Blogger Widgets

Celebrity Story from Different Place

Entertainment story of Bongo land and their work.

Story za wakali wa majuu

Burudani| Video| Tracks na Maisha yao.

Bongo Movie na wasanii wake kwenye maisha yao

News Movie| New Story| New Skendo.

Mafanikio

Story za walio vuka boda na mafanikio yao kama wajasiria-mali.

Elimika na Burudika

Life ya wasio na skendo na wenye skendo| Mafanikio yao na vioo wa jamii.

Friday, November 30, 2012

WASANII WA BONGO FLAVA NA HIP HOP, WALALAMIKIWA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA SHARO MILIONEA. December 1, 2012



Kupitia  kituo cha luninga cha EATV ndani ya kipindi cha Frieday Night Live jana, kuna malalamishi kibao yaliyojitokeza kwa baadhi ya wasanii wa kike waliokuwa wakihojiwa katika kipindi hicho.

Wasanii hao wakike wawili walionekana kukelwa na kushangazwa na kitendo cha wasanii wa miondoko ya bongo Flava hapa nchini kutojitokeza kabisaa katika mazishi ya msanii mwenzao
Hussein Sharo milionea aliyepata ajali tarehe 26 majira ya saa mblili za usiku mkoani Tanga na kupoteza maisha hapo hapo.

Wadada hao walili wakionekana
EAST AFRICA TV wakiongea kwa kuchungu, walidai kuwa wasanii wa hip hop nao waliohudhuria msiba wa Sharo Milionea walikuwa  wa kuhesabu kama Mwana FA, Roma, Ney wa Mitego Shetta na wengine.

Walidai kuhuzunishwa sana kwani wasanii wakubwa ambao pia walitajwa kutohudhuria msiba huo ni pamoja na
AY, Lady Jay Dee, Bob Junior, Timbulo, PNC, Dogo Janja, DJ Choka, Weusi na wasanii kibao. Mtangazaji wa kipindi hicho pia Sam Misago alishangazwa na kitendo cha wasanii wa hip hop kuto hata zungumzia msiba wa msanii Sharo milionea bali walionekana kufanya yao na kutoona umuhimu wa kuhudhulia msiba huo.

Wadada hao walidai kuwa kila msanii wa Bongo anamfahamu meneja wa Sharo Milionea maarufu kwa jina la
HK, meneja ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii kibao.Ni kwanini wakati amefikwa na msiba wa Sharo Milionea hakuna hata msanii mmoja aliyempigia simu kumpatia pole! hata kama walishindwa kuhudhulia msiba huo?

Katika upande wa
Comedy walidai wasanii wote hawakuhudhulia msiba wa Sharo milionea, kitu ambacho kimewakera sana na kuwaasa kujitokeza katika matatizo ya yanapokuwa yamejitokeza kwani na wao wakipata matatizo hayo watahudhuriwa na nani?

Yapo mengi zaidi yaliyozungumziwa katika kipindi hicho cha
Frieday Night Live ya East Africa TV

MASHUJAA BAND WAPATA AIBU YA KARNE

Kiiipe Yayooo...! Mwanamuziki JB Mpiana na bendi yake wakifanya vitu vyao baada ya kupanda stejini kwenye viwanja vya Leaders Club, Kionondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Hapa ilikuwa ni mida ya saa 9:00 baada ya gwiji huyu kusubiri sana kutokana na mizinguo ya umeme wa TANESCO na pia wa jenereta kubwa lililotegemewa mahala hapo kuzalishia nishati hiyo usiku wa kuamkia leo (Desemba 1, 2012).

