Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Monday, December 31, 2012

MASTAA WA BONGO MOVIE WALIOFANYA VIZURI SOKONI KWA MWAKA 2012.

 



Wema Sepetu
Ifuatayo ni orodha ya mastaa 10 ambao wamefanya vizuri na kuuza filamu nyingi kuliko wengine ndani ya mwaka huu.

JACOB STEVEN ‘JB’
Huyu ni mwigizaji mkongwe kunako gemu la filamu Bongo. Kupitia kampuni yake ya Jerusalem, JB anakiri kuwa ndani ya mwaka huu amefanya kazi nyingi. Amecheza filamu 23 na zote zipo sokoni na zinafanya vizuri katika mauzo tofauti na mwaka uliopita. Unaikumbuka DJ Ben?

STEVEN KANUMBA
Marehemu Steven Kanumba alitisha sana mwanzoni mwa mwaka 2012, kila mwezi alitupia kitu sokoni. Alipofariki dunia Aprili 7, filamu zake zote ziligombewa kama njugu sokoni. Filamu zaidi ya 10 ziliuzwa kwa kipindi hicho, mpaka sasa ile ya Ndoa Yangu ambayo ndiyo ya mwisho kuigiza, bado inatamba sokoni.

MZEE MAJUTO
Mwanzoni King Majuto alitisha kwenye filamu na maigizo ya kuchekesha. Ijumaa Wikienda linamzawadia nafasi kwa kuwa kila kona zilipouzwa filamu kulikuwa na muvi aliyocheza na biashara ilifanyika. Unakumbuka ripoti ya kutisha ya utajiri wake iliyotokana na kazi yake ya uigizaji? Mzee yupo vizuri.

VINCENT KIGOSI ‘RAY’
Nafasi hii tunaitoa zawadi kwa Ray kwani kupitia kampuni yake na mwigizaji Blandina Chagula ‘Johari’, RJ Production, aliweza kutengeneza filamu takribani 10 ambazo zipo sokoni na nyingine hazijatoka hadi sasa. Mzigo wa mwisho ni Waves of Sorrow, uliotanguliwa na Sister Mary.

DOKTA CHENI
Jamaa alifanya poa sana sokoni. Alikimbiza na anakimbiza na muvi kibao ambazo bado zinagombewa, mzigo wake wa mwisho ni Majanga.

WEMA SEPETU
Kwa upande wa wanawake, mwanadada Wema ameonekana kuuza katika filamu kibao ndani ya mwaka huu kwani wengi wanavutiwa na muonekano wake, hali iliyosababisha kufanya kazi zaidi. Ndani ya mwaka 2012 alicheza filamu zaidi ya 13 za watu. Mwisho akacheza moja ya kwake ya The Super Star aliyoizindua kwa kishindo kwa kumdondosha Bongo staa wa Nollywood, Omotola Jalade.

IRENE UWOYA
Hakuwa nyuma katika kufanya kazi japokuwa kuna kipindi alionekana kushuka kidogo. Baadaye filamu za watu alizocheza na za kwake zilikamata soko ghafla na kuwa gumzo kila sehemu zilipouzwa.

JACQUELINE WOLPER
Ijumaa Wikienda linamzawadia nafasi hii mwanadada huyu kwani kupitia kampuni yake alifanikiwa kutengeneza filamu saba ambazo zipo sokoni na nyingine kibao alizoshirikishwa na watu ambazo hakumbuki idadi yake.

MONALISA
Mwaka 2012 ulikuwa wa mafanikio kwa mwigizaji huyu kwani alipata tuzo ya msanii bora wa kike ambapo alicheza filamu kibao za kwake na nyingine zipatazo tano alishirikishwa na watu.

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Kabla ya kukumbwa na mkasa wa kuhusishwa kwenye kifo cha Kanumba, Lulu alifanya poa sana mwanzoni mwa mwaka huu. Akiwa mahabusu, hivi karibuni ilitoka filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Dangerous Girl inayofanya vizuri sokoni.

