimwa na kesi hiyo.
Kwa upande wa Babu Seya, ni nguli aliyejenga jina na heshima kubwa nchini kupitia muziki wake, huku akipigiwa mfano kama mpiga solo bora kabisa, lakini historia yake imehitimishwa kwa kifungo cha maisha jela.

TAZAMA VIDEO YA SNURA "NIMEVURUGWA" UONE JINSI SNURA ALIVYOVURUGWA HUMO NDANI, MAUNO MWANZO MWISHO..!!

snura 234 
August 2013 ndio Snura aliishusha single yake ya ‘nimevurugwa’ kwenye radio za bongo ikiwa ni miongoni mwa single zinazopata airtime bila kuwa na video lakini leo November 22 2013 kaishusha video on AyoTV… itazame hapa chini na uache maoni yako mtu wangu, atapita hapa baada ya saa 6. Snura alisema kwenye video ya ‘majanga’ hakuweza kucheza kama inavyotakiwa lakini huku kwenye ‘nimevurugwa’ ndio kajiachia.

Monday, November 18, 2013

Pichaz kutoka Club Bilicanas kwenye usiku wa ‘Ay road to #CHOAMVA’ @AyTanzania

20 
Wakati Watanzania wakiendelea kupiga kura kwa Mtanzania pekee alietajwa kuwania tuzo za Channel O 2013 (Ay) , usiku wa November 17 2013 kulifanyika party club Bilicanas Dar es salaam (AY Road to CHOAMVA 2013) ambapo mastaa kadhaa walionekana kwenye stage kumpa support Ay.

Kumpigia kura Ay unaweza kutembelea www.channelo.com au piga kura kwa Best Gifted male video: sms 1D kwenda +2783142100415 na kwa Best gifted East video: sms 12D kwenda +2783142100415.
1 
Watu wa nguvu kama kawaida walijitokeza.
2 
Rapper Stereo, Wakazi na mtu wa nguvu
3
4 
Dee Andy kutoka XXL ya Clouds FM, Reuben Ndege (Ncha Kalih) na Shadee kutoka @Clouds_TV
5 
B12 kutoka XXL ya Clouds FM, FidQ na Sajjo.
6 
Brothers wameshow love kwa Ay
7 
Young Dee na watu wa nguvu
8 
Jokate na Young D
9 
Hawa Warembo ni miongoni mwa waliofungua show
10
11
12 
Stere.
13
14 
Godzillah
Ommy Dimpoz kazini
16 
Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee
17
18
19
21
22 
T.I.D na Ommy Dimpoz
23
24 
Fid Q na shabiki
25
26
27 
Ikafika zamu ya AY.
28
29
30
31

 

ANGALIA PICHA DIAMOND AHUDHURIA HARUSI YA P-SQUARE

 Pichani ni Diamond Platnumz msanii kutoka bongo akiwa na bwana harusi Peter wa Psquare pale walipokutana huko Lagos Nigeria kwenye harusi ya Peter. Diamond yupo nchini Naija kwaajili ya utengenezaji wa video yake mpya ya wimbo Number One remix aliyomshirikisha msanii kutoka huko huko Naija anaitwa Davido. Nadhani tutegemee mambo mazuri sana kutoka kwa Diamond
 Emanuel Adebayo & Diamond
 Diamond & Iyanya
 Peter & Emanuel Adebayo

JAMBO SQUARDS NA LADY FIRE WATISHIWA KUUAWA ARUSHA

Kuanzia kushoto ni Nigger C, Ordinally na Lady Fire

Exclussive akiongea na DjHaazu wa MJ FM Arusha mmoja kati ya member wanaounda kundi la Jambo Squard NIGGER C a.k.a Chaalii Mtoto wa bibi amefunguka kuhusu wao kutishiwa Kuuwawa na mtu ambaye anajihisi kuwa yeye ndiye Wamemuimbia wimbo unaokwenda kwa jina la KAKA KIBO ambapo ngoma hiyo ilitungwa na Vijana hao na kupewa nafasi ya kuiimba Mdogo wao anayejulikana kwa jina la Lady Fire Manzi ya Ara.
 Nigger C amesema baada ya wimbo huo kuanza kufanya poa kwenye Vituo kadhaa vya radio Nchini hatimaye ametokea Mtu ambaye anadai kuwa wao wamemuimbia yeye na vitu vyote vilivyoimbwa vinamlenga yeye Direct na jina lake ni Kibo na huyo mtu alishawahi kujiita yeye ni manager wa Jambo kitu ambacho wao kiliwaudhi na hatimaye kumkataa na kukaa mbali naye ambapo kilichofuatia ni uhasama uliosababishwa na mtu huyo kuwashikia fedha zao million 3 akidai kuwa anawatengenezea future kibiashara huku akijitapa kuwa na mkwanja wa kutosha na mwishowe wasanii hao walipogundua ni mbabaishaji hatimaye walimbwaga na walipoulizia fedha zao jamaa aliwapa laki 8 tu kitu ambacho kiliwakera wasanii hao.

