Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, October 22, 2012

viongozi wa jumuiya ya uamsho wafikishwa mahakamani zanzibar leo


Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi.
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.

Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.
Gari la Polisi ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linawasili Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Thursday, October 18, 2012

PICHA ZAIDI WAKATI SHEIKH PONDA NA WAFUASI WAKE WALIPOFIKISHWA MAHAKAMANI JANA

 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (mwenye kanzu) akiwa chini ya ulinzi wa askari wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam baada ya kusomewa mashtaka ya wizi, uvunjifu wa amani na uchochezi.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akishuka katika gari lililomleta katika Mahakama ya Kisutu jana
 Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa (mwenye kanzu nyeupe mbele) akiwa katiika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alikofikishwa pamoja na wafuasi wanaomuunga mkono kama wanavyoonekana pichani.
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa (mwenye kanzu nyeupe mbele) akiwa katiika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Hali ya ulinzi ilikuwa kama inavyoonekana, ambapo askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakilinda amani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakitawanyika baada ya Sheikh Ponda na wafuasi wake kurejeshwa mahabusu. 
Sheikh Ponda akipanda gari kurejea mahabusu. Picha zote na Habari Mseto Blog.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, na wafuasi wake 49 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijiji hapa leo mchana,
kwa kosa la uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Shilingi milioni 59.

Sheikh Ponda wanaoshitakiwa pia uvamizi wa kiwanja namba 311/2/4 kilichoko Block T Chang’ombe ambacho ni mali ya Kampuni ya Agritanza,   wanatetewa na wakili wa kujitegemea Nassor Mansoor.

Wakati wakifikishwa na baadaye  kuondoka kwenye viwanja vya mahakama hiyo wakiwa ndani ya magari ya Polisi na Jeshi la Magereza, walikuwa wakisikika wakipaza sauti wakisema; ‘Allah Akbar, Allah Akbar’.
 
Sheikh Ponda pia amefikishwa mahakamani hapo akidaiwa kuwashawishi Waislamu kugomea zoezi la sensa ya watu na makazi, iliyofanyika mwezi uliopita nchini kote na kufanya zoezi hilo kufanyika kwa kusuasua.

Hali ya usalama kwenye mahakama ya Kisutu na maeneo ya jirani iliimarishwa mchana wa leo, wakati Sheikh Ponda aliyekamatwa jana na Jeshi la Polisi na kufikishwa Makao Makuu ya Jeshi hilo katikati ya jiji – akifikishwa hapo na Waislamu wengine walioshiriki uvamizi wa kiwanja Chang’ombe.

Baada ya kukamatwa juzi usiku na kufikishwa Kituo Kiuu cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya Waislamu wanaomuunga mkono walivamia kituoni hapo kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao, kabla ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Hali ya amani imekuwa tata nchini katika siku za karibu, tangu Ijumaa iliyopita, ambapo kundi la watu wanaosadikika kuwa ni Waislamu walivamia kituo cha polisi huko Mbagala Zakhiem wakishinikiza wakabidhiwe kijana aliyedaiwa kukojolea Msahafu.

Baada ya kushindwa kufanikisha azma hiyo, hasira zao zikaishia katika uvamizi wa makanisa, ambayo kadhaa yalichomwa moto, kuharibiwa na kuibiwa kwa vitu mbalimbali na polisi kuwakamata watu zaidi ya 120 kabla ya kuchujwa na kubaki 36 waliofikishwa mahakamani.

Hali haikuwa shwari pia Visiwani Zanzibar, ambako kikundi maarufu cha Uamsho kimefanya vurugu jana, wakimskaka kiongozi wao mkuu Sheikh Farid, aliyedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana juzi usiku.

Kesi ya Sheikh Ponda ambaye alinyimwa dhamana na wenzake itatajwa tena Novemba Mosi mwaka huu, ambapo watarudi mahakamani hapo.

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOPIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER......

SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.

