Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Tuesday, May 21, 2013

Malfred ngoma mpya ya reggae inayokwenda kwa jina Pigana, sikiliza na ku-download hapa

Ikiwa ni mkono mwingine toka Label Ya Maisha Music,Malfred anakuja na ngoma mpya kabisa ya reggae inayokwenda kwa jina Pigana, Ikiwa ina ujumbe mzito kwa jamii haswa vijana wa Kisasa. Pata  ku-Download HAPA Powered by www.vmgafrica.com

HIKI NDICHO KILICHOTOKEA HADI MFANYABIASHARA MAARUFU AYOUB MLAY WA ARUSHA KUUAWA KWA RISASI,



Mwili wa marehemu Ayoub Mlay baada ya kupigwa risasi.


TUKIO la kuuawa kwa mfanyabiashara kijana mwenye mafanikio, Ayoub Mlay, siyo tu linaacha simanzi kwa Watanzania bali pia ni fundisho kwa jamii na serikali.
MLAY, alifariki dunia usiku wa Alhamisi iliyopita, Mei 16, mwaka huu baada ya kupigwa risasi kwenye Klabu ya Ambrosia, iliyopo Kawe Beach jijini Dar es Salaam.
Simanzi inakuja kwa sababu Mlay, 38, alikuwa mfanyabiashara kijana aliyeonesha mafanikio na kupiga hatua kubwa, amefikwa na mauti akiwa bado na moto wa kusaka maendeleo zaidi kwenye biashara zake na maisha kwa jumla.
Kwa Conrad ambaye ni kijana mdogo pia, anaingia kwenye msukosuko lakini nyuma yake kuna funzo la umiliki na matumizi sahihi ya silaha za moto ambazo kwa sasa zimekuwa kama ‘fasheni’ kwa vijana wengi wa mjini.




WOTE NI WATOTO WA ARUSHA
Mlay ni mfanyabiashara wa Arusha ingawa mara kwa mara hupatikana Dar es Salaam kutokana na mizunguko yake ya kibiashara.
Conrad, naye ni mwenyeji wa Arusha, ingawa kwa sasa makazi yake yapo Dar es Salaam.
Kuhusu kazi ya Conrad, mmoja wa watu waliohojiwa na gazeti hili nje ya Klabu ya Ambrosia, alisema: “Kwa kweli huwa tunamuona, wengi tunamuona ni mtoto wa mjini tu, kwani hatujui anajishughulisha na nini.”
Marehemu Mlay enzi za uhai wake.

CHANZO CHA UGOMVI
Mtoa habari wetu aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa Mlay na Conrad ni watu waliokuwa wanafahamiana na kuna jambo walikuwa wanazungumza.
“Siyo rahisi sana kujua walichokuwa wakizungumza ila baadaye yalitokea mabishano. Walitaka mpaka kushikana ili kupigana, watu wakawazuia. Inaonekana Conrad hakukubali, maana aliamua kutoka nje mbio.
“Kwa haraka haikujulikana alifuata nini kule nje, tuliokuwepo tuliamini ameamua kukimbia lakini kumbe alikuwa amefuata bastola. Aliporudi, alikuwa na bastola mkononi, baada ya hapo hata hakutaka kuzungumza maneno mengi, alimpiga Mlay risasi kisha akataka kutoweka,” kilisema chanzo chetu.


WALINZI WALIVYOMDAKA
Chanzo chetu kilibainisha kuwa wakati anapita na bastola kuingia ndani, walinzi walimpisha kwa sababu ya kuhofia usalama wao lakini kipindi cha kutoka, walijipanga kumdhibiti.
Kiliendelea kusema, Conrad akiwa anatoka, walinzi walifanya kama wanampisha na baada ya kupita, walimbana mikono na kumnyang’anya bastola kisha wakamfunga kamba kabla ya kupiga simu kuita polisi.
Dakika kadhaa baada ya kupiga simu, polisi walifika na kufanya mahojiano na watu waliokuwepo eneo la tukio, kabla ya kumchukua mtuhumiwa na kumpeleka Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam.
Vilevile, polisi walimchukua Mlay na kumuwahisha Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Kinondoni, Dar es Salaam ili akapatiwe matibabu lakini baadaye ilibainika alikuwa ameshakata roho.
ACP Charles Kenyela.

