Baadhi
ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma walikufa kutokana
na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori
hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani
hapo.
Miili
ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya
kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala
ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
Baadhi
ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada
katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara
CBE Dodoma.
Asikari
wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu
ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.
Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI
wawili wa chuo cha biashara wamepoteza CBE wamekufa papo hapo kwenye
ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya
kuhalibika.
Ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la
lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea
kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha
ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti
hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo
iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi
ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza
utaratibu wa kuondoka.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo
yenye namba za usajili T 420 CCN waliokuwa wakukitokea barabara ya
morogoro kuingia mjini.
Suzan
aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE
na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM
na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala
kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik
eneo hilo.
Aliongeza
kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na
kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo na ubongo
kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.
0 comments:
Post a Comment