Nigger ameendelea kumiminika zaidi na kusema kuwa wamemrecord mtu huyo wakati akiongea na moja kati ya Viongozi wa GrandMaster record Studio ambayo wanafanyia kazi wasanii hao na sauti hiyo wanayo ya Kaka Kibo huyo akisema kuwa amewatafutia Majambazi vijana hao na amewalipa advance kwa ajili ya kuwalima risasi vijana wa Jambo Squard ambao ni Nigger C na Ordinally a.k.a Kisu kikali a.k.a Jogoo Kichaa na pia kumkata miguu na mikono Mwanadada Lady Fire.

Hata Hivyo wamewaahidi wananchi Kufikisha Sauti hiyo Radioni Leo Jumatatu Na watu watamsikia Mtu huyo akitiririka akiamini kiongozi huyo atakuwa upande wake bila kujua kwamba anarecordiwa na Kiongozi huyo hayuko tayari kuwasaliti vijana wake kisa fedha za mtu huyo.

Jambo Squard wanasema kinachowauma zaidi ni kwamba mtu huyo anasema atasambaza fedha kwa MaDJ na Mapresenter ili ngoma za jambo Squard zisipigwe na kwamba kuna kituo kimoja cha Radio arusha ambacho kimeandika Tangazo kabisa ukutani ukiingia studio kwao kwamba wimbo wa jambo squard usipigwe....

Nigger C amesema hadi sasa wao wanafuatilia RB Kumkamata mtu huyo ambaye inasemekana ana Mabov ya kutosha kumwaga ila wao wanaamini kama YAHAYA aliimbwa na JD na hakumshtaki JD inamaanisha kuwa walikuwa wengi na wao wanawajua Kibo wengi.

MSIKILIZE NIGGER C AKIONGEA NA DJHAAZU HAPA CHINI
KUSIKILIZA CLICK LINK HII >> http://old.hulkshare.com/ow4wkucz81ds

Ndani ya wimbo huo ameimbwa au wamefikishiwa ujumbe watu ambao wanapenda kujioshea au kujibandika vyeo wasivyostahili mfano kuna line inasema " Eti anasema ni Maneger wa Jambo"

SIKILIZA WIMBO HUO KAKA KIBO WA LADY FIRE AKIWASHIRIKISHA JAMBO SQUARDS NA RAMA B  HAPA CHINI

FUATILIA HAPA HAPA KITAKACHOENDELEA

Friday, November 15, 2013

HII NDIO LIST NZIMA YA WASANII WATAKAO PERFORM KATKA SHOW AMBAYO HAIJAWAIFANYIKA KATIKA ARDHI YA BONGO(P SQUARE)

  HABARI MPASUKO: Ben Pol na Joh Makini kupafomu na P-SQUARE

Yule BEAUTIFUL ONYINYE Lazima aambiwe BEI YA MKAA ili awe tayari kuwa WA UBANI na atasema NIKUMBATIE maana NO ONE LIKE YOU.

Mkali wa R&B Bongo Ben Pol na Mkali wa michano toka WEUSIII Joh Makini nao pia ni wasanii watakaopanda jukwaa moja na P-SQUARE siku ya Novemba 23.

Hawa wasanii wanne tu toka Tanzania Lady Jay D, Ben Pol, Profesa J na Joh Makini ndio watapanda jukwaa moja na P-SQUARE ili kukupa muda mrefu wa burudani yenye viwango toka kwa P-SQUARE

Thursday, November 14, 2013

Wafahamu watanzania wanne walioingia kwenye orodha ya matajiri 50 wa Afrika-2013

 Rostam Aziz aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Said Bakhresa na mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji wameingia kwenye orodha ya Forbes ya watu 50 matajiri zaidi barani Afrika.

Rostam Aziz ndiye aliyeibuka kidedea kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 na kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha hiyo.

Huku Mwenyekiti na mtendaji wa makampuni IPP,Reginald Mengi ameshika nafasi ya 34 akiwa na utajiri wa dola Milioni 550  kwenye orodha hiyo ya Forbes.