MADAI KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA SILAHA 
Kwa mujibu mtu aliyejitambulisha kwa jina la Matidau, Conrad alikuwa na mazoea ya muda mrefu ya kuonesha bastola yake na kuwatishia watu aliotofautiana nao.
“Tunamjua Conrad, kuna watu walishamwonya lakini hakusikia, ikafikia wakati kwamba anapoanza ugomvi, basi tunaomjua tunakaa mbali naye kwa sababu lolote linaweza kutokea.
“Kuna kipindi alinyang’anywa bastola kwa sababu ya tabia yake ya kuioneshaonesha ovyo pamoja na kutishia watu. Tukio hili la mauaji ya Mlay linatufanya tujiulize hiyo bastola alirejeshewa katika mazingira gani au ni nyingine?” kilihoji chanzo.


MINONG’ONO KUHUSU FEDHA
Kuhusu kile ambacho Mlay na Conrad walibishana, kulikuwa na maneno ya pembeni kutoka wa watu waliokuwepo eneo la tukio kwamba chanzo cha ugomvi ni fedha.
“Unajua inapotokea matukio makubwa kama haya, watu wa eneo la tukio wakati mwingine ndiyo huwa wa kwanza kupotosha. Kwa mfano, yapo madai kuwa Mlay alimtuma kazi Conrad, sasa baadaye kukawa na mabishano kuhusu malipo.
“Yote yatazungumzwa lakini jambo ni baya sana. Fikiria kwamba Mlay ni mtu aliyekuwa ameajiri watu, ana familia na marafiki, wote hao wataathirika kwa namna moja au nyingine kwa kumpoteza mtu waliyempenda,” alisema mtoa habari wetu.
Mlay enzi za uhai wake.


KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela alisema kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea na akaongeza kuwa Conrad alimfyatulia Mlay risasi ya kifua.
Kuhusu madai kwamba Conrad ni mzoeafu wa tabia za kuchezea silaha na kutisha watu kiasi kwamba hata jeshi lake lina taarifa na liliwahi kumnyang’anya kabla ya kumrudishia kinyemela, Kenyela alijibu: “Hizo taarifa sina, ngoja nizifuatilie kwanza, maana siwezi kuzungumza jambo nisilo na uhakika nalo.
“Nilicho na uhakika nacho ni hiki; kwamba mtuhumiwa tunamshikilia na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.”



KIFUATACHO
Bado kuna maswali kuhusu tukio hili, timu nzima ya Kampeni ya Fichua Maovu ya Global Publishers, imejipanga sawasawa kufuatilia kwa kina na mara itakapokamilika, mambo yatakuwa hadharani kupitia magazeti yake ambayo ni damu moja na hili; Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.



CHANZO : GPL

Makala: Jinsi Nay wa Mitego na Roma walivyoweza kujitengeneza kama wasanii wa biashara

Miongoni mwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo wasanii wa hip hop nchini ni kuingiza fedha kutokana na kazi zao. Bahati mbaya njia pekee na za uhakika za kuingiza fedha kupitia muziki zilizobakia ni malipo ya show na yale yanayotokana na miito ya simu.

page
Ni miaka takriban mitano sasa hakuna tena usambazaji wa albam unaoaminika kama ule wa zamani kwakuwa wasambaji wa muziki wanaonekana kuususia muziki wa Bongo Flava.

Kwakuwa shows na miito ya simu ndio njia pekee zilizobakia kumuingiza fedha msanii wa Tanzania, inahitajika kazi ya ziada kutengeneza nyimbo zinazoweza kuwavutia wadau wanaohusika.

Kwa miaka mingi, wasanii wanaofaidika zaidi ni wale wanaoimba (Ali Kiba, Diamond, Dully Sykes, Ommy Dimpoz na wengine). Watu wengi wameendelea kuamini kuwa Hip hop ni muziki wa kupata heshima tu Tanzania lakini haulipi.

Chukulia mfano wasanii wenye sifa kubwa za kiuandishi kama Nikki Mbishi, One the Incredible, Nash MC na wengi wa aina hiyo kwenye kizazi chao. Rappers hawa licha ya kukubalika kwa uwezo wao usio na kifani, muziki wao umeendelea kubaki kuwapa heshima tu lakini usiowaingizia fedha inayostahili. Lakini hali hii ni tofauti kwa Roma na Nay wa Mitego.

