Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Wednesday, April 17, 2013

HII NDO SABABU YA KIFO CHA BI KIDUDE, SOMA NA SIKILIZA ALICHOKISEMA MJUKUU WAKE

Mjukuu wake aitwaye Omar ameiambia Bongo5 kwa simu muda mfupi uliopita kuwa Bi. Kidude alikuwa amelazwa kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho. “Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” amesema Omar.

HIVI NDIVYO MAUTI YALIVYOMKUTA BI. KIDUDE


Taarifa zilizotufikia muda huu zinasema msanii mkongwe na mahiri katika fani ya muziki wa mwambao Fatuma binti Baraka almaarufu kama Bi Kidude amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Taarifa zilizothibitishwa na mwandishi wa habari wa ITV Farouk Karim zinasema kuwa Bi Kidude amefariki nyumbani kwake Bubu Zanzibar.
Bi Kidude aliwahi kusema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya, ila inaaminika alikuwa na zaidi ya miaka 90.

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Bi Kidude, Amen

Tuesday, April 16, 2013

Style za Kanga moja laki si pesa ni kama filamu za wakubwa..ni ‘HATARI’ usiende na mtoto au mtu unaeheshimiana nae, maana duh!




Moja kati ya makundi yanayovuma sana kwa kuwapagawisha mashabiki wakiwa jukwaani ni kundi la ‘kanga moja laki si pesa’. Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa sana na hivyo kupiga matamasha wakizunguka Tanzania na kila walikopita wameacha historia ya aina yake.

Lakini Kile wanachokifanya wakiwa jukwaani hakihitaji mwalimu wa nidhamu kuwa karibu nao ama jopo la kuhifadhi maadili ya taifa kushuhudia kwa sababu endapo wakishuhudia inaweza kuzua ‘msalaaa’ si kidogo. Na tukisema ingekuwa enzi za mwalimu, dah, sijui ingekuwaje.....!
 
Style wanazocheza wakiwa jukwaani naweza kuthubutu kusema ni kama movie za wakubwa kwa asilimia kadhaa, na kwa ushauri wa haraka na muhimu ni kwamba watoto ama watu wanaoheshimiana na kuoneana aibu hawashauriwi kabisaa kushuhudia pamoja shangwe hizo za Kanga Moko laki si pesa, ikiwa hivyo mnaweza kupoteana ukumbini kukwepa aibu wakati watu ndo wanazidi kushangilia.

Ipo mitindo mingi ya kushtua wanayoicheza, lakini kati ya hiyo huu wa kumwagiwa kilevi sehemu za faragha kisha kuchezesha maungo yaliyolowana na kuonekana mithili ya karatasi iliyomwagiwa mafuta ya taa na kilaza ili aitumie kuchora kwa urahisi ramani iliyowekwa chini ya karatasi hiyo kwa kufuatisha tu, imetisha!! Hapa naweka kalamu chini nisigusie sana sentensi  hii‘Maadili ya Kitanzania yako wapi?’

Jionee mwenyewe baadhi ya picha za ‘kanga moko’ zilizochukuliwa huko Bukoba wakiwa wanamsindikiza Diamond Platinumz kuwapa shangwe wakazi wa Bukoba, show iliyoweka historia ya aina yake mjini humo.








Wataalam wa mambo wanakwambia 'DON'T TRY THIS AT HOME'.

Kumbe Wimbo mpya wa Diamond ‘Mapenzi basi’ umevuja! Awalaumu AM Records kwa kuvujisha nyimbo zake makusudi, anaweza asifanye nao kazi tena.

                           
Diamond platinumz kila akitoa wimbo hushika attention ya watu wengi na kuwa hit, lakini kumekuwa na mfululizo wa kesi za nyimbo zake kuvuja ikiwa ni pamoja na wimbo wake wa ‘Ukimwona’ na video ya wimbo wake ‘Kesho’.

theHOODinfotainmentimemtafuta Diamond Platinumz ambae alifunguka kuwa wimbo huo ulivuja. Aliwalaumu sana AM Records na kwa kile alichodai kuwa wanajua ni kwanini wao wameamua kuvuja wimbo huo japo wanakwepakwepa.

