Blogger Widgets

Thursday, December 13, 2012

KESHO HISTORIA MPYA ITAJENGEKA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI KWA KILE KITAKACHO KWENDA KUTOKEA

kesho tar 14/12/2012 itajengeka historia nyingine tofauti ambayo ni kwamara ya kunza, haijawahi kutokea.... ni baada ya SALAMA SPOTRS CLUB, Club inayojihusisha na kuinua vipaji tofauti tofauti kama volleybal, football, riadha, netball na basketball. Club hiyo ambayo kesho ndio itaingia kwa kufungua rasmi club hiyo watacheza michezo miwili tofauti kwa mpigo. Ambapo timu ya mpira wa miguu ya SALAMA FOOTBALL CLUB itachuana vikali dhidi ya AJTC STAR'z ambao AJTC STAR'z ndio waenyeji wa mchezo huo, vilevile kutakuwa na mchezo wa pili ambao utahusisha riadha.

theHOODinfotainment imepata fursa ya kuzungumza machache jioni ya leo na mmoja wa Viongozi wa SALAMA SPORT CLUB Bw. Nelson Dausen na kusema kuwa chanzo cha kuanzisha Club hiyo ni kwaajili ya kuwajenga vijana kiafya na kuwafanya wawewanajiepusha na masuala yasikuwa na lazima kwao kama vile kunywa pombe, au kujihusisha na masuala ya mapenzi. Bw. Dausen aliongekua, suala hili ni suala endelevu kwa kila siku kwani ndio mchakato umeanza rasmi.


vilevile Bw. Dausen ametangaza rasmi kikosi cha mpira wa miguu ambacho kitaanza kucheza kesho rasmi, ambao majina yao ni; 1. NDALIKE 
                                 2. ABDUL
                                 3. SAID 
                                 4. ANTHONI (montana)
                                 5. IMMA (manywele)
                                 6. NELSON (mapesa)
                                 7. GEORGE
                                 8. LIVINGSTONE
                                 9. ROBART (chonlee)
                                10. AMANI (moshono)
                                11. JOHN

 hiki ndiko kikosi ambacho kitachuana na AJTC STAR'z kilichowekwa hadharani na Bw. Dausen, Hata hivyo theHOODinfotainment imefanya juhudi za kuwasaka wahusika wa timu ya AJTC STAR'z ili waweze kutupatia ata kikosi chao walicho kiandaa kwa kesho lakini juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya kuweka baya kwamba kikosi chao watakitangaza rasmi hiyo kesho uwanjani.

SALAMA SPORTS CLUB, Ni club iliyoanzishwa ndani ya chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha AJTC kwa dhumuni la kuwaweka sawa wanachuo wanaosomea taaluma hiyo, Hata hivyo timu hiyo imeanzishwa siku chache zilizopita ikiwa kwa kuwapata wanachama wengi na kuleta changamoto ya kimichezo chuoni hapo. 

mchezo huo utafunguliwa rasmi majira ya saa 04:00 pm katika viwanja vya FILD FORCE  na Mkurugenzi wa mafunzo AJTC Bw. Joseph Mayagila na kuitambulisha Rasmi Club hiyo itambulike chuoni hapo.

kesho theHOODinfotainment itakuletea mtanange wa tukio zima... usikose kesho kuangalia picha kali hapa  pia kumbuka kushare na watu wako wa nguvu
karibu Arusha Journalism kwa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji tembelea  
www.ajtc.ac.tz

VOICE FOR VOICELESS

0 comments:

Post a Comment