Hatimaye
mwili wa Mangair umewasili jana kutoka Afrika ya Kusini ambapo
alikumbwa na kifo cha ghafla akiwa katika hatua za mwisho za kurudi
nyumbani baada ya kufanya maonyesho nchini humo.
Albert Kenneth Mangwea alizaliwa Mbeya
tarehe 16 November mwaka 1982 akiwa ni mtoto wa mwisho kwa baba yake
aliyekuwa na watoto 10, na mtoto wa 6 kwa mama yake. Mapema familia yake
ilihamia Morogoro ambapo akajiunga na shule ya msingi Bungo hadi Darasa
la 5 kisha akahamia Dodoma pamoja na baba yake nakumaliza elimu ya
msingi katika shule ya Msingi Mlimwa Dodoma.Alijiunga na shule ya sekondari ,na huko ndiko alikutana na wasanii wenzie akina Mez B, Noorah na wengine na kuanza harakati za sanaa yake.
Alikuja
Dar es Salaam na mwaka 2003 na chini ya P Funk wa Bongo Records
alirekodi kibao kilichomtambulisha rasmi kilichojulikana kama Gheto
Langu na jina la Ngwair likawa rasmi hewani. Ngwair alitoa album yake ya
kwanza 2004 iliyojulikana kama AKA MIMI, album iliyopata tuzo la
Kilimanjaro Music Awards ikiwa ni album
bora ya Hiphop , pia album hiyo ilikuwa na wimbo Mikasi uliyoleta
malumbano katika jamii hata kutajwa na BASATA kuwa upigwe marufuku.
Album
yake ya pili iliitwa Nge iliyotoka 2009, ikawa na nyimbo kama CNN na
Nipe Dili ambao ulimpatia tuzo lnyingine ya Kilimanjaro Music Awards
ukiwa wimbo bora wa Hiphop.
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMEN
0 comments:
Post a Comment