Roma
Jina la Roma lilianza kufahamika kwenye wimbo Mr President na kumtambulisha rapper huyo kwa identity yake ya rap ya ‘kupayuka’ na kama rapper mwenye mrengo wa kimapinduzi zaidi ‘radical rapper.’ Kwa lugha nyingine rahisi, Roma alionekana kama mwanaharakati.

Roma alijitengenezea upekee wake kama rapper anayeukosoa vikali uongozi wa serikali ya chama cha mapinzuzi, CCM. Licha ya Mr President kuwa wimbo wenye style na beat ‘ngumu’ maudhui yake yaliufanya uwe rahisi kuyakuna masikio ya mashabiki yaliyotaka kusikia anachonena. Uwasilishaji wenye Kiswahili rahisi na maneno yanayoeleweka moja kwa moja ni sababu nyingine iliyoupa uhai wimbo huu.

Baadhi ya nyimbo zake zilipata wakati mgumu kupata airtime kwenye vituo vingine vya radio. Baada ya Mr President, Roma aliendelea kutoa nyimbo zenye muelekeo ule ule ukiwemo Pastor uliokuwa ukizungumzia jinsi dini inavyotumika kibiashara na pia Mathematics ambamo alizungumza mengi na kuikosoa serikali na watu binafsi.

Ingawa alikuwa ameshanza kupata mashavu, Mathematics ndio wimbo uliompa mafanikio zaidi.

Mwaka 2011 na mwishoni mwa 2012, Mathematics ilikuwa ni hip hop anthem kwenye kila radio nchini. Umaarufu wa Roma uliongezeka maradufu. Ukubwa wa Mathematics ulidhihirika wazi kwenye tuzo za Kili kwa kuwa wimbo bora wa Hip Hop mwaka 2012.

Pamoja na kufanya hip hop ngumu, Roma amekuwa akipata mashavu kibao ya shows. Ni miongoni mwa wasanii wachache wa hip hop Tanzania wanaojulikana kwa kupiga show nyingi za promotion za makampuni mbalimbali nchi nzima.

Hizi ni baadhi ya sababu zilizomfanya Roma awe msanii wa hip hop wa biashara:

1.Ni kuegemea kwenye utunzi wa nyimbo za kimapinduzi zinazowagusa wananchi wengi hususan vijana waliochoka na jinsi hali ya kiuchumi ilivyo nchini

2. Mashairi yake kuendana na hali halisi ya maisha ya mtaani

3.Ujasiri wake wa kusema mambo kwa uwazi bila kuogopa wahusika anaowataja kwenye nyimbo zake. Ama kwa maana nyingine Roma husema mambo ambayo wengine huogopa kuyasema.

4. Uwezo wake mkubwa wa kulitawala jukwaa wakati wa kuperform kitu kinachosaidiwa na rap yake ya kupayuka ambayo ni nzuri kwenye live performance.

5. Uandishi wa maishari ya kiubunifu yanayoeleweka kwa urahisi. Hatumii sana metaphors kama wana hip hop wengine. Hii ni kwakuwa mashabiki wa kawaida hawapendi kuumiza kichwa kujaribu kuelewa mistari ya wimbo). Pia amekuwa akiepuka matumizi ya mistari ya Kiingereza.

6. Ile hali ya kuonekana kama mwanaharakati.

Nay wa Mitego
Kumekuwepo na mjadala mrefu kuhusiana na kama Nay wa Mitego ni mwanahip hop ama anafanya Bongo Flavour (kwa kuzingatia neno bongo flava linavyotafsiriwa na wengi kama muziki wa kuimba zaidi).
Wadau wengi wa hip hop licha ya Nay kujiweka kama msanii wa hip hop, wanadai kuwa hafanyi hip hop. Mjadala huo tunawaachia mashabiki wanaosikiliza nyimbo zake.

Kama Roma, Nay alianza kwa kujitengeneza kama msanii asiyeogopa kukosoa ama kuponda jambo analohisi haliko sawa. Tofauti na Roma, Nay hakuongelea siasa. Yeye alideal na maisha binafsi ya wasanii wenzie. Kama unakumbuka kwenye Itafahamika, Nay aliwadiss wasanii wengi waliopoteza umaarufu, wakiwemo Inspekta Haroun, Sister P, Rah P, Dudu Baya, P-Funk na wengine.
Aina hiyo ya muziki wake ilimtengenezea maadui wengi hasa wasanii aliowaponda pamoja na mashabiki wao, lakini pia akaanza kujipatia mashabiki wake waliyemuona ni mtu asiyekopesha (asiyeogopa kuongea ukweli).