Kwenye nafasi ya 38 ya orodha hiyo, imeshangaza kuona Said Salim Bakhresa na Mohamed Dewji wakiwa sawa kwa utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.

Hivi Snura na Ngasa ni wapenzi?

Mshambuliaji wa timu ya soko ya taifa,Taifa Stars na Mchezaji wa Yanga  Mrisho Ngasa amenaswa live akiwa na muimbaji wa majanga “Snura Anton Mushi”. Bado haijajulikana wazi kama mastaa hao wawili wanauhusiano wa kimapenzi au labda wanaigiza movie?

Mastaa hao wawili walinaswa live wakiwa kwenye nyumba ya Snura Anton Mushi iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

DIAMOND, PENNY KUMBE NDUGU

Na Shakoor Jongo
MAAJABU! Jambo zito limefichuka kuwa mastaa walio katika uhusiano wa kimapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ ni ndugu, AMANI limepekua na kupata mkanda kamili.
Diamond na Penny katika pozi la kimahaba.
Diamond kwa sasa ndiye mwanamuziki aliye matawi ya juu zaidi kuliko yeyote kwenye Bongo Fleva, akisumbua vibaya na kibao chake cha Number One wakati Penny akiingiza mkwanja kupitia utangazaji katika kituo cha Runinga ya Dar es Salaam ‘DTV’.
ISHU YABUMBURUKA!
Sosi wa karibu, ndani ya familia ya Diamond alinyetisha kwamba, Diamond na Penny ni ndugu wa damu lakini jambo hilo limefahamika hivi karibuni na hivyo wanahaha namna ya kuzima aibu hiyo.
Kwa sharti la kutochorwa jina gazetini, sosi huyo alisema: “Ndugu kwenye familia wanagongana. Wanajaribu kufichaficha hili jambo, lakini inashindikana. Unajua kinacholeta shida zaidi ni kwamba Diamond na Penny watakavyokuwa baada ya uamuzi kupitishwa.”
Alisema, pamoja na ukweli huo kugundulika bila shaka kuwa ni ndugu, bado kuna ugumu wa wapenzi hao waliozama kwenye dimbwi la mahaba kisha kuvunja amri ya sita, kuachana na kubaki wakiheshimiana kama kaka na dada.
“Tatizo ni je, Diamond atakubali kumchukulia Penny kama ndugu yake? Kama atakubali na Penny naye atakuwa tayari? Wote kwa pamoja wanaonekana kama wanapingana na jambo hilo,” alisema.
UNDUGU WENYEWE UKOJE?
Akieleza aina ya unasaba wa Diamond na Penny, sosi wetu huyo alisema, bibi mzaa mama wa Diamond na bibi mzaa mama wa Penny, wamezaliwa na mama mmoja.
Hapa anafafanua: “Kwa sababu hiyo sasa, unaweza kuona kuwa, wale ni sawa tu na mtu na kaka yake. Tena wako ndani ya ukoo kabisa, sema hao mabibi, kila mmoja alikuwa na baba yake, walichangia mama tu.
“Familia imejiridhisha kabisa, halafu isitoshe imeonekana kuwa, undugu wa kuchangia mama ndiyo wa uhakika zaidi kuliko wa baba ambao mtu anaweza kubambikwa hata mtoto asiye wake. Kifupi Penny na Diamond ni ndugu. Sema ndiyo hivyo historia za wazazi wao zinashangaza mpaka basi.”
Kwa mujibu wa sosi wetu, majina ya bibi hao wanaounganisha undugu ni Khadija Said Abas (bibi yake Penny) na Tatu Omar (bibi yake Diamond), wote kwa sasa wametangulia mbele ya haki.
MAMA DIAMOND ACHEKELEA
Wakati jambo hilo likileta msuguano wa kimyakimya ndani ya familia huku wengi wakitaka undugu huo uheshimiwe na uhusiano uvunjwe kabisa, imeelezwa kuwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ anafurahia undugu huo

