SHOO
kubwa ya Serengeti Fiesta 2013 jijini Dar usiku wa Jumamosi ilifunga
mitaa na kusababisha kila aliyehudhuria kutoka na msemo mmoja tu, yaani
noma sana, Ijumaa Wikienda lilikuwa laivu kukupa ripoti kamili.
Snura akionyesha mbwembwe zake jukwaani.
Katika burudani hiyo, timu ya gazeti hili ilijipanga kukuletea kila
kilichojiri ambapo mapaparazi wake, Musa Mateja, Richard Bukos, Shakoor
Jongo na Erick Evarist walikuwa wakiwasiliana na mkuu wao aliyekuwa
makao makuu, Bamaga-Mwenge na kuanika matukio yote katika mtiririko wa
moja kwa moja (laivu) kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni.
Linah akicheza sambamba na Amin ndani ya Serengeti Fiesta 2013.
SAA 2:45 USIKU
Shakoor: Mkuu nipo nyuma ya jukwaa, huku mastaa wamefunikana vibaya kwa mavazi, daah! Aisee.
Makao Makuu: Shakoor ondoka eneo ulilopo, nenda katafute vituko na matukio zaidi siyo kushangaa mavazi ya hao wasanii.
Shakoor: Sawa mkuu, nimekuelewa.
SAA 3: 30 USIKU
MKE ABEBWA JUUJUU NA MUMEWE
Erick: Mkuu nipo getini hapa nje kuna bonge la msukumano kutokana na umati mkubwa wa watu wanaogombea kuingia.
Makao Makuu: Kuna kituko au tukio lolote umelishuhudia hapo?
Erick: Mkuu ngoja kuna mama mmoja amebebwa juujuu na mwanaume mmoja
anadai ni mkewe alikuwa anamsaka tangu mchana akatonywa yupo Fiesta
ndiyo amekuja kumchukua hivyo wanakabana makoo.
Makao Makuu: Waambie kama vipi tutume kikosi cha OFM, achana nao, ingia ndani unipatie kinachojiri.
Erick:
Mkuu nimeshafika mbele kabisa hapa, baada ya H. Baba kumaliza shoo,
Juma Nature ndiyo yupo stejini anapiga bonge sla shoo.
RAY C AGEUKA MPAMBE WA RECHO THT
Makao Makuu: Sijapata vituko vinavyojiri ‘back stage’, hebu chepuka upande huo mara moja.
Erick: Ndiyo naingia hapa, namuona Ray C kageuka mpambe wa Recho wa THT anampepea kabla ya kupanda stejini.
Makao Makuu: Sawa, huyu hapa Bukos, hebu sema kuna tukio gani hapo?
Bukos: Kwa sasa Walter Chilambo ndiyo amepanda anapagawisha.
Makao Makuu: Hebu tafuta matukio makubwa kwa mashabiki.
Bukos: Sawa lakini mkuu sasa ni zamu ya Godzillah anawaimbisha watu na wamemkubali kinoma na Lakuchumpa Lakuparama.
SAA 4: 40 USIKU
LINAH, AMINI MAHABA MH!
Makao Makuu (anampigia Shakoor): Shakoor mbona kimya ina maana huoni matukio?
Shakoor:
Mkuu ameshuka Joh Makini na Weusi G-Nako na Nikki wa Pili wamefanya
bonge la shoo, wamekula bonge la shangwe kisha wamewapisha Linah na
Amini ambao wanaimba kimahaba.
Makao Makuu: Ngoja nimpokelee Erick anapiga.
Erick: Mkuu sasa hivi Barnaba amepanda kuungana na Amini, wamefanya bonge la shoo kwa kutumia ‘laivu bendi’.
Makao Makuu: Oke.
Bukos: Mkuu sasa ni zamu ya Msechu, shangwe ni za kawaida.
Makao Makuu: Bukos sasa hivi nataka matukio kwa mashabiki.