Mwanzo Nay alichukuliwa kama rapper anayetumia njia ya kudiss wenzie ili kupata ‘cheap publicity’ ama njia ya kupata umaarufu wa haraka. Japo ni ngumu kuthibitisha kama hiyo ndio ilikuwa dhamira yake, Nay ameendelea kuwa msanii wa aina hiyo hiyo. Nyimbo zake nyingi za rap zimekuwa na ujumbe unaoendana na zinazozua mjadala.

Breakthrough yake kibiashara ilichangiwa na ngoma yake ‘Nasema Nao’. Humo aliwadiss watu wengi zaidi. Kauli yake kuwa wasichana wengi wa Bongo Movies ni machangudoa iliwafanya waigizaji wengi wa tasnia hiyo kumuijia juu. Kutokana na wimbo huo, Nay alipata interview nyingi kwenye vituo vya radio na TV vilivyotaka kupata ufafanuzi zaidi wa kile alichokisema. Kuhusu suala la wasanii wa kike wa bongo movie, aliendelea kushikilia msimamo wake na kutoa mifano halisi ya waigizaji aliowashuhudia wakifanya uchangudoa.

Aina ya nyimbo zake, zikamtengenezea mashabiki lukuki nchini.
Mwaka jana alikuwa miongoni mwa wasanii waliozunguka nchi nzima kwenye show za Fiesta. Na huko mara nyingi alikuwa kati ya wana hip hop waliopata shangwe nyingi zaidi. Miaka ya 2012 na 2013 imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara kwake. Amefanikiwa kupiga show nyingi zikiwemo za matamasha makubwa na zile za promotion za makampuni hususan ya simu. Nay ameendelea kupata mashavu kwenye promotion zote za Tigo, Vodacom na Airtel ambazo zimemuingizia fedha nyingi.

Mwaka huu amefanikiwa kutengeneza hit single, Muziki Gani aliyomshirikisha Diamond na ambao umemweka kwenye sehemu nzuri zaidi kibiashara.

Hizi ni baadhi ya sababu zilizomfanya Nay awe msanii wa biashara:
1. Kurap masuala ya ukweli yanayowahusu wananchi wengi bila kukwepesha
2. Kukosoa wasanii wanaofanya mambo yasiyopendeza
3. Kuandika mashairi yenye utata (controversial lyrics)
4. Kuandika mashairi rahisi yanayoeleweka kwa urahisi
5. Uwezo wake wa kubadilika kwendana na soko
6. Ujasiri wake na uwezo wake wa kusimama kwenye kile anachokiamini

Uchambuzi umefanywa na Fredrick Bundala (Bongo5 Head of Content).Twitter: @skywizz

HUYU HAPA NDIO MWANAMKE ALIYEPOTEZA VIONGO VYAKE VYA SIRI, KISA.....


Mwanake mmoja nchini Zimbabwe amekumbwa na balaa la mwaka baada ya kupoteza VIUNGO VYAKE VYA SIRI ( Uke)....

Mwanamke huyo alikumbwa na balaa hilo usiku wa kuamkia tarehe 29 mwezi wa nne mwaka huu...

Kwa mujibu wa mtandao wa Standardmedia, mwanamke huyo alimka usiku na kuelekea chooni kukojoa.Akiwa chooni, alishangaa kuona mkojo hautoki.Alipojichungulia,Ikulu ilikuwa IMEZIBWA..!!!

Taarifa zinadai kwamba, mwanamke huyo alizimia pale pale. 

Kwa mujibu pia wa mtandao wa Zimbabwean ambao nao umeripoti kuhusu tukio hilo, mwanamke huyo anadaiwa kuwa na tabia chafu ya kutembea na waume za watu, hali ambayo ilikuwa ikiwakera wanawake wenzie...

Mtandao huo umedai kwamba , katika siku za hivi karibuni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Mai alimpa ONYO kali mgoni huyo baada ya kugundua kuwa anatoka kimapenzi na mume wake na kumtaka aache mara moja...

