Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, June 5, 2013

ANGALIA PICHA ZAIDI YA 40 HAPA, MAPOKEZI YA ALBERT MANGWEA NYUMBANI KWAO MOROGORO

Msafara wa kupokea mwili wa msanii  marehemu Albert Mangwea ukiwa unaingia morogoro hapa ni eneo la nane nane,Umati mkubwa umejitokeza katika mapokezi hayo jioni ya leo




















 UMATI WA WATU WAKIWA NYUMBANI KWA MANGWEA.
ASKARI AKIONGOZA MSAFARA ULIOBEBA MWILI WA MANGEA MIKESE MKOANI MOROGORO  AMBAPO ULIPOKELWA NA WASAN
II WA FANI MBALIMBALI WAKATI UKITOKEA DAR ES SALAAM



PICHA JUMAMTANDA
 MASHABIKI WA NGWEA WAKIWA WANAKIMBIA SAMBAMBA NA GARI LILILOBEBA MWILI WA NGWEA MIKESE.
 MSAFARA WA MAFARI BARABARA ENEO LA MKAMBARANI ULIKUWA HIVI.
 HAPA MKAMBARANI, KULIA NI BASI LA BM LIKIVURUGA MSAFARA HUO.
MASHABIKI WA MANGWEA WAKIWA KATIKA KANDO YA BARABARA KATIKA MZUNGUKO WA MSAMVU MOROGORO WAKATI MSAFARA UKIELEKEA  NYUMBANI KWA MANGWEA KIHONDA.
 
 MAPOKEZI YA MWILI WA NGWEA ENEO LA MAZIMBU ROAD KIHONDA.
BASI LA ABOOS AMBALO LILIWABEBA WASANII WA FANI MBALIMBALI, HAPA LIKIWA MIKESE WAKISUBIRI  MSAFARA WA ULIOBEBA MWILI WA MANGWEA.

PUMZIKA KWA AMANI ALBERT MANGWEA .... HII HAPA HISTORIA YA MAISHA YAKE HAPA DUNIANI

Hatimaye mwili wa Mangair umewasili jana kutoka Afrika ya Kusini ambapo alikumbwa na kifo cha ghafla akiwa katika hatua za mwisho za kurudi nyumbani baada ya kufanya maonyesho nchini humo.
Albert Kenneth Mangwea alizaliwa Mbeya tarehe 16 November mwaka 1982 akiwa ni mtoto wa mwisho kwa baba yake aliyekuwa na watoto 10, na mtoto wa 6 kwa mama yake. Mapema familia yake ilihamia Morogoro ambapo akajiunga na shule ya msingi Bungo hadi Darasa la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza elimu ya msingi katika shule ya Msingi Mlimwa Dodoma.Alijiunga na shule ya sekondari ,na huko ndiko alikutana na wasanii wenzie akina Mez B, Noorah na wengine na kuanza harakati za sanaa yake.
Alikuja Dar es Salaam na mwaka 2003 na chini ya P Funk wa Bongo Records alirekodi kibao kilichomtambulisha rasmi kilichojulikana kama Gheto Langu na jina la Ngwair likawa rasmi hewani. Ngwair alitoa album yake ya kwanza 2004 iliyojulikana kama AKA MIMI, album iliyopata tuzo la Kilimanjaro Music Awards ikiwa ni album bora ya Hiphop , pia album hiyo ilikuwa na wimbo Mikasi uliyoleta malumbano katika jamii hata kutajwa na BASATA kuwa upigwe marufuku.
 
Album yake ya pili iliitwa Nge iliyotoka 2009, ikawa na nyimbo kama CNN na Nipe Dili ambao ulimpatia tuzo lnyingine ya Kilimanjaro Music Awards ukiwa wimbo bora wa Hiphop.


MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMEN

HIKI NDO KILICHOTOKEA HADI DIAMOND KUTAKA KUSABABISHA TARATIBU ZA KUAGA MWILI WA MANGWAIR KUTAKA KUVURUGIKA


MSANII maarufu wa muziki wa kiazazi kipya nchini Tanzania Abdul Nassib (Diamond Paltinumz) alifika katika viwanja wa Leaders Club na  kupata nafasi ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la aliyekuwa msanii mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.


Mangwea ambaye alifariki Dunia katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini Mei 28 mwaka huu, mwili wake uliwasili nchini Tanzania  jana na kupokelewa na maelfu ya mashabiki wa muziki wake na hatimaye mwili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhifadhiwa.

