Blogger Widgets

Tuesday, April 22, 2014

duh! kweli Wema ni kiboko. SOMA HAPA

 Stori: Mwandishi Wetu

WEMA Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ ameonesha ni kiboko katika sekta ya urembo baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano bab’ kubwa la kumsaka staa wa kike Bongo mwenye mvuto ‘Ijumaa Sexiest Girl 2013-14’.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’akikabidhiwa tuzo ya ‘Ijumaa Sexiest Girl 2013-14’ na msanii Nikki wa Pili.
Fainali za shindano hilo zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo Wema alikuwa akichuana na warembo wengine, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Nelly Kamwel ‘Dokyumetari’ kwanza

Kabla ya kumtangaza mshindi, maelfu ya watu waliokuwa wamefurika ndani ya ukumbi huo, walipata fursa ya kupata maelezo ya kila mshiriki aliyeingia ‘top 5’ sambamba na picha zao kali za mnato kupitia screen kubwa, hali iliyoamsha shauku ya kutaka kumjua mshindi. hariri aelezea mchakato.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akisalimiana na mashabiki wake.
Baada ya mashabiki kuangalia ‘dokyumentari’ hiyo, Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambalo ndilo lililokuwa likiendesha shindano hilo, Amran Kaima alitoa maelezo kuanzia mwanzo wa shindano na njia zilizotumika kupiga kura hadi kumpata mshindi.
“Shindano lilianza tangu mwezi wa tano, mwaka jana, wasomaji wa Gazeti la Ijumaa walipiga kura kupitia namba ya simu ya gazeti, Mtandao wa www. globalpublishers.info, mitandao ya kijamii na barua pepe.
...Akiwapungia mashabiki mkono baada ya kutangazwa mshindi.
“Mchuano ulikuwa mkali na hata warembo walioingia tano bora ilikuwa vigumu kutabiri mshindi kwani wote ni wakali,” alisema Kaima.Nikki wa Pili atangaza mshindi

Baada ya maelezo ya mhariri, msanii kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ aliyepewa dhamana ya kumtangaza mshindi aliitwa stejini ili kumaliza mchezo.
Wema akiwa na tuzo yake.
Bila kupoteza muda, Nikki alifungua bahasha iliyokuwa na jina la mshindi na Wema alionekana kung’ara hivyo kuibua shamrashamra kuashiria kuwa, mrembo huyo mwenye figa bomba na sura ya kuvutia alistahili kuvaa viatu vya mshindi wa mwaka 2012/13, Jacqueline Wolper.
Mbali na tuzo aliyopewa Wema, pia aliahidiwa shilingi milioni moja ambazo angepewa baada ya shindano hilo.
Baada ya Wema kutangazwa mshindi, burudani ya kufa mtu ilianza kuporomoshwa kutoka kwa Kundi la Wanaume Family na Weusi ambao walinogesha fainali hizo. Habari zaidi kuhusu shoo hiyo, nenda ukurasa wa 8.

0 comments:

Post a Comment