Bukos: Nyuma yangu kuna sharobaro kavamia ‘maji’ anafanya fujo
kabebwa na mgambo wanamtoa nje, lazima akifika huku pombe zitamuishia.
Makao Makuu: Piga picha nazitaka ofisini.
SAA 05: 05 USIKU
SHADEE ‘AJIBEBISHA’ KWA YOUNG DEE
Erick: Mkuu hapa kwenye steji ni zamu ya Mabeste ambaye amewarusha mashabiki na Baadaye Sana kisha akampisha Christian Bella.
Makao Makuu: Oke. Shakoor anapiga ngoja nimsikilize.
Shakoor: Hapa nilipo namuona mtangazaji Shadee ‘amejibebisha’ kwa Young D, wamegandana kama ruba.
Makao Makuu: Nirushie picha fasta ngoja nimcheki Mateja.
SAA 05: 50 USIKU
RAY C STEJINI KWA MARA YA KWANZA
Erick: Mkuu
stejini ni zamu ya Recho wa THT, anapagawisha na nyimbo za Ray C.
Mashabiki wanapiga kelele baada ya Ray C kupanda stejini kwa mara ya
kwanza na kuimba naye Wimbo wa Umenikataa. Ray C amekula shangwe kubwa
kinoma.
Makao Makuu: Dah! Kweli ni mshtuko ngoja nimcheki Bukos.
6:05 USIKU
SNURA AMFUNIKA SHILOLE
Bukos: Mkuu baada ya Shilole
amepanda Snura, wewe mwenyewe unaweza kusikia anavyopigiwa kelele jinsi
alivyomfunika Shilole kwa mauno na ngoma zake za Nimevurugwa na Majanga.
Makao Makuu: Safi sana ngoja nipokee simu ya Erick.
Erick: Sasa
hivi ndiyo Linex anashuka Mkuu, naye kapagawisha kwani ameimba kwa
kushirikiana vizuri na mashabiki wake na sasa anampisha Kassim Mganga
ambaye anawarusha kinoma.
SAA 6:25 USIKU
KILA MTU NA WAKE ‘TOILETI’
Makao Makuu: Sawa, sasa hebu nipe vituko nje ya steji.
Erick:
Hapa nilipo kiongozi ni kwamba kila mwanaume anakatiza kuelekea
‘toileti’ na ‘kiburudisho’ chake kwa sababu akiacha aende mwenyewe
lazima midume wapite naye.
Makao Makuu: Duh! Kuna kingine?
7:02 USIKU
SHILOLE AZICHAPA
Erick: Upande wa pili karibu na
nyuma ya steji kuna vurugu…ngoja niwahi. Mkuu hapa namuona Shilole
anazichapa kavukavu na mrembo aitwaye Finance.
Makao Makuu: Kisa ni nini?
Erick: Shilole kamuomba tishu alipomnyima ndipo akammwagia maji kisha zikapigwa. Yule anaelekea Oysterbay kumshitaki Shilole.
7:00- 8:00 USIKU
WASANII WA KIMATAIFA
Makao Makuu: Bukos vipi wasanii wa kimataifa?
Bukos: Kwa sasa Allaine wa Jamaika ndiyo yupo stejini, anawaimbisha watu kibwagizo cha ‘nakupenda pia’, naona shangwe zimekolea.
Makao Makuu: Baada ya huyo nani anafuata?
Bukos: Mkuu listi ya
wasanii wa kimataifa bado ni ndefu, kuna Davido, Mohombi, J-Martins na
Inyanya. Pia bado wasanii kibao wa Kibongo hawajakamua kwa hiyo ngoma
inaonesha itakesha mpaka majogoo.
Makao Makuu: Sawa Bukos, wewe na timu yako endeleeni kufuatilia kila
kitu hatua kwa hatua, tunasubiri mzigo mzima asubuhi ya kesho. Shoo
ikiisha waambie wenzako mkapumzike, asubuhi muwahi ofisini.
Bukos: Sawa mkuu.