Kuanzia kushoto ni Nigger C, Ordinally na Lady Fire
|
Exclussive akiongea
na DjHaazu wa MJ FM Arusha mmoja kati ya member wanaounda kundi la Jambo
Squard NIGGER C a.k.a Chaalii Mtoto wa bibi amefunguka kuhusu wao
kutishiwa Kuuwawa na mtu ambaye anajihisi kuwa yeye ndiye Wamemuimbia
wimbo unaokwenda kwa jina la KAKA KIBO ambapo ngoma hiyo ilitungwa na
Vijana hao na kupewa nafasi ya kuiimba Mdogo wao anayejulikana kwa jina
la Lady Fire Manzi ya Ara.
Nigger C amesema baada ya wimbo huo
kuanza kufanya poa kwenye Vituo kadhaa vya radio Nchini hatimaye
ametokea Mtu ambaye anadai kuwa wao wamemuimbia yeye na vitu vyote
vilivyoimbwa vinamlenga yeye Direct na jina lake ni Kibo na huyo mtu
alishawahi kujiita yeye ni manager wa Jambo kitu ambacho wao kiliwaudhi
na hatimaye kumkataa na kukaa mbali naye ambapo kilichofuatia ni uhasama
uliosababishwa na mtu huyo kuwashikia fedha zao million 3 akidai kuwa
anawatengenezea future kibiashara huku akijitapa kuwa na mkwanja wa
kutosha na mwishowe wasanii hao walipogundua ni mbabaishaji hatimaye
walimbwaga na walipoulizia fedha zao jamaa aliwapa laki 8 tu kitu
ambacho kiliwakera wasanii hao.
Nigger
ameendelea kumiminika zaidi na kusema kuwa wamemrecord mtu huyo wakati
akiongea na moja kati ya Viongozi wa GrandMaster record Studio ambayo
wanafanyia kazi wasanii hao na sauti hiyo wanayo ya Kaka Kibo huyo
akisema kuwa amewatafutia Majambazi vijana hao na amewalipa advance kwa
ajili ya kuwalima risasi vijana wa Jambo Squard ambao ni Nigger C na
Ordinally a.k.a Kisu kikali a.k.a Jogoo Kichaa na pia kumkata miguu na
mikono Mwanadada Lady Fire.
Hata Hivyo wamewaahidi wananchi Kufikisha Sauti hiyo Radioni Leo Jumatatu Na watu watamsikia Mtu huyo akitiririka akiamini kiongozi huyo atakuwa upande wake bila kujua kwamba anarecordiwa na Kiongozi huyo hayuko tayari kuwasaliti vijana wake kisa fedha za mtu huyo.
Jambo Squard wanasema kinachowauma zaidi ni kwamba mtu huyo anasema atasambaza fedha kwa MaDJ na Mapresenter ili ngoma za jambo Squard zisipigwe na kwamba kuna kituo kimoja cha Radio arusha ambacho kimeandika Tangazo kabisa ukutani ukiingia studio kwao kwamba wimbo wa jambo squard usipigwe....
Nigger C amesema hadi sasa wao wanafuatilia RB Kumkamata mtu huyo ambaye inasemekana ana Mabov ya kutosha kumwaga ila wao wanaamini kama YAHAYA aliimbwa na JD na hakumshtaki JD inamaanisha kuwa walikuwa wengi na wao wanawajua Kibo wengi.
MSIKILIZE NIGGER C AKIONGEA NA DJHAAZU HAPA CHINI
KUSIKILIZA CLICK LINK HII >> http://old.hulkshare.com/ow4wkucz81ds
Ndani ya wimbo huo ameimbwa au wamefikishiwa ujumbe watu ambao wanapenda
kujioshea au kujibandika vyeo wasivyostahili mfano kuna line inasema "
Eti anasema ni Maneger wa Jambo"
SIKILIZA WIMBO HUO KAKA KIBO WA LADY FIRE AKIWASHIRIKISHA JAMBO SQUARDS NA RAMA B HAPA CHINI
CLICK HAPA >>> http://www.reverbnation.com/grandmastertz/song/18838396-kaka-kibo-lady-firejambo-squad9grandmaster
FUATILIA HAPA HAPA KITAKACHOENDELEA
0 comments:
Post a Comment