Baada ya siku chache kupita tangu onyo hilo litolewe, mwanamke huyo alijikuta amenyofolewa nyeti zake....

Source: standardmedia
Shukrani kwa Dj Teddy

Wema aingia mkataba unaofanya awe staa anayeongoza kulipwa fedha nyingi


Wema-sepetu-Darling-Hair-Tanzania-1
Wema-sepetu-Darling-Hair-Tanzania
Wema-sepetu-Darling-Hair-Tanzania-0
Wema-sepetu-Darling-Hair-Tanzania-3
Wema-sepetu-Darling-Hair-Tanzania-2
Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amepata shavu la nguvu baada ya kuingia mkataba na kampuni nywele, Darling Hair Tanzania kuwa msemaji na muuza sura wao.

Kwa mujibu wa fashion designer na meneja wa Wema, Martin Kadinda, mkataba huo unamfanya wema awe staa anayeongoza kwa kulipwa fedha nyingi kuliko wote Tanzania. “#SheIsOfficial #MostExpensive Celeb in Tz #Thank DarlingHairTz #Ninachakujivunia kwa muda niliofanya kazi na wewe @wemasepetu.”

Martin Kadinda ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hakusema mkataba huo ni wa kiasi gani. Mkataba huo unamfanya Wema ahusike kwenye upande wa promotion; yaani kuwa msemaji na sura ya Darling Hair Tanzania. So far mafaniko yameanza sababu websites kibao, ikiwemo hii ya Maraha Laivu, zimeanza kuandika na kuipatia kampuni hiyo publicity ya bure.

Video: G-Nako na Weusi, live performance at New Maisha Club

NAY WA MITEGO NA DIAMOND PLATINUMZ WAFUNIKA KWENYE UZINDUZI WA VIDEO '' MUZIKI GANI'' DAR LIVE!


Nay wa Miego akiburudisha umati wa watu waliojitokeza kwa wingi Darlive!

DAR Live usiku wa kuamkia leo ilitikisika baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la pamoja kati ya wanamuziki wawili nyota wa kizazi kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Ney wa Mitego ambao walikuwa wakizindua video ya wimbo wao wa 'Muziki Gani'.

Wanamuziki hao kwa pamoja walitoa burudani ya nguvu ambayo ilizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika ukumbi huo wa maraha uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar.
Diamond Platnumz akiwapa hi mashabiki.
Ney wa Mitego akiwarusha wapenzi wa burudani. 
Nyomi iliyoitikia shoo hiyo. Mnyamwezi huyo!!Kitu na box full kimyaaa!!!Nipe na mimi Hi jamani Diamond...Jamaa nuksi huyu...Raha utamu hapaWasafiiii...Diamond akiachia vitu vyake jukwaani huku mashabiki wakiwa wanataka kumvuta chini..Jukwaa likitetemekaMama VanessaHii balaa jukwaani jamani...Nay na Diamond wakitupia maneno ya kwenye Video Muziki gani jukwaani live...Jamani nani zaidi??? Hip Hop na mbana pua!!!

Diamond na Ney wakiwapagawisha mashabiki. 
Ney wa Mitego akisema na wapenzi wake.
Diamond Platnumz akionyesha umahiri wake stejini.

Diamond akifanya makamuzi sambamba na kundi lake.
ilikuwa show moja matata sana hip hop v bongo flava

HIVI NDIVYO MADEE ALIVYOMPONGEZA DOGO JANJA




Na Elizabeth John

KIONGOZI wa Kundi la Tip Top Connection, lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally ‘Madee’, amesema amevutiwa na kazi ya msanii nyota katika muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulazizi Chende ‘Dogo Janja’ inayoendelea kufanya vyema katioka vituo mbalimbali vya radio.



Kauli hiyo imekuja baada ya wapenzi wa muziki huo, kufikiria kwamba Madee angeichukia ngoma hiyo ya Dogo Janja inayokwenda kwa jina la  ‘Ya Moyoni’ kwa kuhisi kuwa imemzungumzia yeye lakini haijawa hivyo.



Akizungumza Dar es Salaam jana, Madee alisema kuwa bado ni shabiki mkubwa wa Dogo Janja na anampongeza sana kwa kufanya vizuri na ngoma hiyo inayoendelea kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio.