Mwandishi wa habarimpya.com aliyekuwa katika viwanja hivyo alimshuhudia Diamond pamoja na baadhi ya wasanii wenzake  wakiuungana na maelfu ya watanzania waliofika katika viwanja  hivyo.

Akiwa amevalia nguo za rangi nyeusi kama ilivyo kawaida ya watu wanaojua kubangilia mavazi kulingana na matukio huku wengine pia wakitupia kitu cha rangi nyeupe,hata hivyo msanii huyo kipenzi cha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hususan wakina dada kutoka nyimbo zake za kulilia mahaba ya warembo alijikuta akiharibu utaratibu mzima wa kuuaga mwili wa Mangwea.

Ingawa Kamati ya mazishi ilishatangaza kufunga zoezi la kuuaga mwili huo, Diamond aliinuka kwenye kiti chake kwa lengo la kuondoka uwanjani hapo, ghafla alivamiwa na mashabi wa muziki wake waliokuwa wakihitaji kuongea naye. Tukio hilo lilisababisha umati wote uliokuwa wakisubiri msafara wa mwili wa Mangwea kuondoke uwanjani hapo kutawanyika na kumkimbilia Platinumz hadi kweneye gari lake ambapo aliingia na bado wakaendelea kulifukuzia gari lake likiondoka viwanjani hapo.

Angalia Picha za M2 The P ametoka hospitali. Bado hajui kama Ngwair amefariki

M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitali
M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitaliMsanii M2 the P aliyekutwa mahuhuti pamoja na Ngwair ambaye alifariki, anaendelea vizuri kiafya na ameshatoka hospitali. Mpaka sasa M To The P hajui kama Mangwea amefariki na anadhani mwenzake ametangulia kwenda Dar es Salaam.
m2-the-p-0

m2-the-p-1

"Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad"- Jestina George
“Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad”- Jestina George
m2-the-p-3

Kwa mujibu wa Jestina George, Magie amekuwa karibu sana na M2 The P na alikua karibu na marehemu Albert “Ngwair” Mangwea kwa muda waliokuwa Africa Kusini. kama inavyoonekana pichani, leo Magie alienda kumcheki M2 The P, kumpa moyo na kumchangamsha. Alipo fika alimkuta M2 The P amejawa na mawazo huku kikombe chake cha chai kiko mezani ikabidii aanze kumtania tania angalau aondokane na mawazo. Bado anamuuliza rafiki yake kipenzi Mangwea maana hajui yaliyo mfika. Tuendelee kumuombea M2 The P maana ana mtihani mkubwa mbele yake akija kujua ukweli, na ni Mungu pekee ndo ataweza kumsaidia

LIVE TAZAMA PICHA TOKA MOROGORO AMBAKO ALBERT MANGWEA ATAZIKWA BAADA YA KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS CLUB



 Wageni waliofika msibani Morogoro kwa marehemu Mangwea. 
 Masufuliya ya chakula kwa watu waliokuwepo msibani morogoro.
 Wakipanga jambo kutokana na eneo la nyumbani kwao marehemu Mangwea kuwa padogo.

KIJANA ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIMBAKA BINTI WA MIAKA 10 MKOANI IRINGA


Mkazi mmoja wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi baada ya kukutwa akimbaka binti wa miaka kumi.

Tukio hilo linaelezwa kutokea jana saa nane mchana, pale ambapo mazazi wa binti huyo alipomsikia mwanaye akilia kwa uchungu, na aliposogea kujua kulikoni, alimshuudia kijana huyo akiendelea na ubakaji jambo lililosababisha apige kelele kuomba msaada wa wananchi.


 
Kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ubakaji katika eneo hilo, mtuhumiwa huyo alijikuta akipokea hasira za wananchi kwa kupigwa na kunusurika kuchomwa moto baada ya baadhi ya wananchi wengine kushauri afikishwe polisi.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Iringa akivuja damu kichwani.

ANGALIA PICHA ZA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ALBERT MANGWEA ZINAENDELEA KUTOLEWA.



Dah this is it ndugu yetu mpendendwa ndo ametangulia mbele za haki na sasa ule muda wa kutoa heshima za mwisho ndo umewadia. Mungu awape nguvu wale wote waliofikwa na msiba huu. Image credit DJ Choka

Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho

Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens. Sasa naskia watu badala ya kwenda na kuaga wao wako busy wanapiga picha kha hizi teknolojia aiseee tutajutaaaa 
Baadhi ya ma super star wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga.

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Diamond

d8fdca7eccf211e2a7ed22000a1f8f24_7



1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.

2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.

3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.

4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.

5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.


6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.

7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.


8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.

9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.

10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.