Mwili wa marehemu Ayoub Mlay baada ya kupigwa risasi.
TUKIO
la kuuawa kwa mfanyabiashara kijana mwenye mafanikio, Ayoub Mlay, siyo
tu linaacha simanzi kwa Watanzania bali pia ni fundisho kwa jamii na
serikali.
MLAY,
alifariki dunia usiku wa Alhamisi iliyopita, Mei 16, mwaka huu baada ya
kupigwa risasi kwenye Klabu ya Ambrosia, iliyopo Kawe Beach jijini Dar
es Salaam.
Simanzi
inakuja kwa sababu Mlay, 38, alikuwa mfanyabiashara kijana aliyeonesha
mafanikio na kupiga hatua kubwa, amefikwa na mauti akiwa bado na moto wa
kusaka maendeleo zaidi kwenye biashara zake na maisha kwa jumla.
Kwa
Conrad ambaye ni kijana mdogo pia, anaingia kwenye msukosuko lakini
nyuma yake kuna funzo la umiliki na matumizi sahihi ya silaha za moto
ambazo kwa sasa zimekuwa kama ‘fasheni’ kwa vijana wengi wa mjini.
WOTE NI WATOTO WA ARUSHA
Mlay ni mfanyabiashara wa Arusha ingawa mara kwa mara hupatikana Dar es Salaam kutokana na mizunguko yake ya kibiashara.
Conrad, naye ni mwenyeji wa Arusha, ingawa kwa sasa makazi yake yapo Dar es Salaam.
Kuhusu kazi ya Conrad, mmoja wa watu waliohojiwa na gazeti hili nje ya
Klabu ya Ambrosia, alisema: “Kwa kweli huwa tunamuona, wengi tunamuona
ni mtoto wa mjini tu, kwani hatujui anajishughulisha na nini.”
Marehemu Mlay enzi za uhai wake. |
CHANZO CHA UGOMVI
Mtoa
habari wetu aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa Mlay
na Conrad ni watu waliokuwa wanafahamiana na kuna jambo walikuwa
wanazungumza.
“Siyo
rahisi sana kujua walichokuwa wakizungumza ila baadaye yalitokea
mabishano. Walitaka mpaka kushikana ili kupigana, watu wakawazuia.
Inaonekana Conrad hakukubali, maana aliamua kutoka nje mbio.
“Kwa
haraka haikujulikana alifuata nini kule nje, tuliokuwepo tuliamini
ameamua kukimbia lakini kumbe alikuwa amefuata bastola. Aliporudi,
alikuwa na bastola mkononi, baada ya hapo hata hakutaka kuzungumza
maneno mengi, alimpiga Mlay risasi kisha akataka kutoweka,” kilisema
chanzo chetu.
WALINZI WALIVYOMDAKA
Chanzo chetu kilibainisha kuwa wakati anapita na bastola kuingia ndani,
walinzi walimpisha kwa sababu ya kuhofia usalama wao lakini kipindi cha
kutoka, walijipanga kumdhibiti.
Kiliendelea kusema, Conrad akiwa anatoka, walinzi walifanya kama
wanampisha na baada ya kupita, walimbana mikono na kumnyang’anya bastola
kisha wakamfunga kamba kabla ya kupiga simu kuita polisi.
Dakika kadhaa baada ya kupiga simu, polisi walifika na kufanya mahojiano
na watu waliokuwepo eneo la tukio, kabla ya kumchukua mtuhumiwa na
kumpeleka Kituo cha Polisi Kawe, Dar es Salaam.
Vilevile, polisi walimchukua Mlay na kumuwahisha Hospitali ya Mkoa wa
Kitabibu, Kinondoni, Dar es Salaam ili akapatiwe matibabu lakini baadaye
ilibainika alikuwa ameshakata roho.
ACP Charles Kenyela. |
MADAI KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA SILAHA
Kwa
mujibu mtu aliyejitambulisha kwa jina la Matidau, Conrad alikuwa na
mazoea ya muda mrefu ya kuonesha bastola yake na kuwatishia watu
aliotofautiana nao.
“Tunamjua
Conrad, kuna watu walishamwonya lakini hakusikia, ikafikia wakati
kwamba anapoanza ugomvi, basi tunaomjua tunakaa mbali naye kwa sababu
lolote linaweza kutokea.
“Kuna
kipindi alinyang’anywa bastola kwa sababu ya tabia yake ya
kuioneshaonesha ovyo pamoja na kutishia watu. Tukio hili la mauaji ya
Mlay linatufanya tujiulize hiyo bastola alirejeshewa katika mazingira
gani au ni nyingine?” kilihoji chanzo.
MINONG’ONO KUHUSU FEDHA
Kuhusu kile ambacho Mlay na Conrad walibishana, kulikuwa na maneno ya
pembeni kutoka wa watu waliokuwepo eneo la tukio kwamba chanzo cha
ugomvi ni fedha.
“Unajua inapotokea matukio makubwa kama haya, watu wa eneo la tukio
wakati mwingine ndiyo huwa wa kwanza kupotosha. Kwa mfano, yapo madai
kuwa Mlay alimtuma kazi Conrad, sasa baadaye kukawa na mabishano kuhusu
malipo.
“Yote yatazungumzwa lakini jambo ni baya sana. Fikiria kwamba Mlay ni
mtu aliyekuwa ameajiri watu, ana familia na marafiki, wote hao
wataathirika kwa namna moja au nyingine kwa kumpoteza mtu waliyempenda,”
alisema mtoa habari wetu.
Mlay enzi za uhai wake. |
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP
Charles Kenyela alisema kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea na akaongeza
kuwa Conrad alimfyatulia Mlay risasi ya kifua.
Kuhusu madai kwamba Conrad ni mzoeafu wa tabia za kuchezea silaha na
kutisha watu kiasi kwamba hata jeshi lake lina taarifa na liliwahi
kumnyang’anya kabla ya kumrudishia kinyemela, Kenyela alijibu: “Hizo
taarifa sina, ngoja nizifuatilie kwanza, maana siwezi kuzungumza jambo
nisilo na uhakika nalo.
“Nilicho na uhakika nacho ni hiki; kwamba mtuhumiwa tunamshikilia na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.”
KIFUATACHO
Bado kuna maswali kuhusu tukio hili, timu nzima ya Kampeni ya Fichua
Maovu ya Global Publishers, imejipanga sawasawa kufuatilia kwa kina na
mara itakapokamilika, mambo yatakuwa hadharani kupitia magazeti yake
ambayo ni damu moja na hili; Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
CHANZO : GPL
0 comments:
Post a Comment