SOURCE: Na Gladness Mallya (Global Publishers)

SALAMU SPECIAL ZA MWAKA MPYA HIZI HAPA

theHOODinfotainment kupitia crew yake inayofuraha kubwa kukutakiwa heri ya mwaka mpya huu wa 2013, kwani wewe umekua na mchango mkubwa katika blog hii kwa miezi kaadha katika mwaka 2012, kutokana na mchango uliuonesha mwaka 2012 tunaomba uoneshe mchango mwingine zaidi ya uliuonesha mwaka jana. theHOODinfotainment pia, inatoapongeze za dhati kwa watu wanaoifuatilia kwa kina blog hii kila siku na kuifanya blog hii iendelee kutuburudisha na kutuhabarisha kila kukicha.
Mapungufu yalijitokeza katika habari tulizozitoa tunaomba radhi kwa hilo, ila kwa mwaka huu tunaoenda kuaanza pale ambapo tutakuwa tumekosea tunaomba utulishe na sisi hatunabudi kurekebishe kile ambacho kitakua tofauti, vilevile pale ambapo tutakuwa tumefanya vyema, ni njema utupe pongezi zetu. 



PENDEKEZO: wewe kama mdau mkuu wa theHOODinfotainment ungependa kitu gani katika blog hii kiongezwe au kipunguzwe?


LET THE SORROWORS BE OUT AND HAPPINESS BE IN SLOWLY AND STEADILY LET THE NEW YEAR BEGIN...!!!

CHADEMA INAUMALIZA MWAKA VIBAYA KWA MWENDELEZO WA MAKAMANDA WAKE KUCHANA MAGWANDA

KUJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA KUACHIA NYADHIFA ZOTE ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA NA KUJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA


