Katibu wa Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda (mwenye kanzu) akiwa chini ya ulinzi wa askari wakati akitoka
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam baada ya kusomewa
mashtaka ya wizi, uvunjifu wa amani na uchochezi.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akishuka katika gari lililomleta katika Mahakama ya Kisutu jana
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda
Issa (mwenye kanzu nyeupe mbele) akiwa katiika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, alikofikishwa pamoja na wafuasi wanaomuunga mkono kama
wanavyoonekana pichani.
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda
Issa (mwenye kanzu nyeupe mbele) akiwa katiika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Hali ya ulinzi ilikuwa kama inavyoonekana, ambapo askari wa Kikosi cha
Kuzuia Ghasia (FFU) wakilinda amani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, wakitawanyika baada ya Sheikh Ponda na wafuasi wake kurejeshwa
mahabusu.
Sheikh Ponda akipanda gari kurejea mahabusu. Picha zote na Habari Mseto Blog.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda, na wafuasi wake 49 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijiji
hapa leo mchana,
kwa kosa la
uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Shilingi milioni 59.
Sheikh Ponda wanaoshitakiwa pia uvamizi wa kiwanja namba 311/2/4 kilichoko Block T Chang’ombe ambacho ni mali ya Kampuni
ya Agritanza, wanatetewa
na wakili wa kujitegemea Nassor Mansoor.
Wakati wakifikishwa na baadaye kuondoka
kwenye viwanja vya mahakama hiyo wakiwa ndani ya magari ya Polisi na Jeshi la
Magereza, walikuwa wakisikika wakipaza
sauti wakisema; ‘Allah Akbar, Allah Akbar’.
Sheikh Ponda pia amefikishwa mahakamani hapo akidaiwa
kuwashawishi Waislamu kugomea zoezi la sensa ya watu na makazi, iliyofanyika
mwezi uliopita nchini kote na kufanya zoezi hilo kufanyika kwa kusuasua.
Hali ya usalama kwenye mahakama ya Kisutu na maeneo ya
jirani iliimarishwa mchana wa leo, wakati Sheikh Ponda aliyekamatwa jana na
Jeshi la Polisi na kufikishwa Makao Makuu ya Jeshi hilo katikati ya jiji –
akifikishwa hapo na Waislamu wengine walioshiriki uvamizi wa kiwanja Chang’ombe.
Baada ya kukamatwa juzi usiku na kufikishwa Kituo Kiuu cha
Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya Waislamu wanaomuunga mkono
walivamia kituoni hapo kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao, kabla ya polisi
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Hali ya amani imekuwa tata nchini katika siku za karibu,
tangu Ijumaa iliyopita, ambapo kundi la watu wanaosadikika kuwa ni Waislamu
walivamia kituo cha polisi huko Mbagala Zakhiem wakishinikiza wakabidhiwe
kijana aliyedaiwa kukojolea Msahafu.
Baada ya kushindwa kufanikisha azma hiyo, hasira zao
zikaishia katika uvamizi wa makanisa, ambayo kadhaa yalichomwa moto, kuharibiwa
na kuibiwa kwa vitu mbalimbali na polisi kuwakamata watu zaidi ya 120 kabla ya
kuchujwa na kubaki 36 waliofikishwa mahakamani.
Hali haikuwa shwari pia Visiwani Zanzibar, ambako kikundi
maarufu cha Uamsho kimefanya vurugu jana, wakimskaka kiongozi wao mkuu Sheikh
Farid, aliyedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana juzi usiku.
Kesi ya Sheikh Ponda ambaye alinyimwa dhamana na wenzake itatajwa tena Novemba Mosi mwaka huu, ambapo watarudi mahakamani hapo.
0 comments:
Post a Comment