Mbunge wa
Nyamagana, Ezekiel Wenje, leo amechafua hali ya hewa bungeni baada ya
kusoma hotuba yaake iliyowakasirisha wapinzani wenzao wa Chama cha CUF,
jambo lililomfanya Naibu Spika Job Ndugai, kuahirisha Kikao cha Bunge
mapema asubuhi.
.....
Wabunge
wa Chama cha CUF wamezua tafrani hiyo Bungeni mjini Dodoma leo wakati
Mbunge huyo wa Nyamagana, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wenje
akiendelea kusoma hotuba hiyo ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud
Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai, akipinga
maneno yaliyokuwa yameandikwa katika ukurasa wa nane wa hotuba hiyo
yaliyosomeka Hivi:-
Mheshimiwa
Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa
kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania
haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa
tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni,
ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn
Featherstone kutoka Chama cha Libera Democratis.
Baada ya
hapo wabunge wa Cuf walisimama na kusema wakitaka maneno hayo yafutwe
ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukurasa huo wa
hotuba wakati huo msomaji alikuwa amefika kwenye ukurasa wa nne.
Baada ya
kuona mabishano na kutoelewana ukumbini humo, Naibu Spika , Job Ndugai,
alitumia busara zake na kutangaza kusitisha shughuli za Bunge kabla
mambo hayajawa mabaya maana kulikuwa na kila dalili za kuanza kushikana
mashati baada ya baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuanza kufoka kwa
sauti kubwa ndani ya Bunge, bila kufuata utaratibu.