Blogger Widgets

Tuesday, March 12, 2013

AIBU: HUU NDIO UCHAFU ULIOTAWALA NDOA NYINGI ZA LEO



Hii Tabia ya Kutembea  na Waume au Wake za Watu  itaisha lini jamani?. Mbona Wanaume Ma-Bachelor Wapo Kibao? Ukimwi Nao Je? Kuna Nini Huko Katika Ndoa ???

Uchunguzi uliofanywa  na mtandao huu  umebaini kuwa siku  hizi watu wanaolewa au kuoa ili kuifurahisha jamii tu. 

Ndoa zetu zimejaa usaliti wa kila hali.Chanzo cha maovu hayo ni tamaa ya pesa, kutoridhika kimapenzi,  ushawishi wa kupandishwa  kazi   na mambo mengine kibao




=> USHAURI  WANGU  KWA WANAWAKE....

Kama mtu  ana akili nzuri naamini  atakuwa ni mwerevu. Nawasihi wanawake  muache tabia  ya  AIBU.Muulize kinachomsibu mumeo.

Kama unaogopa kumwambia basi unaweza kumwanzisha tu pole pole wakati wa mnafanya mapenzi. Mwambie leo nataka unishike hapa. Leo tujaribu staili hii, napenda ukifanya hivi, usiwe unakuja mapema...Dear uko bize mno, naomba uwe unanijali na tufanye mara kwa mara...

Wanaume ni kama watoto wadogo na ukiwa mjanja unaweza kumbadilisha unavyotaka hasa katika mambo ya mapenzi...Vinginevyo  utakuwa ni mtu  wa  kuibiwa kila leo.

Hata huko nje utapata mume wa mtu. Mwanzoni mambo yatakuwa moto lakini baadaye mtazoeana na mambo yatakuwa yale yale.

Halafu kama ni mume wa mtu na anafanya nje  ya ndoa , unajuaje kama hana mnyororo wa wanawake huko nje?. Mmoja tu akiwa na UKIMWI kwenye huo mnyororo basi kila memba wa huo mnyororo anaishia kuudaka....





=> USHAURI  WANGU  KWA  WANAUME:...

Ni jambo la busara  sana kumjali mkeo.Wanaume  wengine mnajitakia  wenyewe.Unakuta mwanaume yuko  busy   masaa   24  yote.....
Hajui nyumbani wamekula nini,  kurudi kwake ni usiku, tena  akiwa  amelewa.
Akiulizwa  alikuwa  wapi ,ugomvi  unaanza.Akipewa penzi, basi ni bao moja  tu, hoi.Unategemea  huyu mwanamke  akimpata  wa kumbembeleza  huko nje  atamkataa  kweli?.....Mfanye mkeo ajivunie  kuwa  na  wewe.

Inashangaza sana kuona kuwa mwanaume yuko tayari   apate  lunch na secretary wake, lakini kwa  mkewe anakuwa bahiri......
Jamani, wapendeni wake zenu. Tenga  muda wa kutosha  ku enjoy  na mkeo.....Na  wakati wa  tendo la  ndoa, usikurupuke.Mwandae vizuri  mkeo na hakikisha unamfikisha kileleni




****************
=> Narudia tena kwenu mliooa. Hakikisheni kuwa wake zenu wanaridhika kimapenzi. Vinginevyo ni matatizo tupu. Nitafurahi sana kama mtakuwa amesikia ushauri wangu. Na wengine  toeni ushauri wenu jamani ili tuiokoe ndoa zetu....
 =>>JAMANI, VYOMBO  VYAHABARI  VIMEELISHA VYA KUTOSHA. NI  WAKATI   WETU   KUBADILIKA SASA.....

EPUKA  KUJICHAFUA KATIKA MAGAZETI. HESHIMU NDOA YAKO.  


CHANZO: http://seifjr.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment