TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI
KUANZIA
JUMATANO, TAREHE 5 DISEMBA 2012
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi
zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 5 Disemba 2012. Pamoja na kutambua
bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia
yafuatayo.
(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli,
Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la
tarehe 07 Novemba 2012.
Katika toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli na
Dizeli zimeongezeka kwa viwango vifuatavyo: Petroli Sh 70/lita sawa na asilimia
3.4; Dizeli Sh 10/lita sawa na asilimia 0.53.
Bei ya Mafuta ya Taa imepungua
kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.1. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya
mawili zimeongezeka kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh 69.56/lita sawa na asilimia
3.52; Dizeli kwa Sh 10.04/lita sawa na asilimia 0.52.
Bei ya Mafuta ya Taa
imepungua kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.15. Mabadiliko haya ya bei
yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kidogo
kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za
bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea
kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi
ya bidhaa za mafuta.
(c) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya
petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price
cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na ambayo
ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa
za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta,
punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
Pale
ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta
kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha
ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri
kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(e) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi
ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na
bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa
mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu
kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora
kisichofaa.
0 comments:
Post a Comment