Madee alisema amependa zaidi kiitikio kilichofanywa na PNC lakini ameongeza kuwa kama angeisikia kabla ya kupelekwa redioni angependekeza yafanyike marekebisho kadhaa.



Miezi kadhaa iliyopita Madee na Dogo Janja walikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya Tanzania baada ya Madee kushutumiwa kumtumia msanii huyo isivyotakiwa kiasi cha kufanya aondoke katika kundi hilo.

" MATOKEO YA KIDATO CHA SITA".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA



MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha. 

“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.

 "Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja kwa moja katika kumudu mitihani bali ni kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila kuwaandaa.

" Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika na wanafunzi wapya, yaani kama wanaanza kidato cha kwanza wawe wanapewa mitihani ya kupimwa kwa kuzingatia alama mpya na waendelee nazo hadi mitihano yao ya mwisho. 

“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato cha tano mara wanapoanza shule, kila mitihani wanayopewa isahihishwe na kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka NECTA. 

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya alama, alama mpya zilizokuwa zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34 hadi sifuri; badala ya alama hiyo F kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia 35 tofauti na awali, yaani alama 21. 

Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha sita tofauti na muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa kidato cha nne ambapo matokeo yalitangazwa na kisha kufutwa ili kuyapanga upya kwa kutumia alama za zamani. 

Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema; “Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa kuandaa matokeo ya kidato cha sita unaendelea, siwezi kusema lini hasa utakamilika lakini nina uhakika ni katika muda muafaka.” 

Kuhusu matokeo ya kidato cha sita kucheleweshwa kutokana kupangwa upya ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana na matumizi ya alama mpya za kufaulu, Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa kuzingatia alama za zamani) yamekuja wakati mchakato wa kuandaa matokeo ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa kufuata maagizo hayo.” 

Hata hivyo, hakuweka bayana kama matokeo ya awali kabla ya maagizo ya Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia alama za zamani yamewafanya wanafunzi wengi kufeli na badala yake akasema; “Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu mchakato wa matokeo hayo haukuwa umefika mwisho. Takwimu rasmi hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si sahihi kusema rasmi walifeli.” 

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa matokeo yanayotarajiwa ya kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi 50,000 wamepata unafuu katika matokeo yao tofauti na awali. 

Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha nne mwaka jana yaliyotangazwa Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani huo walifaulu. 

Katika matokeo hayo idadi ya wasichana waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi 80,686 na idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361. 

Katika matokeo hayo watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni 15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903 lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo itabadilika kwa sababu ya alama kuongezwa kwa watahiniwa hao wa mwaka 2012. 

Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja na vituko walivyofanya baadhi ya wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani na kutokana na makosa hayo, watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao. 

Source: Raia Mwema.

Thursday, May 16, 2013

NU JOINT> Cash clan Yaja Tena na "Wakali wa Kitaa"

Cash clan Yaja Tena na "Wakali wa Kitaa", Ngoma ambayo wamerekodi pande za noizmekah studios Arusha Tanzania kwa usimamizi wa producer Defxtro, Pata kuusikiliza HAPA na endelea kusupport muziki wa Tanzania

PICHA YA LEO:KAMA WEWE NI MWANDISHI WA HABARI HII PICHA UNGEIPA JINA GANI?


Wednesday, May 15, 2013

"HAPPY BIRTHDAY ADAM MCHOMVU (baba Jonii)" KUTAMBULISHA MIXTAPE YAKE YA KWANZA SIKU YA BIRTHDAY YAKE LEO MAY 16 2013


Adam Mchomvu a.k.a baba jonii Radio presenter clouds fm mwenye crown ya best presenter, anatarajia kutoa mixtape yenye  ngoma kumi na nane alioshirikiana na wasanii mbali mbali kama Jose Mtambo, Banana Zorro, Illimatix, Cliff mitindo, G.nako, Nikki wa 2, Babuu wa kitaa, TID, na wasanii wengine wengi kama zawadi kwa mashabiki wake ibaki kama kumbukumbu kwa kile anachokifanya hewani (on air) ... mixtape itaingia kitaani soon baada kupreview ngoma hizo ndani ya double XL (XXL) kuanzia leo saa tisa alasiri kwa hot 3 @ 3 ..... big up baba la baba!