LUCKY DUBE ATIMIZA MIAKA KADHAA HII LEO TOKA AFARIKI

Naweza kusema kwamba katika muziki wetu wa Reggae hapa Africa tulimpoza mwenzetu ambaye alitutangua katika njia za haki huyu si mwingine alis Lucky Philip Dube lakini katika upande wa muziki mashabiki wanamfahamu kwa jina la Lucky Dube.Sasa basi kwa siku ya leo amefikisha miaka mitano toka afariki siku kama hii ya leo tarehe 18 october.Rest in peace For him tutaendele kumkumbuka kwa kazi zake nzuri za muziki wa hapa African.
 

VURUGU ZANZIBAR ZA CHUKUA SURA NYINGINE, ASKARI AUAWA KINYAMA KUFUATIA VURUGU ZA WAFUASI WA UAMSHO.


 Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.

 Mwandishi wa Habari wa Hits FM Mustafa akiuliza maswali katika Mkutano wa Jeshi la Polisi juu ya fujo na ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi,hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano wa Jeshi la Polisi kuelezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.

 
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Bububu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani leo, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo  yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana. 
Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama  sheria za nchi zinavyowaelekeza.
Amesema mpaka hivi sasa watu 10 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliyotokana na vurugu za jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa Sheikh Farid unaendelea. 
Ameongeza kuwa  kutekwa kwa Sheikh Farid kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka kwake kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said ambae alikuwa dereva wake katika hatua za mwisho  maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua umeme.
“Sheikh Farid alimuamuru Said amuache katika eneo hilo aende nyumbani kupeleka umeme na wakati huo akaendelea na mazungumzo na watu wengine  walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya NOAH  ambayo nambari zake hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.     
Amesema fujo hizo zilisababisha hasara  kubwa kwa Serikali, Chama tawala na  wananchi ikiwemo kuchoma na kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani za CCM za Kisonge na Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari kuvunjwa vioo na kuvunja duka la pombe na kuiba mali iliyokuwemo ndani. 
Hata hivyo amedai hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote.
Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, na kutoa taarifa za watu waliohusika na  vurugu pamoja na  mauaji ya Coplo Said Abdulrahaman.      

Wednesday, October 17, 2012

Zanzibar Yachafuka Kukamatwa Kiongozi Wa Uamsho


vurugu mtaani

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari, Kuhusu Msiba Wa Wachezaji Wa Rusumo FC


 RAMBIRAMBI MSIBA WA WACHEZAJI RUSUMO FC Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya wachezaji watano wa timu ya Rusumo FC ya mkoani Kagera vilivyotokea jana jioni (Oktoba 16 mwaka huu).

Tamko La Waislamu Kulaani Uchokonozi Wa Kidini

 Sheikh kutoka Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda (kushoto) akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na kile walichokiita kadhia iliyotokea tarehe 10.10.2012 ya kunajisiwa kwa kitabu kitufu cha Qur’ani. Sheikh kutoka Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda (katikati) akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na kile walichokiita kadhia iliyotokea tarehe 10.10.2012 ya kunajisiwa kwa kitabu kitufu cha Qur’ani.  


Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini Tanzania wametoa tamko kufuatia kitendo cha kijana Emmanuel Josefati (14) kukojelea kitabu kitukufu cha Qur’an na kusababisha mgongano wa mawazo miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao wamesema ‘Tunalaani Kitendo cha kukojolewa Qur’an Tukufu ambayo ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam Wote Duniani’.
‘Tunataka kusikia tamko la serikali la kulaani kitendo cha kukojolewa Qur’an’.
‘Tunataka serikali kukemea kitendo cha Jeshi la Polisi kushambulia Misikiti, waumini na Kuvuruga ibada’.
‘Tunalaani vitendo vya uchokozi wa kidini’. ‘Tunalaani matumizi ya matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya raia yaliyofanywa na Polisi’.
‘Tumehuzunishwa sana na kitendo na kitendo cha kushambuliwa Misikiti na Makanisa kilichotokea Mbagala’.
‘Tunatoa siku 7 ndani ya siku hizi Waislamu wanaoshikiliwa na Polisi wapewe haki yao ya dhamana’.