Penny akimlisha keki mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’.
“Kinachoshangaza sasa, mama Diamond amefurahi sana na amezidisha mapenzi yake kwa Penny, ndiyo maana hataki kusikia mwanaye anakuwa na mwanamke mwingine zaidi ya Penny.
“Mwenyewe anasema, kwanza undugu siyo wa karibu sana hivyo haina madhara lakini pia anajua Diamond atampenda, kumheshimu na hatamnyanyasa kwa sababu ni sehemu ya damu ya familia yao,” sosi aliendelea kutiririka.
HAPA AMANI, KULE DIAMOND
Amani lilifanya juhudi za kumsaka Diamond katika simu zake zote za mkononi bila mafanikio, likahamia kwenye mitandao ya kijamii, likamnasa ambapo awali mahojiano yalikuwa na kigugumizi lakini baadaye mambo yalikuwa hivi;
AMANI: Mzee vipi, mbona hupatikani kwenye simu zako zote? Kuna jambo nataka kukuuliza bwana mkubwa.
DIAMOND: Niko Nigeria. Vipi, kuna nini tena?
AMANI: Kuna stori fulani... eti ni kweli bibi yake Penny mzaa mama na bibi yako wewe ni ndugu wa damu kwa maana wamezaliwa na mama mmoja?
DIAMOND: Yeah but wamechangia mama, kila mmoja na baba yake.
AMANI: Kwa hiyo Penny ni dada yako kiasili si ndiyo?
DIAMOND: Yap!
AMANI: Duh! Majanga... kwa hiyo unatembea na dada yako wa damu?
DIAMOND: Nilikuwa najua basi kaka?!
AMANI: Kwa hiyo sasa baada ya kugundua hivyo, unaachana naye au?
DIAMOND: Kama nilivyokuambia, niko Nigeria... halafu niko gym sasa hivi, nitakutafuta nikitoka.
AMANI: Sawa, naomba ujibu hili swali la mwisho. Tumesikia kuwa, mama yako anampenda sana Penny, ni kwa sababu amegundua kuwa una undugu naye?
DIAMOND: Ha! Ha! Ha! Nikitoka gym nitakupigia simu tuzungumze vizuri.
Diamond hakufanya hivyo. Hata alivyotafutwa baadaye kwenye mtandao huo, pia hakuonekana kuwa hewani.
PENNY MIKONONI MWA AMANI
Penny alipopatikana juzi Jumanne, kwa njia ya simu alielezwa ilivyo ambapo alisema: “Ni kweli Diamond ni ndugu yangu wa damu. Tumegundua tukiwa tayari tumeshakuwa wapenzi.
“Hakuna jinsi tena, sanasana naona kama mapenzi yetu ndiyo yamezidi kuimarika. Nampenda sana Diamond wangu na sababu hiyo haitoshi kututenganisha maana kama ni makosa tayari yameshatokea.”
MAMA DIAMOND
Kwa upande wake mama Diamond, baada ya kusimuliwa kila kilichofika mezani mwa Amani na kutakiwa kueleza msimamo wake alijibu kwa kifupi: “Ndiyo ni kweli unayosema, lakini kwa sasa nipo huku Kariakoo (Dar), sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza. Njoo nyumbani jioni, tuzungumze vizuri.”
Diamond na Penny wamekuwa kwenye penzi lenye kasheshe nyingi kufuatia mwanamuziki huyo kuhusishwa na wanawake wengine akiwemo aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Wema Isaac Sepetu.

CHANZO: www.globalpublishers.info

Wednesday, November 13, 2013

ANGALIA PICHA ZA SHEREHE YA MIAKA 75 YA RAIS MSTAAFU, BENJAMIN MKAPA

 Mandhari ya ukumbi uliofanyika sherehe ya kumpongeza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ya kutimiza miaka 75, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam,jana usiku.
 Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akijumuika na mkewe Mama Anna Mkapa na sehemu ya Familia yake kukata Keki, ikiwa ni ishara ya kupongezwa kwa kutimiza miaka 75.
 Shambra shambra ukumbini wakati wa sherehe hiyo......
 Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa,akizima mishumaa
 Baadhi ya wageni waalikwa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal, (kushoto) Mama Zakia Bilal na baadhi ya viongozi, wakijumuika kumpongeza Mkapa.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
 Zawadi ya Benjamin kutoka kwa marafiki zake wakaribu......
 sehemu ya wageni waalikwa......
 Wageni waalikwa .......
 wageni waalikwa......
 Msanii akitoa burudani.....
 Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akilishwa keki na mkewe Mama Anna Mkapa....
 Unyenyekevu....
 Baadhi ya wageni waalikwa.....
 Mkapa na keki yake.....
 Mkapa akipongezwa na mke wa Rais, Mama Salma......
 Waalikwa......
 Wageni waalikwa wakigonganisha glasi wakati wa sampeni......
 Zawadi.......akikabidhiwa mkapa......
 Rais Mstaafu Mkapa, akizungumza wakati wa sherehe hiyo...
 Makamu wa Rais Dkt.Bilal, akizungumza kwa niaba ya Serikali.....
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal. akimpongeza Mkapa......
Picha ya pamoja (picha na Sufiani Mafoto)