Mwisho wa kusubiri ni kesho-MwanaFA

Mwanamuziki anayesifika kwa tungo zenye uwezo wa kusambaza misemo mitaani, Hamees mwin'jumah, au MwanaFA kama wengi walivyozoea kumuita, sasa ametangaza kuiachia mtaani ngoma yake ya Kama Zamani ambayo mwanzoni ilikuwa iingie mtaani Februari 25 mwaka huu(..kama inavyoonekana kwenye Poster)
"Kulikuwa na sababu za kibiashara, ikabidi ingoje lakini sasa, the wait is over, na kuanzia kesho itakuwa ikiuzwa kwenye mitandao na pia itakuwa ikisikika redioni.
Katika wimbo huo MwanaFA amewashirikisha wanamuziki kutona The Kilimanjaro Band pamoja na Man'dojo na Domokaya

SERIKALI BAADA YA KUZUIA UNYWAJI NA UZALISHAJI WA VIROBA HATIMAYE KINYWAJI CHA SODA CHAANZA KUPIGWA MARUFUKU NA CHENYEWE

*Yakatazwa shuleni, watoto chini ya miaka 12
*Sasa yabainika kuwa ina sumu inayoua taratibu
*Yagundulika kupumbaza na kusababisha uteja

SIKU chache baada ya gazeti la Mtanzania kuripoti madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda, katika utafiti wake gazeti hilo limebaini mengine mapya.
Kwa mujibu wa utafiti huo, imebainika kuwa soda imepigwa marufuku kutumiwa na watoto walio na umri chini ya miaka 12 na walio shuleni katika baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani, kutokana na madhara ya kiafya yanayosababishwa na kinywaji hicho.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la The Press Television Technology Advertising and Branding (Adweek) zinazonukuu taarifa ya kampuni moja kubwa duniani inayozalisha kinywaji aina ya soda, imeamua kupambana na unene (obesity), unaosababishwa na unywaji wa soda kwa kuondoa matangazo ya vinywaji vyake kwenye vyombo vya habari.

Kampuni hiyo kupitia taarifa yake hiyo iliyotolewa katika moja ya sherehe zake, ilieleza kuwa lengo la kuondoa matangazo hayo ni kuwanusuru watoto wadogo na matumizi ya vinywaji aina ya soda vilivyobainika kuwa na madhara katika mwili wa binadamu.

Nchini Marekani, tayari imekwishapitishwa sheria inayokataza watoto walio na umri wa chini ya miaka 12, kunywa kinywaji aina ya soda.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, alieleza kuwa mipango ya mbeleni ya kampuni yake ni kutengeneza kinywaji hicho kikiwa na kiwango kidogo cha Kalori na kubuni kinywaji cha aina hiyo ambacho kitakuwa hakina Kalori.

Alisema mipango hiyo itatekelezwa duniani kote ambako kinywaji cha aina ya soda kinatengenezwa na nchini Marekani tayari imekwishaanza kutekelezwa.

Aidha, Kampuni hiyo imeahidi kuweka wazi virutubisho vyote vinavyotumika kutengeneza bidhaa zake na kuahidi kutoa misaada ya hali na mali kwa nchi zote 200 duniani ambako kinywaji cha soda kinauzwa.

Mbali na Marekani, kinywaji cha aina ya Soda kimekwishapigwa marufuku shuleni katika nchi za Uingereza, Ufaransa na katika majimbo ya Los Angeles, Philadelphia na Miami nchini Marekani na kwa watu wazima matumizi yake yanaelekezwa kuwa ya kiwango kidogo sana.

Vyombo vya habari vya nchini New Zealand, mwezi Machi mwaka huu viliripoti kuwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Natasha Harris (31), alifariki kutokana na unywaji wa soda nyingi.

Shirika la habari la AFP la Ufaransa, liliripoti tukio hilo kwa kueleza kuwa Natasha alikuwa akinywa soda nyingi kila siku, jambo ambalo liligeuka kuwa sehemu ya maisha yake kwa kipindi cha miaka mingi.

Kwamba familia ilikuwa ikimuita teja wa soda, baada ya meno yake kuoza kwa sababu ya kunywa soda, alijifungua mtoto ambaye hakuwa na fizi jambo ambalo liligundulika baadaye kuwa lilisababishwa na matumizi makubwa ya kinywaji hicho.