Tuesday, October 16, 2012

Monday, October 15, 2012

Pombe,Sigara Na Ukahaba Marufuku Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku biashara ya ukahaba, matangazo yote ya pombe na uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu katika visiwa vya Unguja. Hayo yamebainika kufuatia marekebisho ya kifungu cha sheria cha 112, cha mswada wa sheria kuhusiana na hifadhi na usimamizi wa vihatarishi vya afya ya jamii na afya ya mazingira na mambo yanayohusiana na hayo iliyopitishwa ndani ya Baraza la Wawakilishi jana.Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba kutokana na michango mingi ya wajumbe kutaka suala la matangazo ya pombe, uvutaji wa sigara, na biashara ya ukahaba vipigwe marufuku, serikali imekubaliana na maoni ya wajumbe hao. Waziri Duni amesema, kuanzia sasa kwa mujibu wa sheria hiyo itakuwa ni marufuku kutangaza au kushajiisha matangazo ya pombe kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo ufadhili au matamasha ya muziki na starehe katika visiwa hivyo. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema anakubaliana na maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuondoa kabisa matangazo ya pombe na kwamba serikali imefanya vyema, kwani hivi sasa Shirika la Afya Duniani WHO, Umoja wa Ulaya EU na baadhi ya nchi ikiwemo Sweden tayari zimezuia matangazo ya pombe na Zanzibar kufuata sheria hiyo ni jambo la busara.

WEMA SEPETU VS AUNT EZEKIEL'WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAAMUA KUOMBA RADHI KUTOKA NA PICHA CHAFU WALIZOPIGA WAKATI WA FIESTA


Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamewaomba radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za Fiesta.

Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa kupigwa picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.


Wakiongena waandishi wa habari Aunty Ezekiel amesema ameumizwa na kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, ndugu jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao wanaowapenda na kuwaheshimu.
Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye chanzo kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu za wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa kunipiga picha wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti yao, hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana.”

Waigizaji hao waliongozana na katibu Mkuu wa shirikisho la filamu Tanzania, TAFF, Wilson Makubi.

Sunday, October 14, 2012

WAKULIMA NA WAFUGAJI WATOLEANA UVIVU - POLISI WAINGIA MITINI



*Mwananchi mmoja achomwa mkuki,Polisi wakimbia.
Ugomvi baina ya Wafugaji wa Wakulima umezuka katika Kijiji cha Simike - Utengule Usangu, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya na kusababisha mwananchi mmoja anayefahamika kwa jina Abeli Mwakyoma kujeruhiwa baada ya kuchomwa mkuki na kundi la wafugaji wa jamii ya Kisukuma.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ACP LIBERATUS BARLOW.

Kamati ya maandalizi ya mazishi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow, kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi, inapenda kuwajulisha wananchi wote utaratibu wa mazishi utakavyokuwa kuanzia mwili kuagwa Mkoani wa Mwanza, Dar es Salaam na kuzikwa nyumbani kwao Mkoani Kilimanjaro.
Jumapili tarehe 14/10/2012 mwili wa Marehemu utaagwa Mkoani Mwanza.
Jumatatu tarehe 15/10/2012 mwili wa Marehemu utasafirishwa kutoka mwanza kuelekea Dar es Salaam nyumbani kwake Ukonga.
  • Jumanne tarehe 16/10/2012 mwili utaagwa nyumbani kwake Ukonga Jijini Dar es Salaam na baadae kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano tarehe 17/10/2012.
Taarifa zitaendelea kutolewa mara kwa mara kadiri ya mipango itakavyokuwa inaratibiwa katika  kila Mkoa mwili utakapofika.
Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Polisi Makao Makuu

Mabingwa Watetezi.... Wafuzu Kwa Kombe La Mataifa Ya Afrika 2013


Zambia, wakiwa ugenini Kampala, waliweza kuwafunga wenyeji wao Uganda magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuutetea ubingwa wao, katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013,