Blogger Widgets

Friday, November 30, 2012

MASHUJAA BAND WAPATA AIBU YA KARNE

Kiiipe Yayooo...! Mwanamuziki JB Mpiana na bendi yake wakifanya vitu vyao baada ya kupanda stejini kwenye viwanja vya Leaders Club, Kionondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Hapa ilikuwa ni mida ya saa 9:00 baada ya gwiji huyu kusubiri sana kutokana na mizinguo ya umeme wa TANESCO na pia wa jenereta kubwa lililotegemewa mahala hapo kuzalishia nishati hiyo usiku wa kuamkia leo (Desemba 1, 2012).

Litapona kweli...? Watu wakiwa wamelizunguka jenereta lililokuwa linawazingua wakati wa uzinduzi uliofeli wa albamu ya pili ya mashujaa kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Desemba 1, 2012). (Picha: Zote kwa Hisani ya issamichuzi.com)
Gundu la aina yake limeikumba bendi ya Mashujaa inayoundwa na wanamuziki kadhaanyota akiwamo Chaz Baba baada ya uzinduzi wake kukwama usiku wa kuamkia leo kutokana na kukatika hovyo kwa umeme wa TANESCO na pia 'mizinguo' ya kuwaka na kuzima kila mara kwa jenereta kubwa liliotarajiwa kutoa huduma ya nishati hiyo kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa mizinguo hiyo ya umeme ilimchanganya kuliko kawaida mmiliki wa bendi ya Mashujaa, Mamaa Sakina, ambaye inasemekana alianguka na kupoteza fahamu kiasi cha kukimbiziwa hospitali akiwa hoi.

Tatizo hilo lilidumu kwa masaa kibao na kuwafanya mafundi kuihangaikia jenereta huku na huko huku mwanamuziki wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyealikwa kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo, JB Mpiana akilazimika kusubiri sana -- hadi mishale ya saa 9:00 usiku -- ndipo alipopata nafasi ya kupanda jukwaani na kundi lake kufanya kazi iliyowapa fursa ya kutua nchini kwa mbwembwe.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walishakereka mida hiyo na kutimkia zao, hivyo kukosa uhondo uliotarajiwa katika onyesho hilo ambalo awali lilikuwa na ratiba 'tamu' sana kwa wapenzi wa burudani.

Hakukuwa na taarifa za kina kuhusiana na hali ya kiafya ya Mamaa Sakina hadi kufikia leo asubuhi ya leo (Jumamosi Desemba 1, 2012); kwa mujibu wa EMMANUEL SHILATU

0 comments:

Post a Comment