“Tumegundua kwamba, kwa kuzingatia ushahidi uliopo, kama sio unywaji wa soda uliopitiliza, Natasha Harris asingekufa katika muda ule na katika hali alivyokufa

“Ripoti ya Daktari aliyechunguza maiti yake (Pathologia), iligundua kwamba ini lake lilipanuka sana, likawa na mrundiko mkubwa wa mafuta kutokana na kula sukari kwa wingi. Kuwepo kwa madini aina ya ‘potasiam’ kwa kiwango kidogo sana kwenye damu yake, pia kulitokana na unywaji wa soda.” Taarifa ya kitabibu katika Hospitali aliyofia nchini New Zealand ilieleza.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi zilizo kwenye mitandao ya wanasayansi waliobobea duniani, unywaji wa soda humpumbaza mtumiaji na kumsahaulisha kula vyakula vyenye madini muhimu mwilini.

Moja ya andishi linalotahadharisha utumiaji wa kinywaji cha soda na kukitaja kuwa cha hatari kwa matumuzi ya binadamu, ni Jack Winkler, Profesa wa sera za lishe katika Chuo Kikuu cha Metropolitan nchini London, linaloeleza kuwa Soda ni bidhaa ya kishetani inayoua binadamu taratibu baada ya kinywaji hicho kumzalishia magonjwa mengi mwilini yanayomfanya kuwa tegemezi wa dawa.

Wakati msomi huyo akieleza hayo katika utafiti wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Dk. Raymond Wigenge, amelieleza gazeti hili soda siyo kinywaji hatari kwa matumizi ya binadamu kwa sababu kinatumiwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano ofisini kwake wiki iliyopita baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda katika mwili wa binadamu, Dk. Wigenge alisema pamoja na changamoto zilizopo katika kinywaji hicho, taasisi yake haipingi uwepo wa kinywaji hicho sokoni.

“Soda haina shida kwa binadamu na hata mkiendelea kuandika suala hili, sisi tutaendelea kuueleza umma kwamba waendelee kupata kinywaji, hivyo kama ambavyo tumekuwa tukifanya,” alisema.

Alipoulizwa kama anakubaliana na tafiti za wanasayansi bingwa wa magonjwa ya binadamu walioeleza katika tafiti zao kuwa unywaji wa soda una madhara katika mwili wa binadamu, alisema hizo ni changamoto za kawaida, kwa sababu madhara yaliyomo kwenye soda hayamuathiri mtu mara moja bali huchukua muda mrefu.

Wakati Dk. Wigenge akieleza msimamo wake kuhusu kinywaji aina ya soda, nchini Mexico, taasisi ya El Poder del Consumidor inayojihusisha na kutetea walaji, inashinikiza Serikali ya nchi hiyo kuzilazimisha kampuni za soda kuorodhesha madini na chembechembe zote za kemikali zinazotumika kutengeneza kinywaji hicho.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Alejandro Calvillo, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa unywaji wa soda ni hatari na hilo limethibitishwa na wataalamu wa afya duniani kuwa soda ni sumu mbaya, inauwa taratibu.

Tafiti mbalimbali za wanasayansi zinaeleza kuwa soda ina asidi aina ya ‘phosphoric’ yenye uwezo wa kuvuruga madini ya ‘calcium’ yaliyoko mwilini na kusababisha mifupa na meno kudhoofika.

Aidha, asidi aina ya ‘phosphoric’ huvuruga asidi aina ya ‘hydrochloric’ iliyo tumboni mwa binadamu na hivyo kuharibu mfumo wa kusaga chakula.

Viwanda vya soda ndio watumiaji wakubwa wa sukari na wanasayansi wanasema sukari hupandisha kiwango cha ‘insulin’ ambayo husababisha kasi ya mzunguko wa damu, ugonjwa wa moyo, kupanda kwa ‘Cholesterol, kisukari, kuzeeka mapema, ongezeko la uzito na maradhi mengine.

Aidha inadaiwa kuwa viwanda vya soda pia hutumia dawa ya kulevya aina ya kafeini. Wataalamu wanasema vinywaji vyenye kafeini, husababisha kupanda kwa mapigo ya moyo, kasi ya mzunguko wa damu na matatizo ya kizazi.