Litapona kweli...? Watu wakiwa wamelizunguka jenereta lililokuwa linawazingua wakati wa uzinduzi uliofeli wa albamu ya pili ya mashujaa kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Desemba 1, 2012). (Picha: Zote kwa Hisani ya issamichuzi.com)
Gundu la aina yake limeikumba bendi ya Mashujaa inayoundwa na wanamuziki kadhaanyota akiwamo Chaz Baba baada ya uzinduzi wake kukwama usiku wa kuamkia leo kutokana na kukatika hovyo kwa umeme wa TANESCO na pia 'mizinguo' ya kuwaka na kuzima kila mara kwa jenereta kubwa liliotarajiwa kutoa huduma ya nishati hiyo kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa mizinguo hiyo ya umeme ilimchanganya kuliko kawaida mmiliki wa bendi ya Mashujaa, Mamaa Sakina, ambaye inasemekana alianguka na kupoteza fahamu kiasi cha kukimbiziwa hospitali akiwa hoi.

Tatizo hilo lilidumu kwa masaa kibao na kuwafanya mafundi kuihangaikia jenereta huku na huko huku mwanamuziki wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyealikwa kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo, JB Mpiana akilazimika kusubiri sana -- hadi mishale ya saa 9:00 usiku -- ndipo alipopata nafasi ya kupanda jukwaani na kundi lake kufanya kazi iliyowapa fursa ya kutua nchini kwa mbwembwe.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walishakereka mida hiyo na kutimkia zao, hivyo kukosa uhondo uliotarajiwa katika onyesho hilo ambalo awali lilikuwa na ratiba 'tamu' sana kwa wapenzi wa burudani.

Hakukuwa na taarifa za kina kuhusiana na hali ya kiafya ya Mamaa Sakina hadi kufikia leo asubuhi ya leo (Jumamosi Desemba 1, 2012); kwa mujibu wa EMMANUEL SHILATU

TANZANIA YAITAKA CNN KUACHA UPOTOSHAJI JUU YA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI



    
 
                                            Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km)  ikiwa ni pamoja na  nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.
Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani  imekuwa ikiendesha  kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.
Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI

Wednesday, November 28, 2012

safari ya mwisho ya mpendwa wetu sharo milionea mchana wa leo

 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.Picha Kwa Hisani ya Jiachie Blog

Thursday, November 22, 2012

Kitabu kipya cha Hadithi| Miss Tanzania.

Katika kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka Masimulizi Entertainment wanakuletea kitabu cha hadithi ya Miss Tanzania amabayo ni tamu na itakusisimua zaidi kuliko ulivyo tarajia. Kitabu hichi cha masimulizi kitatoka na kuingia sokoni hivi karibuni. Kuweka oda yako mapema, wasiliana na MASIMULIZI Blog kupitia 0755 780131, 0764 294499, 0658 780131


Cheki Dude lililodondoka usiku wa manane Kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.

 
Kitu kinachosadikiwa ni bomu

     Wataalamu wa mabomu kutoka Jehsi la wananchi wa Tanzania JWTZ kambi ya Biharamulo wameanza kazi ya kukagua kitu ambacho kimeanguka kwenye eneo la Ruganzo wilayani Ngara mkoani  Kagera.

Kituo hicho ambacho baadhi ya watu wanasadiki kuwa ni bomu kina ukubwa wa sentimeta 50 na umbo kama la yai huku kikiwa na nyuzinyuizi kimeanguka jana usiku katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amesema wataalamu hao wa mbomu ndio watabaini kitu hicho na kuweza kukitolea maelezo pmoja na hatua za kuchukua.
 
Wapo waliodhani kuwa kitu hicho
ni Kombora la masafa marefu
 lililorushwa kutoka nje ya Nchi

 Ni kitu kisichofahamika ni nini, Wapo waliodhani kuwa kitu hicho ni Kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka nje ya Nchi,wapo waliodhani kuwa ni Kimondo,wapo wanaodhani kuwa ni Satelite!..LAKINI  Majibu yatatolewa katika Ripoti itakayotolewa na timu/kikosi cha wanajeshi naohusika na masuala ya Mlipuko. tayari kikosi kutoka Biharamulo kimeagizwa KUCHUNGUZA.