“AM record wenyewe sijui wanachonitafuta ni nini nikirekodi nyimbo kwao wanakuwa wanazivujisha yani makusudi. ” Alifunguka Diamond. Alisisitiza kuwa anajua AM Records ndio wako responsible kwa zoezi la kuvujisha nyimbo zake, “yani ni wao mi najua kabisa ni wao, wanaongea ila wanakuwa kama wanakwepakwepa ila mi najua kabisa ni wao.”

Huu sio wimbo wa kwanza kwa Diamond platinumz kuwa na matatizo kutoka AM Records, ‘Ukimwona’ pia ni wimbo ambao ulivuja na ulipikwa na AM Records, lakini Nataka kulewa iliyozua gumzo pia ilifanyika katika studio hiyo hiyo chini ya producer Maneck.

‘Kesho hit maker’ amesema baada ya wimbo wake ‘Ukimwona’ kupigwa sana japo hakuitoa officially na imeshahit basi ameamua kuacha ipigwe tu wakati anaangalia ngoma yake nyingine ya kuachia.
 
  theHOODinfotainment inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Manecky wa AM Records ili kujua kwa upande wake nini kinatokea hadi nyimbo za Diamond zinavuja kutoka katika studio hiyo.
 
chanzo: kwa msaada wa leotainment

Jokate na Penny wazungumzia tetesi za uhusiano kati ya Diamond na Irene Uwoya

Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni kumezuka tetesi kuwa staa huyo wa ‘Ukimuona’, ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.
page
Baadhi ya magazeti ya udaku nchini yameandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako yalidai walienda kufanya yao.
DIAMOND3
Kufuatia tetesi hizo, Bongo5 imezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.
Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha kupitia Bongo5 taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.
JOKATE
“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema Jokate.

chanzo:  bongo5

Wajanja wajaribu kumtapeli Bob Junior

Imebainika kuwa kuna mtu aliyetengeneza line mpya kwa kutumia namba ya Bob Junior aliye barani Ulaya kwa sasa na kutaka kuwatapeli watu wake wa karibu kuwa hitmaker huyo wa Nichum yupo hoi na anahitaji msaada haraka.
72910_10151418615904962_719201817_n
Taarifa hiyo imetolewa na baba yake mdogo, Guru Ramadhan ambaye ni mmiliki wa G Records. Kupitia Facebook, Guru aka G Lover ameandika:
“Hii sijaipenda kabisa ni too much sasa..eti mtu yupo Europe na simu yake inaita bongo ukipiga duh kumbe mtu katengeneza line mpya na kutumia namba ya Bob Junior na pia jamaa anayetumia hiyo line ya simu eti anaomba msaada kwa watu kuwa Bob Junior anaumwa sana Ulaya anahitaji msaada wako ili arudi Bongo.
Hivi nini maana ya kusajili namba?…makampuni ya simu ya Bongo mjipange sanaaa…hili limemkuta msanii Bob Junior siku chache hizi, mpaka imeripotiwa polisi eti ndio wamejidai kui block number…t.g. mmeniboaje?..so guyz mnaosafiri muwe makini sana mkisafiri maana mnaweza kukuta madeni kibao mkafa na presha bure…wizi mtupu…I hate dat.”

Monday, April 15, 2013

MAGAZETI YA LEO APRIL 16 2013 KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZENYE STORI NZITO

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

WABUNGE WATOANA MAPOVU BUNGENI.....NENO "IMPOTENCY" LAWAFANYA WALUMBANE

Ilikuwa  ni wakati wa kuchagia hotuba ya Waziri mkuu ambapo Mheshimiwa Wenje (CHADEMA) aliichamba  serikali na kuonyesha kwamba haina uwezo wa kutatua matatizo.

Ikafika mahala mheshimiwa Wenje akatumia sentensi mbili za kiingereza na akatamka kwamba it shows that the gorvement is IMPOTENT.

