Moja kati ya makundi yanayovuma sana kwa
kuwapagawisha mashabiki wakiwa jukwaani ni kundi la ‘kanga moja laki si pesa’.
Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa sana na hivyo kupiga matamasha
wakizunguka Tanzania na kila walikopita wameacha historia ya aina yake.
Lakini Kile wanachokifanya wakiwa jukwaani
hakihitaji mwalimu wa nidhamu kuwa karibu nao ama jopo la kuhifadhi maadili ya
taifa kushuhudia kwa sababu endapo wakishuhudia inaweza kuzua ‘msalaaa’ si
kidogo. Na tukisema ingekuwa enzi za mwalimu, dah, sijui ingekuwaje.....!
Style wanazocheza wakiwa jukwaani naweza
kuthubutu kusema ni kama movie za wakubwa kwa asilimia kadhaa, na kwa ushauri
wa haraka na muhimu ni kwamba watoto ama watu wanaoheshimiana na kuoneana aibu
hawashauriwi kabisaa kushuhudia pamoja shangwe hizo za Kanga Moko laki si pesa,
ikiwa hivyo mnaweza kupoteana ukumbini kukwepa aibu wakati watu ndo wanazidi
kushangilia.
Ipo mitindo mingi ya kushtua wanayoicheza,
lakini kati ya hiyo huu wa kumwagiwa kilevi sehemu za faragha kisha kuchezesha
maungo yaliyolowana na kuonekana mithili ya karatasi iliyomwagiwa mafuta ya taa
na kilaza ili aitumie kuchora kwa urahisi ramani iliyowekwa chini ya karatasi
hiyo kwa kufuatisha tu, imetisha!! Hapa naweka kalamu chini nisigusie sana
sentensi hii‘Maadili ya Kitanzania yako
wapi?’
Jionee mwenyewe baadhi ya picha za ‘kanga
moko’ zilizochukuliwa huko Bukoba wakiwa wanamsindikiza Diamond Platinumz
kuwapa shangwe wakazi wa Bukoba, show iliyoweka historia ya aina yake mjini
humo.
Wataalam wa mambo wanakwambia 'DON'T TRY THIS AT HOME'.
0 comments:
Post a Comment