Eneo la Ruganzo

   
Kitu hicho kilichondoka kutoka angani hadi ardhini Usiku wa Jumatano November 21 kuamkia Alhamisi November 22, 2012 saa nane Usiku na  kuleta kishindo kikubwa kilichopelekea hali inayofanana na tetemeko la ardhi,wakazi wengi wa eneo la Ruganzo kata ya Kibimba wilayani  Ngara mkoani Kagera  wamekumbwa na hofu kutokana na kitu hicho.
Aidha  kwa mujibu wa mkuu wa Ngara Bw.Kanyasu AMEPIGIWA SIMU NA MAAFISA WA BURUNDI WAKIMUULIZA JUU YA MIUNGURUMO ILIYOSIKIKA UPANDE WA TANZANIA.

JWTZ WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO NA WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ZAIDI. BADO HALIJARIPUKA. HUENDA WAKALITEGUA.
Chanzo:Radio Kwizera FM

Monday, November 19, 2012

KAMA ULIMISS PICHA ZA RED CARPET YA CHANNEL O HIZI HAPA

Kama wewe ulimiss kuangalia Channel O Music Video Awards mwaka huu siku ya Jumamosi huko nchini South Africa basi hii ndio time yako ya kuangalia jinsi mastaa mbalimbali walivyotisha katika Red Carpet!!!!!!!!!!!

MaEezy from Teargas. Looks like delelas are back.
I love this dress..
DJ Zinhle reminding us why we need to go to the gym…
Nigerian artist, Mo Cheddah.


DJ Cleo please shave tuu?
Or do I need to get Mandoza’s bodyguard to make you do it…

Ice Prince (left) the Oleku/Superstar hitman co hosted the show with Bonang
Moruti Kabelo Mabalane was one of the presenters…
DJ Cleo le Mandoza…
wild Channel O Presenter Denrele
DJ Switch  on some “bosso ke mang”swag
Wildin it out
I still haven’t forgiven Vimbai for mistreating Karen in the big brother house…
Not sure about these shoes with that but she’s pretty…
On that bridesmaid swag…
Channel O’s SK looking fresh as always…
I wonder if he was signing an autograph?
More red carpet fashion looks…
…poses…
Jokate
Yeah…

Wednesday, November 14, 2012

HATIMAE MTOTO ANETH SASA AENDELEA VIZURI BAADA YA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO JANA

MTOTO ANETH AKIWA ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUMKATA MKONO WAKE WA KUSHOTO JANA
ANETH AKUTAYARISHIWA CHAKULA NA MAMA YAKE MDOGO SLIVIA ANAEMUHUDUMIA HOSPITALINI HAPO
KWA UJUMLA MTOTO ANETH SASA ANAENDELEA VIZURI NA ANAKULA CHAKULA VIZURI PIA TAARIFA TULIZOPATA MUDA SI MREFU MAMA YAKE MZAZI YUPO NJIANI KUJA MBEYA TOKA KAGERA

KIPINDI CHA POWER BREAKFAST CHAMZAWADIA MENEJA WA OMMY DIMPOZ TIKETI YA NDEGE....


Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm kimemzawadia Meneja wa Ommy Dimpoz Mubenga Tiketi ya ndege Go and Return kama zawadi yake ya siku yake ya kuzaliwa....Birthday ilifanyikia
New Maisha Club.
Dimpoz,Halima Kimwana & Fetty

Tuesday, November 13, 2012

Dk. Margaret Mhando afanya ukaguzi wa Ujenzi wodi pamoja na mabasi ya wagonjwa wa Fistula CCBRT.

 
 Mkurugenzi  wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Februali 25.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu ya CCBRT, Dr. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, akipokea zawadi kutoka kwa moja ya wagonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT wakati alipofanya ukaguzi wa wodi mpya za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Rais. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja nae ni Mkurugenzi  wa Idara ya huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wauguzi wa wodi za wagonjwa wa Fistula wa hospitali ya CCBRT, alipofanya ukaguzi wa wodi hizo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mapema Mwezi huu. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo. Dr Wilbroad Peter Slaa.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akiwapiga picha kupitia simu yake ya mkononi watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akifurahi pamoja na watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.