Sheikh
kutoka Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda
(kushoto) akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na kile
walichokiita kadhia iliyotokea tarehe 10.10.2012 ya kunajisiwa kwa
kitabu kitufu cha Qur’ani. Sheikh
kutoka Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda
(katikati) akitoa tamko mbele ya vyombo vya habari kuhusiana na kile
walichokiita kadhia iliyotokea tarehe 10.10.2012 ya kunajisiwa kwa
kitabu kitufu cha Qur’ani.
Taasisi
na Jumuiya za Kiislamu nchini Tanzania wametoa tamko kufuatia kitendo
cha kijana Emmanuel Josefati (14) kukojelea kitabu kitukufu cha Qur’an
na kusababisha mgongano wa mawazo miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao wamesema ‘Tunalaani Kitendo cha kukojolewa Qur’an Tukufu ambayo ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam Wote Duniani’.
‘Tunataka kusikia tamko la serikali la kulaani kitendo cha kukojolewa Qur’an’.
‘Tunataka serikali kukemea kitendo cha Jeshi la Polisi kushambulia Misikiti, waumini na Kuvuruga ibada’.
‘Tunalaani vitendo vya uchokozi wa kidini’. ‘Tunalaani matumizi ya matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya raia yaliyofanywa na Polisi’.
‘Tumehuzunishwa sana na kitendo na kitendo cha kushambuliwa Misikiti na Makanisa kilichotokea Mbagala’.
‘Tunatoa siku 7 ndani ya siku hizi Waislamu wanaoshikiliwa na Polisi wapewe haki yao ya dhamana’.
0 comments:
Post a Comment