Binafsi sina matatizo na English, neno IMPOTENT na deritaives zake nalifahamu maana zake nyingi, na katika public maana yake kubwa ni hiyo aliyotumia Mh. Wenje.

Niliendelea kusikiliza bunge nikijua kwamba wabunge wetu nao hawana tatizo na kiingereza na sikutarajia lolote na matumizi ya neno hili kama ambavyo siwezi kutegemea matatizo Julius Nyerere alipomwambia Augustine Mrema kwamba { I cant go to sleep in Butiama and let my country go to dogs}

Wakati ule Nyerere alimjibu Mrema kuwa aache kampeni zake za urais kwani yeye kama Nyerere atampigia kampeni Benjamin Mkapa.

Mrema aliibuka na kutangaza kwamba Nyerere kawatukana wapinzani kuwa ni mbwa.

Leo, wabunge wa CCM wakanikumbusha kituko hiki cha Mrema kwa wao kusema kwamba Mh. Wenje afute kauli yake kwani IMPOTENT maana yake ni kuwa Hanisi yaani kutokuwa na uwezo wa kutozaa.

Mwanzoni nilidhani ni mmoja tu, bwana, wameibuka wawili wakidai afute kwa maana hiyohiyo na wengine wana CCM wakishangilia hata waliokuwa mawaziri ambao wanasafiri kila siku kwenda Uingereza na Marekani kunakozungumzwa kiingereza.

Je, neno IMPOTENT lina maana hiyo kweli? Nimefungua dictionary yangu, {Oxford Advanced Learner's Dictionary, Seventh Edition, ISBN: 9780194316613, pg.749}inasema hivi: 1: Having no power to change things or to influence a situation. E.g. POWERLESS {Without the chairmans support the commitee is impotent}, {She blazed with impotent rage}.
2:
(of a man): unable to achieve an erection and therefore unable to have full sex


Na hata online dictionary mnaweza kusoma wenyewe kwenye link hii (Click Here)
Neno IMPOTENT linatokana na neno la kitalini yaani POTENT literacy meaning "being powerful". Ndiyo maana unaposema Afrika ina mali POTENTIAL maana yake nguvu ya mali iliyojificha.

TUnaposema mlima una potential volcano maana yake ni volcano yenge nguvu iliyofichika. Wakatoliki husema kanuni yaani Imani kwa kilatini wakisema {Credo in unum Deum, Patri OMNIPOTENTE}. Maana yake Nasadiki kwa Mungu mmoja, baba mwenye nguvu zilizoenea pote. Hapa neno OMNIPOTENTE maana yake ni Mungu aliyeenea kote.

Kama wabunge  hawajui asili na maana ya neno POTENT na kama nao walipita shule za kata hawajui POTENTIAL VOLCANO wakadhani ni volkano yenye matusi, basi ile tume ya kuchunguza kufeli kwa form four ipite na kwao pia.

JB AJITOSA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015


Na Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI ‘namba wani’ Bongo mwenye heshima kubwa, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ yupo mguu sawa kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kugombea ubunge mwaka 2015.
Jacob Stephen Mbura ‘JB’.
Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda muafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii,” alisema JB.
Hata hivyo, ‘mheshimiwa’ huyo hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea akisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja kubwa lenye upinzani mzito kila ukifika wakati wa uchaguzi.
“Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi,” alisema JB.
Source : Global Publisher

BAADA YA UWOYA NA DIAMOND KUNASWA WAKILA BATA HOTELINI, JOKATE AMCHEKA UWOYA. HIKI NDO ALICHOKISEMA



Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ameangua kicheko baada ya kusikia mwigizaji Irene Uwoya kunaswa hotelini na Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Jokate aliangua kicheko hicho juzikati jijini, Dar wakati alipozungumza na paparazi wetu na alipogusiwa kuhusu suala la Uwoya kunaswa na Diamond, alicheka sana huku akimshangaa.
“Hahaha sasa ndiyo nini tena, yeye si aliwahi kunisema mimi nakwapua mabwana? Sasa leo imetokea kwake tena!” alisema Jokate.