Ndugu wanahabari naomba mnifikishie taarifa hii kwa Watanzania
wenzangu wenye uchungu na nchi hii;
Deogratius Kisandu (kulia)
1.1. UTANGULIZI
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na hisia hasi juu yangu na mkoa wa Tanga
kwa ujumla juu ya ushiriki wangu kwenye shughuli za chama. Natambua
kwamba wapo ambao tayari wameniona mnafiki, mamluki na msaliti
kwasababu tu ya kutopenda kutambua ukweli juu ya mwenendo wa chama
changu cha CHADEMA.
Nimeamua kuandika waraka huu nikitambua ya kwamba, kutambua ukweli ni
njia ya kuibua fikra chanya, kuamini matendo chanya kuelekea kupata
mafanikio zaidi. Ni heri kuzungumza ukweli ulio wazi kuliko kuwa
kondoo na mnafiki ndani ya chama. Kupitia barua hii naomba nitoe
dukuduku langu la moyoni kwa manufaa ya chama changu cha CHADEMA.
1.2.UCHAGUZI WA 2010.
Mwaka wa 2010 nilikuwa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Sebastian
Kolowa(SEKUCo). Kwa ujasiri mkubwa niliamua kuchukua fomu na kugombea
ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Lushoto mkoani Tanga, japo kuwa sikuwa
mzawa wala mkazi wa Lushoto.
Pamoja na kujenga mazingira mazuri kisiasa, nasikitika kusema kwamba
viongozi wa chama changu ngazi ya Taifa wamekuwa wepesi sana kupuuza
mkoa wa Tanga ikiwamo wilaya ya Lushoto katika ujenzi wa chama.
Wamekuwa wepesi sana kulaumu viongozi wa chama kuliko kufika katika
maeneo husika na kuona hali halisi. Kumbukeni kwamba tangu uchaguzi
wa 2010 mkoa wa Tanga umesahaulika kabisa na kususia viongozi wa
wilaya na majimbo. Vilevile ikumbukwe kwamba ujenzi wa chama ni kazi
ya kujitolea, hivyo kazi hii haiwezi kufanikiwa bila mawasiliano
mazuri na viongozi wa kitaifa.
1.2. CHAGUZI NDOGO ZA MADIWANI.
Uaminifu finyu kwa viongozi wa chini wa chama ni sababu ya kufanya
vibaya. Kumekuwepo na mgawanyo mbovu wa madaraka ndani ya chama
unaokiuka misingi ya katiba ya chama. Kumejengeka utamaduni wa
viongozi wa juu wa chama kuhodhi madaraka ya viongozi wa chini wa
chama na kuvuruga utendaji wa viongozi kwa kisingizio kwamba viongozi
wa chini ni mamluki takribani nchi nzima. Hatuwezi kupata mafanikio
makubwa ya kisiasa na kujenga mtandao imara wa chama kama tutaendelea
na utamaduni huu wa kudharau viongozi wa chini wa chama.
1.3. ZIARA ZA M4C.
Ziara za M4C zimekuwa za kiupendeleo zaidi bila kuzingatia maeneo
ambayo hayakufikiwa na kampeni za Urais mwaka 2010. Mkoa wa Tanga
umekuwa ukitengwa sana na kutokuthaminiwa katika ujenzi wa chama.
Pamoja na ukweli kwamba chama kimejengwa kwa misingi ya kujitolea,
ubinafsi wa viongozi ni kikwazo kikubwa kwa CHADEMA. Ushindi wa
CHADEMA hautatokana na baadhi ya mikoa ya Tanzania bali wastani mzuri
wa kura kwa kila mkoa wa Tanzania.
Ninashindwa kuelewa vigezo vya M4C katika kuchagua viongozi
wanaotakiwa kushiriki ziara za vuguvugu la mabadiliko(M4C).
Inanishangaza kuona mwanachama aliyejiunga jana CHADEMA akitokea CCM
leo anapewa kipaumbele kuliko viongozi waliojenga chama kwa muda mrefu
kwa nguvu ya kujitolea hasa ma wilayani, majimboni na mikoa kwani
viongozi hawa wa chini hawalipwi chochote zaidi ya nguvu zao na mwisho
wa siku wanaitwa majina mengi mara mamluki, wasaliti, wametumwa na
CCM. Kwa mwendo huu hatuwezi kufika wakati viongozi waliopo juu
wanalipwa mishahara na wanaojenga chama huku chini wanaitwa majina ya
kila aina.
1.4. UDHAIFU WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA(BAVICHA).
Baraza hili limeshindwa kabisa kufanya kazi yake ya kuwa unganisha
vijana bali limekuwa ndio chanzo cha migogoro. Migogoro yote
inayoendelea CHADEMA hivi sasa inatoka na Baraza hili kutokuwa makini
na utendaji kwani imekuwa kila mtu ni kibaraka, mamluki, kirusi,
anatumiwa hata kama anaongea ukweli, je tukipewa nchi nani atasimamia
rasilimali za nchi?
Unaweza sema baraza linafanya kazi kwa maana ya Mwenyekiti na Katibu
wake. Tunaposema baraza tunamaanisha wajumbe wote wa majimbo, wilaya
na mikoa wanashiriki vipi kujenga chama kupitia Baraza lao. Ukiangalia
vikao vya Taifa vya BAVICHA tangu vianze vimekuwa vikishirikisha
wenyeviti wa mikoa kinyume na katiba ya chama na mwongozo wa Mabaraza
upande wa BAVICHA ibara ya 6.8.6 wajumbe wa kamati tendaji ambapo
makatibu wa mikoa ni wajumbe lakini kinyume chake kikao kilichofanyika
Morogoro mwaka huu walishiriki wenyeviti badala ya makatibu tena
makatibu tumekuwa tukiletewa taarifa na wenyeviti. Lazima demokrasia
ichukue mkondo ndani ya chama tusifanye mambo kwa kupeana fadhila za
uchaguzi. Na hii ni ukritimba ndani ya chama na ulafi wa madaraka.
1.5. BUSARA IMEPOTEZA MWELEKEO CHAMANI.
