Kitu kinachosadikiwa ni bomu |
Wataalamu wa
mabomu kutoka Jehsi la wananchi wa Tanzania JWTZ kambi ya Biharamulo wameanza
kazi ya kukagua kitu ambacho kimeanguka kwenye eneo la Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera.
Kituo hicho
ambacho baadhi ya watu wanasadiki kuwa ni bomu kina ukubwa wa sentimeta 50 na
umbo kama la yai huku kikiwa na nyuzinyuizi kimeanguka jana usiku katika eneo
hilo.
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu amesema wataalamu hao wa mbomu ndio
watabaini kitu hicho na kuweza kukitolea maelezo pmoja na hatua za
kuchukua.
Wapo
waliodhani kuwa kitu hicho
ni
Kombora la masafa marefu
lililorushwa kutoka nje ya Nchi
|
Ni
kitu kisichofahamika ni nini, Wapo waliodhani kuwa kitu hicho ni
Kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka nje ya Nchi,wapo waliodhani kuwa
ni Kimondo,wapo wanaodhani kuwa ni Satelite!..LAKINI Majibu yatatolewa katika Ripoti itakayotolewa
na timu/kikosi cha wanajeshi naohusika na masuala ya Mlipuko. tayari kikosi
kutoka Biharamulo kimeagizwa KUCHUNGUZA.
Eneo la Ruganzo |
Kitu hicho
kilichondoka kutoka angani hadi ardhini Usiku wa Jumatano November 21 kuamkia
Alhamisi November 22, 2012 saa nane Usiku na kuleta kishindo kikubwa kilichopelekea hali
inayofanana na tetemeko la ardhi,wakazi wengi
wa eneo la Ruganzo kata ya Kibimba wilayani Ngara mkoani Kagera wamekumbwa na hofu kutokana na kitu hicho.
Aidha kwa mujibu wa mkuu wa Ngara Bw.Kanyasu
AMEPIGIWA SIMU NA MAAFISA WA BURUNDI WAKIMUULIZA JUU YA MIUNGURUMO ILIYOSIKIKA
UPANDE WA TANZANIA.
JWTZ
WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO NA WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ZAIDI. BADO HALIJARIPUKA.
HUENDA WAKALITEGUA.
Chanzo:Radio Kwizera FM
0 comments:
Post a Comment