 
Irene Uwoya.


 

Saturday, April 13, 2013

HII NDIYO NDEGE ILIYOONDOA UHAI WA BILLIONEA BABU SAMBEKE!!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwDVmNLH5jSpHD_gfTs-owBQ-APTwrlyzziZpryIWKICDiswoOusdqp7emzSG8sCBECS-zSt8upGP_-Sl-NhIzQr5gGaAYXtMs8O99LLT97dorsRRFDN53NjzwewkZx-Xca0xm06girWk/s1600/ndege.jpg
  HABARI za kusikitisha tulizozipokea muda mfupi uliopita ni kwamba mfanya biashara maarufu mkoani Kilimanjaro  anayefaamika kwa jina la Babu Sambeke amefariki dunia kwa ajali ya ndege huko mkoani Arusha, ndege hiyo ambayo mmiliki alikuwa ni marehemu NYAGA MAWALLA,aliyefariki dunia siku chache zilizopita, inasemekana imepata ajali jana jioni na kupelekea vifo vya watu wawili ambao ni Babu Sambeke na mtu mwingine ambaye mpaka sasa jina lake kalijatambulika. Inasemekana ajali hiyo imetokea jijini arusha ambapo babu alikwenda kwa shughuli zake za Kibiashara.

HII NDO LAANA INAYOTENDEKA SASA MOMBASA


The 21st century generation seems to have thrown all caution and the respectable ways that the forefathers fought so hard to see their children grow up with are no longer there.

In Mombasa at some night clubs this is what goes down.
 

HUYU NDO MBUNGE ALIYELIOMBA BUNGE KURUHUSU KILIMO CHA BANGI, KWANI HAINA MADHARA KAMA SIGARA.



MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ali Kessy Mohammed (CCM) ameishauri Serikali kuachana na kuhamasisha kilimo cha tumbaku kwa vile kinasababisha magonjwa ya kansa; badala yake iruhusu kilimo cha bangi.
Akiuliza swali la nyongeza jana bungeni, Kessy alisema zao la tumbaku linapingwa kote duniani; hivyo sio vyema kwa Serikali kuendelea kuhamasisha kilimo chake na ni vyema ikaruhusu bangi kwa vile ina uwezo wa kuliletea taifa fedha za kigeni.
“Kwa nini tusiruhusu kilimo cha bangi kuliletea taifa fedha za kigeni badala ya kuhamasisha kilimo cha tumbaku?” Alihoji mbunge huyo na kusababisha wabunge kulipuka kwa kicheko.
Katika majibu ya Serikali, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima alisema ni kweli kwamba zao la bangi limesharuhusiwa katika baadhi ya nchi hapa duniani.
Lakini alisema kwa hapa nchini hawawezi kuruhusu kilimo cha zao hilo kwa sababu bangi bado inachukuliwa kama ni zao la dawa za kulevya na linapingwa katika baadhi ya nchi.
“Siku tukijiridhisha kuwa bangi imepata uhalali duniani kote na imekubaliwa kulimwa na sisi tutaelekea kwenye kilimo cha zao hilo lakini kwa sasa hatukiruhusu,” alisema Malima.
Alisema katika kipindi hiki sio wakati wa kupuuza kilimo cha tumbaku kwa vile ndilo zao pekee ambalo kwa sasa linalipatia taifa fedha nyingi za kigeni.

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/04/huyu-ndo-mbunge-aliyeliomba-bunge_14.html#ixzz2HjCHFJTV

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII:JAMAA AKATATWA UME BAADA YAKUFUMANIWA AKIMBAKA MTOTO WA MIAKA 15.


Jamaa mmoja kutoka Kenya ambaye jina lake bado alijajulika amepata ya kupata baada ya kujaribu kumbaka mtoto chini ya
miaka kumi na nane na kushindwa adhabu yake ikawa kukatwa UME wake tunaomba radhi kwa picha hii
  source by Masai Nyotambofu: Chanzo- BongoClan