Si kila mwenye kosa anastahili kuvuliwa uanachama, ukombozi wa
watanzania unahitaji kulindana na kujengana kwani wapinzani bado tuko
wachache sana, wengi ni mashabiki tu. Tunapofukuzana kwa makosa
madogomadogo hatujengi chama bali tunaongeza chuki na kupoteza imani
kwa wananchi. Mgogoro wa madiwani wa Arusha na Mwanza haikuwa njia
nzuri ya kuwafukuza madiwani bali ilitakiwa kuwajenga na kuwa fanya
wawe imara. Unajua hata mamluki kama wanavyo dai kwenye mitandao ya
kijamii wanaweza kubadilika kwa busara nzuri.
Nakumbuka hata kule nyumbani kwetu wilaya ya kahama viongozi waliokuwa
kamati tendaji ya jimbo la kahama pamoja na aliyekuwa mgombea wa
ubunge walivuliwa uanachama na Mwenyekiti wa wilaya na viongozi wa
Taifa wakabariki, nimesikia majuzi tu mwezi desemba 2012 kule Mbeya
kuna viongozi wamevuliwa uanachama. Hizi ni sampo tu.
Style hii ya vuavua uanachama haitawezesha chadema kushika dola, kwani
chama makini hakifukuzi bali humjenga mtu ili abadilike. Mimi binafsi
na kerwa sana na hali hii ya fukuzafukuza kwa kutumia kigezo cha
Katiba ya chama, watu wamekuwa wakikomoana kupitia katiba ya chama ili
kuoneshana ubabe. Hii hata mikoani imetawala sana kutokana na hofu ya
baadhi ya watu kutaka kuwa viongozi au baadhi ya viongozi kuonekana
wanang’aa kisiasa au kukubalika kuliko wengine. Hii pia kisaikolojia
inaweza kuwa ni hofu ya wabunge kuzidiwa kete na baaadhi ya vijana au
viongozi majimboni na wilayani na kuogopa kukosa nafasi zao kipindi
kijacho.
1.6. USHAURI WANGU.
Kama CHADEMA ina dhamira ya dhati ya kushika dola basi itambue mtu au
kiongozi anapo dai haki msimwite mamluki au katumwa na CCM hii
itasaidia kujenga chama, kwani viongozi wanajua fika mawazo yao katika
vikao hayawezi kukubalika kutokana na imani na kuabudu watu badala ya
kufata misingi ya chama.
1.7. URAIS 2015
Tangu nilipotangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015 viongozi wajuu wamekuwa wakijikanyagakanyaga na kuhoji nani
kamtuma huyu kijana. Chadema hakuna demokrasia ya kweli ndani ya chama
kwani watanzania mmeona wenyewe John Shibuda alipotangaza kuutaka
urais akaitwa mamluki, msaliti. Na Zitto Kabwe alipotangaza kuutaka
Urais anaitwa majina mengi mara msaliti, ooh anatumika na CCM. Sasa
mimi nashindwa kuelewa nini maana ya demokrasia, au nani anafaa kusema
anataka kuwa Rais ndani ya chama.
Nchii hii sasa ina siasa za kiliberali, tumeshatoka kwenye siasa za
Chama Kimoja ambao ulikuwa ni mfumo wa Chama cha Mapinduzi. Sasa kama
mambo yenyewe ndio hivi CCM itatuwia vigumu kuwapokonya utawala.
Nilichojifunza ndani ya chama wanaogopa kasi ya vijana wenye uwezo
walioko chini na kuanza kuhofu nafasi zao, ndio maana wengine wanasema
BAVICHA wanatakiwa waheshimu wakubwa(ARFI awaonya bavicha-Mtanzania ya
29/12/2012). Hivi hawa wakubwa waheshimiwe hata kama wanatupeleka
kusiko.
Urais ni uwezo wa mtu na karisma ya mtu, kama wewe huwezi muache
mwenzako, wewe unapiga kelele eti Kisandu hawezi kuwa Rais, sawa mbona
wewe hujatangaza nia ya kuwa Rais? Tuache ujinga wa kuendekeza kila
kitu kinacho semwa na Fulani ndio sahihi. CHADEMA kuna wanachama wa
aina tatu 1. walio anzisha chama 2. waliokipokea chama na 3. wanachama
waliowapatikana kipindi cha uchaguzi mkuu 2010 amabapo na mimi
nilikuwa mgombea wa ubunge jimbo la Lushoto na baada ya uchaguzi mkuu
huo, hawa wanachama namba3 hawa kijui chama vizuri wao wanaenda na
upepo tu, yaani kiongozi wa juu akisema kitu Fulani ni sahihi hata
kama kakosea au anataka ushauri. Ona Chadema tuko mstari wa mbele
kuipinga CCM na serikali yake kwa uongozi mbovu, sasa naomba vyama
vyote vya siasa hasa viongozi wa juu hapa Tanzania acheni ubinafsi na
ukritimba wapeni nafasi vijana msiwabanie.Jifunzeni kutoka Kenya
jirani zetu muone walivyo pewa vijana nafasi za kutetea nchi yao.
Mambo kama haya ndio yaliyo mfanya mwenyekiti wa vijana wa ANC Afrika
kusini kuvuliwa uanachama. Hebu turuhusu demokrasia.
1.8. HITIMISHO.
Nachukua maamuzi magumu japo mtaona nimekurupuka au nimepoteza dira
lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Naachia nyazifa zote za uongozi
nilizo nazo ndani ya chama(Katibu wa BAvicha mkoa wa Tanga na Kaimu
katibu wa wilaya ya Lushoto) na ninajivua uanachama wa Chadema na
kubaki mwanachi huru.Fanyieni kazi niliyowaambia kuimarisha chama.
Maamuzi ya kujiunga na chama kingine ni demokrasia. Msimamo wangu wa
Urais uko palepale .
DEOGRATIUS KISANDU.
ALIYE KUWA KATIBU WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA(BAVICHA)
MKOA WA TANGA.
.29/12/2012

Askari Aliyepiga Picha Na Lema Atokomea


 Na : Nuzulack Dausen

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.
“Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:
“Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.”
Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.”
Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa ripoti kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa utata uliogubika suala hilo.
Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.”
Alifafanua kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanya kazi katika taasisi yeyote ya Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na kufanya kazi hiyo mpaka atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa kurejea jeshini.
“Kuna kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti ya kuvua magwanda, hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na baadaye kurudi jeshini kuendelea na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:
“Askari akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote atakazopewa zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za jeshi zisizofungamana na siasa.”

KWA WENYE LOVE NA DIAMOND PLATNUMS

.

Sunday, December 30, 2012

HIVI NDIVYO WALIFANYA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ JUZI JE, KESHO WATAFANYA NINI? TOA THAMINI YAKO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HAWA MARAIA.

...Chezea Diamond wewe!
Watu weweee: Kila mmoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
...Platinumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.

Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.

USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

TAARIFA YA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

Ndugu Wananchi,

Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.

Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

(1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
(2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
(3) Mwanza-28 Februari, 2013;
(4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;

(5) Mbeya-30 Aprili, 2013.
Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.

Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi

Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz

Ndugu Wananchi,

Nawashukuru kwa kunisikiliza

HAYA NDIO MAGAZETI YANAYOTUFUNGIA MWAKA HII LEO, SOMA HAPA















ANGALIA HAPA PICHA YA DIAMOND KATIKA Interview YA X-LIVE JANA KUHUSIANA NA USIKU WA WASAFI 1/1/2013 MAISHA CLUB....












& Romy J

& Quick Rocka







Kwa mara ya kwanza jana kipindi cha X-Live kinachoendeshwa na mwanadada Peniel wa Dtv....
Kiliruka hewani na President nilipata nafasi yakualikwa katika kipindi hicho na nilijiskia furaha
kuwa msanii wa kwanza kufanyiwa Interview katika kipindi hicho cha X-Live...
Tulizungumza mengi ikiwemo Video zangu zote mbili Nataka Kulewa na Kesho ila kubwa kuliko ni
Show ya Wasafi itakayofanyika pale New Maisha Club siku ya Tareh 1/1/2013 USIKOSE